Meremeta & TANGOLD Revealed!

Kuhani, kuna wakati unajenga hoja zinaingia kichwani lakini kuna wakati (kama huu) ambapo kuzipangua hoja zako ni rahisi kama kumchomolea mlevi.

Sheria zinaundwaje?
Jamii hujitungia sheria baada ya kuona haja au ulazima wa kufanya hivyo. Endapo kuna mahali fulani katika barabara ambapo panatokea ajali nyingi na baada ya uchunguzi ikaonekana ni kwa sababu ni karibu na shule na hakuna alama za kuvukia basi jamii inaweza kufanya maamuzi kadhaa, kuhamisha shule, kufunga barabara wakati watoto wanavuka n.k n.k Lakini jamii hiyo inapopima na kuona kuwa labda mahali hapa "panapaswa" kuwa na kivuko cha waendao kwa miguu.

Ni kutokana na kupasa huku basi wanaamua kuweka alama za kivuko cha miguu. Endapo pamoja na kivuko hicho madereva bado hawasimami na ajali zinaendelea pasipo tofauti kubwa kwa sababu hakuna adhabu yeyote ile, na kwa vile kwenye vitabu hakuna adhabu ya kwenda kasi, basi jamii au chombo husika kinaona inalazima "kutunga sheria" ya kutoa adhabu ya wanaoenda kasi n.k

Sasa, Usalama wa Taifa jinsi ulivyo sasa ni wazi una mapungufu, na mapungufu hayo si ya utendaji tu bali ni mfumo na sheria. Hivyo mwakilishi wa watu anapoonesha matatizo hayo na kupendekeza suluhisho hilo si kuota ndoto. Ni kulikabili tatizo. Kama hakuna sheria inayosema kuwa Usalama wa Taifa uangalie pia masuala yanayohusiana na uchumi n.k basi hatuwalaumu TISS bali sheria iliyowaunda.

Sasa tunaweza kukubali basi "sheria ndivyo ilivyo" au tukasema sheria zimetengenezwa na sisi wenyewe na ni sisi wenyewe tunapaswa kuzifanyia mabadiliko Hivyo tunapendekeza mabadiliko ya sheria ili kuipa nguvu taasisi hiyo. Sasa huu ni utaratibu wa nchi inayofuata sheria na Katiba.

Sasa "kupasa" huko tunakokuzungumzia kunatokana na haja (a need) na haja inatokana na hali halisi. Unapojaribu kuvuka mto unakuwa na maamuzi ya kutumia mitumbwi, kuogelea, au kujenga daraja. Haja inapoonekana kuwa daraja ni suluhisho bora na salama zaidi basi jamii inaona inapaswa kuwa na daraja na hivyo wanafanya mchakato wa kujenga daraja.

Unachoweza kunishawishi ni kusema kuwa TISS haihitaji mabadiliko yoyote, kuwa sheria iliyopo sasa inatosha kabisa na kuwa hakuna haja ya kuboresha kitu chochote na hivyo hakuna kinachopaswa kufanyika. Hiyo inaweza kuwa hoja.
 
kwanza, hao viongozi wanaoitwa mafisadi sio wana ccm hao. Ni mapandikizi ya upinzani ambao watatolewa muda si mrefu.

Sikujua Lowassa, Mkapa na Chenge ni mapandikizi ya upinzani. Kujiunga na JF kumenisaidia kujifunza mengi.
 
Huu ndio mchango wa maandishi lakini pia nimeyaongea mengi ya humu. Nikipata ule mchango wa sauti nitawaletea baada ya watu wa hansard kukamilisha kazi yao.
Mheshimiwa Spika, Katika kikao hiki na vilivyotangulia tumekuwa tukirudia kukumbushana juu ya wajibu wa Bunge lako hili tukufu, wajibu ambao kikatiba unatajwa kuwa ni pamoja na kuishauri na kuisimamia serikali. Lakini zaidi pia ambacho hatujakumbushana kwa uzito wake ni kuwa sisi ndio watunga sheria wa nchi hii; ndio wenye wajibu wa pekee wa kusema chombo gani kifanye kazi vipi, nini kiwepo, nini kisiwepo n.k Tuna nguvu ya Kikatiba ya kutunga sheria ambazo nyingi kati ya hizo zinaathiri maishi ya kila Mtanzania. Nguvu hii hii wanayo ndugu zetu wa Baraza la Wawakilishi kwa mambo yale yasiyo ya Muungano au ambayo yanahitaji ridhaa yao.


Ni kwa sababu hii Mhe. Spika naweza kusema kuwa changamoto kubwa inayotukabili kama watunga sheria, washauri na wasimamizi wa serikali yetu ni nafasi ya Taasisi na sera yetu ya Usalama wa Taifa katika kujenga na kuhakikisha uwepo wa Taifa lililo huru, lenye watu walio sawa na ambalo lina nafasi ya kufanikiwa katika jumuiya ya Mataifa ya ulimwengu. Katika kufanya hayo, Taasisi ya Usalama wa Taifa inasimama katika uwanja wa peke yake.


Ninafahamu Mhe. Spika kwamba hatujawahi kuwa na mjadala wa kina na mzito kuhusu sera na sheria zetu za usalama wa Taifa. Jambo hili limekuwa kama mwiko. Mara nyingi tumefanyia mabadiliko vipengele mbalimbali vya sheria zetu za usalama wa Taifa hasa ile ya 1970 na ile iliyounda TISS ya 1996. Karibu mara zote tumefanya hivyo pasipo mjadala mkubwa wa kuangalia athari na matokeo ya mabadiliko ya sheria hizo katika usalama wa nchi yetu. Umekuwa ni mwiko mkubwa wa kutokugusa katika sakafu hii suala la Usalama wa Taifa. Yawezekana hiyo ni kwa sababu ya unyeti wake, na hasa kutokana na sifa ya taasisi hiyo ambayo kwa baadhi ya watu yawezekana kuwa si sifa nzuri. Mhe. Spika, kwa heshima kubwa kwa Taifa letu, kwa Bunge lako tukufu, na kwa vyombo vyetu vya Usalama na hasa Usalama wa Taifa, naomba leo hii nivunje mwiko huo.


Matukio ya hivi karibuni, yametuthibitishia kuwa Taasisi yetu ya Usalama wa Taifa imelega lega, ni dhaifu, na kama tukiendelea nayo jinsi ilivyo, tutafika mahali ambapo kamwe hatukutaka kufika, tutakuwa hatuna tena Usalama wa Taifa. Tukiendelea jinsi ilivyo, pasipo kufanya mabadiliko ya haraka na ya lazima, tutakuja kujuta kwani tumeshaziona dalili za nini kinatungojea mbeleni.


Mheshimiwa Spika usalama wa Taifa umelegalega ndio maana tuko hapa tulipo leo. Leo tunazungumzia mambo ya mikataba mibovu, tunazungumzia wizi kama wa kutoboa gunia la sukari kwa panga, katika taasisi zetu hasa Benki Kuu, tunazungumzia uundwaji wa makampuni feki mengine yakiwa na viwanja si umbali mrefu kutoka maslahi ya Taasisi hii. Leo hii tunazungumzia jinsi gani watu wachache wameweza kutengeneza mtandao wa uhalifu wa fedha na ukashamiri, mtandao ambao kama Usalama wetu wa Taifa wangekuwa wanajua uwepo wake tusingefika hapa tulipofika. Mlolongo wa matukio ya kitapeli, msururu wa matukio ya kilaghai ambayo yamesababisha upotevu wa mabilioni ya shilingi zetu, ni ushahidi dhahiri kuwa Usalama wetu kama Taifa, uko matatani.


Leo hii Mheshimiwa spika, tunalazimishwa kupiga magoti na kuchuchumaa mbele ya wezi. Tunaambiwa kwamba waliohusika na upotevu wa fedha za EPA pale Benki Kuu ni kama watu waliotuteka nyara na wameshikilia bomu mkononi. Ati tukiwasukuma sana kuwadai wanaweza kulilipua. Hivyo leo hii kuna baadhi yetu wanalazimika kuzungumza nao kwa "upole" ili tusiwaudhi hao mafisadi. Tunalazimika kufanya vikao na watu waliochota fedha zetu, na tunalazimika kuficha hata majina yao. Mheshimiwa Spika, Usalama wa Taifa letu uko matatani.


Mheshimiwa Spika leo hii tunalipia mamilioni ya shilingi kila siku kwa kampuni ambayo imeichukua mkataba wa kampuni ambayo haikuweza kuingia mkataba wa awali kwani kampuni hiyo ya awal haikuwepo kisheria. Tunawalipa Dowans mamilioni ya shilingi, fedha ambazo zingeweza kutumika kumalizia miradi kadhaa ya mabwawa ya kuzalishia umeme. Tunawalipa kwa sababu Taifa letu liliacha kuingia mkataba na kampuni ambayo haikuwa na uwezo, haikuwa na historia, na haikuwa na vifaa vya kutufulia umeme wa dharura. Kampuni ambayo kama Usalama wetu wa Taifa wangekuwa makini isingepewa hata nafasi kuangika pendekezo lao la biashara.


Kwa kuangalia unyeti wa sekta ya nishati, ni jinsi gani ina athari katika shughuli za uchumi, kitendo cha Taifa kuruhusu mkataba ule kuingiwa pasipo uchunguzi wakina na taarifa ya clearance kutoka Usalama wa Taifa ni upungufu mkubwa kabisa wa sheria yetu ya Usalama wa Taifa. Na kwa vile bado tunaendelea kufanya kazi katika sheria hiyo hiyo ni wazi kuwa tusijekuombea tunapatwa tatizo jingine kubwa la nishati, kwani taratibu na sheria bado hazijabadilika na makosa kama ya Richmond yanaweza kurudiwa tena. Mheshimiwa Spika, Usalama wa Taifa letu uko matatani.


Mheshimiwa Spika kuna wawekezaji wanakuja kutoka kila kona duniani. Kuna wale ambao tumewapa eneo kubwa la ardhi yetu kiasi kwamba wanafikiri wana ubia na nchi yetu. Kuna wale ambao kutokana na sababu wanazozijua wao wenyewe wanafikiri wanaweza kuwanyanyasa Watanzania katika Taifa lao wenyewe kwa sababu tu "wamewekeza fedha nyingi". Wengine wamefikia kuwa na kiburi wakiamini kuwa wamewaweka baadhi ya viongozi mifukoni mwao. Tukiacha hali hii iendelee siyo tu tunawapa kibali cha ufisadi bali pia tunahatarisha usalama wa Taifa letu.


Mheshimiwa spika, tumefikia mahali kwamba mambo muhimu ya Taifa yanafichwa kwa kisingizio cha Usalama wa Taifa. Tumeshuhudia wote siku ya Ijumaa wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu alipozungumzia suala la Meremeta na makampuni mengine yanayodaiwa kuhusika na ufisadi Benki Kuu. Tumetakiwa kukubali kuwa uchimbaji wa madini wa Meremeta ulifanywa kwa ajili ya Usalama wa Taifa letu. Kwamba makampuni ya Deep Green, Mwananchi Gold, Tangold na Meremeta yote yaligawiwa mabilioni ya Shilingi bila kukaguliwa na mtu yeyote kwa ajili ya Usalama wa Taifa. Kwamba tumetakiwa kukubali kuwa Meremeta haijakaguliwa na Mkaguzi Mkuu kwa vile kuchimba kwake madini, kuyauza na kupata fedha vyote ni kwa ajili ya Usalama wa Taifa.


Mheshimiwa Spika huo Usalama wa Deep Green, huo Usalama wa Mwananchi Gold, huo usalama wa Tangold, huo usalama wa Meremeta, ni usalama wa Taifa gani?! Ni usalama na ulinzi wa watu wa nchi gani!? Mbona sisi wawakilishi wa wananchi wa Taifa hili ambalo Meremeta na wenzake wanatulinda, hatuna taarifa ya walinzi hao? Kama ni Usalama wa Taifa letu hawa wakurugenzi wa Afrika ya Kusini wanafanya nini humo? Je kwa kuhusisha wageni siyo kwamba tunacompromise national security?


Mheshimiwa Spika, tukikubali hilo itakuwa ni sawa na kumruhusu mtu aje shambani kwako, alime, apande, vikue na avune, kisha aende kuuza na faida kuiweka mkononi, na ukimuuliza akuambie amekuja kukutunzia shamba. Ukimwambia uone mapato aliyoyapata anasema "ni siri yake kwa ajili ya usalama wako"! Ukimwambia nani alimtuma anasema "ni siri yake kwa ajili ya usalama wako". Usalama huu wa Taifa wa Meremeta ni usalama wa nani?


Sasa Mheshimiwa Spika, kama ni usalama wa CCM, kama ni usalama wa baadhi ya watu katika serikali, kama ni Usalama wa watu fulani kwenye jeshi letu basi tuambiwe kwanini ni usalama wao!? Lakini kama kweli ni Usalama wa Taifa hili na kama kweli Jeshi letu ambalo linaitwa "la wananchi" linahusika kwa namna yoyote na mambo ya Meremeta, Tangold, Deep Green na Mwananchi Gold basi sisi wawakilishi halali wa wananchi hao tunataka kujua na tujue sasa.


Mheshimiwa Spika, wakati umefika wa kusema "enough is enough". Sasa imetosha, tunaitaka nchi yetu irudishwe. Tunataka sheria zetu zifuatwe na wavunjaji sheria hizo kuadhibiwa pasipo upendeleo, woga, hofu, au aina yoyote ile ya utwana. Tunataka Usalama wa Taifa ambao kweli utahakikisha usalama wa fedha yetu, usalama wa mali na raslimali zetu, na kwa hakika usalama wa kila kitu kiitwacho cha Mtanzania. Hatuwezi tena kuendelea kuitikia kibwagizo cha mafisadi na kuimba wimbo wa lele mama mbele yao. Umefika wakati Bunge lako tukufu Mheshimiwa Spika lichukue msimamo, Msimamo ambao utaimarisha, utaisafisha, na kwa hakika kabisa utaipa uhai mpya idara yetu ya Usalama wa Taifa, ili iwe ya kisasa zaidi, wazi zaidi, na inayowajibika zaidi kwa Taifa lake. Hilo lazima tufanye.


Mhe. Spika, Tunahitaji mabadiliko katika sehemu kubwa mbili. Tunahitaji mabadiliko ya kisheria na tunahitaji mabadiliko ya kifikra linapokuja suala la idara ya Usalama wa Taifa. Hilo la pili ni gumu zaidi, lakini hilo la kwanza ni rahisi na liko ndani ya uwezo wetu. Nimesema hapo nyuma kuwa tunajukumu la kuishauri na kuisimamia serikali, lakini jukumu letu la kwanza kabisa kama wabunge ni kutunga sheria. Hivyo hili la kufanyia mabadiliko upande wa sheria kuhusu Usalama wa Taifa limo ndani ya uwezo wetu.


Kwenye upande wa sheria, hatuna kuandika upya sheria yetu ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970. Sheria ile ilitungwa wakati dunia imegawanyika katika pande mbili, nchi za kisoshalist na zile za Kibepari, iliandikwa wakati wa Vita Baridi ambako sera yetu ya nje ilikuwa ni ya kutofungamana na upande wowote. Iliandikiwa miaka tisa tu tangu Tanganyika iwe huru na miaka sita tu tangu tuungane. Ni kweli kuna mabadiliko ya hapa na pale tuliyoyafanya, lakini naamini ipo haja ya kukaa chini na kuangalia hali ya ulimwengu leo hii, hali ya kiuchumi na kisiasa barani mwetu na duniani na hivyo kuangika sheria mpya itakayoakisi hali halisi duniani sasa hivi. Sheria hiyo mpya lazima izingatie uelewa wetu wa haki za raia na binadamu na dhana nzima ya utawala bora.


Lakini mabadiliko makubwa Mhe. Spika yanahitajika katika Taasisi yetu ya Usalama wa Taifa. Nimekuwa nikijiuliza kwa muda sasa ni jinsi gani Bunge hili liliweza kupitisha sheria iliyounda TISS ya mwaka 1996. Kwa yeyote anayeweza kuisoma sheria hiyo anaweza kushtushwa na jinsi taasisi hiyo ilipoundwa na wakati huo huo kufungwa mikono kufanya kazi yake ya Usalama wa Taifa. Inawezekana vipi tuwe na Taasisi ya Usalama wa Taifa ambayo haina nguvu ya kumkamata mtu?


Ibara ya tano ya sheria hiyo inafanya kazi ya TISS kuwa butu. Kwamba TISS wana jukumu la kukusanya habari za kijasusi lakini chochote wanachokipata inabidi wapeleke kwa mtu mwingine akifanyie kazi. Kipengele cha pili cha ibara hiyo hiyo kinaikataza TISS na ninaomba ni nukuu "(2) It shall not be a function of the Service-

to enforce measures for security;" Yaani, TISS inakatazwa kuchukua hatua za kiusalama kama vile kumweka mtu kizuizini, kukamata vitu n.k! Halafu leo tunashangaa fedha zimekombwa Benki Kuu!


Lakini zaidi pia tunahitaji kuondoa mawazo kuwa Usalama wa Taifa lengo lake ni kufuatilia watu hasa wale wanaoonekana kuikosa serikali, kuipinga au kwa njia halali kukataa utendaji wake. Leo hii bado kuna hofu miongoni mwa watu wetu kuwa ukifanya jambo fulani basi Usalama wa Taifa wanakufuatilia wanataka kujua wewe ni nani.


Usalama wa Taifa lazima iwe ni taasisi ya wananchi wa Taifa hili. Utaratibu wake wa ajira uwekwe wazi ili watu wajue na kama kuna mtu anataka ajira basi ijulikane. Mheshimiwa Spika leo kijana wa nchi kama Marekani au wa Uingereza anayetaka kutumikia Taifa lake katika maeneo ya Usalama wa Taifa haitaji kwenda mbali vigezo vyote na fomu zinapatikana kiurahisi tu kwenye mtandao. Sijui ni wangapi kati yetu humu wanajua mtumishi wa Usalama wa Taifa wa Tanzania. Sijui ni wangapi wanajua kuwa kutokana na Sheria hii ya 1996 Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaajiriwa kwa makubaliano tu kati yake na Rais (Ibara 6:2). Ni wangapi hapa wanajua kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaweza kumuajiri mtu yeyote kwa shughuli za Usalama kama anavyoona inafaa (ibara 7:2 a, b).


Hivi kwa mtindo huu wa ajira ambapo Bunge halina uamuzi wa mtu muhimu kama Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa kweli tunashangazwa na yote yanayotokea? Ni jukumu letu kusahihisha makosa yetu wenyewe, ili hatimaye tuwe na Usalama wa Taifa ambacho kitakuwa kweli ni chombo kilichowazi, chenye taratibu zinazoeleweka, na ambacho kiko mikononi mwa wananchi wenyewe na hivyo kuepukana na haya maneno ya kutumia jina la Usalama wa Taifa.


Nimalizie kwa kusema hivi. Wakati matukio ya Septemba 11 yametokea kule Marekani serikali ya nchi hiyo haikuacha mambo hayo yapite tu hivi hivi. Rais Bush kwa kufuata maagizo ya Bunge lao aliunda Kamati ya Kuangalia matukio ya Septemba 11 na kutoa mapendekezo yake. Kati ya vitu walivyoangalia ni suala zima la jinsi gani jumuiya yao ya Intelligencia licha ya kuwa na vifaa vingi vya kisasa na mtandao mkubwa duniani walishindwa kutabiri kwa uhakika na hatimaye kuzuia matukio yale. Tume ile ilipomaliza kazi yake ilipendekeza mabadiliko makubwa katika Usalama wa Taifa la Marekani kwa kuunda Kurugenzi mpya ya Usalama wa Taifa na kulazimisha idara ambazo zilikuwa hazitakiwa kuwasiliana kisheria zianze kushikiriana na kupashana habari. Kosa la kushindwa katika mambo ya kijasusi wenzeti wa Marekani hawakuliacha lipite tu kama mapenzi ya Mungu.


Sisi leo hii tuna matukio mengi ambayo yamedhihirisha kuwa Jumuiya yetu ya mambo ya Intelligensia haijaenda na wakati na bado hakuna legal framework ambayo inalazimisha taasisi zetu za Usalama kuwasiliana na kupashana habari. Ni matumaini yangu kuwa serikali itakaa chini na kuja na kufanya utafiti na upembuzi yakinifu wa jinsi gani tunaweza kuiboresha idara yetu ya Usalama wa Taifa ili kweli tujiandae na ushindani katika nyanja zote za maendeleo na tusiachwe nyuma tena. Tunao watanzania wengi ambao wako nje ya nchi na ambao wako kwenye taasisi mbalimbali ni wakati wa kuanza kuwatumia hawa na nina uhakika kama tungekuwa makini suala la Richmond lingekwepeka mapema sana kwani baadhi ya ndugu zetu walioko Marekani walishatuambia tangu siku ya kwanza kwamba kampuni hiyo ni feki.

This was excellent. Academically, one could say you scored High Distinction, or A+
 
kwanza, hao viongozi wanaoitwa mafisadi sio wana ccm hao. Ni mapandikizi ya upinzani ambao watatolewa muda si mrefu.
Du, ndugu yangu Masaka sijui umeanzia kilabu la mataputapu ya namna gani aisee. Unasema viongozi mafisadi wa CCM ni mapandikizi ya upinzani kweli? Yaani hata Mkapa na Lowasa ni mapandikizi ya upinzani?.

Aisee itabidi upunguze hiyo dozi unayotumia, inakudhuru akili.
 
raisi alipomteua pinda alitakiwa afanyembadiliko pia na makatibu wa wizara ilikumpa pinda katibu mwingine.lakini kuwaacha wale wa lowasa,haya ndio matatizo yake.
hawa wataendelea kumpinda pinda mpaka na yeye ataondoka kama mwenzake.kuna hatari ya kuwa na mawaziri wakuu wanne kabla jk ajamaliza muda wake.

I hope you mean 2010!
 
Du, ndugu yangu Masaka sijui umeanzia kilabu la mataputapu ya namna gani aisee. Unasema viongozi mafisadi wa CCM ni mapandikizi ya upinzani kweli? Yaani hata Mkapa na Lowasa ni mapandikizi ya upinzani?.

Aisee itabidi upunguze hiyo dozi unayotumia, inakudhuru akili.

Ndio maana kuna wachangiaji wengine wamesema huyu jamaa ni Schizo:


...Nimesoma ile habari ya michuzi kuhusu ziara ya Kelly Rowland uwanja wa fisi

Kwa dakika 30 zilizopita nimekuwa naona hii picha huku machozi yakinitoka pwacha pwacha. Hali hii imenitisha na kuniogopesha kuhusu mwelekeo wa nchi yetu. ..

...Kwa kuona haya, nitakuwa najidanganya kuendelea kutetea chama changu cha ccm hapa mtandaoni kama haya yanatokea wakati wachache tu kwenye chama wakinufaika na pesa zote za Tanzania. Sitaki tena kuwatetea wana ccm hapa mpaka watakapoanza kushughulikia matatizo ya wananchi.

...Nawaomba msamaha wana JF ambao niliwasumbua hapa wakati ambao nyie mnajaribu kupigana kwa hali na mali kuisaidia Tanzania itoke kwa mafisadi wachache ndani ya chama chetu.
 
Masaka nenda taratibu siasa za kutishana zimepitwa na wakati. Juzi juzi tu umeomba msamaha hapa kwamba umeelewa kuwa chama chako cha CCM kimekuwa kinafanya makosa leo unasema CCM watu watawekwa ndani especially Zitto na Dr Slaa. taratibu kijana!
 
Tena Pinda ukome kabisa na sura yako ya mbuzi wakati unapewa tu hicho cheo ulituapia kuwa ukila rushwa Mungu akuue sasa nataka kukukumbusha kuwa hata kutetea ufisadi ni dhambi kubwa kuliko kula kula rushwa na kwa taarifa yako usijekulogwa watanzania wakakuchukia utakiona hicho cheo ni shubiri

Samahani ndugu Major nadhani lugha uliyotumia si nzuri. Huo si mwendo wa JF
 
Halafu wakuu...Rejea hiyo quote hapo juu...

Naomba kama kuna anayejuwa anijibu hili.
Rais huchagua mkurugenzi wa Idara ya Usalama ambaye ndiye mwajiri wa wanausalama.
Je...Mkurugenzi wa usalama wa MKAPA NA KIKWETE NI MMOJA AMA TOFAUTI?
NA KAMA NI TOFAUTI...BASI LAZIMA MMOJAWAPO NDIO WA KUSIKILIZWA

Wakuu hakuna mwenye jibu la kuhusu wakurugenzi wa usalama?
wa mkapa na JK?
 
jmushi... ungekuwa unasoma mada nyingi kuhusu Usalama wa Taifa ungepata majibu. Mambo haya yameshadiliwa vya kutosha. So, just google "Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa"... work a little bit to find answers my friend.
 
It was a question for everbody.
We work together towards a common GOAL...JUSTICE!
AREN'T WE?
Kwani niliuliza swali lenye kuhitaji majina mawili tu ya wakurugenzi wa usalama wa TAIFA wa awamu ya TATU NA NNE na si mambo ya mjadala!
Any ways nitafanya hivyo.
 
Samahani kama nitakuwa nimechelewa kidogo kutoa pongezi, ila ningependa kumpatia Mheshimiwa Zitto hongera na asante nyingi for spending his weekend working for wananchi, kama alivyotuahidi.

Kuna thread mbili zilikuwa zikizungumzia ama zikitafuta majibu ya kwanini wabunge wetu wana matumbo makubwa. Now I get the answer about SIRI ya ku-maintain weight nzuri, which is kutumia wikiendi efficiently kwa kujiandaa vizuri kwa wiki inayofuatia (matokeo yake unakuja na hoja fresh na zenye nguvu siku ya jumatatu), kama ndugu yetu Zitto alivyofanya, na sio ku-spend the weekend kwenye bia na kitimoto kama the majority of wawakilishi wetu wanavyofanya (matokeo yake ni kulala bungeni asubuhi na mapema siku ya jumatatu kwa sababu ya mafuta waliyokula wikiendi yanakuwa bado hayajawa digested vizuri).

Asante sana ndugu yetu Zitto kwa kuiweka hoja hii vizuri. Tanzania ingekuwa mbali sana kama tungekuwa na wachapa kazi kama 10 tu bungeni kama wewe.
 
Asante sana ndugu yetu Zitto kwa kuiweka hoja hii vizuri. Tanzania ingekuwa mbali sana kama tungekuwa na wachapa kazi kama 10 tu bungeni kama wewe.

Au hata mtu tano hivi.

Sasa hivi kuna wangapi, wawili watatu. Tungepata nondo nyingine kama tatu hivi, sisiemu wangekoma.

Duuh, kazi njema Zitto.
 
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia hotuba hii ya Ofisi ya Rais ambayo inajumuisha masuala ya Utumishi, Utawala, TAKUKURU, Usalama wa Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini leo tunapozungumza hapa na Waziri wa Zambia alikuwepo hapa. Nchi ya Zambia inajenga reli mbili. Moja kuelekea Bandari ya Msumbiji, na nyingine kuelekea Bandari ya Angola. Reli zile ndizo zitakazosafirisha copper yao na ndizo zikazosafirishwa madini yao mengine yoyote ama kwenda Rwanda au kwenda Manyika Msumbiji. Madhara yake ni nini? Ni kwamba TAZARA itakufa, TAZARA haitapata mizigo ya kusafirisha kutoka Zambia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya kati hii haitapata mizigo ya copper kutokea Mashariki ya Kongo kwa sababu watajenga reli kutokea Rungumbasi kwenda Lusaka kuunganisha mpaka kwenda kule Rwanda. Hii ndiyo kazi ya Usalama wa Taifa ilipaswa kufanya. Ilipaswa tufanye economic espionage kuweza kuona madhara ya maamuzi ya nchi zingine ambazo zinatuzunguka.

Nilishawahi kuzungumzia kuhusu bandari yetu ya Dar....Kama Muungwana angeacha kushamilia wawekezaji wa madini tu na kusahau mali asili isiyoisha ambayo ni bahari na kilimo leo tungekuwa mbali sana....mimi naamini tungeitumia port yetu ipasavyo,fedha ambazo zingepatikana hapo zingeweza kujenga barabara zote Tanzania bara.

Wazambia,Wazaire,Wamalawi,Warwanda na Waburundi wote wamechoshwa na urasimu unaoendelea hapo Dar Port hata sisi waTanzania wengi tu tunatumia Mombasa port.....Sidhani kama Muungwana kuwa halijui hili Zambia kujenga reli....kama sikosei wakati wa kampeni alinena sana mambo ya kuendeleza bandari yetu.

Cha ajabu alipochukua Ikulu,basi ametulia as if Ikulu ni holiday place...hakuna alichofanya zaidi ya kuwakumbatia kina Sinclair and co...hence smile isiyokauka.
 
Hawa watu toka wamwue KOMBE KWA VISINGIZIO VYA UJAMBAZI SINA IMANI KUBWA NA WAO!
ILA NINA UHAKIKA USALAMA WA TAIFA INAHITAJI MABADILKO KWANI USALAMA SI WA WANANCHI BALI WA IDEOLOGY ZA UJAMAA ZILIZOKUWA ZIKILINDWA KULIKO HAKI NA UBINADAMU WA MWANADAMU HUYO HUYO WALIOKUWA WAKIJIDAI KUMTETEA!NI hatua nzuri kudai hiyo revamption...HOWEVER...WE WANT ACTION!

Tumenyanyaswa (Walimnyanyasa marehemu Baba yangu) sana na hawa the so called "Usalama wa taifa" kwa kutaka kulinda Ideology za ujamaa ambazo hazijafika popotee.
Lakini zaidi pia tunahitaji kuondoa mawazo kuwa Usalama wa Taifa lengo lake ni kufuatilia watu hasa wale wanaoonekana kuikosa serikali, kuipinga au kwa njia halali kukataa utendaji wake. Leo hii bado kuna hofu miongoni mwa watu wetu kuwa ukifanya jambo fulani basi Usalama wa Taifa wanakufuatilia wanataka kujua wewe ni nani.
Asnte kwa kusema hilo Mhe Zitto kwa sababu wakati wa miaka hiyo ya nyuma Nyerere aliitumia sana na watu ambao walikuwa tofauti naye na Idea zake, na hii kitu ilimlinda, alituma sana watu nyumbani kwetu. Asante sana Kaka.
 
Usalama si lolote si chochote.Wewe nenda ofisi yeyote ya RSO ucheke mwenyewe.UTAKUTA MAKABATI YA MAFAIL YA MAJINA YA WATU yamejazana hukooooooo,we??.Sisi tulikuwa tunawacheka kuwa wako tuition.Uliza Implementation sasa duuu ziro.

Yani aibu.
 
kuhani.. umeshindwa kuona jambo moja dhahiri katika hoja ya zitto, TISS wameshindwa kufanya kazi zao si kwa sababu ya utendaji bali kutokana na sheria iliyopo. Sheria iliyopo na sera ya usalama wa Taifa (ambayo sijui nani anayo) inafanya vigumu sana kwa usalama wa Taifa kufanya kazi ambayo tunaamini inapaswa kuwepo katika ajenda yao.

Ukiangalia sheria ya Usalama wa Taifa utaona majukumu ya Idara hiyo, majukumu ambayo kimsingi hayasimamii usalama wa Taifa bali kukusanya habari tu.

Hivyo suala la kubadili sheria ni msingi mkubwa wa kuleta mabadiliko katika utendaji.

Asante mkuu...Nadhani sasa Kuhani atakuwa ameelewa! Taratibu tunaanza kuwekana sawa hapa..ingawa wengi bado wanachechemea ila tutafika tu.

Wembe
 
Back
Top Bottom