Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Hebu msome kwa kutulizana, ama sivyo nyie ndio mnakuwa (as you like to put it) "wakurupukaji"

Mleta habari hapo juu amesema, "Nimesikia TBC leo asubuhi kwamba Mh. Masha kama Waziri wa Mambo ya Ndani amempa siku saba Mr Mengi athibitishe kauli alizo toa . Kazi imeanza."

Keyword, kama waziri wa mambo ya ndani....Hivyo, kutokana na habari hapo juu, Masha hajasema kuwa Mengi athibitishe maneno yale yametoka kwake.

Ama la, labda habari haijakuwa quoted kama ilivyokuwa reported. Slow your roles!

Tena Masha alisema anamwadikia barua leo, hivyo suala hilo sasa limechukuliwa kiserikali. na akaongeza kuwa kama siku saba zitaisha bila kuthibitisha hatua za kisheria zitachukiliwa dhidi ya Mengi.
 
masha kama waziri anayehusika na mambo ya ndani ana kila haki ya kuuliza hilo. Hapa hautishiwi usalama wa mtu mwingine bali mengi mwenyewe. Mengi ana kila sababu ya kutaja jina la huyo waziri aliyemtuhumu kwa vitisho.

vp kama yeye ndiye mshutumiwa?
Haki itatendekaje?
Mwanasheria mkuu wa serikali hapa ana nafasi gani ktk hili?
Dpp?
Igp?
Rpc?

He have been to law school but i guess he got stupid.hata kuongea kuongea kwa uangalifu kuhusu mauaji ya albino anashindwa licha ya kushindwa kudhibiti.
 
Tena Masha alisema anamwadikia barua leo, hivyo suala hilo sasa limechukuliwa kiserikali. na akaongeza kuwa kama siku saba zitaisha bila kuthibitisha hatua za kisheria zitachukiliwa dhidi ya Mengi.

- Haya ni kutimiza sheria tu ya jamhuri inavyotaka, Masha hawezi kujiuzulu eti kwa sababu Mengi ana tatizo na waziri flani kwenye serikali, thet is absurd, hapa ni kuruhusu tu sheria ikafuata mkondo wake, and I hope waziri wa ndani wa jamhuri yuko serious on this one!
 
Haya ni matokeo ya uteuzi wa shukrani. Mr. M ameajiri mtoto wangu na binti wa mkuu wa nyumba ya SMZ ni lazima awe waziri hata kama hana sifa. Matokeo yake kusema ovyo; leo mauaji ya albino ni jambo dogo, kesho Mengi apewa siku saba!!! Mengi yanakuja.

Kipindi kitakacho zungumzia sakata la maalbino kitarushwa hewani leo usiku kwenye Kipima-joto - ITV.
Will Masha be in the house?
 
Mengi hapaswi kumtaja mtu yeyote na sidhani kama serikali kupitia kwa waziri Masha ilipaswa kujibu tuhuma za Mengi kupitia kwenye Luninga, otherwise Masha katumia ule msemo wa 'mwaga mboga mie nimwage ugali'. Mheshimiwa waziri alipaswa amwandikie barua rasmi ya kiofisi (kama Waziri wa mambo ya ndani), na kama si yeye basi ni DPP au AG kumtaka athibitishe madai yake kimaandishi ikiwa ni pamoja na kutoa vielelezo. na hii isiwe ni kwa ajili ya kumtisha bali kupata ukweli na kumsaidia, ili raia huyu awe na haki yake ya Kuishi na kufanya kazi zake vizuri bila ya bughuza.

Kama Mengi alitaka simpathy, nadhani Masha hapa ameomba double simpathy, kwakuwa hisia za hofu ya Mengi zinaelekezwa kwake na watu wengi humu kwenye forum. Taratibu zipo, zifuatwe. At least Mengi alianzia Polisi.
 
Nakubaliana na hoja ya Kisura, hapa katika kumpa Mengi siku saba a' la Lyatonga style tatizo sio kana kwamba Mengi amaeongopa!! Problem inayowapata hawa mafisadi ni kwamba mbinu zao chafu walizodhamilia kumfanyizia Mengi zimegundulika[ kama wakina GUNINITA pia] sasa cha kufanya ni kutafuta jinsi ya kuweza kufahamu siri zao zimevuja vipi? Unafikiri Reginald atadivulge sources zake ?
 
Mengi you have our support in as far as we know you never mentioned anyone by name. Let Masha blow his head off.

kama kusupport ni hiari ya mtu na sema WEWE unampa support do not say OUR SUPPORT, wewe unawakilisha KIKUNDI GANI?????????

HUO NI UMBEA MTU MZIMA ANAKURUPUKA NA KUSEMA HOVYO, KAMA KILA MTU ATAKUWA NA TABIA HIYO NCHI ITAFIKA WAPI??????
 
- Cha muhimu ni kwamba sasa hili tatizo lita tatuliwa kisheria, to me that is the bottom line, mengine yote tisa. Pande zote husika zitapewa nafasi under sheria na Mengi ni lazima amtaje huyo waziri kama sheria itakavyodai huko mbele.
 
watu wenye limited access ya internet utawajua tu. siku nzima hukuwepo hapa halafu sasa hivi umeibuka na muda si mrefu utaondoka tena. wabeba maboksi utawajua tu...heheheheheeee

'Myonge mnyongeni, haki yake mpeni'. Jamaa amemsifia MMKJJ kuwa ana speed kali ya typing tena very analytical. Huu bado unasimama kuwa ni ukweli maana kuna watu sio wabeba mabox na wana net 24/7 lakini hawafiki hata robo ya speed ya Mzee. Mimi ni mmoja wa hao wa 24/7 najikuta mostily naishia kusoma nondo zikishuka, kuandika ni issue kwa sie wengine wetu.

Pia naamini wako wabeba mabox wanaochangia vizuri na haraka kuliko hata hawa wa 24/7.
'Its the contents that maters, not what one does' ndio maana tuna wachangiaji vilaza as well as best brains and its only the contents that can distinguish not the 'boxes' not the '24/7'.
 
Mkuu FMES, umeandika mengi lakini sijaona unachosema. Ninachotaka kujua ni taratibu zinazotumika serikali inaposhutumiwa. Ipo mifano na wa karibuni zaidi ni wa MwanaHalisi na HabariLeo.
MwanaHalisi lilipoandika habari za kuikashifu serikali, waziri aliyeliingilia hili alikuwa ni anayehusika na habari, si wa mambo ya ndani. Kumbuka ninachozungumzia hapa ni kukashifiwa serikali, si media iliyotumika kuikashifu serikali. Habari leo lilipolalamikiwa na Sendeka bungeni kwa kuwachafua baadhi ya wabunge, aliyetakiwa kutoa maelezo ni waziri wa habari na si waziri wa mambo ya ndani. Kwa nini katika hili, kama serikali iliyotuhumiwa ni ile ile, suala liingiliwe na waziri wa mambo ya ndanibadala ya yule tuliyemzoea kushughulikia masuala kama hayo?
 
He have been to law school but i guess he got stupid.hata kuongea kuongea kwa uangalifu kuhusu mauaji ya albino anashindwa licha ya kushindwa kudhibiti.

Hadi sasa yeye si mshutumiwa hadi hapo Mengi atakapotaja.
Its is too much to call someone stupid; so to say you can be the same may be.
 
- Kama nilivyosema jana, kwenye hili Mengi ameenda nje ya mstari hawezi kuanzisha serikali yake ndani ya serikali ya jamhuri, ameanzisha mwenyewe wakati kuna njia nchungu nzima angeweza kuzitumia kutatuta tatizo lake, mara mashehe mara waziri kesho itakua rais, it has to be stopped tena now.

- Taifa tunaongozwa na sheria, sio uhuni uhuni wa kukusanya habari za walevi mitaani na kuzigeuza dhana za kutishia walevi, mimi sinyiwi pombe na nina marafiki 75% wanaolewa kila siku, sasa nikijali maneno yao ya ulevi sitakua na rafiki hata mmoja. Kwenye kesi yake against Manji nilikuwa mmoja wa waliomtetea sana Mengi kwa wahusika wa uamuaji ile kesi kuwa anaonewa lakini not this time, kwa sababu this one yuko nje ya mstari tena out na ninaunga mkono kwa 100% any response kwa wale wote aliohusika na kuwarecord au kuwapiga video na picha wakiwa kwenye ulevi, kama ndio sababu ya claims zake against viongozi wa serikali.

- Priviledge ya kumiliki media au kuwa na uwezo wa kuandika kwenye vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na magazeti na mitandao haiwezi kuwa sababu ya wale wenye hizo access kuchafua majina ya wengine kuwa ni mafisadi na the rest of the story bila sababu wala ushahidi, hapa ndipo tunapomheshimu sana Dr. Slaaa, kwa kuweka mambo yote ya ufisadi kwa kalamu na ushahidi usiopingika.

- Masha hana sababu ya kujiuzulu kwa kusimamia kiapo chake kwa jamhuri, yaani kulilinda taifa kwa njia zote zilizopo chini ya uwezo wake kisheria, ni wajibu wa waziri wa ndani kuhakikisha kua wananchi hawabughudhiwi na viongozi au wananchi wengine, na wale wanaobughudhiwa ni wajibu wao kufikisha matatizo yao kwenye vyombo vya dola kwa ufumbuzi wa kisheria iwapo wanao ushahidi wa kisheria, kama sheria yetu inavyosema. Sasa anapotokea mwananchi yoyote mwenye kuamua kwenda kinyume na sheria zetu, regardless ya who he is serikali ni lazima isiamie sheria tena kwa nguvu zote ilizonazo.

- Ninarudia tena kwamba ni wajibu wa waziri wa ndani kusimamia mambo ya ndani bila ya kujali ni waziri gani anayetajwa au asiyetajwa, Mengi ni lazima afikishwe kwenye sheria na atoe ushahidi wake uliopatikana kisheria ili kuiridhisha sheria ya jamhuri, ambayo waziri wa sasa wa ndani amekula kiapo kuilinda kwa nguvu zake zote na uwezo wake wote. Tunaishi kwa kuongozwa na sheria sio uhuni uhuni wa kukurupuka kwenye public na tuhuma nzito kwa viongozi wetu wa juu kwenye media, ni kujaribu kuwatisha ili wasifanye kazi zao walizopewa na na sisi wananchi kwa mujibu wa sheria. Hata US sheria iko wazi kuwa ukilia moto kwenye sehemu kama ya cinema wakati moto hakuna, unachukuliwa hatua za kisheria tena kali sana, sasa hapa ni wajibu wa serikali yetu ya jamhuri ikiongozwa na waziri wa ndani ambaye ndiye kisheria mhusika mkuu kuhakikisha kuwa Mengi anapewa haki yake so is waziri aliyetajwa pia akipewa haki yake na pia kutulinda sisi wananchi wengine wa kawaida na viongozi in the future na this kind of Mengi's accusations, hakuna anayekataa haki za Mengi kulindwa na sheria, lakini ni lazima huheshimu sheria za jamhuri na utaratibu wetu wa kisheria.

- Ninamuunga mkono kwa 100% kitendo cha waziri wa ndani kumpa Mengi muda wa kutoa ushahidi wake kwa serikali, na pia kumpa waziri anayehusishwa nafasi ya kusema pia mbele ya sheria, na sheria iamue nani mwenye makosa kisheria na nani hana, lakini the important ishu ni kuhakikisha kua next time Mengi anakwenda kwenye vyombo vya sheria bdala ya media, hawezi kusema kua haviamini kwani vimewahi kumpa nafasi ya kujitetea na akashinda kesi, tena against waziri wa jamhuri, ni lazima Mengi ajifunze kupeleka malalamiko yake kwenye sheria, kama sheria inavyotaka.

- Wote sisi ni wananchi wa Tanzania, na hili taifa ni letu sasa tusitishane na hizi tabia mpya za kujifanya wanamapinduzi, kwa kutaka kulazimisha kwa nguvu hoja za kuwaita walioko kwenye power tuliowachagua kisheria kuwa ni mafisadi just because hatuwataki au tuna chuki zetu za binafsi, dawa ni kudai tu kwa nguvu kuwa ni mafisadi kwa sababu ni wimbo unaokubalika kirahisi na wananchi bila hata ushahidi ulio wazi, hili sio taifa la walevi au wajinga wajinga, tunazo sheria na ni lazima zitekelezwe kwa nguvu zote.

Hatuwapendi mafisadi, lakini ni lazima kuwa na ukweli juu ya uifisadi wao, na ni wajibu wa waziri wa jamhuri kulinda sheria, bila kujali kama ni Mengi au anybody.

Mungu Aibariki Tanzania.

FMES, umetoa maelezo mengi ya maana sana. Ila jambo moja ni dhahiri kuwa uhuru wa kujieleza ni wa kila Mtanzania. Mengi pia anayo haki ya kufanya hivyo. Kama alivyoeleza kwa kifupi jinsi uendeshaji wa vyombo vyake vya habari unavyofanywa, ni dhahiri kuwa kama kuna kilichoandikwa na chombo chake chochote na kumuudhi yeyote, basi sheria unazotaka zifuatwe zingeweza kuchukua mkondo wake kwa taratibu zilizopo kwa chombo kilichohusika kufanya hivyo, na si kwake binafsi.

Kwa wahusika kutotumia utaratibu wa kufuata mkondo wa kisheria kupata haki zao, vile vile Mengi anayo haki/sababu ya kutofuata mkondo huo. Labda akidhani kuwa kwa kuwaeleza wao moja kwa moja na kwa kueleza umma wa Tanzania moja kwa moja kuwa anazijua mbinu zinazopangwa dhidi yake, suala hili linaweza kuisha bila kusumbuana na masuala marefu na yenye gharama kubwa ya kisheria.

Ninahisi kuwa kumshinikiza kutaja au kuthibitisha kauli zake ni suala linalotakiwa kufanywa na taasisi husika za kiserikali badala ya wanasiasa. Nadhani pia kwamba, serikali ikitaka kupata maelezo kutoka kwake, ni vyema nao wakaacha kutumia vyombo vya habari kufanya hivyo. Maana, najua kuwa huo sio utaratibu wa kiserikali kushughulikia mambo.

Narudia, kila Mtanzania anayo haki ya kujieleza na kutoa dukuduku lake na hata kuelezea wasiwasi wake kuhusu usalama wake kwa njia yoyote anayoona inafaa.
 
- Kama nilivyosema jana, kwenye hili Mengi ameenda nje ya mstari hawezi kuanzisha serikali yake ndani ya serikali ya jamhuri, ameanzisha mwenyewe wakati kuna njia nchungu nzima angeweza kuzitumia kutatuta tatizo lake, mara mashehe mara waziri kesho itakua rais, it has to be stopped tena now.

- Taifa tunaongozwa na sheria, sio uhuni uhuni wa kukusanya habari za walevi mitaani na kuzigeuza dhana za kutishia walevi, mimi sinyiwi pombe na nina marafiki 75% wanaolewa kila siku, sasa nikijali maneno yao ya ulevi sitakua na rafiki hata mmoja. Kwenye kesi yake against Manji nilikuwa mmoja wa waliomtetea sana Mengi kwa wahusika wa uamuaji ile kesi kuwa anaonewa lakini not this time, kwa sababu this one yuko nje ya mstari tena out na ninaunga mkono kwa 100% any response kwa wale wote aliohusika na kuwarecord au kuwapiga video na picha wakiwa kwenye ulevi, kama ndio sababu ya claims zake against viongozi wa serikali.

- Priviledge ya kumiliki media au kuwa na uwezo wa kuandika kwenye vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na magazeti na mitandao haiwezi kuwa sababu ya wale wenye hizo access kuchafua majina ya wengine kuwa ni mafisadi na the rest of the story bila sababu wala ushahidi, hapa ndipo tunapomheshimu sana Dr. Slaaa, kwa kuweka mambo yote ya ufisadi kwa kalamu na ushahidi usiopingika.

- Masha hana sababu ya kujiuzulu kwa kusimamia kiapo chake kwa jamhuri, yaani kulilinda taifa kwa njia zote zilizopo chini ya uwezo wake kisheria, ni wajibu wa waziri wa ndani kuhakikisha kua wananchi hawabughudhiwi na viongozi au wananchi wengine, na wale wanaobughudhiwa ni wajibu wao kufikisha matatizo yao kwenye vyombo vya dola kwa ufumbuzi wa kisheria iwapo wanao ushahidi wa kisheria, kama sheria yetu inavyosema. Sasa anapotokea mwananchi yoyote mwenye kuamua kwenda kinyume na sheria zetu, regardless ya who he is serikali ni lazima isiamie sheria tena kwa nguvu zote ilizonazo.

- Ninarudia tena kwamba ni wajibu wa waziri wa ndani kusimamia mambo ya ndani bila ya kujali ni waziri gani anayetajwa au asiyetajwa, Mengi ni lazima afikishwe kwenye sheria na atoe ushahidi wake uliopatikana kisheria ili kuiridhisha sheria ya jamhuri, ambayo waziri wa sasa wa ndani amekula kiapo kuilinda kwa nguvu zake zote na uwezo wake wote. Tunaishi kwa kuongozwa na sheria sio uhuni uhuni wa kukurupuka kwenye public na tuhuma nzito kwa viongozi wetu wa juu kwenye media, ni kujaribu kuwatisha ili wasifanye kazi zao walizopewa na na sisi wananchi kwa mujibu wa sheria. Hata US sheria iko wazi kuwa ukilia moto kwenye sehemu kama ya cinema wakati moto hakuna, unachukuliwa hatua za kisheria tena kali sana, sasa hapa ni wajibu wa serikali yetu ya jamhuri ikiongozwa na waziri wa ndani ambaye ndiye kisheria mhusika mkuu kuhakikisha kuwa Mengi anapewa haki yake so is waziri aliyetajwa pia akipewa haki yake na pia kutulinda sisi wananchi wengine wa kawaida na viongozi in the future na this kind of Mengi's accusations, hakuna anayekataa haki za Mengi kulindwa na sheria, lakini ni lazima huheshimu sheria za jamhuri na utaratibu wetu wa kisheria.

- Ninamuunga mkono kwa 100% kitendo cha waziri wa ndani kumpa Mengi muda wa kutoa ushahidi wake kwa serikali, na pia kumpa waziri anayehusishwa nafasi ya kusema pia mbele ya sheria, na sheria iamue nani mwenye makosa kisheria na nani hana, lakini the important ishu ni kuhakikisha kua next time Mengi anakwenda kwenye vyombo vya sheria bdala ya media, hawezi kusema kua haviamini kwani vimewahi kumpa nafasi ya kujitetea na akashinda kesi, tena against waziri wa jamhuri, ni lazima Mengi ajifunze kupeleka malalamiko yake kwenye sheria, kama sheria inavyotaka.

- Wote sisi ni wananchi wa Tanzania, na hili taifa ni letu sasa tusitishane na hizi tabia mpya za kujifanya wanamapinduzi, kwa kutaka kulazimisha kwa nguvu hoja za kuwaita walioko kwenye power tuliowachagua kisheria kuwa ni mafisadi just because hatuwataki au tuna chuki zetu za binafsi, dawa ni kudai tu kwa nguvu kuwa ni mafisadi kwa sababu ni wimbo unaokubalika kirahisi na wananchi bila hata ushahidi ulio wazi, hili sio taifa la walevi au wajinga wajinga, tunazo sheria na ni lazima zitekelezwe kwa nguvu zote.

Hatuwapendi mafisadi, lakini ni lazima kuwa na ukweli juu ya uifisadi wao, na ni wajibu wa waziri wa jamhuri kulinda sheria, bila kujali kama ni Mengi au anybody.

Mungu Aibariki Tanzania.

Ndugu maandishi yote haya unaongea kitu cha kujirudia rudia.

Pili kwani nani hapa hataki ushahidi,nadhani sote tunataka na pia tunataka kumjua huyo waziri kijana ikitajwa bila sisi kunganisha dot kwa guess work tunazofanya.
Ila swali linakuja itakuwaje akiwa mhusika ni waziri wa mambo ya ndani(Masha)?
Hapa nadhani tuko kwenye kujadili zaidi ya ku take side.

Je wewe usingipenda kusikia mtu kama RPC akisughulikia hili, mimi naona kidogo ingekuwa pina.Tena si amepeleka polisi hii habari au maana hapa hapasomeki vizuri taharifa zingine polisi wanadai hawana habari!

Kijana anaonekana kunasa kwenye mtego wa nungunugu
 
Kwa nini katika hili, kama serikali iliyotuhumiwa ni ile ile, suala liingiliwe na waziri wa mambo ya ndanibadala ya yule tuliyemzoea kushughulikia masuala kama hayo?

- Mkuu umeongea machache sana lakini sijaona hoja, mambo ya usalama wa wananchi na viongozi yanamhusu waziri wa ndani, na ya waandishi wa habari yanahusu waziri wa habari.

- Na sidhani kama ni the ishu hapa!
 
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w z y z, they are 26 one to one letters. For this reason, Masha's term should be once. Hafai hata kwa kuongoza familia yake imejaa matatizo kibao. Kazi machangudoa tu. Hivi pale Rose Garden ameshahamisha kijiwe??? Linakunywa hadi linakaa juu ya meza ili watu walione na utumbo wake!!! Hana calibre huyo. Kwanza anajidai anatishia raia na silaha huyu. Kwanza hata ukimwangalia tu physically kwa wale mlio wataalam wa Psychology, jamaa anaonekana incompetent in every aspect except ngono na sampuli za wanawake. Mwambieni atutafute na sisi tunaomripoti huku kwenye blogs mbalimbali atutafutie visa.

Kwa hakika ni kwamba mafisadi wanatafuta vibaraka wa kuwatumia ili kuhakikisha wanawamaliza wale wote wanao habarisha kuhusu ufisadi wao. Hapo sio Mengi tu. Mafisadi wamepanga kuwamaliza wote one after another, kuanzia serikalini na watu binafsi. So ni wakati wote tunaojua tunapinga ufisadi tutembee kwa machale na kuwa waangalifu na marafiki wa ghafla wanaojitokeza kama alivyojitokeza Deus Malya kwa marehemu Wangwe. Please, watch out!!!! From my heart Mengi watch out and the Editors too. Ni hayo tu.
 
Ndugu maandishi yote haya unaongea kitu cha kujirudia rudia.

Pili kwani nani hapa hataki ushahidi,nadhani sote tunataka na pia tunataka kumjua huyo waziri kijana ikitajwa bila sisi kunganisha dot kwa guess work tunazofanya.
Ila swali linakuja itakuwaje akiwa mhusika ni waziri wa mambo ya ndani(Masha)?
Hapa nadhani tuko kwenye kujadili zaidi ya ku take side.

Je wewe usingipenda kusikia mtu kama RPC akisughulikia hili, mimi naona kidogo ingekuwa pina.Tena si amepeleka polisi hii habari au maana hapa hapa someki vizuri

- Ni haki yangu kutoa mawazo yangu kama ilivyo yako, Mengi ametuhumu waziri sasa ishu inakuwa ni waziri level sio RPC, kwani waziri hajui hizo sheria?

Later saa ya kibarua!
 
Swali : Hivi ni nani aliyeanzisha uzushi huu? ..Nadhani ni Mengi... Awe mwanaume and see it to the end... He cannot just use his media outlets to trump up allegations na kukimbia? Let him substantiate his claims and see it to the end...
 
kama kusupport ni hiari ya mtu na sema wewe unampa support do not say our support, wewe unawakilisha kikundi gani?????????

Huo ni umbea mtu mzima anakurupuka na kusema hovyo, kama kila mtu atakuwa na tabia hiyo nchi itafika wapi??????

wewe vp raia nalalamika unauliza anayemsupport nani sisi;mimi huyo unayemuuliza na wengine!

Tunachukulia madai yake ni ya ukweli mpaka pale atakaposhindwa kuthibitisha.

Akijulikana ni mwongo tutaomba apewe adhabu kwa mdili wa sheria

na mimi nashupalia sheria ifuate mkondo wake ,kama aliropoka itakuwa lesson.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom