Mfalme Juha !

Karibu sana Mfalme Juha, ila nachelea kwamba wananch wako wameshaujua uJuha wako!
And guess what your days are numbered. tk tak tit tak
 
Binafsi nimeishaamua labda Lowasa mwenyewe
aseme msinichague yaani ajitoe,lakini hata Mbowe akihama
na kwenda kuongea Nyota TV
Mimi na UKAWA tu mpaka kieleweke.
 
Kitabu cha Mfalme Juha ni kitabu cha Fasihi kwa Shule za Sekondari, mwandishi anatuasa juu ya tamaa mbele mauti nyuma. Tamaa ya madaraka na kutaka kuonekana mzuri kwa watu, kutaka kulazimisha majawabu ili uwaridhishe watu, hata pale ambapo utaalamu unahitajika zaidi.

Katika kitabu hiki, Mfalme Juha anajaribu kulazimisha kila kitu kiuzwe kwa thamani ya latili moja, bila kujali thamani halisi ya kitu. Hapa Mfalme Juha alikuwa na tamaa ya madaraka na kutaka kuwaridhisha na kuwafurahisha wananchi wake bila kufuata uhalisia wa mambo na utaalamu.

Hapa napafananisha na Sera ya utumbuaji Majipu, ambapo suluhisho pekee limekuwa kutumbua Majipu hata pale ambapo utaalamu unahitajika zaidi ya tamaa ya kuonekana kwenye luninga na kutaka kuwaridhisha wananchi.

Tamaa hii ya madaraka na kutaka kuonekana kwenye vyombo vya habari na kuwaridhisha wananchi ni kukosa uelekeo halisi wa nini hasa mpango, dira na dhamira ya viongozi wetu katika kutumia utaalamu na uwezo wao wa kiuongozi katika kutatua matatizo na migogoro katika sekta wanayoiongoza.

Si kila mahali una apply utumbuaji majibu, sehemu nyingine unahitajika utaalamu na uwezo wa kiuongozi zaidi ili kutatua migogoro na matatizo ya wananchi.

Wazembe na wabadhilifu washughulikiwe lakini
tusifikie mahali tukafanya kama Mfalme Juha wa Latili moja kwa kila bidhaa.
 
hakuna kitu rahisi katika dunia hii kama kuwaongoza watanzania.,maana ukishajua juu udhaifu wao bhaaaaaaaasi!!! Kila utakalo fanya au kuongea wao watakuwa pamoja na wewe.tumekuwa watu wa kupokea mambo kama yalivyo bila hata kutumia even a minute to think.leo ukisema "nafanya haya yote kwa ajili ya kutetea watanzania masikini na wanyonge" watu watapiga makofi na kukuita jembe au mkombozi wao.INAUMA KIKUKWELI. It meanz hawa watoto wa vigogo nao hawana haki kwenye taifa lao au!!!!
 
Mi nilishakataa hizo habari kitambo.

Inaonekana mpaka JF tumekubali ujuha huo.

Kuna mtu kaweka article inambonda mfalme kutoka The Economist naona imetolewa siioni tena.

http://www.economist.com/news/middl...s-good-governs-impulsively-government-gesture

Tatizo lako upo outdated kuhusu kinachoendelea hapa Jamiiforums lakini unataka tudhani upo updated.

Hii habari ilishajadiliwa hapa mwezi uliopita lakini wewe unataka kujenga hoja kama MOD's hawafanyi kazi zao inavyotakiwa.

Kwa kukusaidia kama unataka mjadala kuhusiana na suala hilo pitia kwenye thread hii;
 
hakuna kitu rahisi katika dunia hii kama kuwaongoza watanzania.,maana ukishajua juu udhaifu wao bhaaaaaaaasi!!! Kila utakalo fanya au kuongea wao watakuwa pamoja na wewe.tumekuwa watu wa kupokea mambo kama yalivyo bila hata kutumia even a minute to think.leo ukisema "nafanya haya yote kwa ajili ya kutetea watanzania masikini na wanyonge" watu watapiga makofi na kukuita jembe au mkombozi wao.INAUMA KIKUKWELI. It meanz hawa watoto wa vigogo nao hawana haki kwenye taifa lao au!!!!
Umetumia kipimo/vipimo gani vinavyotambuliwa kimataifa kufikia hitimisho kuwa ni rahisi sana kuiongoza Watanzania ukijua udhaifu wao?

Udhaifu wa Watanzania ni upi?

Unaufahamu vipi huo udhaifu wa Watanzania?

Nielimishe!
 
Tatizo lako upo outdated kuhusu kinachoendelea hapa Jamiiforums lakini unataka tudhani upo updated.

Hii habari ilishajadiliwa hapa mwezi uliopita lakini wewe unataka kujenga hoja kama MOD's hawafanyi kazi zao inavyotakiwa.

Kwa kukusaidia kama unataka mjadala kuhusiana na suala hilo pitia kwenye thread hii;
Hiyo link uliyonipa imenipa message " page not found"

Imeondolewa?
 
Back
Top Bottom