Meneja wa kampeni UKAWA/CHADEMA hafai, aondolewe mara moja

Meneja wa kampeni UKAWA/CHADEMA hafai, aondolewe mara moja

Kwani kampeni meneja wa Ukawa ni nani.
 
Naona ukawa wamelewa kwa mafuriko ya miji mikubwa huko kwenye miji midogomidogo na vijijini wamepasahau sasa naomba msije Fanya vurugu tu kuwa ccm imeiba kura za mgombea wenu maana kuna maeneo mengi tu hayajafikiwa.Magufuli ushindi mapema tu
 
Zinaitwa Kampeni, na katika Kampeni za Kisiasa kuna njia kuu nne za kuwafikia wapiga kura ambazo ni;

1. Kukutana na wapiga kura moja kwa moja yaani Direct Voters Contact (DVC) kupitia Mikutano ya hadhara (Impact ni Ndogo kwa maana ya kuwafikia wapiga kura wachache)

2. Vipeperushi na machapisho (Still Billboards, Electronic Billboards, Posters na Leaflets); impact yake ni ya kati maana idadi ya watu wanaofikiwa ni wengi kiasi tena karibu kila siku;

3. Mass Media (Redio na TV). Njia hii ina impact kubwa kwani inawafikia watu wengi kwa mpigo, Katika hili CHADEMA na UKAWA wamefanya chini ya Wastani. Kwa mfano Mkutano wa leo Arusha watu wengi walijipanga kuufuatilia kupitia Vyombo vya Habari cha kushangaza hakuna linaloendelea. Jamani kushinda uchaguzi sio kazi nyepesi.

Kwa nini UKAWA haitumiii vyombo vya habari kuwafikia wananchi wengi? Njia nzuri na rahisi ni Redio kwani angalau kila kaya hapa nchini ina Redio maana hata simu (Feature Phone) zina Redio. UKAWA hamtumii hii njia hivi tatizo nini? Yaani leo mmeboa sana. Huyu Kampeni meneja wa UKAWA/CDM hafai kabisa. Kushinda uchaguzi kwa Mazingira haya si rahisi. Tusijidanganye!!. CCM wanatumia TV na Redio tena zile ambazo zinawafikia watu wengi. Amkeni jamani wananchi wanahamu ya kuwasikia na kusikia Sera zenu.

4. Mtu kwa Mtu, Hii hutumika katika scale ndogo ambapo wagombea hutembelea katika Kaya au maeneo ya mikusanyiko mfano Vituo vya Mabasi, Vijiwe nk. Njia hii ina impact ndogo sana.

USHAURI:
Kama tatizo sio fedha, basi huyo meneja wa Kampeni hafai kabisa anawashauri vibaya. Tanzania ina vijiji zaidi ya 20,000 (ishirini elfu), je mtavifikiaje vyote? Njia rahisi ni vyombo vya habari.

Ninashauri Mgombea wa Urais na Timu ya Kampeni Kitaifa afanye Press Conference kabla ya siku ya Kupiga KURA ili wananchi kwa upana waweze kumsikia. Tena hiyo Press conference irudiwe mara kwa mara. Vinginenvyo tutasema kura zetu zimeibiwa kumbe hatukujipanga vizuri. Huu ni ushauri wangu mpenda mabadiliko.

Kazi kwenu.

msigongane vichwa bure na kumtafuta mchawi nani, ni hivi lowassa hapiti hata akalale nec bhaaaaasi!
 
hii ni kweli kabisa kampeni za mwaka huu si za nguvu kama zile za 2010
 
attachment.php

mkuu binafsi ni mpenda mabadiliko na nawapongeza sana wana arusha. kwa mwitikio wa watanzania walioko mtaani kama UKAWA wangekuwa na vikosi imara vya kampeni ushindi ni saa nne asubuhi. tatizo kila kitu kimeachwa kwa mgombea mwenza na mgombea urais hilo ni kosa kubwa kikampeni....
 
Naona ukawa wamelewa kwa mafuriko ya miji mikubwa huko kwenye miji midogomidogo na vijijini wamepasahau sasa naomba msije Fanya vurugu tu kuwa ccm imeiba kura za mgombea wenu maana kuna maeneo mengi tu hayajafikiwa.Magufuli ushindi mapema tu

nakiri hili kwa unyonge mkubwa....
 
Tatizo ni dharau ya 4U Movement...Makene aliambiwa yeye pamoja na team yote ya M4C wakajiunge 'Red Brigade' na wawaachie wakongwe wa 'run the show'...haya maneno yaliwa demoralize sana kina Makene na wenzake...
 
Wakati mwingine mnawabebesha lawama kubwa hao UKAWA...

Wamiliki wengi wa vyombo vya habari vikubwa nchini wanabanwa na ukada wao wa CCM...

Hivi kwa mfano ulitarajia Star TV au TBC kuonesha mkutano kama huo hata kama wanalipwa?

Kumbukeni hii nchi bado ina serikali na serikali hiyo ni ya CCM waliopo hatarini kutolewa madarakani...
 
kuna hujuma imefanyika ..si bureee tatizo kingunge kaharibu kitendo cha kutangazwa atakuwepo kimesababisha vyombo vya habari viingiliwe kazi zao .........kingunge angefanywa kama suprise leoooooo...tatizo wamemtangaza sana hadi ccm wakaogopa leooo

Huku ndo kukosa weledi wa kisiasa huo.
Arusha ni ngome ya Chadema hawahitaji kushawishiwa na Kingunge kupiga kura.
Sauti ya Kingunge ingeelekezwa kwny mamilioni ya watz ambako kuna impact.
 
Napata wasiwasi inawezekana kunajambo limejificha sababu haiwezekani tunaomba waratibu wa hizi kampeni wawe active, tunasema waache kutuletea huu upumbavu nasema ivi! hatuitaji upuuzi huu. Kama wanatupata basi wafanyie kazi maoni yetu la sivyo ni bora siku ya kupiga kura nilale nyumbani

Ha ha ha.
Mbowe alisema treni imeshashika kasi ukibanwa na ukataka kuchimba dawa ruka dirishani
 
Wameshindwa hata TV, Radio, hata matangazo tu......
Nawapigia Kura Chadema ila mnaangusha sana watu wengi wanalalamika hamtoi coverage yakutosha... kama wakifata media coverage lazima mshindwe
Inauma sana sitaki piga kura afu nishindwe tena mara ya pili

Hii nyota ya kukatwa itakufuata tu yaelekea.
Kawapigie ACT labda ha ha
 
Back
Top Bottom