Meneja wa kampeni UKAWA/CHADEMA hafai, aondolewe mara moja

Meneja wa kampeni UKAWA/CHADEMA hafai, aondolewe mara moja

bango kubwa la roundabout Impala limewekwa picha mbili ya kwake na lowasa. sasa wako boti moja..hakun jinsi walishamsamehe..

Mungu adhiakiwi watavuna walichopanda,nakumbuka kauri ya zitto alisema baada ya uchaguzi watamkumbuka lipumba na slaa,
 
Zinaitwa Kampeni, na katika Kampeni za Kisiasa kuna njia kuu nne za kuwafikia wapiga kura ambazo ni;

1. Kukutana na wapiga kura moja kwa moja yaani Direct Voters Contact (DVC) kupitia Mikutano ya hadhara (Impact ni Ndogo kwa maana ya kuwafikia wapiga kura wachache)

2. Vipeperushi na machapisho (Still Billboards, Electronic Billboards, Posters na Leaflets); impact yake ni ya kati maana idadi ya watu wanaofikiwa ni wengi kiasi tena karibu kila siku;

3. Mass Media (Redio na TV). Njia hii ina impact kubwa kwani inawafikia watu wengi kwa mpigo, Katika hili CHADEMA na UKAWA wamefanya chini ya Wastani. Kwa mfano Mkutano wa leo Arusha watu wengi walijipanga kuufuatilia kupitia Vyombo vya Habari cha kushangaza hakuna linaloendelea. Jamani kushinda uchaguzi sio kazi nyepesi.

Kwa nini UKAWA haitumiii vyombo vya habari kuwafikia wananchi wengi? Njia nzuri na rahisi ni Redio kwani angalau kila kaya hapa nchini ina Redio maana hata simu (Feature Phone) zina Redio. UKAWA hamtumii hii njia hivi tatizo nini? Yaani leo mmeboa sana. Huyu Kampeni meneja wa UKAWA/CDM hafai kabisa. Kushinda uchaguzi kwa Mazingira haya si rahisi. Tusijidanganye!!. CCM wanatumia TV na Redio tena zile ambazo zinawafikia watu wengi. Amkeni jamani wananchi wanahamu ya kuwasikia na kusikia Sera zenu.

4. Mtu kwa Mtu, Hii hutumika katika scale ndogo ambapo wagombea hutembelea katika Kaya au maeneo ya mikusanyiko mfano Vituo vya Mabasi, Vijiwe nk. Njia hii ina impact ndogo sana.

USHAURI:
Kama tatizo sio fedha, basi huyo meneja wa Kampeni hafai kabisa anawashauri vibaya. Tanzania ina vijiji zaidi ya 20,000 (ishirini elfu), je mtavifikiaje vyote? Njia rahisi ni vyombo vya habari.

Ninashauri Mgombea wa Urais na Timu ya Kampeni Kitaifa afanye Press Conference kabla ya siku ya Kupiga KURA ili wananchi kwa upana waweze kumsikia. Tena hiyo Press conference irudiwe mara kwa mara. Vinginenvyo tutasema kura zetu zimeibiwa kumbe hatukujipanga vizuri. Huu ni ushauri wangu mpenda mabadiliko.

Kazi kwenu.
..................
Nauliza tu ,hivi Mtanzania wa leo unahitaji matangazo ya redio na Television kuikataa CCM ? Kama haitoshi hivi bado unahitaji hotuba reeeeeeeeeefu kukuelimisha madhara ya CCM ? Na zaidi je bado unahitaji uelimishwe kama mwaka huu ni mwaka wa kubadilisha chama Tawala ? Mabadiliko ndio ! mabadiliko sio Lowasa au Magufuli , mabadiliko ni kuiondoa CCM madarakani.
Mnaolalama kuwa Lowasa anatumia dakika chache ni wazi hata Kingunge ameishawapiku !
 
Ukawa tunahujumiwa na vyombo vya habari ila mungu yupo nasi
 
Nafikiri vyombo vya habari vinatumika vyema vinapokuwa na mgombea anayejenga hoja na kugusa matamanio ya mpiga kura kwa hisia sawia. sasa unapokuwa na mgombea ambaye hawezi kujenga hoja na kuvuta hisia za wapiga kura, ukitumia media ndo unawafukuza zaidi wapiga kura. Bora wakae hivyo hivyo kimya, uwezo wa Lowasa ni mdogo sana ama haupo kabisa wa kuweza kumshawishi mpiga kura ambaye ni yupo ktk UNDECIDED MODE. Lowasa atapata kura kutoka kwa wale ambao ni tayari decided. Hana uwezo Lowasa, hana sera na haelewiki pia anapoongea anakusudi kueleza nini.

Mfano leo amesema bodaboda ulaya wanalipwa fedha za kujikimu ni boda boda gani hao ulaya wanaolipwa hivyo?
 
Chama hiki kilishauzwa siku nyingi na walionunua wanakiendesha kutoka mfukoni Naona mnamsakama tumaini bure kampeni inaratibiwa NA team lowasa NA ofisi zao hazipo mikocheni NA huko tumaini hafiki.Wale wote wanaofwatan naEl hawana shida NA ushindi WAKE wengi vilaza hata akishinda hawatapata kitu kwahiyo wao ni kuzichomoa tu .wananifurahisha ccm hoyeee kinana anawasambaratisha
 
Mmeanza kushikana mashati, naona mnahaha mnabwabwaja tu huku mnyika.........mara tume ya uchaguzi, mara polisi, mara CCM wamejiandaa kuiba kura , Mara mmegundua mbinu zote za uizi wakura yaani mnaweweseka huku CCM wakitulia na kuwaangalia.
 
Wamuogope kingunge kama nani?
Kwa lipi alilonalo LA kutisha!
ila niwasaidie ndugu zangu wenye akili wanawashangaa kumuona slaa na zito na lipumba kama takataka na kuinua shangwe na vigelegele kwa kingunge
Ni aibu,watu wanawacheka tu,

You can fool everyone else but you can't fool your mind
 
Hakuna siku waliyoonyesha dharau kwa wapenzi wao kama leo. Huyu tumaini Makene wamweke pembeni ama akajiunge na Dr Mihogo


umeme umekatwa, wafany nini sasa? na wamesema watarudia baada ya taarifa ya habari itv, lkn najua watakata tena
 
Ninashauri Mgombea wa Urais na Timu ya Kampeni Kitaifa afanye Press Conference kabla ya siku ya Kupiga KURA ili wananchi kwa upana waweze kumsikia. Tena hiyo Press conference irudiwe mara kwa mara. Vinginenvyo tutasema kura zetu zimeibiwa kumbe hatukujipanga vizuri. Huu ni ushauri wangu mpenda mabadiliko.

Kazi kwenu.

Hamjakoma tu na kubadilisha gia angani? kwanza kampeni meneja wa Lowassa ni nani?
 
Hizo point zako nne zote ndizo wanazozitumia CCM kwa sasa. UKAWA mmevaa koti la mende matako yapo wazi yaani nyie mnafuatana tu na lowasa anakoaenda na kuacha sehemu zingine zikiwa wazi. najiuliza maeneo ambayo lowasa ameishapita siku nyingi kama swanga, ruvuma katavi saizi hali kule ipoje? angalieni ccm wanashambulia kila kona ya nchi kwa wakati mmoja mpaka vijijini. Jana Magufuli alikua Arusha akaenda Kilimanjaro, Nchimbi alikua Kilimanjaro maeneo ya Same, Mwigulu alikua Tanga Lushoto, Kinana alipotoka Arusha akaenda Mwanza, Mama samia alikua Kigoma, Kigwangala alikua Sikonge yaani jamaa wametawanyika na wana timu za kampeni za kata zinatembea nyumba kwa nyumba bado operation nimestuka. Mjiangalie sana wenzenu baada ya kuona tafiti zinaonyesha wanashinda kwa 65% wameongeza nguvu kuhakikisha inafika 80% Ukawa wameongeza nguvu kubishana na tafiti
 
Mzee Mwanakijiji kalike uzi..... Kumbe moyo wako bado unatamani mabadiliko.....
 
Chama hiki kilishauzwa siku nyingi na walionunua wanakiendesha kutoka mfukoni Naona mnamsakama tumaini bure kampeni inaratibiwa NA team lowasa NA ofisi zao hazipo mikocheni NA huko tumaini hafiki.Wale wote wanaofwatan naEl hawana shida NA ushindi WAKE wengi vilaza hata akishinda hawatapata kitu kwahiyo wao ni kuzichomoa tu .wananifurahisha ccm hoyeee kinana anawasambaratisha

Nilikua sielewi kwanini kinana anaitwa Komredi. Kampeni za mwaka huu kazipanga kwa mbinu za kivita UKAWA hawachomoki nakuambia. Mwigulu anapambana nao angani na kuna timu zinachakaza ardhini.
 
Back
Top Bottom