Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

Marando kashindwa kueleza Itikadi ya Chadema! Hata hapa JF wanachama wa Magwanda hawajui Itikadi ya Chama chao! Nguvu ya Umma Sio Itikadi ni falsafa! Magwanda nawauliza tena Itikadi(Imani) ya Chama chenu ni nini? Jana Nape na Jussa wamefanya vizuri kwenye mdahalo huwezi linganisha na yule mzee wenu Marando

Hata CCM walishindwa kueleza itikadi yao vizuri -- ya wizi na ufisadi. Mtu wao Nape hata hakujua anafanya nini kuhusu vita yake ya magamba ambayo yamemkatalia kuondoka.
 
Penye red: Na hapo ndipo CUF huwa inajididimiza na kukimbiwa na wafuasi. na hii yote inatokana na ndoa na ndiyo maana alichaguliwa Jussa (mwanandoa) kuliko tatiro.

CUF Bara inabidi iamke sasa, itoe agizo kwa wafuasi na viongozi wao kwamba CCM ndiyo adui wao mkubwa, na si CDM.

Nami kitu hicho cha CUF kuungana na CCM kushambulia CDM ndicho kinanishangaza, na ndiyo maana niliamua kuondoka CUF na kuingia, CDM. Na bila shaka wengi wamefanya hivyo. Itikadi ya CUF wala haijulikani, akina Lioumba wanaendeshwa kwa pua na akina Seif kwa masilahi yao kule Zanzibar.
 
Mwehu wewe, kama hujui kitu ni bora uombe usaidiwe, kwa adhabu yako naweka maandiko ya Nyerere hapa kwa lugha ya kikoloni ili jue tofauti ya ujamaa wa wazungu na ujamaa wa kiafrika.

''These two revolutions planted the seeds of conflict within society, and not only was European socialism born of that conflict, but its apostles sanctified the conflict itself into a philosophy. Civil war was no longer looked upon as something evil, or something unfortunate, but as something good and necessary.

As prayer is to Christianity or to Islam, so civil war (which they call "class war") is to the European version of socialism--a means inseparable from the end. Each becomes the basis of a whole way of life. The European socialist cannot think of his socialism without its father--capitalism!

Brought up in tribal socialism, I must say, I find this contradiction quite intolerable. it give capitalism a philosophical status which capitalism neither claims nor deserves. For it virtually says "Without capitalism, and the conflict which capitalism creates within society, there can be no socialism!" This glorification of capitalism by the doctrinaire European socialists, I repeat, I find intolerable.

African socialism, on the to her hand, did not have the "benefit" of the Agrarian Revolution or the Industrial Revolution. it did not start from the existence of conflicting "classes" in society. Indeed I doubt if the equivalent for the word "class" exists in any indigenous African language; for language describes the ideas of those who speak it, and the idea of "class" or "caste" was nonexistent in African society.

The foundation, and the objective, of African socialism is the extended family. The true African socialist does not look on one class of men as his brethren and another as his natural enemies. He does not form an alliance with the "brethren" for the extermination of the "non-brethren." He rather regards all men as his brethren--as members of his ever extending family. that is why the first article of TANU's creed is "Binadamu wote ni ndugu zangu, na Afrika ni moja." If this had been originally put in English, it could have been "I believe in Human Brotherhood and the Unity of Africa." "Ujamaa," then, or "familyhood," describes our socialism.

It is opposed to capitalism, which seeks to build a happy society on the basis of the exploitation of man by man; and it is equally opposed to doctrinaire socialism which seeks to build its happy society on a philosophy of inevitable conflict between man and man.

Kutoka Ujamaa: The Basis of African Socialism na Julius Nyerere.

Rudi darasani kidogo, usisome paragraph moja ukasema unajua, soma kiini cha socialism, kitu gani kinadefine socialism, of course there are different schools, zingine zinaangalia aina ya jamii, aina ya uchumi, itikadi za kisiasa na mambo kama hayo, mwisho wa siku kiini cha ujamaa ni namna uchumi wake unavojengwa, na nasisitiza HAKUNA UJAMAA WA KIAFRICA NA UJAMAA WA KISAYANSI

au mwenzangu unasema huelewi unachosoma?
 
Ndugu yangu TAKEURABU

Nadhani ukuwa kwenye kipindi ulihadithiwa maana kama ulikuwa hayo yote uliyoandika yalikuwa nje ya mada hii ndiyo inawasababisha watanzania kufeli mtihani CCM na CUF walikuwa nje ya point anywy nadhani walikuwa wamepania huku CDM akijua anachokifanya ndiyo raha ya msomi bwana yote uliyoyaandika yalikuwa nje ya mada ila naweza kukujibu japo mawili au yote
1.yeye hatetei mafisadi wale walioshtakiwa sikweli wanamakosa mpaka mahakama ihukumu.Hili ndilo tatizo la watanzania kuhukumu bila kuwa na uwakika na mkosaji kama kweli kakosa.
2.CHADEMA kigoma hawakushirikiana kwa maana ya kuungana na kuongoza kigoma bali kila chama kiliongoza kwa kipindi tofauti,tofauti na CUF na CCM ambao wote wako pamoja huku sera zao ziko tofauti
3.Kila chama duniani kinaushirikiano lakini sikwamba vyama vyote vinamlengo mmoja maana kila kimoja kinaongoza kutokana na nchi zilizopo nafahamu kuwa wakati wakuanzishwa hakuna hata kimoja nitawi la mwingine.
4.Hawezi kueleza hatma ya shibuda kwakuwa sio kilichompeleka pale.Pia Shibuda anatakiwa afukuzwe kwa kufuata utaratibu hata madiwani walifukuzwa kwa kufuata utaratibu bahatinzuri CHADEMA hawakurupuki
5.Kumbuka kuwa DR Slaa yeye alipendekezwa na uongozi wa CHADEMA sikama wengine wanaotamani kuongoza nchi kama wanavyofanya wengine yeye alitaka kuendelea kuwa mbunge lakini ilionekana anafaa kugombea urais kuomba mshahara huo nikuwa ameze kujikimu kimaisha baada yakuukosa Urais

Hayo matokeo uliyoandika hiyo nitafsili yako maana yawezekana hujawahi kwenda kwenye mijadala kama ulikwenda basi unaonekana unakurupuka kujibu au kutoa michango nje ya mada
NDUGU YANGU MAZOKO
Mimi niliona ule mdahalo live star tv wala sijasimuliwa: mambo hayo matano hayakuwa nje ya mada ngoja nikueleze kama ifuatavyo;

si kweli kuwa hoja nilizotoa hazikuwa kwenye mada; 'mada ilikuwa itikadi ya vyama SIASA na tanzania tunayoitaka'
si kuwa tu hoja zote hizo zinahusu itikadi lakini pia zilianza kuchokozwa na marando mwenyewe!!
  • swala la mafisadi linahusu itikadi ya vyama lakini pia lilianza kuibuliwa na marando kwa hiyo limo ndani ya mada
  • swala la madiwani wa chadema kushirikiana na ccm kigoma linahusu itikadi na lilianza kuibuliwa na marando alipokuwa anaikandia cuf kushirikiana na ccm zanzibar na wenzake nao wakamjibu mbona chadema walishirikiana nao kigoma
  • kuhusu itikadi ya chadema kama ni mlengwa wa kulia au kati nalo pia lipo ndani ya mada na ndio kiini haswa cha mada yenyewe
  • swala la posho za wabunge ni la kiitikadi ya chama na liliibuliwa na marando mwenyewe aliposema kuwa wabunge wa chadema wamekataa kuchukua posho, ndipo wenzake wakamuuliza shibuda ni mbunge wa chama gani? mbona yeye anapokea na ametangaza hadharani? kwa nn chama hakijamchukulia hatua yoyote?
  • hata swala la slaa nalo ni la kiitikadi hivyo lipo ndani ya mada kaka, kwa kifupi hakuna hata hoja moja kati ya nilizotoa ambazo zipo nje ya mada hapo kaka
SASA ENDELEA KUPATA MAJIBU YA HOJA ZAKO KWA KINA KAMA IFUATAVYO:
1. swala la ufisadi aliliibua yeye mwenyewe marando wakati anainadi itikadi ya chama chake aliposema kuwa ccm imeshindwa kuwashughulikia mafisadi; ndipo nape alipompelekea dongo kuwa yeye marando ndio anarudisha nyuma juhudi za ccm za kupambana na ufisadi akiwa kama wakili anawatetea mafisadi waliofikishwa mahakamani; badala ya marando kujibu hoja yeye alisema kuwa waliopelekwa mahakamani ni vidagaa; hata kama ni vidagaa bado ni mafisisadi kwa nn aliwatetea?
2. kuhusu swala la kigoma hata mm nilikuwa nafahamu hivyo ulivyoeleza wewe lakini cha ajabu marando hakujibu kabisa hoja hii, kwani angetoa maelezo hayo jussa asingeshangiliwa wakati akielezea swala hilo.
3. kuhusu itikadi maramdo ameshindwa kueleza kuwa chadema inaamini itikadi gani? kwani kinadhalia inaamini mlengwa wa kati, lakini kivitendo inaamini itikadi ya uhafidhina
4. marando kutoeleza chochote kuhusu shibuda hapa pia amechemka, kwa sababu mada ni itikadi ya vyama, shibuda ni miongoni mwa viongozi wa chadema waliokiuka itikadi ya chama kuhusu swala la posho za wabunge ambalo amelizua yeye marando kwenye mdahalo; ndipo akaulizwa kwa nn chadema inashindwa kumchukulia hatua shibuda? nape akasema wanaogopa kusambaratika; kwa hiyo ili kufuta aibu hii marando alitakiwa aeleze msimamo wa chama kuhusu watu kama shibuda jambo ambalo hakufanya.
5.kuhusu swala la SLAA; hoja sio mshahara wa kujikimu hoja ni kwamba kwa nn alisisitiza alipwe mshahara wa kibunge, wakati chadema katika moja ya itikadi yao wanalalamika kuwa wabunge wanalipwa mishahara mikubwa? ndipo jussa aliposema kuwa huu ni unafiki! yeye kama mwanachama, na chama kimemuamini agombee si angesubili chama kimpangie mshahara? kwa nn alilazimisha uwe wakibunge la sivyo hatagombea urais? kumbuka hoja hii marando hakujibu kabisa! alikaa kimya, hata hayo maelezo yako hakutoa


kutokana na uzito wa hoja hizo ndio maana nikagawa maks bila ushabiki kuwa;CCM 55%. CUF 40%, CHDEMA 5%
 
Wakuu hivi ile amri ya Makamba ya wanaCCM kutoingia ktk mdahalo imeondolewa?
 
Daah..,Kaka hujafanya analysis vizuri..,umependelea saana..,haiwezekani CCM ukaipa asilimia nyingi hivyo..,kwa kipi hasa..,kwanza Nape alidanganya sana..,uongo wa nape..
1. CCM bado inafuata siasa ya ujamaa wa mwalimu nyerere..
2.CCM inachukua maamuzi magumu ya kuwafukuza viongozi wabadhilifu..!
3.Amepingana na mwenyekiti wake juu ya suala la utajiri wa Tanzania..,Nape(Tanzania ni tajiri )..,JK(Tanzania ni maskini)
4.Kuhusu ufaulu wa wanafunzi.
5. uongo woote alizungumza
so inabidi uwe fair usichakachue mkuu..!
 
wewe takeurabu bila shaka umelewa baada ya kupewa urabu na ccm?
ndugu yangu jibu hoja acha kuweweseka jifunze kupangua hoja kwa hoja na sio unapangua hoja kwa matusi kwani kufanya hivyo hujibu hoja bali unafanya hoja ya mpinzani kuwa na nguvu zaidi, hata maana ya TAKEURABU sio hiyo ambayo wewe unaifikiria; ngoja nikueleze:
TA=TANZANIA
KE=KENYA
U=UGANDA
RA=RWANDA
BU=BURUNDI
HIZI NI NCHI ZINAZOUNDA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
 
mimi naona katika mjadala ule Nape na Jussa wameng'ara sana! chadema kupitia Marando wamechemka sana. marando ameshindwa kujibu hoja za msingi na muhimu hivyo kusababisha hata hoja zake kuvunjwa; mfano:
1. ameshindwa kujibu kwa nn yeye anatetea mafisadi? kwa hiyo hana uhalali wa kupinga anachokitetea
2. ameshindwa kutetea hoja yake kuhusu cuf kushirikiana na ccm zanzibar; jussa alimuuliza mbona chadema walishirikiana na ccm kwa miaka 5 kigoma? kwa hiyo hapa napo hana uhalali wa kubeza kitu alichowahi kukitenda
3. amejichanganya kueleza itikadi ya chadema; kama ni mlengwa wa wakati, kushoto au mlengwa wa kulia? kama ni mlengwa wa kati mbona wanashirikiana na vyama vya kihafidhina nje ya nchi ambavyo si vya mlengwa wakati na haviamini mageuzi?
4. ameshindwa kueleza hatima ya shibuda ndani ya chadema, mtu anayekiuka utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chadema kuhusu posho, na ameshindwa kujibu hoja kuwa chadema wanaogopa kumtimua shibuda kwa sababu wanogopa kusambaratika?
5. ameshindwa kujibu kuwa wakati chadema wanasisitiza kupunguzwa kwa mshahara wa wabunge na marupurupu mengine; Dr W. B. P. Slaa, moja ya sharti la kuacha kugombea ubunge na kugombea urais lazima alipwe mshahara wa kibunge iwapo atakuwa amekosa urais! marando hakujibu chochote juu ya hili

Kwa kifupi chadema wamesambaratishwa sana kwenye mdahalo ule, na hata wakati mwingine marando alizomewa!

kwa hiyo mimi na rank kama ifuatavyo; CCM=55%; CUF=40%; CHADEMA=5%; naipa chadema 5% kwa sababu hoja hizo hapo juu ni nzito na msemaji ameshindwa kuzijibu

Huo ndiyo ukweli tuachane na ushabiki
 
hi wajumbe;

leo pia tumeshuhudia mjadala mhimu sana wa itikadi za vyama ambapo vyama vikuu viliongozwa na watu wake wanaoaminika huko. Matokeo hayo hapo juu yanatokana na sifa za kimjadala. Katika mijadala hii imeonekana bado chadema inaongoza na kuwaacha wengine kutokana na pengine havijaweza kupata kitu cha kuwafanya wasimame wima yaani bado they are bittiing around the bush kutokana na makandokando yao ya kimuonekano ktka jamii; ccm ikiwa na tatizo kubwa kiuongozi na kushindwa kusimamia maamuzi kwa usahihi; cuf nayo ikionekana kama msindikizaji wa ccm katika mambo yake yote ikiwemo swala la posho; kutosimama kama wapinzani ktk sehemu mbalimbali za maamuzi pale walipi na nafasi hiyo yote yanawafanya vijana wake wanaotuwakilisha washindwe kusonga mbele.

Leo ilikuwa hivi

marando (chadema): Alikuwa focused na swali aliloulizwa; alikuwa hatoki nje ya mada kwa ushabiki; alivumilia vijembe vya wapinzani wake na vingine hakuvijibu kama akiona havina tija; ameeleza itikadi kwa ufasaha na kujipambanua tofauti na wenzake; alijibu maswali yote magumu kwa ufasaha; swala la ufisadi kajieleza maana anatetea mafisadi dagaa mapapa wa ufisadi wa epa hawajafikishwa mahakamani; hivyo wametolewa kafara na yeye ana wajibu kuwaokoa; swala la udini hakuenda ndani saana lakini alisimamia ktk utanzania na kuepuka kupoint fingures kitu ambacho ni mhimu ktk mjadala wa kitaifa na kwa kueleweka hakuulizwa maswali mengi sana kama wenzake

nape (ccm): Alikuwa anazunguka zunguka kutokana na ukweli mambo mengi waliyoyaahiidi kama chama hawajatekeleza; ameulizwa maswali mengi kutokana na kutoelewa kwa watazamaji/wasikilizaji;baadhi ya aliyosema watazamaji waliyakaa pale pale kama lile la elimu; miaka hamsini ya utawala na maendeleo yake nk. Kwa ujumla alikuwa kisiasa zaidi na alikuwa hajui lipi lutawafurahisha watazamaji maana alikuwa anaonekana kama msanii zaidi na mnafiki mbele ya hadhira kuliko mtu anayesimamia kile anachoongea

jusa (cuf): Yeye kama yeye kajitahidi kujieleza ingawa alipotosha baadhi ya hoja kama lile la arusha na kigoma kwa lengo la kufikisha ujumbe kuwa yeye yuko ktk serikali ya kitaifa hata chadema wamewahi kuwa bila kujua alikuwa anapotosha; alikuwa anashughulikia persona attacks zaidi na kushindwa kueleza cuf ni chama cha aina gani kwa sasa aidha cha upinzani au chama tawala; swala la posho hajaeleza ni sehemu ya ilani yao au wanaidandia tu; amejitahidi kuelezea umhimu wa muungano ila hajaeleza kama kutakuwa na miungano je nafasi ya upinzani kama watch wa serikali iko wapi.

Kwa ujumla wote walijitahidi na mjadala ulikuwa mtamu ingawa mapungufu ya hapa na pale; nafikiri kipindi kijacho muda uongezwe zaid ili kutoa wigo kwa watu wengi kuulizwa maswali na k ujibiwa kwa ufasaha. Asanteni karibu. Hizi alama ni kwa mjibu wa analysis ambay nimeifanya tangu mjadala unaanza hadi mwisho bila kuwa biased.
ni vigumu sana ukapona ugonjwa wa ushabiki ulionao maana aliyekuroga anaonekana alikufa siku nyingi pole sana
 
ndugu yangu jibu hoja acha kuweweseka jifunze kupangua hoja kwa hoja na sio unapangua hoja kwa matusi kwani kufanya hivyo hujibu hoja bali unafanya hoja ya mpinzani kuwa na nguvu zaidi, hata maana ya takeurabu sio hiyo ambayo wewe unaifikiria; ngoja nikueleze:
Ta=tanzania
ke=kenya
u=uganda
ra=rwanda
bu=burundi
hizi ni nchi zinazounda jumuiya ya afrika mashariki

kaka hawa ndiyo wanasiasa wa leo (single sided figure)
 
Hata mimi nilivoangalia niliona Jussa kawabwaga wenzake tena kwa asilimia kubwa,sasa nashangaa unakuja na hoja kama hiyo au tuseme ndo ule msemo si chongo ni kengeza,na ndio maana mara nyengine nakua sipendi kupita hata njia hapa siku hizi maana watu kama nyinyi mnatuharibia ile JF yenyewe hasa,ushabiki mbele halafu ndo ukweli... lol! kazi kweli kweli.

Wanafunzi wengi wanashindwa mitihani ya taifa ni kutokana na kutojibu swali aliloulizwa na badala yake kuandika blabla nyingi zenye kumfelisha mtihani. Bora jibu swali kabla ya elaboration.

Kwa wataalamu na wazoefu wa midahalo Nape na Jussa walikuwa hawajibu maswali na badala yake walikuwa wanajikinga kwa personal attack. Kumshambulia mtu kwa hoja nje ya swali uliloulizwa ni kinyume cha kawaida na taratibu za midahalo.

Tatizo watanzania wengi wanafikiria mtu kuwa na maneno mengi na kumshambulia fulani kwa hoja binafsi ndio kuweza kumbe kujibu maswali ulliyoulizwa kwa ufasaha ndiko kunakokupa credit.

Kwa mtazamo huo personal attack ni dalili wazi za kuishiwa hoja au kushindwa kujibu swali na ndilo lililotokea kwa Nape na Jussa. Lakini Marando alitulia na kujibu hoja zake vizuri bila kutumia kinga ya personal attack kama alivyofanya Nape na Jussa.
 
Sikuangalia mdahalo kwenye luninga, lakini nimesoma mdahalo hapa jamvini!! Kwa maandishi yenu nimejiridhisha kuwa Marando alishinda akifuatiwa na Nape na mwisho Jussa. Alama ninazo toa ni 40:32:28[!! ( CHADEMA:CCM:CUF)
NB: 1. Nape na Jussa walipoteza alama kwa kutoka nje ya maada na kufanya personal attacks.
2. Marando amepata alama za ziada kwa kuwa na nidhamu za ki mdahalo
3. Chadema ni chama chenye ajenda anayoeleweka zaidi kuliko CCm na Cuf
 
Hata Obama wakati wa kampeni ya urais wa Marekani alikuwa ana ng'aa kwenye midahalo sababu alikuwa anajibu point na sio ushabika au pesonal attack!

Kwa maoni yangu Marango alikuwa mwangalifu na majibu yake ili asitoke nje ya mada kulinganisha na Nape na jussa.

Nina hakika kwa wale waliufutilia huo mdahalo bila chembe ya mahaba na chama atasema Marando hakutoka nje ya mada na hivyo alikuwa juu.
 
Sishangai watanzania wengi hawajui analysis za kimidahalo, kuna kitu kama nidham hiyo ni prime, kujua hoja iliyo mbele na kutotoka nje ya mada au kurudiarudia kitu kile kile kosa kubwa, kuattack mwenzako personally unaondolewa point, kuchekacheka hovyo bila kujua ni mdahalo serious. Marando ndio maana hakupata 100% kapata 45% kwa sababu hakufanya attacks, kuna akina jusa anaongelea kigoma najua kila chama kiliongoza kwa muda wake sio kuunganisha sera, arusha hata dunia inajua. Nape alikuwa kituko zaidi maana hata hakujua anaongelea nini. Naombeni kabla ya argume msome principle za mijadala na analysis zake maneno mengi sio ushindi wa mjadala. Twende kazi
 
Sishangai watanzania wengi hawajui analysis za kimidahalo, kuna kitu kama nidham hiyo ni prime, kujua hoja iliyo mbele na kutotoka nje ya mada au kurudiarudia kitu kile kile kosa kubwa, kuattack mwenzako personally unaondolewa point, kuchekacheka hovyo bila kujua ni mdahalo serious. Marando ndio maana hakupata 100% kapata 45% kwa sababu hakufanya attacks, kuna akina jusa anaongelea kigoma najua kila chama kiliongoza kwa muda wake sio kuunganisha sera, arusha hata dunia inajua. Nape alikuwa kituko zaidi maana hata hakujua anaongelea nini. Naombeni kabla ya argume msome principle za mijadala na analysis zake maneno mengi sio ushindi wa mjadala. Twende kazi

Wewe wasi wasi wako ni nini, mpe Marando hata alama 100000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000% kama unadhani hii itakupa relief, lakini ukweli unaujua mwenyewe na viongozi wa magwanda siku nyingine watajifunza kupeleka watu wenye akili timamu sio huyo frustrated advocate.
 
HUU mchezo Wa kukana watu kausema hata Marando mwenyewe Kama Shibuda sio Chadema nashindwa kuelewa basi CCM nao waseme Chenge sio CCM. Wana CDM kukubali makosa ndio mwanzo Wa kujirekebisha
<br />
<br />
hapo kwel!!!
 
utakuwa umesimuliwa Marando alichemka kupita maelezo , even ze part ideology ? Kituko , bora comedian Nape kiasi ! ILA JUSA ALIWAFUNIKA SANA SANA SANA INGAWA ALIULIZWA MASWALI MENGI ! CUF NI WAKOMAVU KTK SIASA UTAKE USITAKE MTOA MADA ! GEUZA MAKSI FASTA ! JUSSA 60% , NAPE 25% NA BABA MKWE AKA MARANDO 15 % , Kama ulikuwa unaangalia mdahalo kwa kutumia macho na ubongo ,ILA KAMA ULIKUWA UNAANGALIA KWA MASABURI ACHA MAKSI ZAKO !
 
Ulimi ni kitu kidogo sana lakini matokeo ya madhara yake ni makubwa mno katika historia ya maisha ya kila siku ya binadamu!!!!!!!

Yetu macho mavuno yatakayopatikana kutokana na kauli za ajabu ajabu kama hizi hasa kwa CCM lakini ukweli ni kwamba kamwe haitotoweka bure hata katika ukimya wa nioyo ya wananchi waliowengi.

CCM ndo chama kitakachosababisha machafuko hapa nchini. Maana kauli kama za kina NAPE ni hatari kwa ustawi na mstakabali wa watanzania na tanzania yetu.Tatizo la haya magamba hayasomi alama za nyakati yanafikiri tanzania ya leo ndo ile ile ya enzi za kina kingunge.
 
Back
Top Bottom