Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

mi ningeona ni vema nape atoe majibu yanayoendana na maswali anayoulizwa, na sio kujibu kiujanjajanja kuwapumbaza watanzania.
 
Leo una kazi kuzunguka jukwaa zima, kujaribu kusafisha hali ya hewa baada ya Marando kuachia ushuzi, na bado nasikia Nape ameamua kuomba round na yule babu anayebemenda vijukuu vyake.
Zigo la Jairo lamwangukia Luhanjo Send to a friend
Saturday, 27 August 2011 21:36
0digg

Na Waandishi wetu
WAKATI Bunge limeunda Kamati Teule ya kuchunguza sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, upepo unaonekana kumgeukia Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, baada ya wasomi na wanasiasa kumbebesha mzigo wa tatizo hilo.

Mwenyekiti wa Jukwa la Katiba, Deus Kibamba, amesema kitendo cha kutofautiana kwa viongozi katika kauli zao kuhusu kosa alilofanya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Jairo kinaonyesha Serikaliimegawanyika.Alisema alichofanya Luhanjo kinaifanya Serikali ipoteze uwajibikaji wa pamoja ambao kimsingi katika suala zima la mgawanyo wa madaraka kila mtu amekuwa akitumia vibaya nafasi aliyonayo.

"Waziri Mkuu alituambia kuwa angekuwa ndiye mwenye mamlaka ya mwisho angemfukuza kazi na alisisitiza kuwa anasubiri Rais arudi, lakini ghafla anajitokeza Katibu Mkuu Kiongozi, Luhanjo n kutangaza hatua za kumchukulia mtumishi wa Serikali ziko hivi. Huko ni kumdhalilisha Waziri Mkuu," alisema Kibamba.Alisema hatua zote alizochukua Luhanjo zilionekana kumdhalilisha Waziri Mkuu na pia kitendo cha kutofautiana kwao kinaonyesha dhahiri Serikali haina mshikamano.

"Hii ni hatari kwa taifa, Serikali inaundwa na CCM chama ambacho tayari kimegawanyika na sasa inaonekana nayo imegawanyika," alisema Kibamba.

Shellukindo
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, William Shelukindo, amesema Phillimone Luhanjo ameshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.

Shelukindo ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Rais Ikulu (cheo ambacho sasa kinaitwa Katibu Mkuu Kiongozi) katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi, alisema Luhanjo ameonyesha utovu wa nidhamu na ameidhalilisha Ikulu kutangaza kumrejesha Jairo bila kupitia bungeni.

"Kwa kitendo cha kutangaza kupitia vyombo vya habari kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo badala ya kufikisha bungeni suala lake, amemdhalilisha Rais na Ikulu," alisema.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika Mahojiano maalum, Shelukindo ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, alisema kuliruka Bunge ni kuchonganisha mihimili miwili yaani Serikali na Bunge.

"Sipendi kuzungumza hivi sasa kwa sababu nimeamua kukaa kimya, lakini kwa kuwa naheshimiana na vyombo vya habari na mmetaka nizungumzie suala hili, nasema Luhanjo amemdhalilisha Rais Jakaya Kikwete na alitaka kumchonganisha na mhimili muhimu wa Bunge," alisema Shellukindo.

Alisema Luhanjo amefanya makosa na kumfanya aonekane kwamba hajasoma katiba ya nchi, kwani inaeleza wazi kwamba bunge lina jukumu la kusimamia shughuli za Serikali kwani ni muhimili.

Katiba ya nchi

Shellukindo alisema ibara ya 63 kifungu kidogo cha kwanza ya katiba inasema bunge ni pamoja na Rais kwa sababu wote tumekwenda kwenye uchaguzi kuomba ridhaa ya wananchi ya kuongoza Serikali na ndiyo maana hata mawaziri wanatokana na wabunge.

Mwanasiasa huyo alisema ibara hiyohiyo ya 63 kifungu cha pili kinaeleza kuwa Bunge lina jukumu la kusimamia mihimili hii ya Serikali, hivyo kwa kuwa suala la Jairo kwa lilianza bungeni ripoti yake ilistahili kupelekwa bungeni na isomwe huko na siyo vinginevyo.

Shellukindo alisema kitendo alichofanya Luhanjo kutoa taarifa ya kumrejesha Jairo kupitia vyombo vya habari pia kimemdhalilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi serikalini, baada ya kupelekewa majibu ya uchunguzi juu ya Jairo, Luhanjo alistahili kuwasiliana na Rais Kikwete kutaka ushauri na Rais angewasiliana na Pinda ili aandae taratibu za kutangazwa bungeni na siyo kutangaza kupitia vyombo vya habari.

"Tatizo hapa Luhanjo aliharakisha mno kutangaza suala hili kupitia kwenye vyombo vya habari tena kwa mbwembwe kana kwamba alikuwa na dukuduku moyoni mwake la kuwaonyesha ubabe wabunge," alisema Shellukindo.

Kamati Teule
Spika wa Bunge, Anne Makinda juzi alitangaza majina ya wabunge watano, wanaounda Kamati Teule kuchunguza utaratibu uliotumiwa na Wizara ya Nishati na Madini, kukusanya fedha kutoka katika taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kupitisha wa bajeti.

Alisema kamati hiyo itakayofanya kazi kwa wiki zisizozidi nane pia itachunguza iwapo hatua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Luhanjo, kutangaza matokeo ya uchunguzi dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo uliingilia haki na madaraka ya Bunge.

Hii ni kamati teule ya pili kuundwa wakati wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, lakini kwa wizara hiyohiyo ya Nishati na Madini ambayo hivi sasa inaongozwa na Waziri William Ngeleja.


Maadili ya watumishi
Kuhusu maadili ya utumishi kwa kipindi hiki akilinganisha na alipokuwa Ikulu, Shellukindo alisema nidhamu ya watumishi imeshuka na hili linaiweka pabaya Serikali ikiwamo kuvuja kwa baadhi ya siri za Serikali.

Alisema nidhamu katika utumishi imeshuka hivi sasa ikilinganishwa na wakati wa utawala wa awamu ya kwanza na ya pili, kwani watumishi walikuwa na uzalendo na nchi yao na ilikuwa ni jambo lisilowezekana kuona siri ya Serikali imevuja.

Alilipongeza bunge kwa kuunda kamati ya kuchunguza sakata hilo na kuwataka watumishi nchini kufanya kazi kwa nidhamu ili kusukuma mbele maendeleo ya nchi kwa kujivika uzalendo kwani utaalamu wao unahitajika kwa kiasi kikubwa.

Luhanjo
Jumanne wiki hii Ikulu ilitangaza kumrejesha kazini Jairo baada ya uchunguzi wa tuhuma dhidi yake za kutenga mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuhonga wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara hiyo.

Luhanjo alitangaza uamuzi huo katika mkutano wake na waandishi uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam akisema Jairo hana hatia na siku iliyofuata akatakiwa kurejea kazini.Hata hivyo, wabunge walichachamaa na kutaka kuundwa kwa kamati teule ya Bunge.

Hata hivyo, Rais Kikwete alitengua uamuzi huo na kumrejesha Jairo likizo kupitisha uchunguzi wa Kamati Teule ya Bunge.

Kaiza
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Fordia, Buberwa Kaiza aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa Serikali imepoteza uwezo wa kudhibiti viongozi wake."Katika hili Serikali imepoteza uwezo wa kudhibiti watendaji wake, lakini pia kuratibu shughuli zake, kila mtendaji anatumia nafasi aliyonayo kama mali yake binafsi," alisema Kaiza.
Alisema zipo athari nyingi ambazo hutokana na vitendo hivyo, watu hupoteza imani na Serikali yao kwa kuidharau na kwamba, migogoro ya wazi huweza kuongezeka.

Jaji Mkwawa

Kwa upande wake Jaji Mstaafu, John Mkwawa alisema kugongana kwa utendaji wa mihimili hiyo miwili ni jambo la kawaida na kuwataka wananchi kuzoea.
Jaji Mkwawa alisema kuwa hali hiyo ni ya kawaida hasa kwa nchi ambazo zina mfumo wa vyama vingi.
"Uamuzi huo ni wa kidemokrasia, lakini kikubwa ni hiyo Kamati Teule ya bunge kufanya kazi yake kwa umakini, haya ni mambo ambayo Watanzania wanatakiwa kuyakubali," alisema Jaji Mkwawa.
Alisisitiza kwamba Luhanjo naye ametumia madaraka yake kutokana na uamuzi alichukua huku akisisitiza kuwa hata uundwaji wa tume nao ni jambo ambalo lipo wazi.
"Tusiogope na kulipa jambo hili tafsiri mbaya wakati mwingine tukubali kuwa migogoro huwa ipo, ila lengo ni kufikia katika hatua nzuri," alisema Mkwawa.
Imeandikwa na Burhani Yakub, Geofrey Nyang'oro na Fidelis Butahe.

 
<font size="3">mnh ajabu sana bw jussa kuwapondelea mbali ccm ati wamechoka na hawana jipya kwanza wamekosa mwelekeo hvo wanahitaji kupumzishwa,ssa najiuliza mbna kule zenji hawa mabwana wamefunga ndoa?</font>
<br />
<br />
Sema PIA WALIYOPIGWA NAYO MAGWANDA, LEO AIBU IMEWAKUTA MHHHHHHHH
 
Teh teh teh teh, achana na hiyo lugha ni ngumu kwako.
Wewe jikite zaidi kwenye lugha yako ya Kichagga, ulisoma wapi shule ya kata ya Kishumundu
Scrantty!! bado ujanijibu mpaka leo hilo neno lina maana gani?
 
mlipiga kelele madiwani madiwani kwisha kazi, sasa shibuda, twawauliza lowasa, na chenge vipi?

Unadhani miaka 50 ya experience ni mchezo, subirini mjifunze ku deal na migogoro ndani ya chama, unadhani la Arusha sterling mwisho ni nani? Muulizeni DR Slaa leo alikuja hapa kutaka kuleta uwongo wake watu wamemshushia fact katoka nduki huko kumsaidia Josephine kufunga diaper.
 
mi ningeona ni vema nape atoe majibu yanayoendana na maswali anayoulizwa, na sio kujibu kiujanjajanja kuwapumbaza watanzania.
Nyie MAGWANDA HUU NDANI MSAIDIENI MARANDO KUJITETEA KWANINI AMEKUBALI KUWA WAKILI WA MAFISAIDI WA EPA???? We Nape wewe....mona umemwadhiri babu wa watu HUJUI HUYO NDIO HIRIZI YA CHADEMA????
 
Hi Wajumbe;

Leo pia tumeshuhudia mjadala mhimu sana wa itikadi za vyama ambapo vyama vikuu viliongozwa na watu wake wanaoaminika huko. Matokeo hayo hapo juu yanatokana na sifa za kimjadala. Katika mijadala hii imeonekana bado Chadema inaongoza na kuwaacha wengine kutokana na pengine havijaweza kupata kitu cha kuwafanya wasimame wima yaani bado they are bittiing around the bush kutokana na makandokando yao ya kimuonekano ktka jamii; CCM ikiwa na tatizo kubwa kiuongozi na kushindwa kusimamia maamuzi kwa usahihi; CUF nayo ikionekana kama msindikizaji wa CCM katika mambo yake yote ikiwemo swala la posho; kutosimama kama wapinzani ktk sehemu mbalimbali za maamuzi pale walipi na nafasi hiyo yote yanawafanya vijana wake wanaotuwakilisha washindwe kusonga mbele.

Leo Ilikuwa hivi

Marando (Chadema): Alikuwa focused na swali aliloulizwa; alikuwa hatoki nje ya mada kwa ushabiki; alivumilia vijembe vya wapinzani wake na vingine hakuvijibu kama akiona havina tija; ameeleza itikadi kwa ufasaha na kujipambanua tofauti na wenzake; alijibu maswali yote magumu kwa ufasaha; swala la ufisadi kajieleza maana anatetea mafisadi dagaa mapapa wa ufisadi wa EPA hawajafikishwa mahakamani; hivyo wametolewa kafara na yeye ana wajibu kuwaokoa; swala la udini hakuenda ndani saana lakini alisimamia ktk utanzania na kuepuka kupoint fingures kitu ambacho ni mhimu ktk mjadala wa kitaifa na kwa kueleweka hakuulizwa maswali mengi sana kama wenzake

Nape (CCM): Alikuwa anazunguka zunguka kutokana na ukweli mambo mengi waliyoyaahiidi kama chama hawajatekeleza; ameulizwa maswali mengi kutokana na kutoelewa kwa watazamaji/wasikilizaji;baadhi ya aliyosema watazamaji waliyakaa pale pale kama lile la elimu; miaka hamsini ya utawala na maendeleo yake nk. Kwa ujumla alikuwa kisiasa zaidi na alikuwa hajui lipi lutawafurahisha watazamaji maana alikuwa anaonekana kama msanii zaidi na mnafiki mbele ya hadhira kuliko mtu anayesimamia kile anachoongea

Jusa (CUF): Yeye kama yeye kajitahidi kujieleza ingawa alipotosha baadhi ya hoja kama lile la arusha na kigoma kwa lengo la kufikisha ujumbe kuwa yeye yuko ktk serikali ya kitaifa hata Chadema wamewahi kuwa bila kujua alikuwa anapotosha; alikuwa anashughulikia persona attacks zaidi na kushindwa kueleza CUF ni chama cha aina gani kwa sasa aidha cha upinzani au chama tawala; swala la posho hajaeleza ni sehemu ya ilani yao au wanaidandia tu; amejitahidi kuelezea umhimu wa muungano ila hajaeleza kama kutakuwa na miungano je nafasi ya upinzani kama watch wa serikali iko wapi.

Kwa ujumla wote walijitahidi na mjadala ulikuwa mtamu ingawa mapungufu ya hapa na pale; nafikiri kipindi kijacho muda uongezwe zaid ili kutoa wigo kwa watu wengi kuulizwa maswali na k ujibiwa kwa ufasaha. Asanteni karibu. Hizi alama ni kwa mjibu wa analysis ambay nimeifanya tangu mjadala unaanza hadi mwisho bila kuwa biased.
 
Wakati wa mdahalo wa Star Tv, muda mwingi Nape alikuwa anakunjuakunjua mdomo utafikiri kuna kitu anatafuana.
Hii tabia anayo JK, si kawaida ya Nape lakini nafikiri kaiga kwa mkubwa wake JK.

Kwa kweli alikuwa ananikera. Utafikiri ndio amemaliza kula
kuberi iyo
 
Masaburi ya Matola matamu sana nayapenda ndio maana yake, umenipatata!
Hawa ndio wafuasi wa ccm wakikosa hoja uishia na maneno kama haya, mimi sitokujibu kwa style hii ila nitawaachia wadau wakuone ni mtu wa viwango gani.
Nikiiga tabia yako watu watashindwa kututofautisha. Hongera sana Great Thinker.
 
chadema washindwa kutamka itikadi yao hawaelewek kwenye mdahalo mara mrengo wa kat mara si sawa na cuf mara nguv ya umma
 
Marando is another Shibuda in the party.Anapenda madaraka huyu,eti anadai ukiona wenzako wanapambana kuiondoa CCM madarakani lazima ujiunge!!!!Bila shaka CDM ikiwa weak atahamia CCK huyu.

Teeeeh teeeeh......eti anadai amehama chama mara moja tu!!!!!Huyu kweli ni another Luhanjo kwa Jairo kuwa si bilioni moja ni milioni mia tano tu....ahaaaaa.
 
Wakati wa mdahalo wa Star Tv, muda mwingi Nape alikuwa anakunjuakunjua mdomo utafikiri kuna kitu anatafuana.
Hii tabia anayo JK, si kawaida ya Nape lakini nafikiri kaiga kwa mkubwa wake JK.

Kwa kweli alikuwa ananikera. Utafikiri ndio amemaliza kula
Na yeye kamwiga Bush G.W
 
Nyie MAGWANDA HUU NDANI MSAIDIENI MARANDO KUJITETEA KWANINI AMEKUBALI KUWA WAKILI WA MAFISAIDI WA EPA???? We Nape wewe....mona umemwadhiri babu wa watu HUJUI HUYO NDIO HIRIZI YA CHADEMA????
Walee ni wa tuhumiwa bado hawajahukumiwa, ana haki ya kuwatetea hili ni kutokana na taaluma yake.
Mbona CCM ina watetea na kuwalea wezi waliorudisha hela????
 
Masaburi ya Matola matamu sana nayapenda ndio maana yake, umenipatata!
Acha ujinga.We kweli umeoza.Huwa nikikuta posti zako naziruka kama kinyesi.Duh,huwa unachafua hali ya hewa sana humu wewe.
 
Ulikua mdahalo mzuri kiasi. Napei aliwalenga zaidi watazamaji wengi ambao uelewa wao wa mambo ya siasa ni mdogo. Na yawezekana wale wapenzi sugu wa CCM bado wamemuona shujaa. Jussa alikua popo,siyo ndege wala mnyama. Kwa upande wangu niseme huyu ndiye nlikua nahitaji zaidi kumsikiliza. Chama chake kinapita ktk wakati mgumu sana kisiasa huku bara. Ameshindwa kujua bara wanataka nini. Na hilo ndilo kosa kubwa amelifanya,jinsi ile ile kinavyokosea chama chake. Marandu ameongea zaidi kama mwanasheria kuliko mwanasiasa. Kwa level ya uelewa wa watu wengi nadhani kuna ambao hawakumwelewa. Kwa ujumla wa wote 3, Marandu amenifurahisha zaidi. Kama tungekua na waandishi ama wachunguzi mahari wangechimba sana kwanini amesema wezi wa EPA bado hawajashitakiwa mahakamani.
 
wasira%20na%20mboye%20ana%20kwa%20ana.jpg
 
Back
Top Bottom