Meremeta & TANGOLD Revealed!

Meremeta & TANGOLD Revealed!

Wakuu mtanisamehe pale nitakapokuwa nimekosea unajua umri tena kumbukumbu zinapotea.

Wakati wa uongozi wa jenerali Mbona kuliwahitokea kutunishiana misuli kati ya Mkapa na Mboma katika kipindi ambacho Mboma alikaribia kustaafu. Nyepesi nyepesi zilisema ilikuwa ni mambo ya pesa(labda ndo hiyo Meremeta) ili kumpooza Mboma, vibali vya kuingiza sukari toka nje bila ushuru vilitolewa. Baada ya magazeti kuandika kuhusu utolewaji huo wa vibali na waziri wa fedha(Yona)bila kufuata taratibu wakaona watumie kofia ya jeshi, lakini ukweli ni kuwa matani ya sukari iliyoingizwa yalimnufaisha Mboma, kuanzia ushuru.

Nimekaa nikafikiri kwanini Mkapa amekuwa jeuri kwa kashfa zote hizi, kwanini JK amekaa kimya kuwachukulia hatua hawa majambazi,wakati nchi yake inateketea,kwanini viongozi wetu wanatuibia na kuja kutudanganya waziawazi kama akina Pinda, kwa nini wabunge wetu baadhi wako kimya na wengine wanatetea maafisadi? Hii gut na courage wanaitoa wapi? Nikagundua wanaitoa kwetu sisi wananchi. Yaani kwa kuibiwa kote huku na bado tunadanganywa na viongozi tunaotegemea wachukue hatua, tumeshindwa hata kuandamana tu!!! Viongozi wetu wanajua kama wao nimazumbukuku basi sisi wanachi nimazumbukuku no. 1. Pinda asingekuja na utumbo huu kama angejua kuwa wananchi tutachukua hatua.
Maandamano ya amani ya kushinikiza uwajibikaji, majibu sahihi ya kashfa zote na uchukuliwaji wa hatua kwa wahusika wote ndo dawa.

Mkuu

Nafikiri inatakiwa maandamano ya amani hili kushinikiza serikali Isiendelee kudanganya wananchi na pia iweze kushughulikia mambo yote ya mafisadi.

Sijasikia wapinzani wakiomba kibali kuhakikisha mikoa mbali mbali wanaandamana kuhakikisha haki inatendeka wote walioiba mali zetu bila kuangalia ni nani wanashughulikiwa.
 
Pundit ,

I couldn't agree with you more ! Mheshimiwa Zitto is too loyal to the president . Nakumbuka tulifanya naye Mkutano hapa Houston na nilishangaa sana pale aliposema ya kuwa yeye akubaliani na kitendo cha kumfungulia mashitaka Rais mstaafu ...kwani ana siri nyingi sana za taifa .

Statement ile iliniumiza kichwa kidogo kwani sikutegemea statement kama hiyo toka kwa mbunge wa upinzani lakini zaidi maovu yaliyofanywa na mkapa.

Rufiji,

Some of that may stem from pragmatism, some from too much respect for authority.

The pragmatic concern should be put to rest in a legal process, he is one of our lawmakers.We will not be the first to try an ex president. As to the "too much respect for authority" anything in excess is harmful.

Yaani hawa ndio wapinzani wenyewe tunaowategemea ku challenge status quo? Au tayari na wao ni status quo?
 
1. Wakati wa uongozi wa jenerali Mbona kuliwahitokea kutunishiana misuli kati ya Mkapa na Mboma katika kipindi ambacho Mboma alikaribia kustaafu.

2. Nyepesi nyepesi zilisema ilikuwa ni mambo ya pesa(labda ndo hiyo Meremeta) ili kumpooza Mboma, vibali vya kuingiza sukari toka nje bila ushuru vilitolewa.

3. Baada ya magazeti kuandika kuhusu utolewaji huo wa vibali na waziri wa fedha(Yona)bila kufuata taratibu wakaona watumie kofia ya jeshi, lakini ukweli ni kuwa matani ya sukari iliyoingizwa yalimnufaisha Mboma, kuanzia ushuru.

Mkuu Nyangumi,

Maneno mazito sana haya, yaani ukiyafuatiilia kwa makini na undani wake in details basi unapata jawabu la Meremeta, halafu kuna Warioba pia kwenye hiii ishu!
 
Mwenzio akinyolewa wee tia maji. Naamini sasa tunaelekea kule Harare. Mambo ya kuelekeza Meremeta jeshini ili wananchi washindwe kuhoji ni ujinga. Kama jeshi liko chini ya serikali iliyowekwa na watanzania, basi hawana budi kujibu haya maswali. Ni mradi gani unaweza kuwa siri kwa watanzania kama ni wa kujiendeleza? Watu hawawezi kuendekeza UFISADI kwa mgongo wa Usalama wa Taifa. Huu ni utumbo kama Waziri Mkuu anakuwa na jibu kama hili kwa watanzania. Jamani watanzania tulidhani kama huyu jamaa ni mkweli, muadilifu n.k kumbe na yeye naye ni ka-bomu fulani ambako kameanza kuchemka. Kadri siku zinapokwenda kuna hatari ya haka ka-bomu kuzidi kutoa mionzi yenye athari kubwa kwa watanzania. Mafisadi tayari walishamnywesha mchuzi, na sasa muda mfupi tu tayari ameshasahau kutambua kuwa anawatumikia Watanzania wote na si kikundi kidogo cha watu wenye nia ya kuifilisi Tanzania. Sasa baada ya miaka 2 atakuwaje??
 
jmushi,

Kwa nini unaharibu hii forum ? Kwa ni nini unamtukana Zitto mtu ambaye anatupa insight za ndani kabisa . What is wrong with you huwezi kupingana na mtu kwa hoja bila ya kumtukana ?

Huyu kijana nimeshampa ushauri wa kutumia lugha ya kistaarabu katika majadiliano mbali mbali kuhusiana na hatma ya nchi yetu yanayoendelea hapa ukumbini. Nilimwambia ushauri huo anaweza kuufuata au la, lakini inaelekea ameuweka pembeni. Hajui maneno anayoyatumia siyo tu yanawaudhi wale anaowalenga bali hata wanaJF wengine.

Heshima ni kitu cha bure, pamoja na kuwa wengi wetu tunatumia majina ya bandia bado kuna umuhimu mkubwa wa kuheshimiana vinginevyo wengi wataikimbia JF na hatimaye kuuharibu ukumbi wetu huu ambao umetuunganisha Watanzania wa ndani na nje ya nchi
 
Tusubiri Atakachosema Bungeni!
Kwanza Kigoma Ana Fanya Nini Huko?
Mustabali Wa Taifa Huko Njia Panda, Macho Ya Taifa Yako Dodo...yeye Yuko Kigoma!
Wapi Na Wapi?
Rudi Bungeni Zitto.
Sidhani Kama Nimetake Personal Kama Wapambe Wako Wanavyoelekea Kussugest!
How Ever!
Wakati Wa Kukuomba Msamaha Kama Nikigundulika Nimekosa Utafika Na Mimi Ntafanya Hivyo Regardless Kama Utaupokea Ama La!
 
SIJA edit: Pinda anasema:

MEREMETA, Tangold, Ngeleja naona tutamuonea. Kwa mazingira ya jambo lenyewe suala la Meremeta limejikita ndani ya JWTZ, haukuwa mradi tumeukuta uraiani in unique situation... mimi kuanza kusema kila kitu siwezi.... Ni suala linalohusiana kwa karibu sana na mambo ya ulinzi na usalama wetu, ni lazima tulilinde,,, Kama mtaona inatosha sawa, kama mnataka kunisulubu nitakuwapo pale kwa ajili hiyo

EPA naona ina mvuto mkubwa sana. Kuna fedha ambazo watanzania wanataka kujua zimetokaje BOT, mradi zilikua BoT katika chombo cha serikali, haiwezekani ukamwachia mtu tu akachukua hizo fedha,. Hoja hapa zimekwenda kwa nani, utaratibu umefuatwa? Rais kasema tumwachie, wote tuna interest, sasa kwa mtazamao wangu shauku ni kubwa, watu wangependa leo, nafirikri tufanye subira, muda wenyewe umekwisha labda sana sana watasema muda uongezwe, lakini hapo baadaye tutaulizana maswali oooh zilikuwa za mhindi, ooh zilikua za nani!!! Naomba nitoe rai kwa muda uliobaki tusubiri. Nitakwambia sijui, hata mimi Mwanyika nikimuuliza anasema... Liko la Ballali marehemu na Slaa, serikali itoe taarifa, halafu kuna mahali alisema Slaa, kutotoa taarifa kaa tunachezea, angetamani iundwe kamati ya kuchunguza kifo cha Ballali! Sasa sijui lakini naelewa iko connected kwamba alijua siri, hili wazo kuhusu usiri kama kwamba BAllali ... huyu mtu amefariki na ndugu zake wanasema amefariki, sasa kuendelea kumzungumza huyu marehemu. Kifo chake hofu iko wapi? Labda muombe postmortem, nani asiyejua kwamba hakuwapo. Tungoje taarifa ya mapesa yetu, kama watamtaja basi tungoje, Mkisema niseme, labda ndugu zake, lakini si serikali, hamtutendei haki. Na kwa merehemu akifa, kwa kweli ngumu sana.... Nadhani kwa sasa serikali haioni sababu ya Kamati, EPA kama anahyusika atatajwa tu... Hawa wanasukuma ajenda wana sababu tu. Kama kuna ushahidi zaidi ya tulio nao mtu anaweza kuuleta tukautazama.

KIWIRA nalo mimi najua Dk. Slaa akisema mpaka unaogopa... Wakaniletea maelezo marefu sana. Wakaleta itakusaidia? Mimi siwezi kuingia katika jambo technical, nilidhani ili kuwapa fair pix hii Kiwira, mturuhusu, Ngeleja aje na kauli ya serikali ili apate muda wa kulizungumza kwa upana wake, ili kujua ... Kiwira wakati ikiuzwa ilikua dead proj ilikua katika hali mbaya sana.. Ili tuweze kuwa na benefit ilikuwa smooth exercise ilikuwa interest kupata mwekezaji, ningeomba nipate more details.

NO Pinda keshabatizwa kwenye dini ya ufisadi,hapo ukiangalia kashindwa hata kuwa na mtiririko yaani kupanga statement zake kama mtu anayetoa majibu ya hoja fulani.Yaani kali zake hizo hazifofautiani kabisa na stori za kijiweni na yale yaliyokuwa majibu ya Daktari wa Nyodo kwenye sijui gazeti gani lile....mmmmmmmhhh nimechoka mbaya
 
Huyu kijana nimeshampa ushauri wa kutumia lugha ya kistaarabu katika majadiliano mbali mbali kuhusiana na hatma ya nchi yetu yanayoendelea hapa ukumbini. Nilimwambia ushauri huo anaweza kuufuata au la, lakini inaelekea ameuweka pembeni. Hajui maneno anayoyatumia siyo tu yanawaudhi wale anaowalenga bali hata wanaJF wengine.

Heshima ni kitu cha bure, pamoja na kuwa wengi wetu tunatumia majina ya bandia bado kuna umuhimu mkubwa wa kuheshimiana vinginevyo wengi wataikimbia JF na hatimaye kuuharibu ukumbi wetu huu ambao umetuunganisha Watanzania wa ndani na nje ya nchi

ushauri gani nyie wapambe?
sheria hapa ni za wana jf na wala si KIKWETE WALA ZITTO!
WE OUGHT TO TREAT EVERYBODY THE SAME HAPA KWENYE JAMVI!
MSINIJENGEE SHERIA NA CHUKI KWA KUSEMA NIMEMTUKANA MBUNGE WENU!
SASA NA WATANZANIA WATASEMA NINI KWA YALE NILIYOWAHI KUSEMA KUHUSU MH RAIS?
 
humu ndani wote wana hekima, lakini "hekima" za wengine ni za kupuuza!! Kwa mwelevu upenda kusoma zaidi ya ku-type keyboard!!
 
Tusubiri Atakachosema Bungeni!
Kwanza Kigoma Ana Fanya Nini Huko?
Mustabali Wa Taifa Huko Njia Panda, Macho Ya Taifa Yako Dodo...yeye Yuko Kigoma!
Wapi Na Wapi?
Rudi Bungeni Zitto.
Sidhani Kama Nimetake Personal Kama Wapambe Wako Wanavyoelekea Kussugest!
How Ever!
Wakati Wa Kukuomba Msamaha Kama Nikigundulika Nimekosa Utafika Na Mimi Ntafanya Hivyo Regardless Kama Utaupokea Ama La!

Mkuu Mushi

Zitto siyo mbaya wako mkuu unapoteza mwelekeo angalia mbele mkuu najua sasa umeaisha anza kuwa na hasira punguza mkuu angalia mbele.
 
Huyu kijana nimeshampa ushauri wa kutumia lugha ya kistaarabu katika majadiliano mbali mbali kuhusiana na hatma ya nchi yetu yanayoendelea hapa ukumbini. Nilimwambia ushauri huo anaweza kuufuata au la, lakini inaelekea ameuweka pembeni. Hajui maneno anayoyatumia siyo tu yanawaudhi wale anaowalenga bali hata wanaJF wengine.

Heshima ni kitu cha bure, pamoja na kuwa wengi wetu tunatumia majina ya bandia bado kuna umuhimu mkubwa wa kuheshimiana vinginevyo wengi wataikimbia JF na hatimaye kuuharibu ukumbi wetu huu ambao umetuunganisha Watanzania wa ndani na nje ya nchi


Mimi namlaumu Moderator kwa kuintertain hii tabia .Na kama wakimwachia aendelee na hiyo tabia basi hii forum itaharibika
 
Hahaha,

Probably the diplomatic type, muheshimiwa Zitto ukimfuatilia hapa anaonyesha kuwa mpinzani fulani mwenye core beliefs katika respect for authority.At a time when one may expect prominent opposition leaders to rightfully unleash salacious and even malicious tirades against the president, muheshimiwa Zitto distinguished himself by cautioning people here to "Respect the presidency if not the president himself"

Having said that, muheshimiwa Zitto is not outside the domain of all politicians, a lot that is characteristically driven by ambition. Ambition can allow some azzkissin to the extent of excusing an obvious "error" under the guise of "PM kadanganywa"

Good thing I asked because my guess is as good as yours, but different.

Zitto (Hon.) went toe to toe up against Samuel Sitta and Minister Karamagi when everybody else had their tails too curled in between their legs to call out the Richmond chicanery, plus all the venal bigwigs who tried to cover it. So Zitto (Hon.) is anything but a wussy.

My guess is that he does not understand Pinda. He thinks - he assumes - that Pinda has goods intentions and that every fumble he commits, is because of bad advice. Same good old 'bad advice defense.'

Worse case scenario is that Zitto (Hon.) does not appreciate what the role of a Prime Minister is. Nikifufukammekwisha just pointed out "Waziri mkuu inampasa awe makini katika lolote analolisema ambalo lina maslahi kwa Raia."

Perhaps Zitto (Hon.) does not understand that. As I said, that is worse. Worst case guess, though, is that Zitto (Hon.) knows and understands every little thing going on here. Each and every thing. But he's obfuscating. For some mysterious artistic reasons.
 
mwenzio Akinyolewa Wee Tia Maji. Naamini Sasa Tunaelekea Kule Harare. Mambo Ya Kuelekeza Meremeta Jeshini Ili Wananchi Washindwe Kuhoji Ni Ujinga. Kama Jeshi Liko Chini Ya Serikali Iliyowekwa Na Watanzania, Basi Hawana Budi Kujibu Haya Maswali. Ni Mradi Gani Unaweza Kuwa Siri Kwa Watanzania Kama Ni Wa Kujiendeleza? Watu Hawawezi Kuendekeza Ufisadi Kwa Mgongo Wa Usalama Wa Taifa. Huu Ni Utumbo Kama Waziri Mkuu Anakuwa Na Jibu Kama Hili Kwa Watanzania. Jamani Watanzania Tulidhani Kama Huyu Jamaa Ni Mkweli, Muadilifu N.k Kumbe Na Yeye Naye Ni Ka-bomu Fulani Ambako Kameanza Kuchemka. Kadri Siku Zinapokwenda Kuna Hatari Ya Haka Ka-bomu Kuzidi Kutoa Mionzi Yenye Athari Kubwa Kwa Watanzania. Mafisadi Tayari Walishamnywesha Mchuzi, Na Sasa Muda Mfupi Tu Tayari Ameshasahau Kutambua Kuwa Anawatumikia Watanzania Wote Na Si Kikundi Kidogo Cha Watu Wenye Nia Ya Kuifilisi Tanzania. Sasa Baada Ya Miaka 2 Atakuwaje??

Wana Mpiga Ramli Wao Anayekwenda Kwa Jina La Mzindakaya!
Huyu Labda Kawaambia P Stands For Pinda Haki!
Wakakubali!
Wameliwa!
Huku Tuliko Hatujarogwa Bado!
Ila Jf Inatuunganisha...
Jf Mbele!
 
Watanzania wenzangu, the moment of the truth for the future of our country is NOW and we should not leave this momentum slip away. Let's keep the same pressure to this corrupt government.
 
good Thing I Asked Because My Guess Is As Good As Yours, But Different.

Zitto (hon.) Went Toe To Toe Up Against Samuel Sitta And Minister Karamagi When Everybody Else Had Their Tails Too Curled In Between Their Legs To Call Out The Richmond Chicanery, Plus All The Venal Bigwigs Who Tried To Cover It. So Zitto (hon.) Is Anything But A Wussy.

My Guess Is That He Does Not Understand Pinda. He Thinks - He Assumes - That Pinda Has Goods Intentions And That Every Fumble He Commits, Is Because Of Bad Advice. Same Good Old 'bad Advice Defense.'

Worse Case Scenario Is That Zitto (hon.) Does Not Appreciate What The Role Of A Prime Minister Is. Nikifufukammekwisha Just Pointed Out "waziri Mkuu Inampasa Awe Makini Katika Lolote Analolisema Ambalo Lina Maslahi Kwa Raia."

Perhaps Zitto (hon.) Does Not Understand That. As I Said, That Is Worse. Worst Case Guess, Though, Is That Zitto (hon.) Does Understand Every Little Thing Going On Here. Each And Every Thing. And He's Obfuscating. For Artistic Reasons.

He Didn't Understood Mr President To Begin With..so No Wonder He Didn't Understand Pinda Haki!
Patriotism Should Come Before Friendship!
 
mnahukumu watu mapema sana.... ningekuwa mimi nyinyi ningesubiri nimsikie Zitto atakapotoa mchango wake Bungeni, theni ningejajudge kile. Alichosema hapa ni kuzungumza na washkaji zake n.k lakini tunataka kujifanya kama tuko kwenye Bunge letu wenyewe ambapo ni baraza la wenye haki, wasiokosea. Tunajigeuza kuwa self rightious to the point kwamba we have to be right. No room for mistakes or erros.

I have been wondering a lot... and I continue to wonder. Hekima inatulazimisha kutofanya haraka kuhukumu ili tutakapotoa hukumu basi iwe ni hukumu inayokaribiana na haki kweli.
 
Mkuu Nyangumi,

Maneno mazito sana haya, yaani ukiyafuatiilia kwa makini na undani wake in details basi unapata jawabu la Meremeta, halafu kuna Warioba pia kwenye hiii ishu!

Nimeona sura ya Mkapa inarudi kwa nguvu kubwa sana katika suala la Meremeta. haki ya nani Mkapa Mkapa Mkapa, hivi Mwalimu akirudi si utakimbia kabisa.

watanzania walimkosea nini huyu baba mpaka akawatwisha watanzania mizigo namna hii. Nafikiri hata hawa akina pinda wanapindisha mambo kulinda Mkapa.
 
mnahukumu watu mapema sana.... ningekuwa mimi nyinyi ningesubiri nimsikie Zitto atakapotoa mchango wake Bungeni, theni ningejajudge kile. Alichosema hapa ni kuzungumza na washkaji zake n.k lakini tunataka kujifanya kama tuko kwenye Bunge letu wenyewe ambapo ni baraza la wenye haki, wasiokosea. Tunajigeuza kuwa self rightious to the point kwamba we have to be right. No room for mistakes or erros.

I have been wondering a lot... and I continue to wonder. Hekima inatulazimisha kutofanya haraka kuhukumu ili tutakapotoa hukumu basi iwe ni hukumu inayokaribiana na haki kweli.

It is all about expression Mwanakijiji.

Hufikiri kuwa input yetu hapa inaweza kumu inform yeye kuhusu Watanzania wanavyomfikiria na kufikiria kuhusu issues na ku influence atakachosema bungeni?

I would think that to be better than harbor misgivings about him and let him expose his positions and commit his stand, only to be lambasted belatedly.
 
Back
Top Bottom