Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Baada ya kuwatukana kiungwana na kisiasa, ngoja nitoe hii nukuu kama hamjaiongelea au kuiona, tujiulize kulikoni Tanzania?

Je Mengi kuwa mshika bango kuhusu uwajibikaji anaundiwa mkakati na Serikali wa kunyanyaswa na kudhulumiwa? Je tuna Serikali ya namna gani?

Hii pekee ni kithibitisho kuwa Serikali yetu bado inafanya mambo si kwa ajili ya Taifa, bali ni kwa ajili ya kikundi au genge fulani. Inapofikia hatua madai ya kusema "Ameshiriki kutukifisha mahali pagumu sana, hata kusababisha serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa" kutolewa na Serikali na hata kuonekana kuwa ni sawa kutoka baadhi ya wanasiasa na watendaji wa Serikali, huku kunaashiria kukosa nindhamu ndani ya Serikali na kunanipa mashaka kama kweli kwa Serikali na Wanasiasa tulionao leo hii, Tanzania inaweza kupata maendeleo na haswa zaidi kuishi katika demokrasia.

Kauli kama hizi zinaonyesha kuwa Serikali yetu na viongozi wake au kadhaa ni sawa na kundi la kihalifu la Mafia!

Ningependa sana kupata ufafanusi kutoka kwa huyo mbunge aliyedai kuwa Mengi kaifikisha Serikali mahali pagumu. Ni kivipi Serikali imefikishwa pahali pagunmu? na nyongeza anapodai kuwa Mengi anasababisha Serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa, ni kwa minajili gani?

Ikiwa Mkaguzi mkuu wa Mahesabu anaonyesha ufujaji wa hali ya juu ndani ya Serikali na matumizi mabaya ya fedha, je hilo ni kosa la Mengi?

Ikiwa ujambazi unaongezeka, uhujumu, uhalifu, magonjwa, njaa, rushwa, migomo na maudhi mengine yanayokera jamii yanaongezeka kila siku, je ni Mengi aliyetuletea haya?

Iweje Serikali leo imlaumu mtu au kundi la watu wanaoikosoa kuwa kulaumu Serikali au kuishupalia ifanye kazi zake kwa umakini ni kuwa kikwazo kwa Serikali kufany akazi zake sawasawa?

Tanzania tumeshereheka miaka 47 ya uhuru juzi, je ni Uhuru gani tuliokuwa tukishehekea ikiwa Uhuru wa maoni, mawazo na kukosoa unawekewa nta, gundi na kupigiliwa misumari?

Say what you will about FMES, love him or hate him, but he nailed it when he said "viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe". That's as real as it can get.
 
I'm tryin to immagine how the govt would make Mr. Mengi bankrupt with super inflated tax claims....if he is indeed a clean businesman with no financial problems at all...please help me on this!!
 
Kila autakae ukubwa basi na amrudie muumba wake, maana ukubwa wote upo kwake. Tukipigiana kelele na kutanua misuli tutaumizana bure. wana JF tukemee haya kwa nguvu zote.
 
Mwanakijiji ngoja nianze kukujibu hoja zako kama ulivyozianisha jana mnaaake nimeshakueleza ila hautaki kulelewa Mkuu Mwenzagu

Ninapenda sana mtu anayejaribu kujibu hoja zangu; bahati mbaya jana hukufanya hivyo ulirusha vijembe vya kitoto na tuhuma zisizo na mguu wala kichwa. Ukathibitisha mwenyewe chuki yako dhidi ya Mengi kwa sababu tu unamchukia Mengi. Kwa maneno yako mwenyewe hakuna chochote ambacho Mengi amefanya, atafanya au anaweza kufanya kikakufanya uwe upande wake. So, ninaposoma hoja zako ninaliangalia hilo.

1.Mauaji ya Albino

Mkuu Mwanakijiji ulimaanisha atoe siku saba kwa akina nani? Waganga wa jadi au mapolisi? Mapolisi ambao hawana hata ushahidi ni waganga wangapi wanahusika na mauaji haya (in contrast na suala la mengi ambaye ana ushahidi kuwa kuna waziri flani alisema so anaweza kutoa ushahidi). Suala la siku saba hapa umeliingiza la nini?

Point yangu haikuwa atoe siku saba kwa nani, point yangu ni kuwa hakutakiwa kutoa siku saba kwa mtu yeyote!

Mkuu Mwanakijiji, suala la Maalbino kama alivyosema Mhe. Masha siyo watanzania wote wanohusika na suala la mauaji haya (rejea kipindi kile suala la Mapanki wewe ulisimama wapi?).

Sasa hiyo nayo ni hoja? Hivi kuna mtu duniani anaamini Watanzania wote wanahusika? Huwezi kukanusha kitu ambacho hakipo. Hakuna mtu, au chombo chochote cha habari nyumbani au nje ambacho kimedai kuwa Watanzania wote wanahusika na mauaji ya Albino.

Hata hivyo, tunachosema ni kuwa yeye kama Waziri wa Mambo ya Ndani ameshindwa kumobilize resources, talents, and expertise kukabiliana na mauaji haya. Zaidi ya watanzania 30 wameuawa kwa sababu ya ngozi yao na utetezi unaoleta ni kuwa "siyo Watanzania wote wanahusika"?

Yaani umeridhika na mwitikio wa Waziri huyo kwenye suala hili? Nina bahari ya kushuhudia operesheni dhidi ya poachers kule Ngorongoro, na baadaye dhidi ya vitendo vya wakimbizi kule Ngara na Kigoma ambapo task force ya Polisi ilitumwa kuingilia kati na kuhakikisha wanarudisha usalama.

Mauaji ya Albino yanaendelea na mwitikio ni minimal; kwa sababu hatutaki kuonesha kuwa kila Mtanzania anahusika. Ndio maana kauli yake yeye mwenyewe imewaudhi walemavu kwani kama wewe ametrivialize the gravity of the situation and the threat that our brothers and sisters are constantly facing.

2.Vifo vya watoto 19 Tabora
Suala la vifo lilishaundiwa kamati na mawazo yalishatolewa na kinachoendelea ni suala la DPP kuangalia ushahidi aliopelekewa kama unatosheleza kufungua mashtaka juu ya waliohusika.

Hapa tena umemuingiza Masha kwa suala lisiloshabihiana na suala la Vifo vya Tabora. (Mengi ana ushahidi wa kutosha kuhusiana na anachokisema). Hapa Masha asingekurupuka kusema natoa siku saba watu flani waweke ndani sababu wanahusika bila kuanya uchunguzi (Kumbuka Masha aliomba Mengi awasilishe ushahidi within 7 days kw yale anayoyasema).
once again, una miss point. Ilimchukua muda gani kwa Masha kutoa kauli kuhusu Mengi? Na ilimchukua muda gani kwa yeye kutoa kauli kuhusu vifo vya watoto. Uongozi siyo kusema unaongoza lakini pia kuonekana unaongoza. Polisi Tabora walitakiwa wawe sehemu ya uchunguzi, na kuna watu walitakiwa wawajibishwe, Masha amefanya nini kuhusu hilo?

3.Madai ya Rostam Aziz
Hapa Tena.Madai ya Rostam yalikuwa ni ya kwake Binafsi na wafanyabiashara tusiowaju kama vile wewe na yule mnavyoweza kudai mnatishwa na hili linaweza kushughulikiwa na Mkuu wa kituo tu. Ila Mengi alikuwa akimtuhumu kiongozi wa serikali mwenye Dhamana na serikali na pia ukumbuke kuwa alisema walizungumza hayo katika kikao cha siri cha serikali. Hivyo serikali inahusika kwa kumtishia Mengi (unaweza kujiuliza kwanini walikuwa wakimjadili Mengi?). Haiwezekani mtu akazungumza siri za vikao vya juu vya serikali na asichunguzwe!.

Hiyo serikali yenye siri ni serikali ya mbinguni!? Kuvujisha siri za serikali zenye athari kwa mtu mmoja au jamii nzima siyo tu ni lazima lakini ni jukumu la dhamira. Serikali haiwezi kula njama dhidi ya mwananchi wake halafu watu wakubaliane kukaa kimya ati kwa vile ni "serikali".

Kuna siri zinazotakiwa kulindwa, lakini siri ya kumharibia mtu jina lake, kazi yake au kumuonea ni siri ya kijinga na serikali inayotaka siri ya namna hiyo kulindwa inapoteza legitimacy yake! Serikali au maafisa wa serikali hawawezi kula njama kumdhulumu au kumdhuru raia wake.

Nawatia moyo watendaji wote ambao wanavujisha siri za kijinga!

Rostam hakuituhumu serikali ila Mengi alituhumu serikali, hivyo Masha Was Right?!
Serikali ni ya watu, inatoka kwa watu, na ni kwa ajili ya watu! Rostam alitoa tuhuma ambazo ni nzito na alitumia vyombo vya habari kutoa tuhuma hizo. Ni tuhuma nzito ambazo zimetolewa na Mbunge (siyo mkulima wa kijijini kwetu); Mbunge anapotoa tuhuma dhidi ya raia ni jambo la kawaida lakini raia akitoa tuhuma dhidi ya mbunge inakuwa tatizo!

kwenye nchi yenye kuheshimu uhuru, yote mawili yanawezekana! Tatizo yule mbunge akitoa tuhuma asiwe katika nafasi ya kutekeleza tishio lake. Masha yuko kwenye nafasi ya kutekeleza tishio kutokana na nafasi yake. He is prone to abuse of power!

Hoja ni nyingi sana ulizojenga ,lengo ni kuchochea masha ang'oke tu ili iwe furaha yako kwamba umeweza kufanya flani atolewe.Binafsi siipendi tabia binafsi ya Masha ila utendaji wake ni thabiti na ninaweza kukuthibitishia hilo.

Sikufichi, mimi sina kiongozi ninayemsujudia; kiongozi yeyote aliyechaguliwa na wananchi anaweza kuondolewa wakati wowote pasipo tatizo kwangu. Hakuna kiongozi mwenye haki ya kuongoza! Haijalishi huyo kiongozi ni msomi, ni maarufu, ni rafiki au vyovyote vile akiharibu mojawapo ya options zilizopo ni kujiuzulu. Anayeangalia urafiki, udugu, ukabila, dini, ukaribu, au hisia zake katika kushughuilikia mafisadi hafai katika mapambano.

Standard yetu hapa ni kumkoma nyani giledi mchana kweupe! Sina utii kwa kiongozi yeyote wala mapenzi ya kudumu kwa mtu yeyote yule. Ukiharibu utawajibishwa, na ukiharibu sana utang'olewa; Masha is bordering the later!

Mie nachoona ni kosa ni suala la Mengi kuzungumza mambo ya vikao vya seri vya serikali.

Pili.Nani alkimwambi Mzee huyu wa IPP kuhusia na viako vya siri vya serikali na ningependa mzeehuyu awajibike kwa kutoa siri za serikali.(sheria Ipo).

Oh stop! kama kuna sheria nendeni mahakamani! siyo kutoa vitisho. Kwa sababu angalau huko tutajua hizo siri zilijadiliwa wapi, na akina nani na kwanini ni "siri". Tunavujisha siri za "serikali" kila kukicha lakini leo ndio imekuwa nongwa?

a. Mkataba wa Richmond umevuja - ulikuwa siri
b. Mkataba wa Buzwagi umevuja - ulikuwa siri
c. Mkataba wa Airbus 320 umevuja - ulikuwa siri
d. Akaunti za mafisadi zimevuja - ziliikuwa siri

n.k

Siri za kijinga siyo tu zinavuja zinapaswa kuvujishwa kama mapakacha yanayojaribu kujazwa maji!

Jana Mzee Mwanakijiji ulichemka, na sababu ya wewe kuandika ni kukurupuka na inaonesha ulishirikishwa jambo usilolijua vyema.
sorry, nina bahati ya kujua mengi kuliko unavyodhania; Hivi hujajiuliza ni kwanini hadi leo hakuna Waziri hata mmoja aliyejitokeza kutake side na Masha; not even a Prime Minister? Niulize nitakuambia...

Kumbuka wewe ndiyo ulikuwa wa kwanza hapa kusema Waziri aliyehusika ni Masha kabla haujaedit mwenyewe
Nilisema habari yako iko nilivyoisimamia na bado ipo nilivyoipost! Mengine tukiyaandika hapa kuhusu hilo la Masha, mtatuona wanga!

So wewe angalia kutoka katika mwanga wa chuki dhidi ya Mengi, na mimi nitaliangalia kutoka katika mwanga wa kuchukia watawala wanaotumia nafasi zao vibaya kwa sababu wao ni watawala!
 
FMES: Post yangu ni ya jumla, hailengi specific post maana sijaweza kuzisoma posts zote, na unajua mimi siwezi kukurushia mawe, maana mimi nipo kwenye nyumba ya kioo...ukirudisha itakuwa balaa.

respect mkuu, tuendelee kukata mbuga, tutafika tu...

- Sawa sawa mkuu tupo ukurasa mmoja hapa, naomba kunawa kutoka hii topic na maneno yafuatayo ni kwamba,

serikali na viongozi wake wanaogopa wananchi wenye habari zao za kweli na sio za uongo, tunapojadili habari za uongo huwa wanafurahi sana, ila tukijadili ukweli huwa simu zinalia kila kona, sasa tutafute habari za ukweli wakuu.

- Kwa hayo machache naomba kunawa na hii topic, mpaka later kama nilivyosema ninapoandika hapa Mengi yupo Arusha na mkuu wa kaya waliyeenda naye kwenye ndege moja, na Masha yupo Geneva, tupo on top of this ishu mpaka kieleweke.

- Mafisadi wako njiani kwenye sheria, wanasubiriwa majaji warudi kutoka likizo Jan, tarehe 13 kuna kesi ya Makamba na mbunge mmoja mbele ya kamati ya bunge ya ethics hiyo itakua aibu kubwa maana mkuu ameshikwa pabaya, sasa tupo ontop kama kawa,

Sasa tuna viongozi wakuu wawili wa taifa wataondoka weekenend na wanakuja wengine wawili mwishoni mwa wiki, kwa hiyo wakuu typo ontop, yaliyopita sio ndwele sasa tunasonga mbele.

Taifa mbele, JF itadumu tu milele na kumkoma nyani giladi! na amani na JF members wote na amani iwe nanyi, amina na milele!

Respect Wakuu!
 
FMES: Post yangu ni ya jumla, hailengi specific post maana sijaweza kuzisoma posts zote, na unajua mimi siwezi kukurushia mawe, maana mimi nipo kwenye nyumba ya kioo...ukirudisha itakuwa balaa.

Kwi kwi kwi kwiiiiii Heri mimi sijasema!
 
Lakini kuna deal nyingi chafu huyu mkulu kazicheza na wewe unazijua lakini hutaka hata kucoment hata kidogo licha kusema tusubili sheria.Naona hii picha kwako imekuwa chungu sana kuhusu Lau kila mmoja anaelewa wewe na Gembe mmebeba dhamana ya kumlinda Lau na kumtetea kwa misingi ya sheria.
Gembe fuata upepo....bora FMES ambae alimuendesha na kumpeleka Masha airport na kwenye interview...alafu si unajua Masha alikuwa anatumia gari la dataz man wakati yao yakiwa yanakatiza Atlantic kuja bongo.
 
Baada ya kuwatukana kiungwana na kisiasa, ngoja nitoe hii nukuu kama hamjaiongelea au kuiona, tujiulize kulikoni Tanzania?

Je Mengi kuwa mshika bango kuhusu uwajibikaji anaundiwa mkakati na Serikali wa kunyanyaswa na kudhulumiwa? Je tuna Serikali ya namna gani?

Hii pekee ni kithibitisho kuwa Serikali yetu bado inafanya mambo si kwa ajili ya Taifa, bali ni kwa ajili ya kikundi au genge fulani. Inapofikia hatua madai ya kusema "Ameshiriki kutukifisha mahali pagumu sana, hata kusababisha serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa" kutolewa na Serikali na hata kuonekana kuwa ni sawa kutoka baadhi ya wanasiasa na watendaji wa Serikali, huku kunaashiria kukosa nindhamu ndani ya Serikali na kunanipa mashaka kama kweli kwa Serikali na Wanasiasa tulionao leo hii, Tanzania inaweza kupata maendeleo na haswa zaidi kuishi katika demokrasia.

Kauli kama hizi zinaonyesha kuwa Serikali yetu na viongozi wake au kadhaa ni sawa na kundi la kihalifu la Mafia!

Ningependa sana kupata ufafanusi kutoka kwa huyo mbunge aliyedai kuwa Mengi kaifikisha Serikali mahali pagumu. Ni kivipi Serikali imefikishwa pahali pagunmu? na nyongeza anapodai kuwa Mengi anasababisha Serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa, ni kwa minajili gani?

Ikiwa Mkaguzi mkuu wa Mahesabu anaonyesha ufujaji wa hali ya juu ndani ya Serikali na matumizi mabaya ya fedha, je hilo ni kosa la Mengi?

Ikiwa ujambazi unaongezeka, uhujumu, uhalifu, magonjwa, njaa, rushwa, migomo na maudhi mengine yanayokera jamii yanaongezeka kila siku, je ni Mengi aliyetuletea haya?

Iweje Serikali leo imlaumu mtu au kundi la watu wanaoikosoa kuwa kulaumu Serikali au kuishupalia ifanye kazi zake kwa umakini ni kuwa kikwazo kwa Serikali kufany akazi zake sawasawa?

Tanzania tumeshereheka miaka 47 ya uhuru juzi, je ni Uhuru gani tuliokuwa tukishehekea ikiwa Uhuru wa maoni, mawazo na kukosoa unawekewa nta, gundi na kupigiliwa misumari?

Mimi nawaonea huruma sana ndugu zangu ambao bado wanaamini CCM "itabadilika". Katika hali iliyonayo sasa na bado unaona ujinga kama huu unazungumziwa ndani ya hivyo vikao nyeti na bado kuna watu wanadhani ni sawa kabisa na zaidi mawazo kama hayo yanatokana kwa vijana ambao wanadai kuwa walijiunga na CCM ili kupata nafasi ya kubadili mambo wakiwa ndani, bado kuna wenzetu wanajipa moyo kuwa mambo yatabadilika?

Poleni sana vijana wenzangu na imani yenu kuwa Tanzania bila ya CCM haiwezekani.....

Dawa ya CCM ni kuipumzisha na kuwapa nafasi ya kufanya selfcleansing wakati wakiwa mbali na madaraka waliyonayo sasa ambayo yanawafanya kuvutia kila aina ya wapenda maovu....

Tanzanianjema
 
FMES: Post yangu ni ya jumla, hailengi specific post maana sijaweza kuzisoma posts zote, na unajua mimi siwezi kukurushia mawe, maana mimi nipo kwenye nyumba ya kioo...ukirudisha itakuwa balaa.

Tofauti na wewe mimi mawe ruksa kwa anayetaka kurusha lakini hayataninyamazisha kuita koleo kwa jina lake halisi - nikinyamaza hayo mawe yatapiga mayowe. Nitawaachia watu makini watofautishe pumba na mchele. Masha lazima akumbushwe kuwa cheo ni dhamana, period.
 
Ndio yale yale, hata mtu akiwa nje ya mstari anashindwa kuambiwa kisa ataonekana anarusha mawe. Kama mwanasiasa na academician, that one is your ...... Hii kauli nitakukumbusha siku moja, nitakwambia hufai kuwa kiongozi kwa sababu hauna clearly depicted principles. Viongozi wababaishaji ambao wako vuguvugu hawafai. Amua kuwa moto ama baridi. Hizi ni zama za mabadiliko vijana.

Endelea kudumisha amani na utulivu huku mafisadi wakikata mawingu.
You have blown this whole thing out of proportion mama, you needed to put my response to FMES in proper context. Nitashukuru siku ukinikumbusha maana nitapata fursa ya kukufanulia bayana! Many thanks, though.
 
I'm tryin to immagine how the govt would make Mr. Mengi bankrupt with super inflated tax claims....if he is indeed a clean businesman with no financial problems at all...please help me on this!!

The government, using it's objectionable ombudsmen and obstructionist obfuscating obscurantism can interpret any tax law any way it likes or even make some new ordinances and Draconian decree ones on the fly, if not by cajoling its CCM MPs to make laws the proper way but with skewed intentions.

Of course it can also achieve the same by just enforcing, albeit selectively, the current law, which says so much about Mr. Mengi and his reputation.
 
You have blown this whole thing out of proportion mama, you needed to put my response to FMES in proper context. Nitashukuru siku ukinikumbusha maana nitapata fursa ya kukufanulia bayana! Many thanks, though.

Kitila,

I will go the mama's way! You equally shocked me by buying peace with FMES on something you sounded quite opposite to his position! Is it the sweet words FMES said about you! Your first message was clearly from a patriotic person!

At least you should have accepted the compliments (rushwa) from FMES by keeping quiet, au hata kwa PM basi!
 
The government, using it's objectionable ombudsmen and obstructionist obfuscating obscurantism can interpret any tax law any way it likes or even make some new ordinances and Draconian decree ones on the fly, if not by cajoling its CCM MPs to make laws the proper way but with skewed intentions.

Naona SIJUI KIINGEREZA 🙂

Pundit, kwa watu tuliosoma kila shule lugha nyingine, hapa unatuacha hoi. Umeshaombwa uandike KIINGEREZA cha Kitanzania, ila mwenzetu kila kukicha unaandika sijui cha wapi ............ Hii kusoma huku una Dictionary mkononi inachosha, inachobaki tunakuwa tunaruka makala zako, too sad maana huwa ni nzuri kusoma.
 
Ndio yale yale, hata mtu akiwa nje ya mstari anashindwa kuambiwa kisa ataonekana anarusha mawe. Kama mwanasiasa na academician, that one is your ...... Hii kauli nitakukumbusha siku moja, nitakwambia hufai kuwa kiongozi kwa sababu hauna clearly depicted principles. Viongozi wababaishaji ambao wako vuguvugu hawafai. Amua kuwa moto ama baridi. Hizi ni zama za mabadiliko vijana.

Endelea kudumisha amani na utulivu huku mafisadi wakikata mawingu.

Kitila,

I will go the mama's way! You equally shocked me by buying peace with FMES on something you sounded quite opposite to his position! Is it the sweet words FMES said about you! Your first message was clearly from a patriotic person!

At least you should have accepted the compliments (rushwa) from FMES by keeping quiet, au hata kwa PM basi!

Hakitupu na Mama,

Na mimi nakubaliana nanyi 100%. Nadhani Kitila katingishika. Ujumbe wake wa kwanza ulikuwa blunt and to the point. Baadae akau water down, kuua soo!

Unafan' mchezo na Field Marshal!

Mkuu anatisha yani. Kwanza hiyo mi font yake tu, unaweza ukarudi nyuma mwenyewe!! Halafu ana tactic yake moja kwenye playbook yake anaweza kukwambia "wewe nakuheshimu sana..." halafu anakuachia. Yani kwamba angeweza kukuchana chana vibaya vibaya ila kakuweka pending tu! Ha ha haaaaaa...

Namba nyingine ile Field Marshall!
 
Naona SIJUI KIINGEREZA 🙂

Pundit, kwa watu tuliosoma kila shule lugha nyingine, hapa unatuacha hoi. Umeshaombwa uandike KIINGEREZA cha Kitanzania, ila mwenzetu kila kukicha unaandika sijui cha wapi ............ Hii kusoma huku una Dictionary mkononi inachosha, inachobaki tunakuwa tunaruka makala zako, too sad maana huwa ni nzuri kusoma.

Tatizo nishaandika Kiswahili kikawa na ulimbwende wa mvita vile vile 🙂

Mie "teja" wa usanifu, kunradhi.

Maybe it is time for you to step up your game now.

Back to the subject.
 
Tatizo nishaandika Kiswahili kikawa na ulimbwende wa mvita vile vile 🙂
Mie "teja" wa usanifu, kunradhi.

Maybe it is time for you to step up your game now.

Back to the subject.

Pundit,
I wish ningelifanya hivyo. Ila kama nilivyosema kila sehemu natumia lugha nyingine. Hapa Kiingereza na Kiswahili, nikirudi nyumbani Kinyamwezi na nikiongea na MY WIFE WANGU (according to Michuzi) inakuwa Kipare. Kwenye Zege huko tunasema KISWA-NGLISH. Sasa mwisho wa siku hata unashindwa "ku-Step up my game" kuwe katika lugha ipi. Kibaya zaidi sisi Mafundi Mchundo wengi (siyo wote) tunajulikana kwa tatizo la kutokujua Kiingereza vizuri. Kuna jamaa yangu mmoja nasikia alikuwa akisoma Ukraine. Kwa mahesabu, fizikia, Kemia, nk alikuwa mzito sana. Siku moja dada mmoja Mzambia akamaliza kupika na kutaka kuzima jiko. Jamaa nasikia akasikika akisema "Don't put off, i too want to COOK ON HIM......"
Sawa, ntajitahidi nije huko juu kukufuata, ila nawewe shuka kidogo ili twende bega kwa bega katika kumkoma nyani.
 
Hakitupu na Mama,

Na mimi nakubaliana nanyi 100%. Nadhani Kitila katingishika. Ujumbe wake wa kwanza ulikuwa blunt and to the point. Baadae akau water down, kuua soo!

Unafan' mchezo na Field Marshal!

Mkuu anatisha yani. Kwanza hiyo mi font yake tu, unaweza ukarudi nyuma mwenyewe!! Halafu ana tactic yake moja kwenye playbook yake anaweza kukwambia "wewe nakuheshimu sana..." halafu anakuachia. Yani kwamba angeweza kukuchana chana vibaya vibaya ila kakuweka pending tu! Ha ha haaaaaa...

Namba nyingine Field Marshall!

Haya bwana nakubali mie kushindwa. Sincerely, sijui/sikujua kama FMES ndiye aliyesema kwamba wanaomsema Masha wana wivu. Kama yeye ndiye aliyesema hivyo basi post yangu inamhusu sana!
 
"sorry, nina bahati ya kujua mengi kuliko unavyodhania; Hivi hujajiuliza ni kwanini hadi leo hakuna Waziri hata mmoja aliyejitokeza kutake side na Masha; not even a Prime Minister? Niulize nitakuambia..."

Mkuu Mkkj,

Hii point niliipick huko nyuma lakini kila nikimsubiri mkuu Gembe akuulize naona hajauliza. Naomba nikuulize mimi sasa.

Hivi ni kwanini hadi leo hakuna Waziri hata mmoja aliyejitokeza kutake side na Masha; not even a Prime Minister?...
 
Mwisho wa siku utaskia kiongozi flani kawaita mengi na masha; kawapatanisha!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom