Mchengerwa amsimamisha kazi Mganga mkuu sumbawanga Manispaa na wengine. Akiwamo Engineer na Afisa Manunuzi kwa matumizi mabaya ya pesa za miradi.
=====
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuwasimamisha kazi aliyekuwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Sumbawanga, Dkt. Archie Hellar, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi, Eng. Denis Eliakim na aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Obedi M.
Mwakalinga.Hatua hiyo imekuja baada ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufanya ukaguzi na ufuatiliaji maalum wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na vituo vya afya vya Mollo na Matanga katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na ukaguzi wa matumizi ukabaini uwepo wa kasoro mbalimbali zinazohusiana na ukiukwaji wa taratibu za fedha na ununuzi, usimamizi hafifu wa miradi uliochangia kutokamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya pamoja na kukosekana kwa ushirikishwaji.
“Matokeo ya ukaguzi na ufuatiliaji huo yamebainisha kuwa, miradi iliyofanyiwa ufuatiliaji ilipokea jumla ya Sh 3,990,259,916 na jumla Sh 3,932,705,441 zimetumika sawa na asilimia 98.56 ya fedha zote zilizopokelewa kutoka Serikali Kuu”“Kutokana na taarifa ya ukaguzi huo Waziri Mchengerwa ameielekeza TAKUKURU kuwachukulia hatua Watumishi wote waliobanika kusababisha changamoto kwenye miradi hiyo ikiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jacob Mtalitinya ambaye kwa sasa amehamia Taasis nyingine”