Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,095
- 43,302
Mkuu,
Chochote kile Zitto (Mh.) atakachokisema Jumatatu, chochote kile, ameshatuambia tayari kwamba itakuwa ni kuwa call out wanao mdanganya Pinda. Tatizo sio Pinda, Mbunge anasema. Wengine tunamkosoa kwa kusema tatizo sio Pinda. Hilo halihitaji kusubiri maelezo. Kesha lisema. Wakati wengine - na wewe ukiwemo - tumedhani Pinda kaharibu.
Mwanakijiji hilo umesha likubali, na umeenda kwenye rekodi kwa mara ya kwanza leo kusema Pinda ana mushkeli kwa kutoleta ukweli. Hapa, Zitto (Mh.) kasema tatizo sio Pinda. Kwa hiyo wewe, logically, lazima utafautiane na Zitto (Mh.).
Aidha hivyo, au useme umekurupuka kumshutumu Pinda. Mwombe msamaha Pinda kwa kumfungulia thread ya kumkosoa kwa mara ya kwanza toka achaguliwe. Hii si maoni yangu. Ni masharti ya logic. Aidha Zitto kakosea kumtetea Pinda au wewe umekosea kumkosoa Pinda. Simple mathematics. Chagua sumu yako mtu wangu!
hii inaitwa "the fallacy of false dilemma" ambapo mtu anatakiwa achagua pande mbili, hata shilingi haina pande mbili! So, what if Zitto is right and I'm right and you are wrong? What if there are some elements of truths in each one of our positions though may be not the whole truth. Nimeangalia kama Zitto kasema "Tatizo si Pinda" au kasema "Pinda amedanganywa"? Sasa, yawezekana sisi sote tumekosea na Pinda yuko sahihi!
Sidhani kama sisi sote tuko mbali sana from each other tunapotazama majibu ya Pinda leo hii. Je tunajua kuwa Pinda hakudanganywa? Does this remind us of mama Meghji na Ballali? Kama Pinda ametaka apewe information kuhusu Meremeta kutoka kwa watu wanaotakiwa kuwa na habari sahihi kuhusu hiyo Meremeta, na wote waliomletea habari hizo walikuwa na jibu moja kuwa ni za "Usalama wa Taifa".. je Pinda kama Pinda ana uwezo gani ndani ya legal channel to assert to the contrary?