Mkuu kuna wakati hawa watu wa media wanapotosha sana ukweli wa mambo. Wanaposema CCM wanarithishana uongozi wana maana gani? Ni nani CCM aliyerithi uongozi kutoka kwa baba yake?
Sioni tofauti kwa watoto wa wana CCM kuingia madarakani kwa style ya George Bush sr wa Marekani, au kwa style ya Yar'adua wa Nigeria.
Wanaozungumziwa huwa wanachaguliwa (yaani wanapigiwa kura) au wanateuliwa. Inawezekana kuwa kuna upendeleo fulani au kuna njama fulani zinazofanyika kabla ya kupata nafasi ya kupigiwa kura au kuteuliwa, lakini it is still far far away from kuritishwa.
Kulia, kucheka zote ni kelele tu!Mkuu kuna wakati hawa watu wa media wanapotosha sana ukweli wa mambo. Wanaposema CCM wanarithishana uongozi wana maana gani? Ni nani CCM aliyerithi uongozi kutoka kwa baba yake? Sioni tofauti kwa watoto wa wana CCM kuingia madarakani kwa style ya George Bush sr wa Marekani, au kwa style ya Yar'adua wa Nigeria. Wanaozungumziwa huwa wanachaguliwa (yaani wanapigiwa kura) au wanateuliwa. Inawezekana kuwa kuna upendeleo fulani au kuna njama fulani zinazofanyika kabla ya kupata nafasi ya kupigiwa kura au kuteuliwa, lakini it is still far far away from kuritishwa.
ulikuwa unatumia kiungo gani kufikiria kuanalyse? katika hali ya kawaida na kwa kutumia common sense Marando alichemsha. nasishauri chadema wamrudishe tena kwenye mjadala kama ule. mbona chadema kuna watu wengi tu makini. kwa nini wasimpeleke mtu kama zitto, slaa, lissu? Jussa wa CUF alijieleza vizuri sana in comparision with others. utaliona hili kama hauko bias tu. Otherwise you wont see it.Hi Wajumbe;
Leo pia tumeshuhudia mjadala mhimu sana wa itikadi za vyama ambapo vyama vikuu viliongozwa na watu wake wanaoaminika huko. Matokeo hayo hapo juu yanatokana na sifa za kimjadala. Katika mijadala hii imeonekana bado Chadema inaongoza na kuwaacha wengine kutokana na pengine havijaweza kupata kitu cha kuwafanya wasimame wima yaani bado they are bittiing around the bush kutokana na makandokando yao ya kimuonekano ktka jamii; CCM ikiwa na tatizo kubwa kiuongozi na kushindwa kusimamia maamuzi kwa usahihi; CUF nayo ikionekana kama msindikizaji wa CCM katika mambo yake yote ikiwemo swala la posho; kutosimama kama wapinzani ktk sehemu mbalimbali za maamuzi pale walipi na nafasi hiyo yote yanawafanya vijana wake wanaotuwakilisha washindwe kusonga mbele.
Leo Ilikuwa hivi
Marando (Chadema): Alikuwa focused na swali aliloulizwa; alikuwa hatoki nje ya mada kwa ushabiki; alivumilia vijembe vya wapinzani wake na vingine hakuvijibu kama akiona havina tija; ameeleza itikadi kwa ufasaha na kujipambanua tofauti na wenzake; alijibu maswali yote magumu kwa ufasaha; swala la ufisadi kajieleza maana anatetea mafisadi dagaa mapapa wa ufisadi wa EPA hawajafikishwa mahakamani; hivyo wametolewa kafara na yeye ana wajibu kuwaokoa; swala la udini hakuenda ndani saana lakini alisimamia ktk utanzania na kuepuka kupoint fingures kitu ambacho ni mhimu ktk mjadala wa kitaifa na kwa kueleweka hakuulizwa maswali mengi sana kama wenzake
Nape (CCM): Alikuwa anazunguka zunguka kutokana na ukweli mambo mengi waliyoyaahiidi kama chama hawajatekeleza; ameulizwa maswali mengi kutokana na kutoelewa kwa watazamaji/wasikilizaji;baadhi ya aliyosema watazamaji waliyakaa pale pale kama lile la elimu; miaka hamsini ya utawala na maendeleo yake nk. Kwa ujumla alikuwa kisiasa zaidi na alikuwa hajui lipi lutawafurahisha watazamaji maana alikuwa anaonekana kama msanii zaidi na mnafiki mbele ya hadhira kuliko mtu anayesimamia kile anachoongea
Jusa (CUF): Yeye kama yeye kajitahidi kujieleza ingawa alipotosha baadhi ya hoja kama lile la arusha na kigoma kwa lengo la kufikisha ujumbe kuwa yeye yuko ktk serikali ya kitaifa hata Chadema wamewahi kuwa bila kujua alikuwa anapotosha; alikuwa anashughulikia persona attacks zaidi na kushindwa kueleza CUF ni chama cha aina gani kwa sasa aidha cha upinzani au chama tawala; swala la posho hajaeleza ni sehemu ya ilani yao au wanaidandia tu; amejitahidi kuelezea umhimu wa muungano ila hajaeleza kama kutakuwa na miungano je nafasi ya upinzani kama watch wa serikali iko wapi.
Kwa ujumla wote walijitahidi na mjadala ulikuwa mtamu ingawa mapungufu ya hapa na pale; nafikiri kipindi kijacho muda uongezwe zaid ili kutoa wigo kwa watu wengi kuulizwa maswali na k ujibiwa kwa ufasaha. Asanteni karibu. Hizi alama ni kwa mjibu wa analysis ambay nimeifanya tangu mjadala unaanza hadi mwisho bila kuwa biased.
Nilikuwa makini nifatilia mdahalo kati ya Jusa (CUF), Nape (CCM) na Marando (CDM). Jamaa walijitahidi kujibu maswali ila kama kawaida wote mwanzoni walielekeza mashambulizi kwa CDM jambo lililotuonesha wazi kuwa CDM ni chama pinzani na CCM na wapinzani wengine.
Nape mbali na majibu ya ulaghai na udanganyifu mimi nilipenda alipoulizwa kuwa kwanini viongozi wa CCM wanarithishana uongozi na madaraka kwa watoto wao, kuwa mtoto wa Makamba, mtoto wa Nnauye, Mwinyi, Kikwete, nk.
Hivi ndivyo Nape alivyojibu. " Ni vyema tukamtuhumu mtu kwa utendaji wake. NAMKUMBUKA BABA YANGU MAKAMBA ALIWAHI KUSEMA KUWA PANYA WA MSIKITINI ATAKULA QURAN NA HAITASHANGAZA MTU. ILA IKIKUTWA YUKO MSIKITINI ALAFU ANAKULA BIBLIA BASI WATU WATAPIGWA BUTWAA"
Nilipenda sentensi hiyo iliyokolezwa kwa rangi nyekundu. Kwakifupi alimaanisha kuwa mtu aliyenje ya CCM atakiwi kuingia na huyo ni kama biblia kupatika msikitini
Nilikuwa makini nifatilia mdahalo kati ya Jusa (CUF), Nape (CCM) na Marando (CDM). Jamaa walijitahidi kujibu maswali ila kama kawaida wote mwanzoni walielekeza mashambulizi kwa CDM jambo lililotuonesha wazi kuwa CDM ni chama pinzani na CCM na wapinzani wengine.
Nape mbali na majibu ya ulaghai na udanganyifu mimi nilipenda alipoulizwa kuwa kwanini viongozi wa CCM wanarithishana uongozi na madaraka kwa watoto wao, kuwa mtoto wa Makamba, mtoto wa Nnauye, Mwinyi, Kikwete, nk.
Hivi ndivyo Nape alivyojibu. " Ni vyema tukamtuhumu mtu kwa utendaji wake. NAMKUMBUKA BABA YANGU MAKAMBA ALIWAHI KUSEMA KUWA PANYA WA MSIKITINI ATAKULA QURAN NA HAITASHANGAZA MTU. ILA IKIKUTWA YUKO MSIKITINI ALAFU ANAKULA BIBLIA BASI WATU WATAPIGWA BUTWAA"
Nilipenda sentensi hiyo iliyokolezwa kwa rangi nyekundu. Kwakifupi alimaanisha kuwa mtu aliyenje ya CCM atakiwi kuingia na huyo ni kama biblia kupatika msikitini
Moja, Hongera mama, seems una kipaji cha mipasho, hapo kwenye red panaweza kukupa ajira leo tena au kile kipindi cha mitaarabu cha tbc.
Pili, Mitazamo inaweza kutofautiana. Nape ni mzungumzaji mzuri. Lakini ili uelewe kama anaongea pumba au point ni lazima na wewe uwe unajua mambo, lazima ufahamu wako uwe sawa na wake katika hilo jambo au ufahamu wako uwe mkubwa zaidi katika hicho anachokizungumza, kama wewe mwenyewe kichwani ni mweupe umeumia, na hiki ndicho kilichomkumba nipe tano na kwa hili nitatoa mifano.
1. Nape anasema CCM inaamini na kutekeleza sera za ujamaa, Tofauti kubwa kati ya sera hizi tatu, yaani ubepari, ulibelari na ujamaa ni namna uchumi wa nchi unavoendeshwa, nani anamiliki uchumi. Sifa mbili kubwa za sera ya Ujamaa ni uchumi kumilikiwa na umma na kujikita katika kupunguza tafouti ya kipato kati ya mtu na mtu, Je hiki ndicho CCM wanachosimamia, Nipe tano unaelewa nachozungumza au nshakupeleka kina kirefu? sema tu mama niko tayari kukuelekeza taratibu, sitaki kumuacha mtu nyuma
NOTE: Hakuna Ujamaa wa kisayansi na ujamaa wa kiafrika, hapa msiojua ndio nape anapowapiga bao, mnashabikia tu.
2.Kwamba serikali yake inajitajidi kuwamilikisha wananchi ardhi, yeye akasema eti huku ndio kumilikisha wananchi uchumi, kuna matatizo mawili hapa, moja hii si kweli hata kidogo kwamba serikali inajitahidi kumilikisha wananchi uchumi, Unajua nini kinatokea katika MKURABITA na kinachotokea katika UBINAFSISHAJI na kuna kile kingine wanaCCM wanakipenda sana UWEKEZAJI? kila kimoja ni page nyingi kama nikiamua kuvieleza. Pili, hata kama hii ingekua kweli (Kwamba seikali inajitahidi kuwamilisha watanzania uchumi wao) bado tusingekua tunatekeleza itikadi za ujamaa kwa sababu tungekua tunauacha uchumi wetu mikononi mwa mtu mmoja mmoja, na katika hali hii nguvu ya soko ndio inaamua mambo (huu ni ubepari na sio ujamaa), unakumbuka mwezi wa pili JK alivochemka na kupanga bei ya sukari, leo (miezi sita tu badae) sukari inauzwa sh ngapi?, Unakumbuka kuhusu mafuta mwanzo mwa august leo wiki tatu tu badae mafuta yanauzwaje? nguvu ya soko inaamua mambo na sio order kutoka state house!
Sijaribu kusema ubepari ni mbaya la hasha ila ninapata mashaka kama nape anajua anachokiongea na kama wanaomshangilia wanajua wanachoshangilia.
Mwandhishi wa comment hii ni mchumi kuanzia 2006, anajua vizuri kuhusu UJAMAA, ULIBELARI na UBEPARI, kama tukidiscuss kila kimoja labda utachoka kusoma, ila kwa kifupi NAPE anachanganya sana mambo, kama anashindwa kunifikia anaweza kupata ushauri kwa JUSA bse yeye alionekana anaelewa vizuri tofauti ya hizo itikadi tatu