Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Mwisho wa siku utaskia kiongozi flani kawaita mengi na masha; kawapatanisha!!!!!

n dat wud b de end of de movie....tutaona majina ya waigizaji,ma director n kila kitu..
hence wa tz tumepigwa anaza changa la macho kwa minds zetu kuwa turned to focus on dis upuuzii n forgetin other important issues
 
Mkuu Kitila,

- Be careful mkuu, maana si unajua misery loves company! You are too big kujichanganya na loosers!

- Wazee nipo na viongozi wakuu wa taifa hapa hebu andikeni hoja ili niwaonyeshe, siwezi waonyesha mijadala ya pua, Kitila wewe malizia hiyo PhD, ambayo tunajua inavyokubalika na dunia ili uje liokoa taifa na kuwaelimisha wananchi walioala, ili wajue maana ya kuwa objective na open minded na how to work as a team, badala ya ubinafsi tuu!

Halafu mind you panapofuka moshi chini kuna moto, yaani inaoneakan kuwa somebody ameungua maaana hiki kilio sio kawaida, wakuu kama nimewakwaza samahani sana niko chini ya miguu yenu mnisamehe na sitarudia tena jamani msalieni mtume, nioneeni huruma jamani ! Bwa! ha! ha! ha! ah!

Sauti ya umeme, FMES!
 
Ikawa usiku, ikawa mchana . . . . Siku ya Sita. Ya Saba ya Sabato akapumzika, akaibariki na kuitakasa . . . . . . .

Knock Knock Knokck!! Anybody home?
 
Nimeona kule thread yako Mengi yuko ikulu wanapeana mikono na muungwana.
 
LOL,

Ni kweli Mkuu, sijui kama JK anajua sakata hili, kama analijua na amekula pause tu . . . basi ipo kazi.

FMSE, Masha yupo? Tunataka tuone Movie sasa Trailer imekwisha!
 
AHaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nakumbuka msemo mmoja ktk james bond movies:" you live to die another day"
 
Date::12/12/2008
Mengi asubiri misuli ya Masha
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Reginald Mengi hajawasilisha uthibitisho wa madai yake aliyotoa hadharani kuwa waziri mmoja kijana anataka kumuhujumu biashara zake, na sasa zamu ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kuchukua hatuia baada ya siku saba kuisha.

Masha, ambaye ni mwanasheria, alimpa Mengi siku saba kuwasilisha uthibitisho wa madai aliyoyatoa kwa waandishi wa habari kuwa kuna waziri kijana aliyewasilisha hoja katika kikao nyeti ya kutaka mfanyabiashara huyo abambikiwe kodi kwenye biashara zake ili ashindwe kuzilipa na hivyo kufilisiwa.

Siku hizo saba ziliisha jana huku mamlaka za usalama wa raia zikiwa hazijapokea uthibitisho wowote kutoka kwa mfanyabiashara huyo, wala maelekezo kutoka kwa Waziri Masha, ambaye ameripotiwa kuwa safarini nje ya nchi na ambaye alionya kuwa iwapo mmiliki huyo wa makampuni ya IPP atashindwa kuwasilisha uthibitisho, atachukuliwa hatua za kisheria.

Lakini inaonekana Mengi ametunisha msuli kusubiri kuona waziri huyo akichukua hatua hizo.

Hadi jioni saa 11:30 jana, Mengi hakuwa amewasilisha uthibitisho huo, si wizarani wala makao makuu ya Jeshi la Polisi, huku waziri huyo akielezewa kuwa Geneva, Uswisi ambako yumo katika msafara wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhudhuria mkutano wa wa kimataifa wa wakimbizi.

Mengi aliripotiwa kuwa mkoani Arusha kwa shughuli za kijamii.

Akiongea na Mwananchi, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Manumba aliweka bayana kwamba hadi jana hawakuwa wamepata maelekezo ya serikali kuhusu namna ya kushughulikia suala hilo.

Naye msemaji mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga alithitibisha kwamba hadi jana jioni Mengi hakuwa amewasilisha taarifa yoyote wizarani.

Alisema baada ya kuisha kwa siku saba alizopewa mfanyabiashara huyo, kinachosubiriwa ni kuona hatua ambazo zitachukuliwa kwa mujibu wa Waziri Masha.

"Kwa kuwa alipewa barua ya wiki moja na wiki imekwisha, tusubiri tuone hatua itakayofuata, nafikiri tusubiri waziri atakachosema hapo baadaye," alifafanua.

Msemaji huyo aliongeza kuwa hakukuwa na mawasiliano yoyote na Mengi na hakukuwa na haja ya kufanya hivyo kwani, tayari alipewa barua na waziri hivyo alichopaswa kufanya ni kujibu.

"Yeye alipewa barua, kwa hiyo hakukuwa na haja ya kufanya naye mawasiliano alichopaswa kufanya ni kujibu tu barua ya waziri," alisisitiza msemaji huyo mkuu huyo wa wizara.

Kutowasilishwa kwa ushahidi huo kunamaanisha kuwa Masha sasa anasubiriwa kuchukua hatua dhidi ya mfanyabiashara huyo, ambaye pia aliwahi kupambana na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Wilson Masilingi, katika serikali ya awamu ya tatu.

Habari kutoka kwa watu walio karibu na mfanyabiashara huyo zinasema kuwa Mengi ameweka msimamo ambao haubadiliki kuhusu tuhuma hizo na kwamba badala ya kuwasilisha ushahidi, ni vema waziri huyo akaenda mahakamani.

Awali Mengi alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa kipindi hicho cha siku saba ni kirefu na kwamba ni vema hata angetoa siku moja.

Msemaji wa Mengi, Abdulhamin Njovu hakutaka kuzungumzia suala hilo baada ya Mwananchi kuwasiliana naye kwa njia ya simu.

Sakata hilo tayari limechukua sura na mwelekeo tofauti kutokana na maoni ya watu kugawanyika. Baadhi wanamtetea mfanyabiashara huyo na kuishushia lawama serikali, wakati wengine wanampinga mfanyabiashara huyo na kuitetea serikali.

Wiki iliyopita, Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, bila ya kutaja majina lilitoa tamko kali ambalo liligusa pande zote mbili kwenye mgogoro huo, likiweka bayana kuwa kauli zinazotolewa si fikra za Watanzania, bali ni utashi binafsi wa kibiashara na kisiasa.

Lakini viongozi wengi wa vyama vya siasa wamemtetea Mengi na kulaumu serikali kwa kufanya njama dhidi ya wafanyabiashara wazalendo.
 
Safi mzee wetu wa Nkuu Machame!! Asikubabaishe huyo dogo hana lolote. Yetu macho tuone atakufanya nini. Akitaka aende mahakamani kukushitaki ili utoe ushahidi wako. Anakupa altimatum kama nani huyo??? Eti siku saba. Akamuulize kaka Augustino wa Kiraracha siku saba zake ziliishia wapi??? Japo kwa uhakika angalao kaka wa Kiraracha alikuwa na point kwenye issues nyingine na matokeo tuliyaona. Mwenye uamuzi wa kuchukua hatua ni mhusika Mengi maana ushahidi anao. Kaa kimya mzee wetu ili tuone hako ka kijana katafanya nini na bichwa lake analotunyolea upara wa ki afro-american. Mi ninikuwa najiuliza mbona huyu kijana kipara sana wakati wote kama kafiwa na ndugu wa damu, kumbe ni staili yake aliyotoka nayo kule marekani ati anajifanya tanzania anaijua na mkulu akaamua kumpa wizara nyeti ya ndani ambapo hata jeshi hajakanyaga. Kwanza nashauri apelekwe kwanza ccp Moshi akanolewe!!!! Ingekuwa ni wakati wa mzee wetu Kambarage alipotua hapa tu angepelekwa Kivukoni au JKT au CCP ndipo aufahamu uzalendo uko je. Nasita kusema huenda siyo mzalendo, atuhakikishie kule marekani kama hajaukana urai wetu au ndo mambo ya dual citizenship hayo ambayo hata mswada haujakamilika (if at all the process yake imeshaanza sina hakika). Please, mwacheni mzee Mengi nyie mafisadi na watoto wenu, marafiki zenu, jamaa zenu na vibaraka wenu.
 
Waziri kijana, nyota ya alfajiri, jua likitoka tu, haionekani teeena!

Hivi masha anasahau kuwa ni juzi juzi tu ametoka kuwakoroga walemavu wa ngozi kwa kusema mauaji yanayoendelea juu yao ni madogo?? Thena anasahau kuwa hawa walemavu wa ngozi na watu wengine wenye ulemavu wanampenda sana Mengi kwa misaada anayowapatia kila wakati?? Anafahamu kuwa Mengi hutumia millions of money kuandaa chakula na kula pamoja na watu hawa wenye ulemavu? anasahau kuwa yeye pamoja na ufisadi wake hakuwahi hata kufikiria kushare hizo pesa anazoiba na hawa watu wenye ulemavu?? Anatambua kama hawa watu wenye ulemavu wanatoka kwenye familia zizizo na ulemavu?? Anafahamu kuwa hizi familia zinazolea watu wenye ulemavu wanathamini sana mchango wa Mengi kwa wanandugu wao wenye ulemavu?? ANAFAHAMU KUWA VYOMBO VYAKE YA HABARI VINAWABURUDISHA WANANCHI BUREEEEEEEEEE NA WANA COVERAGE KUBWA HAPA NCHINI?? Hivi ni mwananchi gani atakubali kuona MENGI anafanyiwa vituko na huyu Masha na akakaa kimya?? Ah mi nina hamu kweli ya kuona jinsi huyu Masha anavyoporomoka na kubakia mfugaji wa kuku kama alivyokuwa anafuga mwanzo pale kwenye flat za NAMANGA..... FMES mjibie maana wewe ndo mjibu hoja wake hapa
 
Kama mafisadi wengine waliomtangulia (Manji, Lowassa, Rostam Azizi, etc), Masha ameshindwa kufanya chochote dhidi ya Mengi hata baada ya kutoa vitisho vya siku saba kwa hasira na mikiki mingi.

Kwa mara nyingine, dozi kubwa aliyopata hapa JF imemfanya arudi nyuma na kuacha magazeti mahiri ya Thisday na Kulikoni yaendelee na kazi yao ya kuwapa watanzania habari ambazo serikari inazificha.

Kwa sasa..... Masha umebana weeeee .... na umeachia!

Kama kawaida ya friday hapa JF ..... wana JF kwa kushirikiana na bongo radio na radio zingine zote mahiri nchini, tunasherekea ushindi kwa bonge la muziki wa ngwasuma na sebene toka kwa extra musica (sorry werasoni).

Mods..... it's friday.... what the hell.... please, let it stay here for now.
 
Duh,Ha ha haaa. Hivi huyu jamaa angekaa kimya bila kukurupuka na kutoa siku saba za vitisho si bado angekua anaheshimika? Sasa ame-gain nini katika vitisho vyake zaidi ya kuvuna aibu na dharau tu?Cheki sasa alivyojiaibisha.

Mijitu mingine bwana.Ndiyo maana Wizara ya Mambo ya Ndani iko wazi kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na Tano Tangu Mrema atoke kwenye hiyo wizara.Yaani hakuna waziri
 
Naona siku matumizi ya Li, Mi, Ma yamekuwa popular sana hapa....utasikia mtu anasema Li-flani, Mi-jitu n.k.

Safi sana kuona hii
 
Mengi asubiri misuli ya Masha
Na Ramadhan Semtawa

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Reginald Mengi hajawasilisha uthibitisho wa madai yake aliyotoa hadharani kuwa waziri mmoja kijana anataka kumuhujumu biashara zake, na sasa zamu ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kuchukua hatuia baada ya siku saba kuisha.

Masha, ambaye ni mwanasheria, alimpa Mengi siku saba kuwasilisha uthibitisho wa madai aliyoyatoa kwa waandishi wa habari kuwa kuna waziri kijana aliyewasilisha hoja katika kikao nyeti ya kutaka mfanyabiashara huyo abambikiwe kodi kwenye biashara zake ili ashindwe kuzilipa na hivyo kufilisiwa.

Siku hizo saba ziliisha jana huku mamlaka za usalama wa raia zikiwa hazijapokea uthibitisho wowote kutoka kwa mfanyabiashara huyo, wala maelekezo kutoka kwa Waziri Masha, ambaye ameripotiwa kuwa safarini nje ya nchi na ambaye alionya kuwa iwapo mmiliki huyo wa makampuni ya IPP atashindwa kuwasilisha uthibitisho, atachukuliwa hatua za kisheria.

Lakini inaonekana Mengi ametunisha msuli kusubiri kuona waziri huyo akichukua hatua hizo.

Hadi jioni saa 11:30 jana, Mengi hakuwa amewasilisha uthibitisho huo, si wizarani wala makao makuu ya Jeshi la Polisi, huku waziri huyo akielezewa kuwa Geneva, Uswisi ambako yumo katika msafara wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhudhuria mkutano wa wa kimataifa wa wakimbizi.

Mengi aliripotiwa kuwa mkoani Arusha kwa shughuli za kijamii.

Akiongea na Mwananchi, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Manumba aliweka bayana kwamba hadi jana hawakuwa wamepata maelekezo ya serikali kuhusu namna ya kushughulikia suala hilo.

Naye msemaji mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga alithitibisha kwamba hadi jana jioni Mengi hakuwa amewasilisha taarifa yoyote wizarani.

Alisema baada ya kuisha kwa siku saba alizopewa mfanyabiashara huyo, kinachosubiriwa ni kuona hatua ambazo zitachukuliwa kwa mujibu wa Waziri Masha.

"Kwa kuwa alipewa barua ya wiki moja na wiki imekwisha, tusubiri tuone hatua itakayofuata, nafikiri tusubiri waziri atakachosema hapo baadaye," alifafanua.

Msemaji huyo aliongeza kuwa hakukuwa na mawasiliano yoyote na Mengi na hakukuwa na haja ya kufanya hivyo kwani, tayari alipewa barua na waziri hivyo alichopaswa kufanya ni kujibu.

"Yeye alipewa barua, kwa hiyo hakukuwa na haja ya kufanya naye mawasiliano alichopaswa kufanya ni kujibu tu barua ya waziri," alisisitiza msemaji huyo mkuu huyo wa wizara.

Kutowasilishwa kwa ushahidi huo kunamaanisha kuwa Masha sasa anasubiriwa kuchukua hatua dhidi ya mfanyabiashara huyo, ambaye pia aliwahi kupambana na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Wilson Masilingi, katika serikali ya awamu ya tatu.

Habari kutoka kwa watu walio karibu na mfanyabiashara huyo zinasema kuwa Mengi ameweka msimamo ambao haubadiliki kuhusu tuhuma hizo na kwamba badala ya kuwasilisha ushahidi, ni vema waziri huyo akaenda mahakamani.

Awali Mengi alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa kipindi hicho cha siku saba ni kirefu na kwamba ni vema hata angetoa siku moja.

Msemaji wa Mengi, Abdulhamin Njovu hakutaka kuzungumzia suala hilo baada ya Mwananchi kuwasiliana naye kwa njia ya simu.

Sakata hilo tayari limechukua sura na mwelekeo tofauti kutokana na maoni ya watu kugawanyika. Baadhi wanamtetea mfanyabiashara huyo na kuishushia lawama serikali, wakati wengine wanampinga mfanyabiashara huyo na kuitetea serikali.

Wiki iliyopita, Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, bila ya kutaja majina lilitoa tamko kali ambalo liligusa pande zote mbili kwenye mgogoro huo, likiweka bayana kuwa kauli zinazotolewa si fikra za Watanzania, bali ni utashi binafsi wa kibiashara na kisiasa.

Lakini viongozi wengi wa vyama vya siasa wamemtetea Mengi na kulaumu serikali kwa kufanya njama dhidi ya wafanyabiashara wazalendo.

source;Mwananchi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom