Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Mlalahoi
naona unalazimisha mada hii ionekane ya udini hapa tunajadili mustakabali wa nchi yetu. na mimi ndio nilioanzisha mada hii kwa kutaraji uchambuzi yakinifu.
naona mara unaiita JIHAD mara Mujahidina move.
tafadhali usivuruge mada.
binafsi siko kwenye udini
labda wewe ambaye ulipoanza kuchangia mada ya matatizo ya taifa umenukuu Biblia na upendo na hakuna aliyekuja juu na kusema hiyo ni crusade.
mimi nimekuwa nachangia sana kwenye mada ya Mzumbe ambapo nimekuwa nikimfagilia DR. Warioba dhidi ya DR.Assad Mussa na pia timu nzima ya lecturers wa Mzumbe ninao watetea hakuna muislam.
pili nimepinga Lowassa kutoa milion 60 kwa mufti kuwa ni pesa nyingi sana.
Tatu- nimempiga vijembe Mpemba na mada yake ya Balozi LONDON ambaye kwa vyovyote ni muislam.
Sasa kama unafutilia vyema ktk hii mada hakuna neno jihad nimeweka au Tafiti THEN Jadili sijaona kuchangia hivyo. tafadhali sana naomba kama huna cha kuchangia acha au anzisha mada inayohusu mujahidina.kwani hapa tunatumia muda na pesa kujadili maslahi ya nchi
 
Nungwi
Heshima yako mkuu .Bada ya hili la Mengi na pesa za UN turafukua mambo mengine .Mengi ni mzalendo lakini hatutaki kumpa support wakati anatuibia na kutuhadaa yeye na familia yake wanaishi peponi .Mengi baada ya hili kujulikana kuna mengi tutahoji .Pia baada ya hili tutamuomba Mzee Manumba atueleze nini amepata kuhusiana na watu kugushi na kuitwa ma Dr.Mbona kakalia habari hizi na muda unaenda ?
 
Nungwi!

Keep it up! we have no time to waste on udini and the like. Being the elite of the country, lets discuss burning issues of our society.
 
nungwi said:
pole mkuu Fikiraduni
mimi bado niko msituni ila nasikia kuna file la mheshimiwa Mengi limeanza kushughulikiwa na DCI Manumba ambalo uchunguzi wake ulianza mwaka jana November na IGP Mahita alisimama kidete kuzuia huo uchunguzi. sasa Manumba analifuatilia ila nazidi kuchimba hilo file linahusuana na nini kama huu mlungula ya UN au usanii mwingine? jamani mwenye data zaidi anisaidie.
na watu wangu pale Mambo ya ndani wamesema nisubiri kidogo kwani wanajipanga.
ila haitachukua siku mbili.
Duh kumbe ndo maana siku ile ya ufunguzi wa msikti kule wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mzee Mengi alikuwa bega kwa bega na IGP mstaafu na ikasemwa kama Mengi amechangia sh Mill 40! kwenye ujenzi wa msikiti huo ambao inasemekana ilikuwa ni initoative za Mahita.Hii ilikuwa ni katika pita ya Mahita pale wilayani wakati wa harusi ya jama yake Adadi Rajabu Mahita akaona kama msikiti haukuwa uko katika hadhi nzuri...sasa kumbe ndo aka turn back kwaba Mengi kwa msaada zaidi.
Basi inaonekana kama huyu Mengi ni fundi mzuri wa ku lobi..lakini inasikitisha maana nyumba ya ibada ijengwe kwa mijipesa ya kimazabe na ya ahsante.Sijui waislamu wenyewe wakiisikia hii watasemaje. Bado tunayaweka wazi masikio yetu tusikia mengi ya Mengi huyu, amakweli MENGI ana MENGI ni huyu huyu ambaye pia inasemwa kama ni rafiki wa kila mtu,walemavu,waislamu...duh
 
Mengi ni Mtanzania jasiri na tena ni shujaa, ninakumbuka alivyopambana na waziri wa manjago, Masilingi kuhusu rushwa kwenye kuuziwa wageni hoteli ya Kilimanjaro,

yes, huenda ana some "Problems", lakini the man amefanya mengi mno mazuri kwa taifa, na hasa wananchi na yes, may be unahitaji kuwa kama alivyo ili kuweza kuwa na biashara kama zake kule bongo,

I stand with Mengi!
 
mzee ES,
kwa hili la Manji na lile la Masilingi hata mimi ninaona Mengi is Superb.

Mengine kama lile la Mabilioni ya fedha za wagonjwa Ukimwi? zilizopitia NBC, hapo sina clue!
 
Na mimi nawaunga wale wanaomtetea Mengi! Jamani kwani kosa kubwa alilofanya ni lipi? Kwa nini sisi tunapenda kuongelea sana rushwa lakini mtu kama Mengi akija na gazeti lake na kuandika hayo maovu,watu hawaoni kilichoandikwa ila wanamuona yeye tu! KIlichoandikwa watasema anng'ang'ania hapohapo tu,hana jipya.
Mengi si kafika pale kwa juhudi zake mwenyewe,alianza kwa 'kusokota' peni yeye na mkewe,baadae akatuleletea zile sahani za plastic,then colgate,revola.. etc,na hii biashara ya usambazaji wa hizi colgate umetajirisha sana wahindi,mmoja wao ni Tanna Somaiya,mmiliki wa Shivacom...yeye likuwa ni msambazaji mkuu wa hizo products mikoani,sasa hivi(kwa wale ambao hawamjui) ndio anayeprint na kusambaza voucher za Vodacom,ni tajiri wa kupindukia!
Lets give credit where its due!Jamani huyu ndie mwenye kiwanda cha Coca Cola kilichochaguliwa ni bora Africa South of Sahara bar South Africa!
Hakuna anaye pinga kuwa naye anajisababishia matatizo mengi,but that doesnt hide the fact kuwa he has been very succesful in his endevours.Mimi sidhani kuwa hapa kuna mtu anamsifu Mengi kwa sababu ni mweusi,au mzawa tu,bali kama Mengi,hata kama angekuwa ni muhindi!Anasaidia walemavu,yatima kaanzisha hospitali ya matatizo ya moyo n.k. Hio kesi yake na Malima kwa kifupi ni kuwa kishahukumiwa,kwa sababu kwanza wabunge hawawezi kumtema mmbunge mwenzao hata siku moja,na pili huyo Manji ana pesa ya mchezo,sioni atashindwa nini kumwaga pesa huko kwa hao wabunge ili wammalize kabisa.
 
nungwi said:
Mlalahoi
naona unalazimisha mada hii ionekane ya udini hapa tunajadili mustakabali wa nchi yetu. na mimi ndio nilioanzisha mada hii kwa kutaraji uchambuzi yakinifu.
naona mara unaiita JIHAD mara Mujahidina move.
tafadhali usivuruge mada.
binafsi siko kwenye udini
labda wewe ambaye ulipoanza kuchangia mada ya matatizo ya taifa umenukuu Biblia na upendo na hakuna aliyekuja juu na kusema hiyo ni crusade.
mimi nimekuwa nachangia sana kwenye mada ya Mzumbe ambapo nimekuwa nikimfagilia DR. Warioba dhidi ya DR.Assad Mussa na pia timu nzima ya lecturers wa Mzumbe ninao watetea hakuna muislam.
pili nimepinga Lowassa kutoa milion 60 kwa mufti kuwa ni pesa nyingi sana.
Tatu- nimempiga vijembe Mpemba na mada yake ya Balozi LONDON ambaye kwa vyovyote ni muislam.
Sasa kama unafutilia vyema ktk hii mada hakuna neno jihad nimeweka au Tafiti THEN Jadili sijaona kuchangia hivyo. tafadhali sana naomba kama huna cha kuchangia acha au anzisha mada inayohusu mujahidina.kwani hapa tunatumia muda na pesa kujadili maslahi ya nchi

Usinunue kesi isiyokuhusu.I was responding to Tafiti Then Jadili,not you.How long has this topic been going on and none of you accusers has been able to come with at least a little piece of evidence to substantiate whatever case you have against Mengi?It just sounds like one rumour after another.

As to why I related Tafiti then Jadili's arguements to a jihadist agenda,you need to go to Darhotwire forum to see why did I say that.To make the task easier for you,Tafiti's points were more or less the same with those made by a known mujahidina who contributes regularly in Darhotwire.Sheer coincidence?May be not.

Mnajua mnachokifanya ni kitu kilicho wazi.It's Mengi,not UNAIDS or NBC,waliolalamika kuhusu fedha hizo.Mengi responded to the report kuwa kuna watu wametumia jina lake kuchukua fedha hizo.Pia ifahamike kuwa tukio hilo halikutokea kwa ghafla bali ni process ya miezi minane.Unless someone wants to say that Mengi was trying to take precautions,he did exactly you and I would have done should we be associated with some unscrupulous characters:report the matter to the bank,UNAIDS and Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai.

Mimi nilishaachana na topic hii,kwa vile hardly do I like to involve myself in discussions on matters arising from hear-says.Katika jamii inayothamini utawala wa sheria ninaamini kuwa Mengi is innocent until proven guilty,na badala ya kuendelea na porojo za "nimesikia...nimeambiwa..." ni vema ukaletwa uthibitisho kuhusu tuhuma dhidi yake.Ikumbukwe kuwa "walioibiwa na Mengi (UNAIDS)" ni taasisi ya kimataifa ambayo pengine ina uchungu na fedha zake zaidi ya wewe unaelalamika.Sasa hao sio wapumbavu kiasi cha kumwacha Mengi atokomee na mabilioni yao bila kujishughulisha kumchukulia hatua zinazostahili.Sitetei "ujambazi" bali ugomvi wangu ni hoja ambazo siku nenda siku rudi hazithibitiki.
 
Naam nillipotea kwa muda kutokana na mambo ya hapa na pale na nashukuru nimerejea na kukuta a fair amount of relevant information na watu kurejea katika topic... this is good.

Ndugu yangu katika mapenzi ya nchi yetu Mlalahoi, naona niweke mstari mmoja kukuhusu wewe hapa kwa vile naona umekuwa ukiniandama sana na kila sehemu unaweka jina langu, na kulaumu kuwa kuna ''mada maalum'' huwa nachangia...

Well sijui hii fikra potofu uliyonayo kuhusu uhusiano wangu na jihadist comments umetoa wapi, i have never knowingly let religion of anybody here or in the subjects/personalities i discuss bias me in my views. I never form opinion based on peoples religion/tribes or anything bali maoni yangu hapa na uchambuzi wangu hapa unabase zaidi katika utendaji wa mtu,taasisi au kampuni husika na wachangiaji wa humu ndani nawaheshimu kwa maoni yao sio kwa kuangalia dini zao, beside mtu akijiita Nungwi au Kulikoni, Fikiraduni, Mugishagwe au for that wewe mlalahoi utajua kweli dini yao? ni vigumu lakini unaweza kupata clues kutokana na kauli na michango yao, sasa usichukue njia ya mkato katika mjadala ya kumjadili mjumbe badala ya ujumbe. Sishangai kwa nini unaniandama mimi manake kama alivyowahi kutamka rafiki yangu Mbowe ''MTI WENYE MATUNDA NDIO UNAOPIGWA MAWE''

Nimeona nikuweke sawa katika hizi prejudices zako kabla sijarejea katika mjadala, nashauri kama una bifu na mimi kumewekwa private messages hapa tumia hiyo tutawasiliana, nimeona katika pahala flani upo hapa UK basi tuwasiliane kwa private messages huko tunaweza hata kuonana ana kwa ana!

Wajumbe wengine mniwie radhi kwa haya lakini kwa faida ya wote niliona nimuwekee hii tanabahi mapema ili kuclarify his misleading remarks against me...

Naam sasa tunaingia katika mjadala wetu wa Mengi:

-Huyu mzee nimekuwa na heshima nae kubwa sana kwa muda mrefu sana kutokana na jinsi anavyojiprotray as mtu mwema na mwenye kupenda disavantaged individuals kama vile walemavu na hata walio wazima ambao hawana uwezo wa kujisupport ipasavyo...yes ni kweli anayoyafanya in terms of his corporate image ni mazuri sana na yanabenefit jamii, hapa London kuna watu wangu wa karibu sana nawafahamu walikutana nae for the first time Heathrow Airport mzee Mengi akiwa nae anawasili wale vijana wakaenda kumsalimia mzee tumekuona tumeona tukujulie hali, alifurahi sana kuonana na watanzania wenzie na akasema mniwie radhi sina kitu kikubwa mfukoni lakini hizi zinaweza kuwasaidieni, hapo hapo akatoa paundi mia tatu kwa wale vijana!

Vijana walikuwa na mwenzao Mlemavu aliekuwa akifanya masters hapa wakamueleza mzee Mengi kuwa kijana anastruggle na ada, mzee akachukua contacts zao na kuahidi kufuatilia, baada ya muda kurejea dar akawapigia vijana simu na kutaka details za chuo alipe ada!

Huo ni upande mmoja wa mengi ambao unatia moyo lakini hapa kwa vile tumepose maswali yanazunguka kadhia nzima ya mabilioni ya shilingi zilizotumiwa na wajanja wachache ambazo binafsi naamini inawezekana ikawa sio mengi bali nae alikuwa lazima aisaidie polisi, haitoshi kusema tu through press release kwamba kuna watu wametumia jina langu...naweka masahihisho hapa kwa taarifa ya mjumbe mmoja kuwa amewaarifu polisi, NO ripoti haikusema hivyo...wala pia haikusema kwamba eti mzee ameripoti kwa Manumba, Mengi ameshawahi kunukuliwa na gazeti lake la THIS DAY akimlaumu Manumba kuwa ''anatumiwa'' na Manji..

Tena kwa kulitaja gazeti hili linalosifiwa sana humu maswali mengine yananijia:

-Hivi inawezekana kweli kama Mengi hakuhusika na kashfa hii ya mabilioni ya fedha [takriban sawa sawa na mabilioni ya kwenye episode yao ya NSSF] gazeti hili likae kimya tu bila kutaka kuingia kwa undani zaidi kutaka ku-uncover the truth na that way kum-exonerate mwajiri wao?

-Naomba niweke sawa kauli hiyo hapo juu ieleweke vizuri... mtu ambae ameanzisha gazeti ambalo lina sifa ya kuwa ni investigative paper na linaonekana na baadhi kama ni serious katika kazi hiyo, halafu atokee mtu/au kikundi cha watu ambao wanatumia jina la mwenye gazeti kujipatia mabilioni ya shilingi, kisha waandishi wa investigative paper wasiulize chochote wala kufutatilia..badala yake wanaweka tu press release ya bosi kisha basi!! HAINGII AKILINI...

Hii habari ni explosive kwa kweli na kama alivyowahi kusema na nikamkariri Mugishagwe ni kuwa kuna deep flaws katika fani ya uandishi wa habari tanzania, haiwezekani mwandishi worth his salt asome hii habari na kisha asifuatilie chochote wakati hapa kungekuwa na a lot of credits na kuliokoa taifa na matapeli wachache.

--Mengi ni mfanyabiashara mahiri na wa muda mrefu ambae anaweza kusifika kwa jinsi alivyohodari wa kusafisha his corporate image lakini I am afraid sipo pamoja na wale ambao wamepublicly declare kwamba they stand by him kwa sababu ameshahusika na kashfa nzito nzito ambazo zinafanya mchango wake kijamii kuwa peanut.

Nungwi:

Hiyo issue ya Manumba, my version ni kuwa anadaiwa na TRA 6 bilioni in terms of unpaid taxes ambazo jamaa walikuwa wanaclose in katika kuipeleka kesi katika mahakama ya madai CIVIL COURT ambayo ilikuwa ni normal kuwa wangemdai hizo pesa au wamfilisi to that tune lakini akasubmit baadhi ya returns ambazo zilikuja kugundulika kuwa ni forgeries ikabidi kesi hiyo iende anti fraud squad [wakati huo IGP ni Mahita] sasa Mahita akazuia uchunguzi usifanyike, faili hilo lilikwenda pia kwa DCI [adadi rajabu], mengi akalainisha njia kwa kuchangia hayo mapesa kwenye msikiti uliopo kijijini kwa adadi rajabu ambao ndio huo na mahita alikuwa mhusika.

Wameingia kina Manumba na Saidi Mwema, kesi imefufuliwa na TRA wanaclose in kwa upande wa madai yao ya bilioni sita!

Ndio maana sasa hivi Mengi ameshamlalamikia Manumba publicly wakati wa sakata yake na Manji... Sidhani kwamba Manji amewabankroll hawa watu kumsakama mengi bali ni Mengi mwenyewe ambae anajiponzea ana madeni mengi sana.

Nafuatilia sakata ya Mengi na kaka yake anaitwa Benjamin ameshirikiana na Felix Mosha kumpa PI British national. Wamemzika pounds 3.5 milioni. Suala hili limeandikwa katika magazeti ya UK na limejadiliwa kwenye House of Commons, mtaisoma hapa hapa...
 
Tafiti,
Good to see you again. Hata mimi nimesikia kidogo juu ya sakata hilo la Benjamin. Kwa hiyo nasubiri data kwa hamu.
 
Naona wakina Mengi wanajitahidi kurudisha kile kilichochotwa na 'Wawkezaji' kwi kwi kwi.
 
Mafuchila,
Lakini kama nilichosikia ni kweli, hapa wamefanya uharamia mbaya sana. Walimkaribisha mwekezaji washirikiane, akaja na fedha zake, tena nyingi tu, baadaye wakamzushia sakata. Tusubiri Tafiti alete data zaidi.
 
Huyu Professor Kapuya alibakiwa na nini kichwani mwake?

Leo nimesikia kuwa kuna udini wa hali juu NSSF! ninasikia kama wewe si muislam kufanya kazi NSSF ni kazi NGUMU SANA? JE NI KWELI?

NA HAYA YOTE YALISABABISHWA NA PROFESSOR JUMA KAPUYA WAKATI AKIWA WAZIRI KAZI NA RAFIKI YAKE GAU!

HUYU KAPUYA MWAKA 1995 ALIKUWA NA MALENGO YA KUGOMBEA URAIS LAKINI ALISHINDWA! NA ALIANZA KUTAKA KUTUMIA UDINI! SASA KAMA HOTUBA YA KIKWETE YA JANA HUKO HARVARD UNIVERSITY SI KIINI MACHO AU KAITOA MOYONI TUNAOMBA AMMLIKE HUYU MTU!

WATU WA AINA HII NI WA KUOGOPA KAMA UKOMA/UKIMWI. ANAWEZA HATA KUVUIVURUGA JWTZ HUYU!

WATU WANAOUTUMIA DINI KUTAFUTA VYEO AU UMAARUFU NI WAPUMBAVU WAKUBWA! JAMII YETU HAINA MUDA NA WATU HAO HATA KIDOGO. SOTE WAISLAMU NA WAKRISTU NI WATU WAMOJA TENA WAAFRIKA AMABO HATUKUWA NA DINI BEFORE ILA ZETU ZA JADI!. NA HILI MWALIMU ALIFANIKIWA KUTUUNGANISHA. HAWA WAPUMBAVU WACHACHE WANAOTAKA KUTUMIA DINI KUWAGAWA WATANZANIA TUKIWAACHA WATATURUGA SANA!
 
Jasusi nimekusikia Mkuu,
Ni kweli kabisa inasikitisha sana, lakini si ndio wahenga wanasema "Nyuma ya utajiri wa kupindukia, kuna uharamia wa kutisha" Tatizo kubwa la utajiri wa mwafrika hauwezi kupata historia yake, natumaini taratibu tutabadirika.
 
MLALAHOI
Jihad maana yake juhudi yeyote.

Na Mujahina ni mwenye kujitahidi hiyo ndio tafsiri ya maneno hayo kwa kiarabu.

sioni mjadala huu kuuhusisha na maneno hayo kama ni vita. ila hata wewe unapojitadi kusoma hiyo ni Jihad.

Kwa kazi yako na kitengo kikubwa ulichopo na mjadala huu kuiita rumours nashindwa kukuelewa.
Au kwa vile kaguswa madau mkubwa wa Field yako?
pia mtu kama wewe kuwa na chuki na mambo ya udini kiasi hicho haipendezi au kwa vile unatoka mkoa wenye Madhehebu mengi ya kikristu hapa Tanzania?

Kwa wanabodi endeeleni kuenzi hii forum kwa ujumbe unafika kwa walengwa mimi nilikuwa napita sikujua kama akina Mlalahoi nao wanapita.

Keep it up, Es,FD,tafiti,Zanaki na wote mliopo bila kumsahau Admin. hiki chombo kinasaidia kuyaona au kuyasema ambayo hatungeweza kuyajua.

Mimi ni muislam lakini sipo hapa kumtetea Mahita kisa muislam kwa mantiki hiyo wasitokee watu wakasema JIHAD AGENDA ili kuyaficha maovu yanayorudisha nchi nyuma wao wameshindwa kuyaanika kwenye vyombo vyao(Mlalahoi).

Mafuchila sielewi kama mada ya Kapuya inahusiana na huu mjadala nadhani ungeiweka kwenya NSSF, MENGI NA MANJI ila hayo ni maoni yangu ili tuchangie vizuri huko au ukaiweka mada inayojitegemea mimi ninao mengi hapo
 
mswahili said:

Nafahamu sana nini maana ya jihad.In its simplest term ni kama hayo anayofanya Dau hapo NSSF.
 
Huyu Professor Kapuya alibakiwa na nini kichwani mwake?

Leo nimesikia kuwa kuna udini wa hali juu NSSF! ninasikia kama wewe si muislam kufanya kazi NSSF ni kazi NGUMU SANA? JE NI KWELI?

NA HAYA YOTE YALISABABISHWA NA PROFESSOR JUMA KAPUYA WAKATI AKIWA WAZIRI KAZI NA RAFIKI YAKE GAU!

HUYU KAPUYA MWAKA 1995 ALIKUWA NA MALENGO YA KUGOMBEA URAIS LAKINI ALISHINDWA! NA ALIANZA KUTAKA KUTUMIA UDINI! SASA KAMA HOTUBA YA KIKWETE YA JANA HUKO HARVARD UNIVERSITY SI KIINI MACHO AU KAITOA MOYONI TUNAOMBA AMMULIKE HUYU MTU!

WATU WA AINA HII NI WA KUOGOPA KAMA UKOMA/UKIMWI. ANAWEZA HATA KUVUIVURUGA JWTZ HUYU!

WATU WANAOUTUMIA DINI KUTAFUTA VYEO AU UMAARUFU NI WAPUMBAVU WAKUBWA! JAMII YETU HAINA MUDA NA WATU HAO HATA KIDOGO. SOTE WAISLAMU NA WAKRISTU NI WATU WAMOJA TENA WAAFRIKA AMABO HATUKUWA NA DINI BEFORE ILA ZETU ZA JADI!. NA HILI MWALIMU ALIFANIKIWA KUTUUNGANISHA. HAWA WAPUMBAVU WACHACHE WANAOTAKA KUTUMIA DINI KUWAGAWA WATANZANIA TUKIWAACHA WATATURUGA SANA!
 
Mkira said:
Huyu Professor Kapuya alibakiwa na nini kichwani mwake?

Leo nimesikia kuwa kuna udini wa hali juu NSSF! ninasikia kama wewe si muislam kufanya kazi NSSF ni kazi NGUMU SANA? JE NI KWELI?

NA HAYA YOTE YALISABABISHWA NA PROFESSOR JUMA KAPUYA WAKATI AKIWA WAZIRI KAZI NA RAFIKI YAKE GAU!

HUYU KAPUYA MWAKA 1995 ALIKUWA NA MALENGO YA KUGOMBEA URAIS LAKINI ALISHINDWA! NA ALIANZA KUTAKA KUTUMIA UDINI! SASA KAMA HOTUBA YA KIKWETE YA JANA HUKO HARVARD UNIVERSITY SI KIINI MACHO AU KAITOA MOYONI TUNAOMBA AMMLIKE HUYU MTU!

WATU WA AINA HII NI WA KUOGOPA KAMA UKOMA/UKIMWI. ANAWEZA HATA KUVUIVURUGA JWTZ HUYU!

WATU WANAOUTUMIA DINI KUTAFUTA VYEO AU UMAARUFU NI WAPUMBAVU WAKUBWA! JAMII YETU HAINA MUDA NA WATU HAO HATA KIDOGO. SOTE WAISLAMU NA WAKRISTU NI WATU WAMOJA TENA WAAFRIKA AMABO HATUKUWA NA DINI BEFORE ILA ZETU ZA JADI!. NA HILI MWALIMU ALIFANIKIWA KUTUUNGANISHA. HAWA WAPUMBAVU WACHACHE WANAOTAKA KUTUMIA DINI KUWAGAWA WATANZANIA TUKIWAACHA WATATURUGA SANA!
Wewe Mkira na Mlalahoi msitake kutuvuruga na kamwe hamtafankiwa.Mnataka kutumia kila njia ku divert topik ili ife.Kama alivyosema Kulikoni hii mada haifi mpak iwe exhausted. Mambo ya udini na Kapuya.sijui NSSF siyo yanyojadiliwa kwenye hii thread..ukiweza fungua ya kwako hapa tunajadili kadhia ya upoteaji wa mamilioni nayohusishwa na Mengi. Alla...usituchanganye hapa, kama huna point za kuchangia kaa KIMYA
 
Samahni Ndugu Zanguni Nilitaka Kuiweka Panapohusika. Ninakubali Nimekosea.

Nimeisha Fanya Hivyo.

Cheers Up!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom