Mdahalo Star Tv: Nape, Jussa na Marando

Nazisoma sifa kemkem za hawa mashujaa wenu lakini hadi sasa hivi sijaona lolote linalohusiana na kichwa cha Mada - ITIKADI ZA VYAMA VYA SIASA NA TANZANIA TUNAYOITAKA"..

 
Kutokana na maneno hayo ya Nape. Hii inatupa jibu tosha kwamba kumbe ccm inaogopa kuwatimua EL na AC kwa kuhofia kusambaratika.
 
magwanda leo aibu imewakuta jussa kawasasambua kawaacha uchi mabere kapwaya mno, jussa ni mwanasiasa mzuri anajua kujibu maswali na kujenga hoja.
 
kusema ukweli MABELE kafunika na cuf na ccm ni aibu tupu. nape alitamani kutoroka. na ndiyo niligundua kuwa cuf ni ya dini fulani, kwa kuwa maswali kwa cdm yaliulizwa na watu walovaa mavazi ya dini yangu. nimejisikia vibaya kwa kweli.
 
mjadala mzuri ila uwezo wa Nape ni mdogo sana. CUF wamejitahidi ila siasa zao hazitufai bara. Marando tatizo mtangazaji alikuwa anamnyonga muda halafu cuf walipeleka wahuni wakawa wanamzomea. CUF si wastaarabu hata kidogo. mijadala mizuri ungefanyika mwingine uwahusishe makatibu wakuu
 
halafu ni chama cha dini kabisa si mliona hata maswali waliyokuwa wanauliza akina dada wa cuf?
 
Jussa alijitahidi kujibu hoja vizuri ila pia watu wa cuf walikuwa wanauliza maswali kidini sana na kuonesha cuf ni chama cha kidini kabisa!
 
Tukiacha ushabiki wa kichama, Jussa aliwafunika kwa mbali Marando na Nape. Alikuwa fasaha na haku-panic. Marando alichemka vibaya hasa juu ya UNAFIKI wa kuwasema watuhumiwa wa EPA jukwaanu na kuwatetea KORTINI Sikujua kama Marando ni mweupe kiasi kile! Kuhusu kuzomea wafuasi wa CUF wamejifunza kutoka kwa CDM kumbuka midahalo iliyopita CDM ilikuwa inajaza watu wanazomea kusha munajitangazia ushindi!
 
Acha ujinga.We kweli umeoza.Huwa nikikuta posti zako naziruka kama kinyesi.Duh,huwa unachafua hali ya hewa sana humu wewe.
Nadhani wewe ndio mjinga zaidi, kama huwa unaziruka post zangu leo imekuaje umeisoma.
Nikiangalia ID yako wewe ni mchangga vili vile ni katika wale Mateka wa Mbowe.
Tatizo Pro-CDM-JF, wengi ni pumba hawataki watu waikosoe CDM, nakushari usisome posts zangu utakuwa unaumia endelea kuziruka sawa Mangi, Aikambeee
 
halafu ni chama cha dini kabisa si mliona hata maswali waliyokuwa wanauliza akina dada wa cuf?

Hapo kwenye red; hata mimi nashangaa sana behaviour hii ya wafuasi wa CUF. Mavazi si tatizo ila mienendo na hoja zao - always religious oriented na kaubaguzi ubaguzi fulani hivi. Iko hivi:

Kwa upande wa Tz Bara, CUF isahau, in fact sidhani kama wana mpango wowote, kupata kiti chochote cha ubunge wa majimbo hapo baadaye ukiacha hicho kimoja walichobahatisha hapo Lindi mjini last election. Kwa kuwa wana MoU na CCM, CUF watakuwa wanatumika kuvuruga popote pale ambapo chama kingine cha upinzani kitakapokuwa na nguvu hasa "MAENEO YENYE WAISLAMU WENGI" kwa faida ya CCM.

Kwa hii MoU ya CCM na CUF, kuna kazi ya ziada kuitoa CCM madarakani; as long as kwa upande wa Zanzibar CUF wanayo huruma ya CCM kuwa madarakani; kwa upande wa Bara ni heri tukose wote (upinzani). Hizo ndio siasa za CUF za kidinidini na kinafikinafiki - usashangae hata Bungeni wanaungwa mkono na CCM, wanajua (CCM) wanachokipata toka CUF, yaani CUF inatumika na CCM ama kwa kujua, kutokujua, au kwa ujinga tu na zigo kuu waliloachiwa CUF waibebee CCM ni UDINI huku CCM ikijionesha safi mbele ya jamii.
 
Wote c walewale, kuwatenganisha CUF na CCM ni sawa na kuwatenganisha mume na mke wanaoelewana na kupendana sana tu!
 
Mada zingine hazipaswi kuingia humu,mfano mada ya kimajungumajungu kama hii inatafuta nini humu? Yaani kweli kwa akili zako tuanze kula unit kwa kujadili mdomo wa NAPE kweli? hebu usiwe mvivu wa kufikiri kama huna kitu cha kuweka tukijadili acha, sio kuleta mambo ya kipuuzi great thinkers tujadilli, au basi ungepeleka mada hii huko kwenye vituko sio hapa ambapo tunahitaji mijadala yenye afya yenye kuleta mstakabali mzuri wa taifa letu, kwakweli hata mimi umenikera sana, ni bora uwe msomaji tu sio kuanzisha topic za kitoto kama hii.
Ndugu kama umekereka, nafikiri Nape anakuwezesha, ni haki yako kuudhika, pole sana. Kwani lazima uchangie kama unaona ni upuuzi waachie wengine.
Nape ni mwanasiasa lazima tabia zake zijadiliwe katika jukwaa la siasa.
 
Ulikua mdahalo mzuri kiasi. Napei aliwalenga zaidi watazamaji wengi ambao uelewa wao wa mambo ya siasa ni mdogo. Na yawezekana wale wapenzi sugu wa CCM bado wamemuona shujaa. Jussa alikua popo,siyo ndege wala mnyama. Kwa upande wangu niseme huyu ndiye nlikua nahitaji zaidi kumsikiliza. Chama chake kinapita ktk wakati mgumu sana kisiasa huku bara. Ameshindwa kujua bara wanataka nini. Na hilo ndilo kosa kubwa amelifanya,jinsi ile ile kinavyokosea chama chake. Marandu ameongea zaidi kama mwanasheria kuliko mwanasiasa. Kwa level ya uelewa wa watu wengi nadhani kuna ambao hawakumwelewa. Kwa ujumla wa wote 3, Marandu amenifurahisha zaidi. Kama tungekua na waandishi ama wachunguzi mahari wangechimba sana kwanini amesema wezi wa EPA bado hawajashitakiwa mahakamani.
Great Thinker @ work. huu ni uchambuzi mahiri wa ule mdahalo wa jana, kudos!
 
Mbona CDM nacho ni chama cha Wakisrito, au ndio mambo ya Nyani

Nakubaliana na wewe inawezekana; lakini jambo haliwi kweli kwa kuwa fulani tu kasema ila kwa mienendo na matendo ya wahusika tena kwa ushahidi ulio dhahiri. Hebu tupe kaushahidi kokote kwamba CHADEMA ni cha wakristo angalau kwa tabia na mienendo ya wafuasi wao.
 
hali halisi itavunja ndoa tu siku moja, ndoa zote zinaanzaga kwa upendo mkuu. wats-see ze foto watabloo na kugundua wameingizwa chaka! ngoja bei za sukari ziwatandike sawasawa, ama hawakai bongo?

Wote c walewale, kuwatenganisha CUF na CCM ni sawa na kuwatenganisha mume na mke wanaoelewana na kupendana sana tu!
 
tuseme ukweli japo unaumwa marando katuangusha, jussa kawafunika vibaya, na hili suala la kutumia udini tukubali kuwa ni kwel mimi naliona kanisani habari ya huku ni cdm, tuwakemee hawa viongozi wetu wa dini huku makanisani wanatuharibia chama
 
Nimewasikiliza hawa jamaa ktk mdahalo wao jana nikapata yafuatayo
-nape anasema ccm inatumia mbinu za kibepari kujenga ujamaa
Jussa anadai cuf wanaamini ktk liberalism ccm na sera zake wamechoka na wao wameungana nao zanzibar kwa sababu ya matatizo ya kihistoria na wameunganisha baadhi ya itikadi
-Marando akasema Cdm wao wanajidhihisha kwa matendo yao na sio kusema unafata itikadi fulani kimaneno na kimaandishi na kumbe kivitendo ni itikadi nyingine
Wadau tuyajadili nasi hapa ili tuwekane sawa
 
Aaah!!!! Hahahaaaa!! JADILINI ALIVYOWAPAKATIA LEO MAGWANDA TEPETEPE MNALOOO!!!! Kumbe ndo MAANA HUWA MNAMJADILI SANA HUMU KUMBE MNAJUA KIBOKO YENU

Moja, Hongera mama, seems una kipaji cha mipasho, hapo kwenye red panaweza kukupa ajira leo tena au kile kipindi cha mitaarabu cha tbc.

Pili, Mitazamo inaweza kutofautiana. Nape ni mzungumzaji mzuri. Lakini ili uelewe kama anaongea pumba au point ni lazima na wewe uwe unajua mambo, lazima ufahamu wako uwe sawa na wake katika hilo jambo au ufahamu wako uwe mkubwa zaidi katika hicho anachokizungumza, kama wewe mwenyewe kichwani ni mweupe umeumia, na hiki ndicho kilichomkumba nipe tano na kwa hili nitatoa mifano.

1. Nape anasema CCM inaamini na kutekeleza sera za ujamaa, Tofauti kubwa kati ya sera hizi tatu, yaani ubepari, ulibelari na ujamaa ni namna uchumi wa nchi unavoendeshwa, nani anamiliki uchumi. Sifa mbili kubwa za sera ya Ujamaa ni uchumi kumilikiwa na umma na kujikita katika kupunguza tafouti ya kipato kati ya mtu na mtu, Je hiki ndicho CCM wanachosimamia, Nipe tano unaelewa nachozungumza au nshakupeleka kina kirefu? sema tu mama niko tayari kukuelekeza taratibu, sitaki kumuacha mtu nyuma

NOTE: Hakuna Ujamaa wa kisayansi na ujamaa wa kiafrika, hapa msiojua ndio nape anapowapiga bao, mnashabikia tu.

2.Kwamba serikali yake inajitajidi kuwamilikisha wananchi ardhi, yeye akasema eti huku ndio kumilikisha wananchi uchumi, kuna matatizo mawili hapa, moja hii si kweli hata kidogo kwamba serikali inajitahidi kumilikisha wananchi uchumi, Unajua nini kinatokea katika MKURABITA na kinachotokea katika UBINAFSISHAJI na kuna kile kingine wanaCCM wanakipenda sana UWEKEZAJI? kila kimoja ni page nyingi kama nikiamua kuvieleza. Pili, hata kama hii ingekua kweli (Kwamba seikali inajitahidi kuwamilisha watanzania uchumi wao) bado tusingekua tunatekeleza itikadi za ujamaa kwa sababu tungekua tunauacha uchumi wetu mikononi mwa mtu mmoja mmoja, na katika hali hii nguvu ya soko ndio inaamua mambo (huu ni ubepari na sio ujamaa), unakumbuka mwezi wa pili JK alivochemka na kupanga bei ya sukari, leo (miezi sita tu badae) sukari inauzwa sh ngapi?, Unakumbuka kuhusu mafuta mwanzo mwa august leo wiki tatu tu badae mafuta yanauzwaje? nguvu ya soko inaamua mambo na sio order kutoka state house!

Sijaribu kusema ubepari ni mbaya la hasha ila ninapata mashaka kama nape anajua anachokiongea na kama wanaomshangilia wanajua wanachoshangilia.

Mwandhishi wa comment hii ni mchumi kuanzia 2006, anajua vizuri kuhusu UJAMAA, ULIBELARI na UBEPARI, kama tukidiscuss kila kimoja labda utachoka kusoma, ila kwa kifupi NAPE anachanganya sana mambo, kama anashindwa kunifikia anaweza kupata ushauri kwa JUSA bse yeye alionekana anaelewa vizuri tofauti ya hizo itikadi tatu
 
Back
Top Bottom