Meremeta & TANGOLD Revealed!

Meremeta & TANGOLD Revealed!

Swali: Mlioko Dodoma Tupeni Summary Ya Aliyoongea Mheshimiwa Kijana Wetu, Jemedari, Kiboko Ya Mafisadi, Mshushaji Wa Viongozi Mafala, Zitto Wa Zuberi Kabwe
 
yaani naposoma sa hivi najisemea moyoni more fire, more fire, kama mjamaika vile ingawa sijui zaidi kuhusu alichosema lakini moto tu, yaani i cant wait to read more into it, keep it up Zitto, vijana tuko nyuma yako!
 
Kitu kikubwa kinachowapa kiburi ni hilo jeshi lao na mapolisi wao, maana "wamewatia kiganjani" haswa hawafurukuti na kwa umaskini wao wa akili wala hawajiulizi tofauti ya kimaisha kati yao na hao wanao walinda.. wao wakiambiwa "kamataaa..." mbio.... wanakamata kama mbwa wao wasiohitaji sbb ya kukamata

wanajua kabisa wananchi hatuna uwezo kulinganisha na jeshi lao.... wamesahau habari Tieman Square hawa....

Tieman Square na Yellow Revolution iliyomn'goa Corrupt rule F. Marcos of the Phillipines. Hawajua nguvu ya haki za watu wenye hasira, wanafikiri patakalika?
 
swali: Mlioko Dodoma Tupeni Summary Ya Aliyoongea Mheshimiwa Kijana Wetu, Jemedari, Kiboko Ya Mafisadi, Mshushaji Wa Viongozi Mafala, Zitto Wa Zuberi Kabwe


Vijana Semeni Msiogope Vibaraka!
 
Ladymzuri umepatia saaana, huyo mkemia alichongwa akachongeka akapata nafasi hiyo kupitia haohao
 
Mkemia mkuu msukuma+ Nyenge Msukuma=0000....je hesabu hiyo hailipi???

hesabu kidooogo issue...sijakupata vizuri...pls break it down for me to swallow!

Hapo ana maana kwamba lile sakata la unga unga ndani ya ukumbi wa Bunge limepelekwa kwa Mkemia Mkuu ambaye ni Msukuma na PRODUCER ambaye ni Bwana Chenge ni Msukuma je majibu yatatoka????
 
Hapo ana maana kwamba lile sakata la unga unga ndani ya ukumbi wa Bunge limepelekwa kwa Mkemia Mkuu ambaye ni Msukuma na PRODUCER ambaye ni Bwana Chenge ni Msukuma je majibu yatatoka????
Ukabila tutaumaliza lini jamani?kwa nini tufikirie kuwa majibu hayatatoka kwa sababu mkemia ni msukuma?
 
who is meremeta? mbona hawatajwi kama Richmond? mie nataka niwafaham kwa majina wasanii hao waliokubuhu
 
Nadhani tunazungumzia suala la hotuba ya Zitto Bungeni. Naona tumegeuka kuzungumzia kwenye unga unga na usukuma. focus.
 
Ukabila tutaumaliza lini jamani?kwa nini tufikirie kuwa majibu hayatatoka kwa sababu mkemia ni msukuma?
how long does it take to do the investigations...machemist ebu tuambieni??? yaani all these days, majibu bado tuu au ??
 
Kweli utajulikana tu!Hapa mpaka kieleweke huu ndo mwisho wa mafisadi!Ama kweli za mwizi arobaini!walikuwa wanaiba wakifikiri wanaibia wajinga!Thank God ukweli unaelekea kujulikana!
 
Kwa kuwa Mkemia Mkuu ni Msukuma lazima kuwe na mgongano wa maslahi, kule Usukumani mtu hata akiwa na mamilioni wao huita "VIJISENTI" kutokana na hilo majibu ya "unga unga wa Chenge bila shaka Mkemia Mkuu atatoa jibu la "Yalikuwa maunga unga ya ugali"
 
Tena Pinda ukome kabisa na sura yako ya mbuzi wakati unapewa tu hicho cheo ulituapia kuwa ukila rushwa Mungu akuue sasa nataka kukukumbusha kuwa hata kutetea ufisadi ni dhambi kubwa kuliko kula kula rushwa na kwa taarifa yako usijekulogwa watanzania wakakuchukia utakiona hicho cheo ni shubiri
 
Hapa itabidi ukweli wa Meremeta utoke mambo ya kuwasingizia wanajeshi hayana maana kabisa!
 
Tuandamane na Katibu Tarafa, hebu nisaidieni, hivi wale washauri kibao ambao Lowassa aliomba na akapewa na JK bado wapo Ofisi ya Waziri Mkuu?

raisi alipomteua pinda alitakiwa afanyembadiliko pia na makatibu wa wizara ilikumpa pinda katibu mwingine.lakini kuwaacha wale wa lowasa,haya ndio matatizo yake.
hawa wataendelea kumpinda pinda mpaka na yeye ataondoka kama mwenzake.kuna hatari ya kuwa na mawaziri wakuu wanne kabla jk ajamaliza muda wake.
 
Back
Top Bottom