Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Mchungaji Gwajima: Daudi Albert Bashite alipata division Zero

Kuna mahusiano yeyote kati ya Daudi na Gwajima na kama hayapo inawezekana familia zao kujuana toka awali ?

Baada ya kuwa Mkuu wa Mkoa kuna mabadiliko gani ya ghafla yamefanyika kijijini hapo?

Kijiji hicho kina jumla ya wanakijiji wangapi na vipi kuna ripoti ya vichaa kwenye kijiji hicho?

Ukiacha Daudi na Gwajima ni nani mtu mwingine maarufu anaetokea kijijini hapo?

Familia ya Daudi ina jumla ya watoto wangapi na ni wangapi wapo hadi sasa hapo kijijini?

Daudi na Gwajima nani kajenga kwao (nyumba ya kufikia)

Umbali wa kutoka kwao Daudi na Gwajima ni mwendo wa dakika ngapi?

Wanakijiji wa kijiji hicho sifa yao kuu ni ipi?

Ukimaliza kujibu nitakuwa nimefahamu hicho kijiji na watu wake !!!!!
Akijibu unishtue mkuu
 
Kumbuka ya Lugumi Mkuu hadi hii leo hata kuitaja hatari. Tusishangae Mkuu tusilolitegemea linaweza kabisa kutokea na kutuacha tukishika vichwa na midomo wazi.

Baada ya mchungaji kuweka kila kitu hadharani kuhusu bwana fulani na hatua zikachukuliwa, kwakweli sitapongeza bali nitashangaa sana na nitabaki na maswali yafuatayo kichwani mwangu.

Hivi inakuwaje mchungaji awe na details zote hizo alafu mh.sana asiwe nazo?

Hata kama mwanzoni alikuwa hana taarifa hizi,alishindwa kuagiza uchunguzi ufanyike?

Kama aliagiza ina maana muda wote huu tangu tuhuma hizi zianze kusambaa uchunguzi ulikuwa bado haujakamilika?

Kama mtu binafsi amepata taarifa zote hizi iweje wao washindwe kuzipata tena ndani ya muda mfupi zaidi maana wao wana kila resources?

Kama aliagiza na kupewa taarifa ina maana alipewa taarifa za uongo?

Kama alipewa taarifa za kweli mbona hakuchukua hatua?

Kama alipewa taarifa za uongo basi tunatarajia kuona waliomdanganya wanachukuliwa hatua.

Kama mchungaji kasema uongo basi tunatarajia kumuona akiitwa na kuhojiwa na kisha kuchukuliwa hatua na hili lisipofanyika basi tutamuamini mchungaji.
 
Baada ya kusikiliza sauti ya Baba akiongea na wanawe. Alizungumzia juu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda na akadai amefoji VYETI na jina Hilo si la kweka. Katika Hilo sina la kusema.

Turudi kwa MCHUNGAJI kwa kumbukumbu zangu, mchungaji ni mkaz wa Mwanza na nilianza kumfahamu pale alipomtusi Cardinal Pengo. Nilifatilia zaidi nikagundua kuwa naye alisoma pamba sekondari na alikua kiongoz wa ukwata na form four pia alipata *** kama anabisha alete cheti hadharani na ndalichako ahakiki.
Muhimu::: TUNAOMBA VYETI VYAKO MCHUNGAJI
 
Amesha bashite kwenye kazi, ni mitafaruku na maigizo badala ya maendeleo na elimu bora, aende tu.
 
Swali ni kwamba yeye naye kasoma pamba sekondari aliposoma makonda. Je yeye alipata nini kuna haja ya kumtaka atuoneshe vyake maana nasikia anaitwa dr. Siku hizi
 
Uhakiki wa vyeti una furahisha sana,kwani wanakutaka utaje majina matatu ya wanafunzi uliosoma nao,wako wapi?!
Huyu ndugu,amekuwa akiwadhalilisha watumishi,na sasa ameingia kwa wasanii na wafanyabiashara.!
Kwa kutaka sifa,sasa na yeye anafuatiliwa historia yake!,
Njia aliyoitumia,ya kuwadhalilisha wengine,sasa na yeye anadhalilishwa kwa utaratibu ule ule aliokuwa anautumia kudhalilisha wengine.!
Hii ni aibu kwa Mkuu wake wa kazi na viongozi wengine wasiofuata kanuni na taratibu katika kutenda kazi zao!
 
Maswala haya hayana Itikadi, Mwacheni Ale Mchunga alioupanda, Angetulia zake na Kufanya Kazi Katika Mandate yake na Kwa Nidhamu na Kwa Utu, haya yote yasingempata. Mimi siku Makufuli alipomsifu Makonda kwenye Mkutano wa Wazee nilianza kuhofia Judgement ya Magufuli. Nikaona somehow wanashabihiana! Na alipotangaza kamteua Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Nilinawa Mikono kama Pilato. kisha nikalala kama aliyefiwa na mtu wa Karibu.

Kushabihiana Kwao kunaweza kuwa hata kwenye Maswala yw Vyeti Tatanishi, Na nafikiri iwapo Mkuu hatamfumua huyo entity, basi nitaanza Kuamini pengine kweli yale Madai ya PHdii ya Maganda yw Nini nayo ni Nanilii kama ya huyu Kiumbe! Ila akimtumbua hakuna sababu yakuamini huo uvumi tena.

This fellow is a Deplorable and Irredeemable Bigoted Buffoon! a Drama Queen who probably could as well be a Hermaphrodite trapped in Ovotestis condition.
 
Nasikia
Kama sio CG FM basi VOT(Voice of Tabora)radio ya Rage huko Tabora ndo yupo huyo mwenye jina halisi Paul Christian.
 
Inaweza kuwa ni kweli lakini sioni mantiki kwa anayejiita mtumishi tena wa Mungu kuendeleza vita. Siku zote watumishi wa kweli humkabidhi Mungu vita vyao. Daudi akasema Mungu pigana na wanaopigana nami...zaburi 35:1b
Hapo tayari na wewe umeshakosea kumnyoshea kidole mtumishi wa Mungu ,nakupa siku chache uombe msamaha
 
Swali ni kwamba yeye naye kasoma pamba sekondari aliposoma makonda. Je yeye alipata nini kuna haja ya kumtaka atuoneshe vyake maana nasikia anaitwa dr. Siku hizi

Alimaliza Form Four akafaulu, lakini akakataa kwenda A Level, akaamua kwenda Chuo cha Theologia au Seminary, Nairobi, Korea ya Kusini na Marekani, Kwani hapo Kuna Ubaya? Unafikiri Utaitwa kutow Lecture Marekani au Japan Ukiwa Ni Kilaza kama Nanilii? Jamaa Ukimsikiliza unadhani ni Kilaza?
 
Makonda huyo wa 199x - 20xx hakukuwa na vyeti vya div 0. Hata mie nimemaliza form four kipindi hicho hakukuwa na vyeti vya div 0
Vyovyote itakavyokuwa. Hapa kuna mtu kashashikwa pabaya. Muda utasema.
 
Gwajima weka pemben uchungaj yaweza kuwa ni karama tunataka vyeti vya daud bashite
 
Inaweza kuwa ni kweli lakini sioni mantiki kwa anayejiita mtumishi tena wa Mungu kuendeleza vita. Siku zote watumishi wa kweli humkabidhi Mungu vita vyao. Daudi akasema Mungu pigana na wanaopigana nami...zaburi 35:1b

Nyamaza kimya kwa kutojua Biblia kwa usahihi. Yesu alisema hesabu gharama kabla haujaenda kupigana vitani katika LUKA 14:31-32 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?
Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.

Yalimkuta Gwajima ni zaidi ya kutiwa kidole. Kwa hiyo anyamaze na kumwachia Mungu !?
UNATAKA NITIRIRIKE MAANDIKO ?
Inaweza kuwa ni kweli lakini sioni mantiki kwa anayejiita mtumishi tena wa Mungu kuendeleza vita. Siku zote watumishi wa kweli humkabidhi Mungu vita vyao. Daudi akasema Mungu pigana na wanaopigana nami...zaburi 35:1b

ngwajima huwa simuamini sijui kwanini . kabla ya yote aanze na stori ya Mbasha hapo nitamwelewa
 
Cheti cha zero hakipatikani Ndio sababu hata CCM wakisema Mbowe Ana zero ya form six huwa hawa semi cheti wanacho. Ukiwa Miongo uwe na Kumbukumbu.


Wekeni hadharani hayo Matokeo halisi ya Makonda na ya kughushi!

Mtu Mwenye akili akisikiliza vizuri hiyo audio utasikia namna ya usanii wa Gwajima kwa mfano anajiepusha kwa kutumia Maneno Kama vile a Wana Yule au Kiumbe Yule au kujifanya kasahau Jina la Makonda then Waumini ndio wanataja kwa Sauti then yeye anaendelea kutoa Maelezo. Huu ni aina ya Uongo ambao unausambaza kwa Njia za Ujanja ujanja ili usiingie kwny Mikono ya Vyombo vya sheriay
Kama ambavyo jina liliandikwa Philemon ili timbwili likianza isiwe tabuee. Mungu wetu huwa hachezewi. Tena ni mwaminifu sana.
 
Back
Top Bottom