Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.


- Ni haki yangu kutoa mawazo yangu kama ilivyo yako, Mengi ametuhumu waziri sasa ishu inakuwa ni waziri level sio RPC, kwani waziri hajui hizo sheria?

Later saa ya kibarua!


kwa hiyo waziri level sio
Mwendesha mashtaka atakuwa waziri
hakimu waziri
 
Mi nadhani, kwa sababu Mengi alimtuhumu waziri (kwa kutaja cheo cha uwaziri wa Serikali ya Tz) basi anakuwa ameituhumu serikali.
Kwa hiyo Masha hapa anafanya kazi ya kuitetea Serikali hata kama aliyetuhumiwa si yeye......japo pia naona kwa upande wa pili aliyepaswa kuliongolea ni hili ni yule waziri aliyesuswa na media.

Mkuu,

Sasa Masha anapata wapi hayo mamlaka ya kumtaka Mengi athibitishe? Kwanza hiyo ingekua kazi ya IGP na DCI

Kwanza Mengi athibitishe nini yaani? So far waziri haja-specify kwamba Mengi anatakiwa athibitishe hili na lile.Kama kweli nae Masha yuko serious hebu ajaribu kuwa clear halafu aone mziki wake.

Huyu ni mojawapo wa Vilaza ambao Jk ameweka huko pamoja na akina Nchimbi,Malima amabae aliridhia karamagi kusaini makataba nje ya nchi.

This are bogus ministers from bogus institution
 
Hii kazi ya kutaka Mengi athibitishe tuhuma zake ilitakiwa ifanywe na polisi. Masha kama waziri hawezi kumpa ultimatum Mengi na hapa ndio inaonyesha wazi calibre ya mawaziri wa Jakaya; wengi hawana intergrity wala foresight!!Mengi kamtegea huyu fisadi na kweli kaingia mwenyewe kichwa kichwa na sasa ataipata fresh!!

Hapa umeangalia upande mmoja tu wa Mengi. Mengi kamtuhumu waziri. Hivyo kaituhumu serikali. Mmoja kati ya mawaziri wa serikali kwa kutumia chombo cha serikali kasema kuwa atamwandikia barua mengi athjibitishe usemi wake, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Usiwe biased dhidi ya Masha hata kama unamchukia.
Lakini vile vile Mengi asitumie vyombo vyake vya habari kulalamika kila wakati. Suala hili lilikuwa la kuripoti Polisi au kwa kiongozi wa ngazi za juu zaidi ya huyo waziri kulingana na taratibu za kisheria au kinidhamu.
Kulikuwa na haja gani ya taarifa kamili ya Mengi kutolewa tena baada ya taarifa ya habari juzi usiku? kwangu mimi Mengi anatumia vibaya vyombo vyake vya habari.
Kwa hili nawapongeza watu wa gazeti la Majira walivyotoa habari kuhusu kifo cha Mh. Nyaulawa, utadhani hakuwa mmiliki wa Majira. Simple.
 
Swali : Hivi ni nani aliyeanzisha uzushi huu? ..Nadhani ni Mengi... Awe mwanaume and see it to the end... He cannot just use his media outlets to trump up allegations na kukimbia? Let him substantiate his claims and see it to the end...

Weee Masha ukiumwa na Ruba weka tumbaku ndio litatoka, hivyo nenda mahakamani haraka na sio TBC
 
Kuna jambo la hatari sana kwa watu kutumia dhamana za vyeo vyao kutekeleza yaliyomo au yafurahishayo nafsi zao halafu kwa kutumia kodi zetu.

Huyo kilaza aliyependekeza Mengi abambikiwe kodi ili afilisike ana laana.Hivi hii ni akili gani hii? Kwa nini wasibambikiwe wezi kama akian Rostam Aziz,Manji,jeetu Patel,Mramba na akina Somaiya? au kwa vile Mengi anawamwagia msaada wasiojiweza huku akiiacha CCM solemba.

Tena hiyo Mengi ni cha mtoto,ngoja tukusanye nguvu za kuja kuiua CCM kabisa.Huyu mkuu kama ndiyo yeye basi itabidi aende exile na kama kweli ana uraia wa Marekani na apotelee huko.Tumechoka.


Unajua sometimes,sasa au baadae inabidi chama chochote kikichukua madaraka kiwe makini sana.Mijitu kama hii nikiona CCM imekufa leo nikaona inahamia chama chochote makini na ikapokelewa basi mimi nitaachana na Demokrasia na nitaingia msituni ili kutwaa mamlaka yatakayokufanya uliongoze taifa kwenye neema kama ilivyo Cuba na Libya.Hatutaweza kujirudisha nyuma hatua kumi
 
Haya ni matokeo ya uteuzi wa shukrani. Mr. M ameajiri mtoto wangu na binti wa mkuu wa nyumba ya SMZ ni lazima awe waziri hata kama hana sifa. Matokeo yake kusema ovyo; leo mauaji ya albino ni jambo dogo, kesho Mengi apewa siku saba!!! Mengi yanakuja.


Hapo umenena!!!! Uteuzi wa uswahiba huo regardless of hour mchapakazi one is!!!! Mambo ya IMMA Advocates hayo!!!!!
 
Hivi hii ultimatum ya Masha inaisha siku gani.... mana kuna weekend na sikukuu kibao mwanzo wa Juma?
 
Hiyo ni roho mbaya yao waliyo nayo hawa wakuu.Wanahisi kwamba Mengi anaichangia CHADEMA.Hizo ni hisia zao tu.Sasa hizo hoja zao ni za kitoto.

Kwanza Huyo masha yeye ndiye wa kupewa siku saba za kuthibitisha kwamba vyombo vya habari vinakuza mauaji ya Albino.Hapa ndipo pa kumkandamiza,hii hoja ya Albino tukii-twist left-right,Tutammaliza huyu fisadi maanke mimi ninavyomjua Masha akiwekwa Angle kwa hoja hawezi kujinasua
 
Kwani Masha yeye ni polisi. Hiyo ni kazi ya polisi awaachize wafanye kazi!


ndugu yangu we watakaojishuku watakuwa wengi sana ila kwa upande wa kuwa mapolisi hata sisi tunaweza kuwa mapolisi lakini tukitaka kupeleka watuhumiwa milango hatuionisasa we unafikiri hapo kuna nini tena........
 
Hapa JF Mengi, CHADEMA, na kikundi kingine ni UNTOUCHABLES, ukiwasema tu POST YAKO HAIPITI.

INAKERA.
 
Masha kazaliwa 1970 na kamaliza LLB (UD) 1991...ina maana aliingia UD akiwa 17 yrs old?

Hatari kweli !! Baada ya primary school unaenda miaka mitano kupata High School Diploma !!!

http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=423&vusername=GUEST")
 
Mkuu Kandambili,

Umeshaanza kuikandia JF sio? CHADEMA inasemwa sana na bado post zinakwuepo.Tujaribu kushindanisha hoja mkuu acha kulalamika
 
Hatari kweli !! Baada ya primary school unaenda miaka mitano kupata High School Diploma !!!

http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=423&vusername=GUEST")

hapo kuna jambo jipya,unless taarifa ziwe zimekosea. Au alidanganya umri? Hapa kuna kazi ya ziada inatakiwa.Huyu kilaza ni mpaka akome
 
hapo kuna jambo jipya,unless taarifa ziwe zimekosea. Au alidanganya umri? Hapa kuna kazi ya ziada inatakiwa.Huyu kilaza ni mpaka akome
Masha kasomea marekani primary na high school!huku alirudi kusoma 1STdegree pale UDSM!sasa hapa unashangaa nini?vitu vingine usimuonee Masha eti alidanganya Umri?jamani unaenda mbali sana sasa!
 
...hivi kuna sababu gani Waziri mzima kukurupuka na kuanza kutoa siku saba,hajapelekewa barua yeyote au malalamiko rasmi ni kaskia tuu kama sisi humu JF,kama mengi ana issue legit kuna utaratibu wa kufanya na alichofanya ni kama street talk tuu ambacho waziri hana sababu hata ya kujibu...Masha intergrity ni sifuri kazidi umalaya tuu na kutafuta ujiko kwa machangudoa,wizara yake ni kero kubwa kwa wananchi kuanzia uhamiaji mpaka polisi wa barabarani na kashindwa hata kuwalinda Albino...disgraceful masha must go na utatoka tuu!

Amekumbukia fani yake ya sheria jamani! Anawaza kutuma demand note ndio maana ametoa siku saba.
 
Kama wengi walivyochangia-mengi kasema ameshamsamehe huyo Mh kijana! Kwa hali ya kawaida hayo yameisha. Nashindwa kuelewa kuwa Mh msimamizi wa sera zetu za mambo ya ndani ,msomi, gen X, anapohangaika kujibu suala amabalo halipo tena-mengi kalifunga!!!! Taabu sana ndo maana Gen Powell alianza mbele kumwacha kwenye mataa Mcain kwa poor judgement !
 
- Mkuu umeongea machache sana lakini sijaona hoja, mambo ya usalama wa wananchi na viongozi yanamhusu waziri wa ndani, na ya waandishi wa habari yanahusu waziri wa habari.

- Na sidhani kama ni the ishu hapa!

Sawa kabisa mkuu. Lakini mimi nilidhani mwananchi akilalamika kuwa ametishiwa, anachotakiwa kufanya mwenye dhamana ya usalama wa wananchi ni kuchunguza na kumhakikishia aliyetishiwa usalama wake na si kumtaka athibitishe aliyotishia. naamini kama waziri mhusika angechunguza kuhusu vitisho hivi mwishowe angebaini kama ni vya kweli au vya kutungwa.
lakini kumtaka aliyetishiwa athibitishe, ni kumtega mkuu
 
Hebu msome kwa kutulizana, ama sivyo nyie ndio mnakuwa (as you like to put it) "wakurupukaji"

Mleta habari hapo juu amesema, "Nimesikia TBC leo asubuhi kwamba Mh. Masha kama Waziri wa Mambo ya Ndani amempa siku saba Mr Mengi athibitishe kauli alizo toa . Kazi imeanza."

Keyword, kama waziri wa mambo ya ndani....Hivyo, kutokana na habari hapo juu, Masha hajasema kuwa Mengi athibitishe maneno yale yametoka kwake.

Ama la, labda habari haijakuwa quoted kama ilivyokuwa reported. Slow your roles!

Hiyo ni kazi ya polisi na wala sio ya waziri wa mambo ya ndani. Masha leo kageuka polisi?

Kweli akina Mwakipesile ambao hawajui kikomo cha madaraka yao wako wengi.
 
- Mkuu umeongea machache sana lakini sijaona hoja, mambo ya usalama wa wananchi na viongozi yanamhusu waziri wa ndani, na ya waandishi wa habari yanahusu waziri wa habari.

- Na sidhani kama ni the ishu hapa!

FMES,

Sio kazi ya waziri wa mambo ya ndani kuchunguza tuhuma, hiyo ni kazi ya polisi.

Masha kumpa Mengi siku saba ina maana mbili, moja, anampa siku saba kabla ya yeye kama Masha kumburuza mahakamani. Kama sio kwa nia hiyo basi maana ya pili ni kuingilia madaraka ya polisi, kitu ambacho naamini ni makosa. Awaachie polisi wafanye uchunguzi wao.

Kazi za waziri wa mambo ya ndani sio kuchunguza tuhuma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom