Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

nakubaliana na wewe inawezekana; lakini jambo haliwi kweli kwa kuwa fulani tu kasema ila kwa mienendo na matendo ya wahusika tena kwa ushahidi ulio dhahiri. Hebu tupe kaushahidi kokote kwamba chadema ni cha wakristo angalau kwa tabia na mienendo ya wafuasi wao.
ukitaja oic, mahakama ya kadhi wanazomea
 
ivi zile hotuba za JK... za mwisho wa mwezi kazipotezea??? tunamuhitaji yeye.. na sio watoto hawa wakina NAP
<br />
<br />
amebanwa kidogo na ziara za dunia. Anazungusha bakul kuomba kibaba ili ajazie bajeti.
 
Nilikuwa makini nifatilia mdahalo kati ya Jusa (CUF), Nape (CCM) na Marando (CDM). Jamaa walijitahidi kujibu maswali ila kama kawaida wote mwanzoni walielekeza mashambulizi kwa CDM jambo lililotuonesha wazi kuwa CDM ni chama pinzani na CCM na wapinzani wengine.

Nape mbali na majibu ya ulaghai na udanganyifu mimi nilipenda alipoulizwa kuwa kwanini viongozi wa CCM wanarithishana uongozi na madaraka kwa watoto wao, kuwa mtoto wa Makamba, mtoto wa Nnauye, Mwinyi, Kikwete, nk.

Hivi ndivyo Nape alivyojibu. " Ni vyema tukamtuhumu mtu kwa utendaji wake. NAMKUMBUKA BABA YANGU MAKAMBA ALIWAHI KUSEMA KUWA PANYA WA MSIKITINI ATAKULA QURAN NA HAITASHANGAZA MTU. ILA IKIKUTWA YUKO MSIKITINI ALAFU ANAKULA BIBLIA BASI WATU WATAPIGWA BUTWAA"

Nilipenda sentensi hiyo iliyokolezwa kwa rangi nyekundu. Kwakifupi alimaanisha kuwa mtu aliyenje ya CCM atakiwi kuingia na huyo ni kama biblia kupatika msikitini

Inawezekana mfano wake haukuwa sahihi sana lakini ufafanuzi wake ulieleweka kwa yeyote mwenye kupenda kuelewa! Nakumbuka ktk ufafanuzi wake alisema yeye ni mtu aliyekulia katika mazingira ya CCM kiasi kwamba hata alipokuwa mtoto alikuwa akichukuliwa na babake kwenda kwenye mikutano!!! Kutokana na hilo, sio ajabu kuona nae akiingia kwenye CCM kv amekulia huko ni kama mtoto wa mfugaji anayekulia ktk mazingira ya ufugaji. Akaenda mbali na kusema kwamba yeye yupo CCM kwa ajili ya kubebwa bali kutokana na uwezo wake hivyo angependa apimwe kutokana na uwezo wake kuliko vinginevyo!! Kimsingi, huo ndio ukweli wenyewe; kwani kama issue ni kv baba ake alikuwa kigogo wa chama na serikali basi nafasi hiyo angepewa m2 ambae bado ana support ya mzazi kuliko m2 ambae mzazi wake amefariki miaka kadhaa iliyopita! Hakuna asiyefahamu uwezo wa Nape kkt kucheza na propaganda za kisiasa, hivyo sina shaka yeyote kwamba pale alipo imetokana na uwezo wake zaidi kuliko vinginevyo!! Wata wana-CCM wenyewe wanafahamu kwamba Nape ni m2 anayekubalika na wengi kutokana labda na tabia yake ya kuwa muwazi na firm kwa kile anachokiamini.
 
Hata mimi nilivoangalia niliona Jussa kawabwaga wenzake tena kwa asilimia kubwa,sasa nashangaa unakuja na hoja kama hiyo au tuseme ndo ule msemo si chongo ni kengeza,na ndio maana mara nyengine nakua sipendi kupita hata njia hapa siku hizi maana watu kama nyinyi mnatuharibia ile JF yenyewe hasa,ushabiki mbele halafu ndo ukweli... lol! kazi kweli kweli.

plz changanua kama mwenzako sio kuropoa hovyo hovyo
 
mnaongelea nini maana mi nilikuwa bize naangalia mpira jinsi man utd ilivokuwa inampakaza magundi Aseno...hii mnayoongelea ni nini kwani?
 
CDM ilifanya vizuri jana, Nape na Jussa waliungana kupambana na CDM.

Siku ingine Nape, Msekwa , Mwigilu na Ndugai waletwe wapambane na mjumbe mmoja wa CDM, labda wanaweza kumzidi.
 
Kwa mtazamo wangu hii midaalo magamba wataikimbia tena tu kwani hawana hoja wanaishia kuzunguka ktk kujibu maswali bila kutoa jibu sahihi
 
Kwa maoni yangu -- CDM ni 75%, CCM 20% na CUF 5%. Marando alikuwa top of the world!
 
Huyo Jussa alikuwa anatetea nini? Ndoa? Nasikiavyo Prof Lipumba hakufurahishwa na kitu hii hawa wanaCUF wa Zanzibar wanachofanya. Mtu wa karibu yake amenidokezea kuwa Prof angependelea mtu wa Bara, kama vile Mtatiro ndiyo angekuwa ktk Mdahalo.

Hata hivyo Marando aliwacharaza vibaya sana wenzake.
 
Panya wa Msikitini hula Kurani, akila Biblia watu hupigwa na BUTWAAAA sio?????????????????????
 
Marando kashindwa kueleza Itikadi ya Chadema! Hata hapa JF wanachama wa Magwanda hawajui Itikadi ya Chama chao! Nguvu ya Umma Sio Itikadi ni falsafa! Magwanda nawauliza tena Itikadi(Imani) ya Chama chenu ni nini? Jana Nape na Jussa wamefanya vizuri kwenye mdahalo huwezi linganisha na yule mzee wenu Marando
 
Nadhani Nape alijitahidi sana. Hivi kweli mtu ukiambiwa kwenda mbele ya kadamnasi ukatetee chama hoi km CCM utaenda ukaseme nini? Kwanza kule kukubali tu kwenda kwenye mdahalo inataka moyo.
 
CDM ilifanya vizuri jana, Nape na Jussa waliungana kupambana na CDM.

Siku ingine Nape, Msekwa , Mwigilu na Ndugai waletwe wapambane na mjumbe mmoja wa CDM, labda wanaweza kumzidi.

Penye red: Na hapo ndipo CUF huwa inajididimiza na kukimbiwa na wafuasi. na hii yote inatokana na ndoa na ndiyo maana alichaguliwa Jussa (mwanandoa) kuliko tatiro.

CUF Bara inabidi iamke sasa, itoe agizo kwa wafuasi na viongozi wao kwamba CCM ndiyo adui wao mkubwa, na si CDM.
 
Back
Top Bottom