Meremeta & TANGOLD Revealed!

Zitto God bless and Live long brother.

Hii contribution ya Zitto iwe changamoto kwa vijana wengine wenye uwezo kuingia kwenye siasa. Zitto needs support in the house, jitokezeni vijana 2010 hiyooo, nani atatuwakilisha ipasavyo kama Taifa na sio chama? Think about it vijana.
 
Zitto God bless and Live long brother.

Hii contribution ya Zitto iwe changamoto kwa vijana wengine wenye uwezo kuingia kwenye siasa. Zitto needs support in the house, jitokezeni vijana 2010 hiyooo, nani atatuwakilisha ipasavyo kama Taifa na sio chama? Think about it vijana.

Utawezaje kugombea kama sio mwanachama wa chama chochote?
 
Zitto God bless and Live long brother.

Hii contribution ya Zitto iwe changamoto kwa vijana wengine wenye uwezo kuingia kwenye siasa. Zitto needs support in the house, jitokezeni vijana 2010 hiyooo, nani atatuwakilisha ipasavyo kama Taifa na sio chama? Think about it vijana.

Mama,

You made my day!!!

And here where I see why Zitto is shining... he is shining simply b'se mawazo yake... lazima yawe bora kuliko ya Kingunge, Mzindakaya... Chacha... etc...

We need Kitila nao waingie bungeni...
 
Mama,

You made my day!!!

And here where I see why Zitto is shining... hhe is shining simply b'se mawazo yake... lazima yawe bora kuliko ya Kingunge, Mzindakaya... Chacha... etc...

We need Kitila nao waingie bungeni...

Kasheshe pls Mkuu, edit your post, you can't afford kumwita Mhe. Zitto ... she..
 
Plain and directly to the point, devoid of ambiguous diplomatic double talk.

Just what we need in that august body.

Thanks Zitto for carrying the torch, let's burn them.
 

Natafuta kazi Usalama wa Taifa,hata leo naomba mnipe tena naomba mnipe mapema

Nahitaji kazi ambayo nitaifanya kwa malipo madogo ila kwa ajili ya wanajamii
Nataka kuwasaidia kuwajua kwa undani wale waliochukua Pesa za EPA ili wajulikane
Nataka niajiliwe ili nionane na Rais na nimwambie yaliyo moyoni mwa watanzania

Nataka kazi usalama ili na mie nichukue pesa za EPA na niwagawie watanzania Masikini
Nataka tu sababu najua nikiwaomba pesa kwa njia ya kawaida hawatanipa.
Nafuta kazi ili niwape watanzania habari wanazotaka kujua
Niko tayari kufanya nao kazi kwa masharti ya uwazi na ukweli

Nataka Rais Ajue kwamba watu wanafanya ufisadi wa khali ya juu kwasababu ni rafikize
Nataka nimwambie Rais jinsi wachache wanavyowadharau walio wengi
Nataka nimwambie Rais ni watu wangapi mpaka sasa ni mafisadi wakubwa
Nataka kazi usalama ili nimjue vizuri rais wetu na tabia yake ya maamuzi

Nataka kazi usalama ili nifanye uchunguzi kuhusu BOT,
Nataka nimjue mmiliki wa Kagoda alipewa shilingi ngapi ?
Nataka niwajue waliorudisha Pesa za EPA mpaka sasa
Nataka kazi Usalama ili niwaambie watanzania ukweli ni wapi alipo Balali

Nataka kazi Usalama wa taifa ili nitoe majibu kuhusu Chenge
Natafuta kazi usalama ili niwaambie jinsi Dili ya RDC ilivyosukwa
Natafuta kazi ili nijue je Rais anawachukuliaje walihsuika na Richmond
Nataka kujua ni kwanini serikali hawatoi majibu ya Ripoti ya Richmons na EPA

Natafuta kazi siyo kwa ajili ya kumlinda Kada wa CCM wala kiongozi
Natafuta kazi ili kulisnda heshima ya nchi yetu
Natafuta kazi ili nchi hii iwathamini wafanyakazi na wakulima
Niko tayari kwa mshahara mdogo ila niwe huru kuwaambia wananchi

Ndiyo nataka Kazi Usalama wa Taifa na nataka Nafasi ya Ukurugenzi ndiyo ninayo itaka


Mheshimiwa Spika...Usalama wa Taifa utaratibu wake wa ajira uwekwe wazi ili watu wajue na kama kuna mtu anataka ajira basi ijulikane. Mheshimiwa Spika leo kijana wa nchi kama Marekani au wa Uingereza anayetaka kutumikia Taifa lake katika maeneo ya Usalama wa Taifa haitaji kwenda mbali vigezo vyote na fomu zinapatikana kiurahisi tu kwenye mtandao. Sijui ni wangapi kati yetu humu wanajua mtumishi wa Usalama wa Taifa wa Tanzania. Sijui ni wangapi wanajua kuwa kutokana na Sheria hii ya 1996 Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaajiriwa kwa makubaliano tu kati yake na Rais (Ibara 6:2). Ni wangapi hapa wanajua kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anaweza kumuajiri mtu yeyote kwa shughuli za Usalama kama anavyoona inafaa (ibara 7:2 a, b).

Hivi kwa mtindo huu wa ajira ambapo Bunge halina uamuzi wa mtu muhimu kama Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa kweli tunashangazwa na yote yanayotokea? Ni jukumu letu kusahihisha makosa yetu wenyewe, ili hatimaye tuwe na Usalama wa Taifa ambacho kitakuwa kweli ni chombo kilichowazi, chenye taratibu zinazoeleweka, na ambacho kiko mikononi mwa wananchi wenyewe na hivyo kuepukana na haya maneno ya kutumia jina la Usalama wa Taifa.


Mkuu Gembe, yamefika mwanangu!

Bunge la Tanzania halijawahi kusikia hivi vitu.

Halafu Zitto hakumtetea Pinda. Babu kubwa!

(Assuming hiyo script ya Usalama ilikuwa delivered in the speech. Tusubiri Hansard.)
 
Kasheshe pls Mkuu, edit your post, you can't afford kumwita Mhe. Zitto ... she..

Sorry wakuu... niliandika kwa haraka... lakini hata hivyo wewe ndio wa ku-edit sasa :) kwi kwi kwi...

Mh. Zitto anisamehe hata hivyo na hili!!!
 
Mbona Mkuu wa Usalama wa Taifa na Waziri wa mambo ya ndani hawajakanusha kuhusika na mitaji hiyo , pengine fedha yote inayopatikana huko wanawalipa mainfoma wao ambao wanawapatia habari nyeti ,hata hivyo bado hesabu yao na mahitaji yalikuwa yaunganishwe katika bajeti ya ulinzi yakibeba tagi ya "...matumizi maalum.."
Inawezekana kuna mambo au sehemu fulani yamewekwa rehani na ikiwa Tanzania itavamiwa basi ni jukumu aliepewa sehemu hizo kupigana na kuikomboa Tanzania ,hata hivyo haingii akilini maana vita vya kagera hatukuona tumevamiwa tumepigwa tumejikomboa ,kupeleka majeshi Comoro bado hatujaona faida ya sehemu hizo kuwekwa rehani au ni CCM ndio wametoa sehemu hiyo kwa vigogo wa Usalama wa Taifa ili kuilinda kwa hali na mali kama walivyoenda kuilinda kule Unguja na Pemba ? na Juzi juzi kuwapiga watu kule KITETO ,maana wahusika hatuoni kukamtwa wala kuchukuliwa hatua wanafanya wanavyotaka ,na kwa vile wanaofanya inawezekana kabisa kuwa ni hawa watu wa usalama wa Taifa na mipango yao ya siri kwani ninavyofahamu watu hawa hata wakipelekwa kwenye vituo vya polisi huachiwa na kesi huyayuka na ushahidi kupotezwa na kuwa kila kitu kimemalizika kama hakuna lililotokea mfano mauaji ya Zanzibar 2001 Mauaji ya watu 79 Pemba Unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia 2005 Pemba na upigwaji wa wananchama wa chama cha Upinzani pale KITETO yote haya mambo hayajulikani yameishia wapi na yote yaliripotiwa katika vituo vya polisi na polisi kuahidi kufuatilia lakini hadi naingia mitamboni hakuna lolote na yote yameshawachwa kwenye mataa ,bila ya shaka wahusika ni watu wa Usalama wa Taifa kwani mambo wanayoyafanya huzimika kimya kimya na mnyonge kunyimwa haki yake na ndio inavyoelekea hapo bungeni haki haitapatikana kwa sababu wahusika ni watu wa usalama wa Taifa.
 
Tofauti Hapa Ni Hii...
Zitto Kachagua Upande Mzuri Na Wa Haki Wa Usalama Wa Taifa....where As..kayaanza Mpinda Haki...aliyatetea Ama Ana Itetea MiZENGO Ya Wana Usalama Mafisadi.
 
Hawa watu toka wamwue KOMBE KWA VISINGIZIO VYA UJAMBAZI SINA IMANI KUBWA NA WAO!
ILA NINA UHAKIKA USALAMA WA TAIFA INAHITAJI MABADILKO KWANI USALAMA SI WA WANANCHI BALI WA IDEOLOGY ZA UJAMAA ZILIZOKUWA ZIKILINDWA KULIKO HAKI NA UBINADAMU WA MWANADAMU HUYO HUYO WALIOKUWA WAKIJIDAI KUMTETEA!
NI hatua nzuri kudai hiyo revamption...HOWEVER...WE WANT ACTION!
 
Mama,

You made my day!!!

And here where I see why Zitto is shining... he is shining simply b'se mawazo yake... lazima yawe bora kuliko ya Kingunge, Mzindakaya... Chacha... etc...

We need Kitila nao waingie bungeni...

MBOWEISM inaanza kuingia, na pia kwanini useme WE BADALA YA i?
 
MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia hotuba hii ya Ofisi ya Rais ambayo inajumuisha masuala ya Utumishi, Utawala, TAKUKURU, Usalama wa Taifa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajitahidi muda uwe wa kutosha nichangie maeneo matano. Kwanza, nitaanza na Idara ya Usalama wa Taifa, Tume ya Mipango, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, suala nzima la wastaafu na suala la TAKUKURU.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 Sheria namba 3 na Sheria Namba 15 iliyoanzisha Tanzania Interagency and Security Service -TISS, Sheria namba 15 imeunda Chombo muhimu sana kwa ajili ya usalama wa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ninasikitika kwamba chombo hiki Sheria imekiziba mikono, na sheria imekifanya hasa hasa Sheria ya mwaka 1996 imekifanya chombo hiki kishindwe kabisa kabisa kufanya kazi ambazo kinapaswa kufanya kwa ajili ya ulinzi wa Taifa letu. Na imekuwa ni nadra sana kuzungumzia suala la Usalama wa Taifa katika Bunge hili ni kwa sababu ya unyeti wa Usalama wa Taifa. Lakini tukikaa bila kulizungumza tutaendelea kupata matatizo makubwa sana. Toka mwaka jana Taifa limekuwa likipiga kelele, viongozi mbalimbali wamekuwa wakipiga kelele kuhusiana na masuala ya ufisadi, na masuala haya siyo kwamba ni mazuri sana kuyazungumza. Kwa sababu si kwamba yanatusaidia sana, maana yake ukiangalia flow ya FDI Foreign Direct Investment inaangalia sana masuala kama haya ya ufisadi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ni lazima tuyazungumze kwa sababu ni sawasawa na mtu ambaye anataka kusafisha mtaro, unapotaka kusafisha mtaro wa maji machafu ni lazima kwanza uchafuke uingie kwenye mtaro, uusafishe, utoke uende ukaoge baada ya kuwa mtaro umekuwa msafi. Sasa lakini Serikali imekuwa ikipiga danadana sana katika suala hili nzima, na imekuwa ikipiga danadana kwa sababu hatujaitumia vizuri Idara ya Usalama wa Taifa. Kwa sababu Sheria za Idara ya Usalama wa Taifa zimeibana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano wa masuala matatu tu. Kwa mfano, suala la nishati ni suala la Usalama wa Taifa, national security concerned ilikuwaje nchi yetu ikaingia mikataba ya nishati bila clearance ya Usalama wa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu mikataba kama hii inapaswa kupata clearance ya Usalama wa Taifa ili tuweze kuona kwamba nchi inafaidika au haifaidiki, kufanya espionage kuweza kujua kampuni hii ni halali ama siyo kampuni halali. Lakini matokeo yake tumeingia kwenye matatizo kama nchi na Idara tunayo, watu tunao, tunawa-finance kila mwaka tunapitisha bajeti hapa na wala huwa haijadiliwi kwa kina bajeti ya Usalama wa Taifa, lakini kwa sababu Sheria imesema kazi yao hao ni kutoa ushauri tu, baada ya ushauri hakuna kinachofanyika.

La pili, ni suala ambalo Serikali imetoa kauli hapa juzi ni suala la Meremeta. Nataka kuwahakikishia suala la Meremeta halina uhusiano wowote na Usalama wa Taifa. Leo hii Bunge linaambiwa kwamba Meremeta haiwezi kuzungumzwa kwa sababu ni la Usalama wa Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nataka niwambie Kamati ya Rais ya Madini ilijadili suala la Maremeta. Ndani ya Kamati ya Rais ya Madini kulikuwa na watu wengine ambao siyo Waheshimiwa Wabunge, kulikuwa na watu ambao ni wafanyabiashara tu wala hawajawa vetted wala watu hao hawajala kiapo chochote, lakini tulijadili nao suala la Meremeta na tukatoa mapendekezo mahsusi kuhusiana na suala la Meremeta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Meremeta ni wizi, ni wizi wa waziwazi na ni wizi ambao ni lazima Serikali ije clear na iseme, na kama haiwezi kusema in public ndiyo maana Bunge lina Kamati za Bunge. Tuna Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kamati hii inaweza ikafanya mikutano yake in camera, mikutano ile isionyeshwe na Serikali ikaeleza ukweli kuhusu suala hili ili hayo mambo tuyamalize tuanze kujadili masuala ambayo yanahusu maendeleo ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini anaposimama Kiongozi wa Serikali tena Kiongozi mkubwa kabisa akasema hili hata mnisulubu nalo silisemi, hapana. Nitahitaji Bunge lipate maelezo mapya kuhusiana na suala hili, na kama hayawezi kutolewa humu in floor maelezo hayo yatolewe kwenye Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kwa sababu suala la Meremeta ni wizi na halina uhusiano wowote ule na Usalama wa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nizungumzie kitu kimoja, muone wenzetu jinsi ambavyo wanatumia Idara zao za Usalama wa Taifa sawa sawa. Mwaka 2005 Bunge hili liliamua kupiga marufuku uuzaji wa Tazanite ghafi na madhara ya marufuku hiyo ilikuwa ni kupoteza ajira 500,000, kule India kuna Mji mmoja unaitwa Jai Pool. Idara ya Usalama wa Taifa ya India ina kitengo cha Economic Espionage wakajua madhara ya uamuzi wa Serikali ya Tanzania. Walichokifanya wakaongeza scholarship kwa Tanzania, wakaalika viongozi wetu kule mpaka leo hii Tanzanite bado inasafirishwa ikiwa ghafi. Kwa sababu walifanya espionage wakatuzuia hatukutekeleza maamuzi ambayo sisi tuliyafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini leo tunapozungumza hapa na Waziri wa Zambia alikuwepo hapa. Nchi ya Zambia inajenga reli mbili. Moja kuelekea Bandari ya Msumbiji, na nyingine kuelekea Bandari ya Angola. Reli zile ndizo zitakazosafirisha copper yao na ndizo zikazosafirishwa madini yao mengine yoyote ama kwenda Rwanda au kwenda Manyika Msumbiji. Madhara yake ni nini? Ni kwamba TAZARA itakufa, TAZARA haitapata mizigo ya kusafirisha kutoka Zambia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya kati hii haitapata mizigo ya copper kutokea Mashariki ya Kongo kwa sababu watajenga reli kutokea Rungumbasi kwenda Lusaka kuunganisha mpaka kwenda kule Rwanda. Hii ndiyo kazi ya Usalama wa Taifa ilipaswa kufanya. Ilipaswa tufanye economic espionage kuweza kuona madhara ya maamuzi ya nchi zingine ambazo zinatuzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa rai kwamba ifike mahali Bunge liamue na nimetoa mchango mrefu sana kuhusiana na suala la Usalama wa Taifa nitauwasilisha kama mchango wa maandishi kwa sababu siwezi kupata muda mrefu zaidi wa kuweza kulizungumzia. Bunge liamue kwamba ni lazima tupitie upya Sera yetu ya Usalama wa Taifa, ni lazima tufanye marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa na kifungu kimoja cha Sheria ya TISS ya mwaka 1996 kifungu 5(2)(a) ambacho kinawapa TISS kazi yao wakishaona kama kuna tatizo wanamwambia Waziri tu mhusika hawana uwezo wa reinforce security ndilo tatizo lililotokea katika EPA. Kwa sababu fedha za EPA zinaibiwa zimeibiwa kwa cash, Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa inafahamu, lakini hata kama walitoa ushauri usingeweza kutekelezwa. Nilikuwa naomba suala hilo liweze kuangaliwa kwa kina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ambalo ninataka ni Tume ya Mipango. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais kuunda Tume ya Mipango ni muhimu sana, na ni kitu ambacho kwa kweli kitatusaidia sana huko tunakokwenda. Lakini sikubaliani hata kidogo na wala haina mantiki Tume ya Mipango kuwasilisha Bungeni hapa na Waziri anayehusika na Utumishi na nitawambia madhara yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, mmeshuhudia mchango wa bajeti wa mwaka huu. Waheshimiwa Wabunge, takriban wote wamejikita katika masuala ya fedha, masuala yale ya bajeti ya Wizara ya Fedha. Masuala yote yanayohusiana na mipango ya kiuchumi hayakupewa kipaumbele. Ukiangalia bajeti ambayo Mheshimiwa Hawa Ghasia ameiwasilisha leo ni paragraph mbili tu ndizo zimezungumza kuhusu Tume ya Mipango. Tume ya Mipango inapeleka taarifa yake kwa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala hawawezi kuyajadili hayo mambo. Haya mambo ni ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kutoa rai ninajua kuna wasiwasi wa kwamba wananchi wataona kwamba Mawaziri ni wengi sana, hatuwezi ku-risk kutokuwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayehusika na Tume ya Mipango peke yake, na nitawambia leo hii kila baada ya miaka miwili kuna kitabu kama hiki kinazalishwa na Serikali, Poverty and Human Development Report, hiki kitabu ndicho kinacho-guide Mipango ya Maendeleo ya nchi na juhudi za uzalishaji na juhudi za kupunguza umaskini. Kitabu hiki kinatolewa na aliyekuwa commissioned na Serikali, na miongoni mwa vitu ambavyo vinapaswa kufanywa ukiangalia chapter four ya kitabu hiki inazungumzia mikakati ya ukuaji wa uchumi wa nchi. Lakini ukiangalia katika mpango mzima wa kazi wa Tume ya Mipango ile chart ambayo Mheshimiwa Waziri ametuonyesha hakuna reference yoyote inayoonyesha shughuli kama hizi zitakuwa zinafanywa namna gani? Utakuwa vipi na Tume ya Mipango ambayo haiangalii. Maana yake Tume ya Mipango ni vision 2025, Tume ya Mipango ni MKUKUTA na hii Taarifa ndiyo utekelezaji wa masuala kama hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa namwomba Mheshimiwa Waziri Hawa Ghasia azungumze na Mheshimiwa Rais ni bora tuingie gharama ya kumlipia mtanzania mmoja kwa ajili ya kuwa mwakilishi wa Tume ya Mipango katika Bunge akiwa kama Waziri wa Nchi wa Mipango. Hatuwezi kuwa hivi tunavyokwenda tutapata tabu sana huko tunakokwenda. Kwa hiyo, naomba suala hili liweze kuangaliwa kwa jinsi ambavyo linavyostahili. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu ambalo nataka kulizungumzia ni suala la Maadili ya Viongozi. Tuna tatizo kubwa sana katika Maadili ya Viongozi, Sheria ya Maadili ya Viongozi Sheria namba 13 ya mwaka 1995 ina mapungufu makubwa sana, na kumekuwa na juhudi za kutaka kuifanyia marekebisho. Mimi binafsi nimewasilisha Ofisi ya Spika, Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Viongozi ili tuweze kuifanya iwe na nguvu zaidi. Lakini tumefahamishwa na Waziri kwamba taratibu za ndani ya Serikali za Mabadiliko ya Sheria hii zimeanza kuandaliwa. Lakini tuna tatizo kubwa sana kwamba Taarifa ambazo viongozi tunazitoa kwa ajili ya mali na madeni yetu zinachezewa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kutoa rai kwamba hufanyike uchunguzi maalum tuweze kulinganisha fomu ambazo Waheshimiwa Wabunge wote tulizisaini wakati tumeingia Bungeni na zile za kila mwaka na fomu ambazo zipo Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi kuna baadhi ya fomu tutakuta zimerekebishwe baada ya matatizo fulani fulani kuwa yametokea. (Makofi)

Kwa hiyo, nilikuwa nataka tuchukue fomu zote za Waheshimiwa Wabunge ambazo zipo Ofisi ya Spika, kwa sababu copy moja inabakia katika Ofisi ya Spika, copy nyingine inaenda Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi tuweze kuangalia kuna matatizo makubwa sana. Kwa hiyo, suala hili la maadili ya viongozi liweze kuangaliwa. Mapendekezo ambayo yametolewa na Spika alitoa uamuzi kwamba Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala iiangalie Sheria hii ya Maadili na nilitarajia kwenye Taarifa yao wangeweza kugusia kitu kama hicho, hawakukigusia wameenda tu juu juu.

Lakini pili, tunahitajika kuwawezesha wale watanzania wanaofanya kazi katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi waweze kuwapatia mafunzo mahsusi kwa sababu ni moja ya Idara ambayo inapewa bajeti finyu sana, lakini ina handle mambo nyeti sana, kwa sababu siri zetu zote, mali zetu zote, madeni yetu yote yanafahamika kwa watu wale. Kwa hiyo, ni lazima tuhakikishe kwamba tunawawezesha jinsi ambavyo inavyostahili ili waweze kufanya kazi yao sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, nimesikitika sana kwamba hotuba ya Mheshimiwa Waziri haijagusia kabisa suala la wastaafu, na hao ni watanzania ambao wamefanya kazi ya kujenga nchi yetu kwa miaka yao yote na kuna matatizo makubwa sana ya wastaafu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wastaafu wanapata shilingi 21,000/= kwa mwezi, na sisi Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi tunavyosumbuliwa na wastaafu hao huko kwenye Majimbo kwetu, lakini Mheshimiwa Waziri hajaelezea chochote. Sasa sijui siyo suala ambalo haliko kwenye mandate yake kama Waziri au ni vipi? Lakini nilikuwa nadhani kuna haja ya kuangalia upya suala hilo la wastaafu ili tuweze kuhakikisha kwamba ni watanzania ambao wamefanya kazi tena wengine hata hawakuiba, wamefanya kazi kwa uadilifu, waweze kuishi maisha mazuri huko vijijini ambako wanakwenda au hata hao wengine ambao wapo Mijini ili tuweze kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho kabisa, ni suala la TAKUKURU Msemaji wa Upinzani kuhusiana na Wizara hii amezungumza suala la TAKUKURU ameainisha mambo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nilikuwa naomba Serikali iangalie kuna matatizo makubwa sana ndani ya TAKUKURU. Watumishi na viongozi hawaelewani, kuna kushutumiana, kunawavunja moyo wale wafanyakazi wa ngazi ya chini Mawilayani wa TAKUKURU wanaofanya kazi ya kuchambua matatizo mbalimbali ya kufanya ukaguzi wa masuala yote yanayohusiana na rushwa yakifika Makao Mkuu hayashughulikiwi. Kuna tatizo kubwa sana ndani ya TAKUKURU, inawezekana Serikali inalijua hilo au hailijui.

Lakini pia kumezuka mtindo ndani ya TAKUKURU zinapotokea taarifa mbalimbali zinazohusiana na mambo ya ufisadi na mambo ya rushwa, wafanyakazi wadogo hivi sasa tunavyozungumza kuna Kamati imeundwa ya witch-hunting ya kwamba ni nani ambaye anazungumza mambo ya TAKUKURU nje. Nadhani kuna haja kubwa sana Serikali iliangalie suala hili. Waziri anayehusika nadhani ni Mheshimiwa Sophia Simba aliangalie akae na viongozi wote wa TAKUKURU kuanzia Mkurugenzi, Naibu Mkurugenzi na Wakurugenzi wengine wote kuna matatizo makubwa sana, na ndiyo maana kesi zinazohusiana na ufisadi mkubwa, mikataba mikubwa mbalimbali ambayo Serikali inaingia ambayo ina ufisadi haifuatiliwi, kwa sababu ya migawanyiko iliyopo ndani ya kada ya juu kabisa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yale ambayo nilitaka kuyazungumza nimeyamaliza. Masuala ya Usalama wa Taifa nitampelekea Mheshimiwa Waziri kwa maandishi kwa sababu ni mengi sana. Nimeweza kuainisha matatizo ambayo tumekuwa nayo kama nchi, hali ambayo tunaipitia hivi sasa na Serikali kuwa iko slowly katika ku-respond katika masuala kama haya ambayo yatatuathiri sana kiuchumi huko tunakokwenda. Ni muhimu sana kuboresha Idara hii na kuwawezesha wafanyakazi wa Idara hii ili waweze kupata mafunzo mazuri na ya kisasa tuirekebishe Idara kutokana na mwelekeo wa mwaka 1970 wakati wa vita baridi iwe na mwelekeo wa sasa ili tuweze ku- possession nchi katika hali ambayo tutaweze kupambana katika globalisation lakini pia katika eneo nzima hili la Maziwa Makuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
 
mhe. Kabwe Z. Zitto: Mheshimiwa Mwenyekiti, Napenda Kuchukua Fursa Hii Kukushukuru Kwa Kupata Nafasi Ya Kuchangia Hotuba Hii Ya Ofisi Ya Rais Ambayo Inajumuisha Masuala Ya Utumishi, Utawala, Takukuru, Usalama Wa Taifa Na Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nitajitahidi Muda Uwe Wa Kutosha Nichangie Maeneo Matano. Kwanza, Nitaanza Na Idara Ya Usalama Wa Taifa, Tume Ya Mipango, Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma, Suala Nzima La Wastaafu Na Suala La Takukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria Ya Usalama Wa Taifa Ya Mwaka 1970 Sheria Namba 3 Na Sheria Namba 15 Iliyoanzisha Tanzania Interagency And Security Service -tiss, Sheria Namba 15 Imeunda Chombo Muhimu Sana Kwa Ajili Ya Usalama Wa Taifa Letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lakini Ninasikitika Kwamba Chombo Hiki Sheria Imekiziba Mikono, Na Sheria Imekifanya Hasa Hasa Sheria Ya Mwaka 1996 Imekifanya Chombo Hiki Kishindwe Kabisa Kabisa Kufanya Kazi Ambazo Kinapaswa Kufanya Kwa Ajili Ya Ulinzi Wa Taifa Letu. Na Imekuwa Ni Nadra Sana Kuzungumzia Suala La Usalama Wa Taifa Katika Bunge Hili Ni Kwa Sababu Ya Unyeti Wa Usalama Wa Taifa. Lakini Tukikaa Bila Kulizungumza Tutaendelea Kupata Matatizo Makubwa Sana. Toka Mwaka Jana Taifa Limekuwa Likipiga Kelele, Viongozi Mbalimbali Wamekuwa Wakipiga Kelele Kuhusiana Na Masuala Ya Ufisadi, Na Masuala Haya Siyo Kwamba Ni Mazuri Sana Kuyazungumza. Kwa Sababu Si Kwamba Yanatusaidia Sana, Maana Yake Ukiangalia Flow Ya Fdi Foreign Direct Investment Inaangalia Sana Masuala Kama Haya Ya Ufisadi. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lakini Ni Lazima Tuyazungumze Kwa Sababu Ni Sawasawa Na Mtu Ambaye Anataka Kusafisha Mtaro, Unapotaka Kusafisha Mtaro Wa Maji Machafu Ni Lazima Kwanza Uchafuke Uingie Kwenye Mtaro, Uusafishe, Utoke Uende Ukaoge Baada Ya Kuwa Mtaro Umekuwa Msafi. Sasa Lakini Serikali Imekuwa Ikipiga Danadana Sana Katika Suala Hili Nzima, Na Imekuwa Ikipiga Danadana Kwa Sababu Hatujaitumia Vizuri Idara Ya Usalama Wa Taifa. Kwa Sababu Sheria Za Idara Ya Usalama Wa Taifa Zimeibana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nitatoa Mfano Wa Masuala Matatu Tu. Kwa Mfano, Suala La Nishati Ni Suala La Usalama Wa Taifa, National Security Concerned Ilikuwaje Nchi Yetu Ikaingia Mikataba Ya Nishati Bila Clearance Ya Usalama Wa Taifa. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwa Sababu Mikataba Kama Hii Inapaswa Kupata Clearance Ya Usalama Wa Taifa Ili Tuweze Kuona Kwamba Nchi Inafaidika Au Haifaidiki, Kufanya Espionage Kuweza Kujua Kampuni Hii Ni Halali Ama Siyo Kampuni Halali. Lakini Matokeo Yake Tumeingia Kwenye Matatizo Kama Nchi Na Idara Tunayo, Watu Tunao, Tunawa-finance Kila Mwaka Tunapitisha Bajeti Hapa Na Wala Huwa Haijadiliwi Kwa Kina Bajeti Ya Usalama Wa Taifa, Lakini Kwa Sababu Sheria Imesema Kazi Yao Hao Ni Kutoa Ushauri Tu, Baada Ya Ushauri Hakuna Kinachofanyika.

La Pili, Ni Suala Ambalo Serikali Imetoa Kauli Hapa Juzi Ni Suala La Meremeta. Nataka Kuwahakikishia Suala La Meremeta Halina Uhusiano Wowote Na Usalama Wa Taifa. Leo Hii Bunge Linaambiwa Kwamba Meremeta Haiwezi Kuzungumzwa Kwa Sababu Ni La Usalama Wa Taifa. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lakini Nataka Niwambie Kamati Ya Rais Ya Madini Ilijadili Suala La Maremeta. Ndani Ya Kamati Ya Rais Ya Madini Kulikuwa Na Watu Wengine Ambao Siyo Waheshimiwa Wabunge, Kulikuwa Na Watu Ambao Ni Wafanyabiashara Tu Wala Hawajawa Vetted Wala Watu Hao Hawajala Kiapo Chochote, Lakini Tulijadili Nao Suala La Meremeta Na Tukatoa Mapendekezo Mahsusi Kuhusiana Na Suala La Meremeta. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Suala La Meremeta Ni Wizi, Ni Wizi Wa Waziwazi Na Ni Wizi Ambao Ni Lazima Serikali Ije Clear Na Iseme, Na Kama Haiwezi Kusema In Public Ndiyo Maana Bunge Lina Kamati Za Bunge. Tuna Kamati Ya Bunge Ya Mambo Ya Nje, Ulinzi Na Usalama Kamati Hii Inaweza Ikafanya Mikutano Yake In Camera, Mikutano Ile Isionyeshwe Na Serikali Ikaeleza Ukweli Kuhusu Suala Hili Ili Hayo Mambo Tuyamalize Tuanze Kujadili Masuala Ambayo Yanahusu Maendeleo Ya Nchi. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lakini Anaposimama Kiongozi Wa Serikali Tena Kiongozi Mkubwa Kabisa Akasema Hili Hata Mnisulubu Nalo Silisemi, Hapana. Nitahitaji Bunge Lipate Maelezo Mapya Kuhusiana Na Suala Hili, Na Kama Hayawezi Kutolewa Humu In Floor Maelezo Hayo Yatolewe Kwenye Kamati Ya Bunge Ya Mambo Ya Nje, Ulinzi Na Usalama. Kwa Sababu Suala La Meremeta Ni Wizi Na Halina Uhusiano Wowote Ule Na Usalama Wa Taifa Letu. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nataka Nizungumzie Kitu Kimoja, Muone Wenzetu Jinsi Ambavyo Wanatumia Idara Zao Za Usalama Wa Taifa Sawa Sawa. Mwaka 2005 Bunge Hili Liliamua Kupiga Marufuku Uuzaji Wa Tazanite Ghafi Na Madhara Ya Marufuku Hiyo Ilikuwa Ni Kupoteza Ajira 500,000, Kule India Kuna Mji Mmoja Unaitwa Jai Pool. Idara Ya Usalama Wa Taifa Ya India Ina Kitengo Cha Economic Espionage Wakajua Madhara Ya Uamuzi Wa Serikali Ya Tanzania. Walichokifanya Wakaongeza Scholarship Kwa Tanzania, Wakaalika Viongozi Wetu Kule Mpaka Leo Hii Tanzanite Bado Inasafirishwa Ikiwa Ghafi. Kwa Sababu Walifanya Espionage Wakatuzuia Hatukutekeleza Maamuzi Ambayo Sisi Tuliyafanya. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lakini Leo Tunapozungumza Hapa Na Waziri Wa Zambia Alikuwepo Hapa. Nchi Ya Zambia Inajenga Reli Mbili. Moja Kuelekea Bandari Ya Msumbiji, Na Nyingine Kuelekea Bandari Ya Angola. Reli Zile Ndizo Zitakazosafirisha Copper Yao Na Ndizo Zikazosafirishwa Madini Yao Mengine Yoyote Ama Kwenda Rwanda Au Kwenda Manyika Msumbiji. Madhara Yake Ni Nini? Ni Kwamba Tazara Itakufa, Tazara Haitapata Mizigo Ya Kusafirisha Kutoka Zambia. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Reli Ya Kati Hii Haitapata Mizigo Ya Copper Kutokea Mashariki Ya Kongo Kwa Sababu Watajenga Reli Kutokea Rungumbasi Kwenda Lusaka Kuunganisha Mpaka Kwenda Kule Rwanda. Hii Ndiyo Kazi Ya Usalama Wa Taifa Ilipaswa Kufanya. Ilipaswa Tufanye Economic Espionage Kuweza Kuona Madhara Ya Maamuzi Ya Nchi Zingine Ambazo Zinatuzunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Natoa Rai Kwamba Ifike Mahali Bunge Liamue Na Nimetoa Mchango Mrefu Sana Kuhusiana Na Suala La Usalama Wa Taifa Nitauwasilisha Kama Mchango Wa Maandishi Kwa Sababu Siwezi Kupata Muda Mrefu Zaidi Wa Kuweza Kulizungumzia. Bunge Liamue Kwamba Ni Lazima Tupitie Upya Sera Yetu Ya Usalama Wa Taifa, Ni Lazima Tufanye Marekebisho Ya Sheria Ya Usalama Wa Taifa Na Kifungu Kimoja Cha Sheria Ya Tiss Ya Mwaka 1996 Kifungu 5(2)(a) Ambacho Kinawapa Tiss Kazi Yao Wakishaona Kama Kuna Tatizo Wanamwambia Waziri Tu Mhusika Hawana Uwezo Wa Reinforce Security Ndilo Tatizo Lililotokea Katika Epa. Kwa Sababu Fedha Za Epa Zinaibiwa Zimeibiwa Kwa Cash, Idara Ya Usalama Wa Taifa Ilikuwa Inafahamu, Lakini Hata Kama Walitoa Ushauri Usingeweza Kutekelezwa. Nilikuwa Naomba Suala Hilo Liweze Kuangaliwa Kwa Kina. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Suala La Pili Ambalo Ninataka Ni Tume Ya Mipango. Nampongeza Sana Mheshimiwa Rais Kuunda Tume Ya Mipango Ni Muhimu Sana, Na Ni Kitu Ambacho Kwa Kweli Kitatusaidia Sana Huko Tunakokwenda. Lakini Sikubaliani Hata Kidogo Na Wala Haina Mantiki Tume Ya Mipango Kuwasilisha Bungeni Hapa Na Waziri Anayehusika Na Utumishi Na Nitawambia Madhara Yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kwanza, Mmeshuhudia Mchango Wa Bajeti Wa Mwaka Huu. Waheshimiwa Wabunge, Takriban Wote Wamejikita Katika Masuala Ya Fedha, Masuala Yale Ya Bajeti Ya Wizara Ya Fedha. Masuala Yote Yanayohusiana Na Mipango Ya Kiuchumi Hayakupewa Kipaumbele. Ukiangalia Bajeti Ambayo Mheshimiwa Hawa Ghasia Ameiwasilisha Leo Ni Paragraph Mbili Tu Ndizo Zimezungumza Kuhusu Tume Ya Mipango. Tume Ya Mipango Inapeleka Taarifa Yake Kwa Kamati Ya Bunge Ya Katiba, Sheria Na Utawala Hawawezi Kuyajadili Hayo Mambo. Haya Mambo Ni Ya Kamati Ya Bunge Ya Fedha Na Uchumi. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nataka Kutoa Rai Ninajua Kuna Wasiwasi Wa Kwamba Wananchi Wataona Kwamba Mawaziri Ni Wengi Sana, Hatuwezi Ku-risk Kutokuwa Na Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Rais Anayehusika Na Tume Ya Mipango Peke Yake, Na Nitawambia Leo Hii Kila Baada Ya Miaka Miwili Kuna Kitabu Kama Hiki Kinazalishwa Na Serikali, Poverty And Human Development Report, Hiki Kitabu Ndicho Kinacho-guide Mipango Ya Maendeleo Ya Nchi Na Juhudi Za Uzalishaji Na Juhudi Za Kupunguza Umaskini. Kitabu Hiki Kinatolewa Na Aliyekuwa Commissioned Na Serikali, Na Miongoni Mwa Vitu Ambavyo Vinapaswa Kufanywa Ukiangalia Chapter Four Ya Kitabu Hiki Inazungumzia Mikakati Ya Ukuaji Wa Uchumi Wa Nchi. Lakini Ukiangalia Katika Mpango Mzima Wa Kazi Wa Tume Ya Mipango Ile Chart Ambayo Mheshimiwa Waziri Ametuonyesha Hakuna Reference Yoyote Inayoonyesha Shughuli Kama Hizi Zitakuwa Zinafanywa Namna Gani? Utakuwa Vipi Na Tume Ya Mipango Ambayo Haiangalii. Maana Yake Tume Ya Mipango Ni Vision 2025, Tume Ya Mipango Ni Mkukuta Na Hii Taarifa Ndiyo Utekelezaji Wa Masuala Kama Hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nilikuwa Namwomba Mheshimiwa Waziri Hawa Ghasia Azungumze Na Mheshimiwa Rais Ni Bora Tuingie Gharama Ya Kumlipia Mtanzania Mmoja Kwa Ajili Ya Kuwa Mwakilishi Wa Tume Ya Mipango Katika Bunge Akiwa Kama Waziri Wa Nchi Wa Mipango. Hatuwezi Kuwa Hivi Tunavyokwenda Tutapata Tabu Sana Huko Tunakokwenda. Kwa Hiyo, Naomba Suala Hili Liweze Kuangaliwa Kwa Jinsi Ambavyo Linavyostahili. (makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, Suala La Tatu Ambalo Nataka Kulizungumzia Ni Suala La Maadili Ya Viongozi. Tuna Tatizo Kubwa Sana Katika Maadili Ya Viongozi, Sheria Ya Maadili Ya Viongozi Sheria Namba 13 Ya Mwaka 1995 Ina Mapungufu Makubwa Sana, Na Kumekuwa Na Juhudi Za Kutaka Kuifanyia Marekebisho. Mimi Binafsi Nimewasilisha Ofisi Ya Spika, Muswada Wa Marekebisho Ya Sheria Ya Viongozi Ili Tuweze Kuifanya Iwe Na Nguvu Zaidi. Lakini Tumefahamishwa Na Waziri Kwamba Taratibu Za Ndani Ya Serikali Za Mabadiliko Ya Sheria Hii Zimeanza Kuandaliwa. Lakini Tuna Tatizo Kubwa Sana Kwamba Taarifa Ambazo Viongozi Tunazitoa Kwa Ajili Ya Mali Na Madeni Yetu Zinachezewa Sana. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nataka Kutoa Rai Kwamba Hufanyike Uchunguzi Maalum Tuweze Kulinganisha Fomu Ambazo Waheshimiwa Wabunge Wote Tulizisaini Wakati Tumeingia Bungeni Na Zile Za Kila Mwaka Na Fomu Ambazo Zipo Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Kuna Baadhi Ya Fomu Tutakuta Zimerekebishwe Baada Ya Matatizo Fulani Fulani Kuwa Yametokea. (makofi)

Kwa Hiyo, Nilikuwa Nataka Tuchukue Fomu Zote Za Waheshimiwa Wabunge Ambazo Zipo Ofisi Ya Spika, Kwa Sababu Copy Moja Inabakia Katika Ofisi Ya Spika, Copy Nyingine Inaenda Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Tuweze Kuangalia Kuna Matatizo Makubwa Sana. Kwa Hiyo, Suala Hili La Maadili Ya Viongozi Liweze Kuangaliwa. Mapendekezo Ambayo Yametolewa Na Spika Alitoa Uamuzi Kwamba Kamati Ya Bunge Ya Katiba, Sheria Na Utawala Iiangalie Sheria Hii Ya Maadili Na Nilitarajia Kwenye Taarifa Yao Wangeweza Kugusia Kitu Kama Hicho, Hawakukigusia Wameenda Tu Juu Juu.

Lakini Pili, Tunahitajika Kuwawezesha Wale Watanzania Wanaofanya Kazi Katika Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Waweze Kuwapatia Mafunzo Mahsusi Kwa Sababu Ni Moja Ya Idara Ambayo Inapewa Bajeti Finyu Sana, Lakini Ina Handle Mambo Nyeti Sana, Kwa Sababu Siri Zetu Zote, Mali Zetu Zote, Madeni Yetu Yote Yanafahamika Kwa Watu Wale. Kwa Hiyo, Ni Lazima Tuhakikishe Kwamba Tunawawezesha Jinsi Ambavyo Inavyostahili Ili Waweze Kufanya Kazi Yao Sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, La Mwisho, Nimesikitika Sana Kwamba Hotuba Ya Mheshimiwa Waziri Haijagusia Kabisa Suala La Wastaafu, Na Hao Ni Watanzania Ambao Wamefanya Kazi Ya Kujenga Nchi Yetu Kwa Miaka Yao Yote Na Kuna Matatizo Makubwa Sana Ya Wastaafu. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wastaafu Wanapata Shilingi 21,000/= Kwa Mwezi, Na Sisi Waheshimiwa Wabunge Ni Mashahidi Tunavyosumbuliwa Na Wastaafu Hao Huko Kwenye Majimbo Kwetu, Lakini Mheshimiwa Waziri Hajaelezea Chochote. Sasa Sijui Siyo Suala Ambalo Haliko Kwenye Mandate Yake Kama Waziri Au Ni Vipi? Lakini Nilikuwa Nadhani Kuna Haja Ya Kuangalia Upya Suala Hilo La Wastaafu Ili Tuweze Kuhakikisha Kwamba Ni Watanzania Ambao Wamefanya Kazi Tena Wengine Hata Hawakuiba, Wamefanya Kazi Kwa Uadilifu, Waweze Kuishi Maisha Mazuri Huko Vijijini Ambako Wanakwenda Au Hata Hao Wengine Ambao Wapo Mijini Ili Tuweze Kuwasaidia. (makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, La Mwisho Kabisa, Ni Suala La Takukuru Msemaji Wa Upinzani Kuhusiana Na Wizara Hii Amezungumza Suala La Takukuru Ameainisha Mambo Mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lakini Nilikuwa Naomba Serikali Iangalie Kuna Matatizo Makubwa Sana Ndani Ya Takukuru. Watumishi Na Viongozi Hawaelewani, Kuna Kushutumiana, Kunawavunja Moyo Wale Wafanyakazi Wa Ngazi Ya Chini Mawilayani Wa Takukuru Wanaofanya Kazi Ya Kuchambua Matatizo Mbalimbali Ya Kufanya Ukaguzi Wa Masuala Yote Yanayohusiana Na Rushwa Yakifika Makao Mkuu Hayashughulikiwi. Kuna Tatizo Kubwa Sana Ndani Ya Takukuru, Inawezekana Serikali Inalijua Hilo Au Hailijui.

Lakini Pia Kumezuka Mtindo Ndani Ya Takukuru Zinapotokea Taarifa Mbalimbali Zinazohusiana Na Mambo Ya Ufisadi Na Mambo Ya Rushwa, Wafanyakazi Wadogo Hivi Sasa Tunavyozungumza Kuna Kamati Imeundwa Ya Witch-hunting Ya Kwamba Ni Nani Ambaye Anazungumza Mambo Ya Takukuru Nje. Nadhani Kuna Haja Kubwa Sana Serikali Iliangalie Suala Hili. Waziri Anayehusika Nadhani Ni Mheshimiwa Sophia Simba Aliangalie Akae Na Viongozi Wote Wa Takukuru Kuanzia Mkurugenzi, Naibu Mkurugenzi Na Wakurugenzi Wengine Wote Kuna Matatizo Makubwa Sana, Na Ndiyo Maana Kesi Zinazohusiana Na Ufisadi Mkubwa, Mikataba Mikubwa Mbalimbali Ambayo Serikali Inaingia Ambayo Ina Ufisadi Haifuatiliwi, Kwa Sababu Ya Migawanyiko Iliyopo Ndani Ya Kada Ya Juu Kabisa Ya Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Yale Ambayo Nilitaka Kuyazungumza Nimeyamaliza. Masuala Ya Usalama Wa Taifa Nitampelekea Mheshimiwa Waziri Kwa Maandishi Kwa Sababu Ni Mengi Sana. Nimeweza Kuainisha Matatizo Ambayo Tumekuwa Nayo Kama Nchi, Hali Ambayo Tunaipitia Hivi Sasa Na Serikali Kuwa Iko Slowly Katika Ku-respond Katika Masuala Kama Haya Ambayo Yatatuathiri Sana Kiuchumi Huko Tunakokwenda. Ni Muhimu Sana Kuboresha Idara Hii Na Kuwawezesha Wafanyakazi Wa Idara Hii Ili Waweze Kupata Mafunzo Mazuri Na Ya Kisasa Tuirekebishe Idara Kutokana Na Mwelekeo Wa Mwaka 1970 Wakati Wa Vita Baridi Iwe Na Mwelekeo Wa Sasa Ili Tuweze Ku- Possession Nchi Katika Hali Ambayo Tutaweze Kupambana Katika Globalisation Lakini Pia Katika Eneo Nzima Hili La Maziwa Makuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nakushukuru Sana. (makofi)

Kwa Utaratibu Huu...serkali Ivunjwe Mara Moja!
Nasema Hivi...wananchi...bunge Lisipoivunja Serikali Msikubali!
Tumeshawapa Nafasi Ya Kuweka Ukweli Wazi Na Msipofanya Hivyo Taifa Na Afrika Tutaingia Kwenye Matatizo Makubwa Sana.
 
Halafu Tukisema Hatuko Huru Mnabisha?
Acheni Utani...
We Want Freedom!
We Want It Now!
 
Good job Bw.Zitto lakini experience inaonyesha speech hizi zinaishia hewani tuu na hakuna chochote kitakacho badilika,sasa kuna bill yeyote mezani umetayarisha unayotaka kuweka bungeni ili kubadilisha hayo mambo uliyozungumzia? action plseee!
 
Nyie Mnaojiita Usalama Wa Taifa!
Mlikaa Vipi Kimya Na Watu Binafsi Wakauza Nchi Na Nyie Mkiangalia!
Halafu Wanakuja Bungeni Na Kudai Wameiuza Kwa Usalama Wenu?
Wazalendo Chukueni Nchi!
Mrekebishe Sheria!
Mtupe Uhuru Wa Kujiamulia Mustakabali Wa Mali Zetu Na Taifa Letu...ili Kizazi Kijacho Kisirudi Utumwani!
Kwani Hamuoni Utumwa Unanyemelea?
Ombeni Mungu Ndugu Zangu!
 
Zitto Chukueni Nchi!
Utakaa Vipi Kama Unaona Hayo Yote?
Tafadhali Apewe Sapoti!
 
Back
Top Bottom