Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Mohamed O. Mchengerwa (Mb), amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busega moani Simiyu, ndugu Veronica Vicent Sayore, kuanzia leo tarehe 22 Septemba, 2023 ili kupisha chunguzi.
Mheshimiwa Mchengerwa, amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kuhusu utendaji kazi usioridhisha, kutokuwa na ushirikiano na viongozi wenzake pamoja na kutowashirikisha watendaji katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kutokana na tuhuma hizo, Mheshimiwa Waziri Mchengerwa amemwelekeza Katibu Muu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI kunda timu ya uchunguzi wa mwenendo wa utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo pamoja na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega.
Aidha, Mheshimiwa Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kusimamia dhana ya ushirikishwaji wa viongozi, watendaji na wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuimarisha mahusiano mazuri baina ya viongozi na watendaji ili kujenga timu yenye umoja katika kutekeleza jukumu la kuwahudumia wananchi.