Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

Nilikuwa makini nifatilia mdahalo kati ya Jusa (CUF), Nape (CCM) na Marando (CDM). Jamaa walijitahidi kujibu maswali ila kama kawaida wote mwanzoni walielekeza mashambulizi kwa CDM jambo lililotuonesha wazi kuwa CDM ni chama pinzani na CCM na wapinzani wengine.

Nape mbali na majibu ya ulaghai na udanganyifu mimi nilipenda alipoulizwa kuwa kwanini viongozi wa CCM wanarithishana uongozi na madaraka kwa watoto wao, kuwa mtoto wa Makamba, mtoto wa Nnauye, Mwinyi, Kikwete, nk.

Hivi ndivyo Nape alivyojibu. " Ni vyema tukamtuhumu mtu kwa utendaji wake. NAMKUMBUKA BABA YANGU MAKAMBA ALIWAHI KUSEMA KUWA PANYA WA MSIKITINI ATAKULA QURAN NA HAITASHANGAZA MTU. ILA IKIKUTWA YUKO MSIKITINI ALAFU ANAKULA BIBLIA BASI WATU WATAPIGWA BUTWAA"

Nilipenda sentensi hiyo iliyokolezwa kwa rangi nyekundu. Kwakifupi alimaanisha kuwa mtu aliyenje ya CCM atakiwi kuingia na huyo ni kama biblia kupatika msikitini

Unaonesha jinsi uelewa wako ulivyo mpana sana kupindukia, Unanchekesha.
 
Hi\o asilimia umezitoa wapi? kwa formula ipi? masaburi?
 
'PANYA WA MITAANI' TANZANIA JAPO TUKO WENGI SANA LAKINI HAKI YETU KWA MUJIBU WA CCM NI 'KULA BIBLIAA TU' NDIPO HATUWAPIGISHI WATU BUTWAA KUDANDIA KURANI

Kuhusiana na CCM, mwenendo wake KURITHISHANA UONGOZI WA TAIFA LETU kwa misingi ya VIZAZI TEULE kama ambavyo alivyotubainishia huyu dogo Nape, ni vema tena inatupasha vijana wapiga kura wa kesho tukafikirie upya uhusiano wetu na hiki chama kilichokwishawaponyoka WAKULIMA na WAFANYAKAZI umiliki wake.

Bila ajizi tena hivi sasa ni muda mwafaka Vijana tusikua na udugu na kiongozi yeyote huko wala jamaa katika ule mtandao wao TUKAFIKIRIE UPYA NA KI-UNDANI ZAIDI kabla hatujaonekana PANYA WA MITAANI ambaye haki yake ni KULA BIBLIA na wala si KURANI AMBAYO NI HAKI NA MILIKI YA PANYA MSIKITINI kama ambavyo vizazi teule nchini wanavyoonekana kuendelea kutafuna bila aibu.

Kwa kauli hii ni kielezo tosha ni nini sababu ya Wakulima na Wafanyakazi wasio na uhusiano wowote na wanamtandao jinsi ambavyo inakua ni ndoto kubwa kuelekea kileleni kukiongoza CCM wala serikali yake zaidi ya Mtaalam wa Giza, Profesa Maji Marefu wa Korogwe, kupigiwa chapuo la ki-aina.

Nape, asante sana kwa kutuwekea kweupe huu mfumo tata wa miaka mingi hivi sasa CCM kurithishana uongozi kwa watoto wao hata bila ya uzoefu wowote wa ngazi za chini. Ama kweli Tanzania yetu hii hata KIJANA MKATA MAJANI NYUMBANI KWA WAZIRI naye pia ni waziri wa ki-aaina vile.

KEEEERRRRRRRRRRRRRRRRRROOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Tusio na ndugu wala jamaa huko kwenye network kazi ipo?
 
utakuwa umesimuliwa Marando alichemka kupita maelezo , even ze part ideology ? Kituko , bora comedian Nape kiasi ! ILA JUSA ALIWAFUNIKA SANA SANA SANA INGAWA ALIULIZWA MASWALI MENGI ! CUF NI WAKOMAVU KTK SIASA UTAKE USITAKE MTOA MADA ! GEUZA MAKSI FASTA ! JUSSA 60% , NAPE 25% NA BABA MKWE AKA MARANDO 15 % , Kama ulikuwa unaangalia mdahalo kwa kutumia macho na ubongo ,ILA KAMA ULIKUWA UNAANGALIA KWA MASABURI ACHA MAKSI ZAKO !

Naenda thread nyingine maana hapa watu tunanajadili na wenye kufuata moyo ukipenda na wengine tunajaribu kupambanua na kuelimishana kwa misingi ya kitaaluma, kwa hiyo ni sawa kwa wengine jambo usilojua ni sawa na usiku wa kiza.

Nape na Jusa ni sawa na mashabiki wa mpira uwanjani wanachojua iwe kosa au lisiwe kosa goli lazima lifungwe, na kama timu yake imefungwa kwa uhalali goli hilo halihalalishwi.

Mwamko wa kitaifa na kujali maendeleo ya taifa letu yanafunikwa na watu kama hawa wasiothamini hoja za msingi kwa kipa umbele moyo ukipenda.

Nilihudhuria kwa bahati mdahalo wa Obama na MaCain kugombea urais Marekani uliofanyika mara ya mwisho Volunteer State karibu na Vernderbirt university baada ya kusafiri masaa 8 kwa gari kuwahi mdahalo huo licha ya uchovu wasafari ya angani masaa 7 toka Heathrow airport. Nilichojifunza Obama alikuwa anajibu swali aliloulizwa na kutoa point zenye kueleweka kuliko McCain ambaye alikuwa na mashambulizi binafsi kwa Obama na wazungu hawakupenda hali hiyo na wengine papo hapo walisema wazi sitampa Makain kura zangu hajibu hoja ila mashambulizi binafsi.
Wazurungu walisema, "McCain, oh ****ing shit guy, no point at all, I'm gona vote against him. Obama is the real wonderful guy ever." Na huo mdahalo ulimpandisha chati sana Obama.

Hayo ndiyo tunayowaambieni na kujaribu kuelimishana kutokana na uzoefu wetu. Jibu hoja si kumshambulia mtu binafsi ni kushindwa hoja.

Hoja ya Marando kutetea mafisadi mahakamani ni utaratibu wa kisheria ambao hata serikali mtuhumiwa wa kesi ya mauaji kama hana uwezo wa kupata mwanasheria wa kumtetea serikali hiyo hiyo itatoa mwanasheria wa serikali atakayemtetea mtuhumiwa dhidi ya serikali. Wenye upeo mdogo ndo hawaelewi hayo.
 
Hili la Nape Mnauye, jukumu la kunadi CCM na UTETEZI wake kwa mfumo usiorasmi wa kurithishana uongozi kwa vizazi teule moja kwa moja ni swala nyeti lenye kero sugu nchini ambalo ufumbuzi wake upo kwenye UTUNGAJI WA KATIBA MPYA nchini, uimarishaji wa etekelezaji wa SHERIA ZA MAADILI YA VIONGOZI NCHINI na kutokomeza kabisa hii rushwa ya kupendeleana kupeana uongozi chini ya mfumo wa 'MWENZETU' nchini.
 
Duh ! Watanzania kweli tuna safari ndef, yaani vijembe na majungu ndo vimekuwa vipimo vyetu vya kuonyesha mtu kufanya vizur? Kama ulifuatilia kwa makini jusa na nape walijikita kwenye majungu na fitina zaidi badala ya kujadili mada;
Marando alijikita kwenye hoja zaidi hakuwa na muda wa vijembe kama alivyofanya jusa na nape. Matokeo haya nakubaliana nayo 100% na kwa anaye pinga basi yuko uchi akilini
 
ubora wa mtu ktk kujieleza sio utulivu wake tu kama wengi mlivyochotwa kihisia na Jussa bali FACTS! Asilimia 95 ya aliyosema Marando zilikuwa facts tupu na sio propaganda! Propaganda haziwezi kushindana na FACTS ever!
 
Mvutano mkali wa hoja uliibuka katika mdahalo uliopewa jina la Itaikadi ya vyama vya siasa na Tanzania tunayoitaka, ambao mwakilishi wa chama cha wananchi (CUF) Ismail Jussa alingara kutokana na hoja zake kuonekana kuwazidi nguvu wenzake Mabere Marando wa Chadema na Nape Nnauye wa CCM.

Kung'ara kwa Jussa kulionekana dhahiri wakati wa swali kuhusu itikadi za vyama vya siasa baada ya kueleza vyema itikadi ya CUF, huku washiriki wenzake Marando na Nape wakizungumza kadri wanavyoweza lakini wakashindwa kufafanua kikamilifu itikadi zinazofuatwa na vyama vyao......


Source: Mwananchi 29/08/2011
 
Wewe wasi wasi wako ni nini, mpe Marando hata alama 100000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000000% kama unadhani hii itakupa relief, lakini ukweli unaujua mwenyewe na viongozi wa magwanda siku nyingine watajifunza kupeleka watu wenye akili timamu sio huyo frustrated advocate.
Walewale, badala ya kukabiliana na hoja zilizopo unakuja na personal attacks. Ndio maana wanasema Marando aliwafunika wenzie kimdahalo kwa kuwa alizingatia kanuni za midahalo,hakufanya personal attacks kwa yeyote yule kama walivyofanya wenzie.
 
Ameelezea kama CUF wanategemea lini kumzallia mumewe CCM?
 
Hii ni kauli mbaya sana ambao CCM isipotoa kauli ya kuirekebisha itakuwa inazidi kujichimbia kaburi.
 
Kama unazungumzia weupe ni kweli alingara maana ni mweupeee! ila kama ni hoja ni ziro
 
Inawezekana mfano wake haukuwa sahihi sana lakini ufafanuzi wake ulieleweka kwa yeyote mwenye kupenda kuelewa! Nakumbuka ktk ufafanuzi wake alisema yeye ni mtu aliyekulia katika mazingira ya CCM kiasi kwamba hata alipokuwa mtoto alikuwa akichukuliwa na babake kwenda kwenye mikutano!!! Kutokana na hilo, sio ajabu kuona nae akiingia kwenye CCM kv amekulia huko ni kama mtoto wa mfugaji anayekulia ktk mazingira ya ufugaji. Akaenda mbali na kusema kwamba yeye yupo CCM kwa ajili ya kubebwa bali kutokana na uwezo wake hivyo angependa apimwe kutokana na uwezo wake kuliko vinginevyo!! Kimsingi, huo ndio ukweli wenyewe; kwani kama issue ni kv baba ake alikuwa kigogo wa chama na serikali basi nafasi hiyo angepewa m2 ambae bado ana support ya mzazi kuliko m2 ambae mzazi wake amefariki miaka kadhaa iliyopita! Hakuna asiyefahamu uwezo wa Nape kkt kucheza na propaganda za kisiasa, hivyo sina shaka yeyote kwamba pale alipo imetokana na uwezo wake zaidi kuliko vinginevyo!! Wata wana-CCM wenyewe wanafahamu kwamba Nape ni m2 anayekubalika na wengi kutokana labda na tabia yake ya kuwa muwazi na firm kwa kile anachokiamini.

Nape ni muongo, zuzu, na elimu yake ni ndogo sana. Kwanza hajakaa na babake, ni mtoto wa nje ya ndoa allikuwa katelekezwa kijijini anaishi na mamake..babake kaja kamuokota ukubwani. Anasema kasoma kijijini, halafu anadai alipokuwa mtoto alikuwa akichukuliwa na babake kwenda kwenye mikutano ya CCM. Babake hakuwa anakaa kijijini, alikuwa hakai na babake, ni muongo na ndo mana hata elimu yake haipishani sana na madereva wa wizarani sababu alikuja mjini ukubwani ikabidi apelekwe shule za voda fasta.
 
Sasa mlitaka ajibu vipi???? Huo si ndiyo ukweli wenyewe kuwa kina NAPE ni panya wa msikitini? Au mlitaka ajibu adanganye?
 
Mimi si mshabiki wa vyama vya siasa ila wakati nasoma posti za wengi kuhusu huu mjadala, wengi waliwapongeza kwa asilimia viongozi hao kwa vyama wanavyoshabikia, kutokana na CUF kutokua na nguvu sana hapa JF kulingana na CHADEMA na CCM basi Jusa alikua akishika mkia kimaoni.

Kwa vile nilishawahi kumuona jusa kwenye mijdala kadhaa nlishangaa kidogo na koment za watu, lkn kutokana na hiyo saurce hapo juu, nimelazimika kuwaomba wana jf tuwe wa kweli panapo ukweli hii ndio sifa ya great thinkers.
 
Mvutano mkali wa hoja uliibuka katika mdahalo uliopewa jina la Itaikadi ya vyama vya siasa na Tanzania tunayoitaka, ambao mwakilishi wa chama cha wananchi (CUF) Ismail Jussa alingara kutokana na hoja zake kuonekana kuwazidi nguvu wenzake Mabere Marando wa Chadema na Nape Nnauye wa CCM.

Kung'ara kwa Jussa kulionekana dhahiri wakati wa swali kuhusu itikadi za vyama vya siasa baada ya kueleza vyema itikadi ya CUF, huku washiriki wenzake Marando na Nape wakizungumza kadri wanavyoweza lakini wakashindwa kufafanua kikamilifu itikadi zinazofuatwa na vyama vyao......

Source: Mwananchi 29/08/2011

Katika magazet machache ninayaamin hapa nchini ni pamoja na Mwananchi. Ila katka hili napingana nao, kwanza hawatueleza kuwa majibu ya utafiti wao waliyapataje?
 
Sio ushabiki, zitajwe facts alizozungumza Jussa hapa, zipo chache sana, ile haiba yake ya utulivu ndio iliyowachanganya. Hata JK anasifika kwa haiba ya utulivu anapojenga hoja.
 
Back
Top Bottom