Moja, Hongera mama, seems una kipaji cha mipasho, hapo kwenye red panaweza kukupa ajira leo tena au kile kipindi cha mitaarabu cha tbc.
Pili, Mitazamo inaweza kutofautiana. Nape ni mzungumzaji mzuri. Lakini ili uelewe kama anaongea pumba au point ni lazima na wewe uwe unajua mambo, lazima ufahamu wako uwe sawa na wake katika hilo jambo au ufahamu wako uwe mkubwa zaidi katika hicho anachokizungumza, kama wewe mwenyewe kichwani ni mweupe umeumia, na hiki ndicho kilichomkumba nipe tano na kwa hili nitatoa mifano.
1. Nape anasema CCM inaamini na kutekeleza sera za ujamaa, Tofauti kubwa kati ya sera hizi tatu, yaani ubepari, ulibelari na ujamaa ni namna uchumi wa nchi unavoendeshwa, nani anamiliki uchumi. Sifa mbili kubwa za sera ya Ujamaa ni uchumi kumilikiwa na umma na kujikita katika kupunguza tafouti ya kipato kati ya mtu na mtu, Je hiki ndicho CCM wanachosimamia, Nipe tano unaelewa nachozungumza au nshakupeleka kina kirefu? sema tu mama niko tayari kukuelekeza taratibu, sitaki kumuacha mtu nyuma
NOTE: Hakuna Ujamaa wa kisayansi na ujamaa wa kiafrika, hapa msiojua ndio nape anapowapiga bao, mnashabikia tu.
2.Kwamba serikali yake inajitajidi kuwamilikisha wananchi ardhi, yeye akasema eti huku ndio kumilikisha wananchi uchumi, kuna matatizo mawili hapa, moja hii si kweli hata kidogo kwamba serikali inajitahidi kumilikisha wananchi uchumi, Unajua nini kinatokea katika MKURABITA na kinachotokea katika UBINAFSISHAJI na kuna kile kingine wanaCCM wanakipenda sana UWEKEZAJI? kila kimoja ni page nyingi kama nikiamua kuvieleza. Pili, hata kama hii ingekua kweli (Kwamba seikali inajitahidi kuwamilisha watanzania uchumi wao) bado tusingekua tunatekeleza itikadi za ujamaa kwa sababu tungekua tunauacha uchumi wetu mikononi mwa mtu mmoja mmoja, na katika hali hii nguvu ya soko ndio inaamua mambo (huu ni ubepari na sio ujamaa), unakumbuka mwezi wa pili JK alivochemka na kupanga bei ya sukari, leo (miezi sita tu badae) sukari inauzwa sh ngapi?, Unakumbuka kuhusu mafuta mwanzo mwa august leo wiki tatu tu badae mafuta yanauzwaje? nguvu ya soko inaamua mambo na sio order kutoka state house!
Sijaribu kusema ubepari ni mbaya la hasha ila ninapata mashaka kama nape anajua anachokiongea na kama wanaomshangilia wanajua wanachoshangilia.
Mwandhishi wa comment hii ni mchumi kuanzia 2006, anajua vizuri kuhusu UJAMAA, ULIBELARI na UBEPARI, kama tukidiscuss kila kimoja labda utachoka kusoma, ila kwa kifupi NAPE anachanganya sana mambo, kama anashindwa kunifikia anaweza kupata ushauri kwa JUSA bse yeye alionekana anaelewa vizuri tofauti ya hizo itikadi tatu