Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

Toka lini Marando akawa kada wa CHADEMA? Dr Slaa angetuma mtu anayeifahamu CHADEMA. Marando anaifahamu vizuri NCCR-MAGEUZI.
 
Jussa kaielezea vizuri itikadi ya cuf ambayo ni ya mlengo wa kati,lakini pia ushirikiano wa cuf na ccm sio jambo kutokana na hali maalum ya kisiasa ya zanzibar,kama ilivyo kwa nchi nyingine zenye hali maalum mf.kenya,zimbabwe,uingereza n.k.zilishawahi kuwepo serikali za vyama zaidi kimoja ujerumani,ufaransa n.k. Nape naye kafanya vizuri kuutetea ujamaa tatizo ni kwamba misingi ya ujamaa watangulizi wake wameishavunja hivyo ikampa nafasi jussa kuisambaratisha hoja ya ujamaa.marando ni mzungumzaji mzuri lakini hana mizizi ya chadema tulitaka kuona mwanachadema mwenya kuielewa vizuri cdm,marando kawaacha watanzania hawaijui ITIKADI YA CDM.hata wachangiaji wa jf analiyemwelewa atusaidie ITAKADI ya cdm ni ipi?.UJAMAA ambao Ccm wanajinasibu nao,au ULIBERALI ambao cuf ndio itikadi yao. Au UBEPARI?.wanaosema marando kafanya vizuri watueleze.
 
Mvutano mkali wa hoja uliibuka katika mdahalo uliopewa jina la Itikadi za vyama vya siasa na Tanzania tunayoitaka, ambao mwakilishi wa chama cha wanainchi (CUF), Jussa Ismail Ladhu aling'ara kutokana na hoja zake kuonekana kuwazidi nguvu wenzake, Mabere Marando wa CHADEMA na Nape Nnauye wa CCM.

Jussa aling'ara katika mdahalo huo uliofanyika juzi jioni Dar es salaam ambao uliandaliwa na Taasisi ya Vox Media huku ukiwa umetawaliwa na vijembe vya hapa na pale vya watoa hoja hao upande mmoja na wafuasi wao nao wakikosoana kwa malumbano kwenye ukumbi huo wa mkutano kwa upande mwingine.

Kung'ara kwa Jussa kulionekana dhahiri wakati wa swali kuhusu itikadi za vyama hivyo baada ya kueleza vyema itikadi ya CUF huku washiriki wenzake Marando na Nape, wakizungumza kadri walivyoweza lakini wakishindwa kufafanunua kikamilifu itikadi zinazofuatwa na vyama vyao.

source Mwanainchi.

 
huo mfumo wa kati umemsaidiaje mtz? Na hao ccm niwaambie tu kuwa ujamaa, usoshalist ni kitu kimoja. Labda ukomunist ndio tofauti. Lenin alikiri kuingia kwenye ubepari ili kuwa na taifa la uzalishaji kupitia viwanda. Leo hii tunahubiriwa ujamaa uliozongwa na ubinafsishaji.

Bila kujali itikadi, nyerere alishaweka misingi ni nini cha kufanya. Alisema, tuna maadui watatu; ujinga, maradhi na umasikini. Hadi leo hatujaweza kukabiliana kwa ufasaha na yeyote kati yao.

haya, ili kukabiliana nao akasema tunahitaji vitu vinne; watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

1. Watu ni wagonjwa. Ni wajinga. Hawana maarifa ya kutosha. Wasomi ndio makuwadi. Kuna nini hapo?


2. Ardhi iko wapi? Kuhusu ardhi mtafuteni Mwalimu Bashiru awaeleze vizuri na Haki Ardhi yao

3. Siasa ya leo tunaijua na kuiona. Sina mengi hapo

4. Uongozi bora ndo huo wa kuwa reactive. Rais anakuwa reactive? Watendaji wake waweje?

sijatoka nje ya mada. Kama tunataka kujinasua hapa hatuna haja ya kuangalia angani kutafuta majibu. Cha msingi ni njia zipi zitumike kufikia hayo majibu. Nani kang'ara ni upuuzi tu
 
Aliyesema kupenda ni nusu ya uchizi alikosea. Kupenda ni ujinga, utaahira na uwendawazimu 100% ! Cdm nawaonea huruma kwa kupenda jina la chama tru lol ! Sina chama ila jussa alikuwa ,yuko na atakuwa zaidi ya juu , tatizo hili jukwaa ni kwa ajili ya chadema for gud only , hata wakipotoka wataambiwa bahati mbaya ! Kwa staili hii cdm wakipewa nchi itakuwa ni zaidi ya ccm coz itakuwa ni kusifia tuuu hata sukari ikiwa 20,000/kg! Tuache kupenda mithili ya wendawazimu aaagh !
 
HUYU NAE NI GREAT THINKER ! KAZI IPO . This is tundu lusu hasa !
 
Mvutano mkali wa hoja uliibuka katika mdahalo uliopewa jina la Itaikadi ya vyama vya siasa na Tanzania tunayoitaka, ambao mwakilishi wa chama cha wananchi (CUF) Ismail Jussa alingara kutokana na hoja zake kuonekana kuwazidi nguvu wenzake Mabere Marando wa Chadema na Nape Nnauye wa CCM.
Kung'ara kwa Jussa kulionekana dhahiri wakati wa swali kuhusu itikadi za vyama vya siasa baada ya kueleza vyema itikadi ya CUF, huku washiriki wenzake Marando na Nape wakizungumza kadri wanavyoweza lakini wakashindwa kufafanua kikamilifu itikadi zinazofuatwa na vyama vyao......


Source: Mwananchi 29/08/2011

Hakika hawa wana tofauti kubwa sana. Huwezi hata siku moja kumfananisha Jussa na hao wote akina Marando wala Nape.

Hakika Jussa ni mwanasheria mahir sana na kwa wanaomjua ni mtu ana akali sana shuleni na ana uzoefu mkubwa sana wa siasa kama msaidizi wa Maalim Seif.

Nachelea kusema kuwa hapo ni sawa na kupambanisha mlima na kichuguu kitu ambacho si sawia.
 
Toka lini Marando akawa kada wa CHADEMA? Dr Slaa angetuma mtu anayeifahamu CHADEMA. Marando anaifahamu vizuri NCCR-MAGEUZI.

Kwa Jussa, hata Dr Slaa asingemuweza kwani Jussa ana uzoefu mkubwa sana na mtu makini sana kuliko Dr Slaa. Lakini cha Ziada mwenzake amesomea sheria tofauti na Dr Slaa ambaye amesomea sheria za kanisa katoliki.
 
Hakujibu Swali ila katukana at the same time

Panya anayekula Quran Msikitini na hakuna anayeshangaa ina Maana kuwa Ni bora CCM kuwa na Viongozi wanaojuana toka familia Moja

Huku Yeah wakiwa Msikitini watashangaa akila Biblia sababu ni watu nje ya familia ya kindungu ndani ya CCM
 
Mwandishi wa gazeti hili tunamjua ni mfuasi wa chama gani.Tunaomba kabla ya kuandika habari kama hii atuambie kwanza harakati zake za kuwania ujumbe wa baraza kuu cuf zimefikia wapi?
 
SWALI HILI NI GUMU SN KWA CCM KWANI LINA UKWELI MTUPU HVY hata ANGEULIZWA NYERERE INGEMUWIA VIGUMU SN KULIJIBU SAWASAWA NA WATU WAKAMWELEWA NA KURIDHIKA
 
Kwa Jussa, hata Dr Slaa asingemuweza kwani Jussa ana uzoefu mkubwa sana na mtu makini sana kuliko Dr Slaa. Lakini cha Ziada mwenzake amesomea sheria tofauti na Dr Slaa ambaye amesomea sheria za kanisa katoliki.
Huyu atakuwa sio Jussa huyu aliyepewa Ubunge na JK! Kama ni yeye tema mate chini. Sifa hizi ulizomlundikia hana.
 
Mh. Jussa amethibitisha na kuonyesha tofauti kati ya chama cha siasa chenye itikadi sahihi inayoelezeka na kueleweka na "genge la wajasiriamali" wanaotumia siasa kujingezea mitaji ya biashara na uwekezaji
 
Jussa alisema itikadi ya CUF ilibadilika kutoka kwenye sera ya utajirisho na kuwa ya uliberali wa kati na kuongeza; 'Tulipoanzisha chama tulisema hivyo, lakini tulibadilisha katika Mkutano Mkuu wa mwaka 2009. Tulisema hatutaki ujamaa wala ubepari, bali uliberali wa kati.

"Binadamu mwenyewe ana haki ya kusimamia misingi yake, kuheshimu haki za binadamu, Demokrasia na utawala wa sheria uliberali wa CUF siyo wa kulia wala kushoto."

Alikiponda CCM kwa kutumia sera ya ujamaa na kujitegemea huku kikiwa kimeuza mashirika yote na kutegemea wafadhili kwa asilimia 40.

Pia alikirushia kombora chadema akisema kimeshindwa kupambanunua sera yake na kuwaonya watanzania kutokishabikia, "nawaonya watanzani kutoshabikia vyama visivyokuwa na mwelekeo wa kiitikadi. kule zambia MMD iliingia kwa nguvu ya umma, ikapoteza mwelekeo kwa muda mfupi"

Source mwananchi 29/8/2011.
 
mm si mshabiki wa vyama vya siasa ila wakati nasoma posti za wengi kuhusu huu mjadala, wengi waliwapongeza kwa asilimia viongozi hao kwa vyama wanavyoshabikia, kutokana na cuf kutokua na nguvu sana hapa jf kulingana na cdm na ccm bac jusa alikua akishika mkia kimaoni, kwa vile nilishawahi kumuona jusa kwenye mijdala kadhaa nlishangaa kidogo na koment za watu, lkn kutokana na hiyo saurce hapo juu, nimelazimika kuwaomba wana jf tuwe wa kweli panapo ukweli hii ndio sifa ya great thinkers

Hilo ni gumu sana na bora unyamaze mkuu hapa anaeshabikiwa hata akiongea utumbo atasifiwa na asieshabikiwa hata akikaanga maini yake wanajf wale watamponda!
 
Mh. Jussa amethibitisha na kuonyesha tofauti kati ya chama cha siasa chenye itikadi sahihi inayoelezeka na kueleweka na "genge la wajasiriamali" wanaotumia siasa kujingezea mitaji ya biashara na uwekezaji
Itikadi sahihi ni pamoja na ule muafaka? Katiba ya JMT imeukataa ule muafaka!
 
Itikadi sahihi ni pamoja na ule muafaka? Katiba ya JMT imeukataa ule muafaka!

Kwanza ujifahamu ww usiyoijuwa itikadi ya chama chako, halafu uje hapa useme huo "uliberali wa kati" una reflect vipi na "muwafaka?", muwafaka haukufanywa kwa katiba ya JMT kwa kuwa haihusu mambo ya Zanzibar!
 
Back
Top Bottom