Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sumbawanga, kuchukuliwa hatua kwa Usimamizi mbovu wa Miradi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,617
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwachukulia hatua watumishi wote waliobainika kusababisha changamoto kwenye miradi inayotekelezwa Sumbawanga akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa hiyo Jacob Mtalitinya.

Hatua hiyo inakuja baada ya Tamisemi kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na vituo vya afya vya Mollo na Matanga katika halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga na kubaini kasoro zikiwemo ukiukwaji wa taratibu za fedha na ununuzi.

Kasoro nyingine ni usimamizi hafifu wa miradi uliochangia kutokamilika kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya pamoja na kukosekana kwa ushirikishwaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa kitengo cha mawasiliano Tamisemi, miradi hiyo ilipokea jumla ya Sh3.99 bilioni na Sh3.93 bilioni zimeshatumika sawa na asilimia 98.5 lakini kumekuwepo kasoro zilizosababisha kutokamilika kwa miradi hiyo.

“Kutokana na taarifa ya ukaguzi huo Waziri Mohamed Mchengerwa ameielekeza Takukuru kuwachukulia hatua watumishi wote waliobanika kusababisha changamoto kwenye miradi hiyo ikiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jacob Mtalitinya ambaye kwa sasa amehamia taasisi nyingine.

“Halkadhalika, amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi kuwasimamisha kazi watumishi wafuatao: aliyekuwa mganga mkuu wa manispaa Dk Archie Hellar, aliyekuwa kaimu mkuu wa Idara ya Ujenzi Mhandisi Denis Eliakim pamoja na Obedi Mwakalinga ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha manunuzi” imeeleza taarifa hiyo.

Pia amemuelekeza Katibu Mkuu kuwachukualia hatua za kinidhamu na kisheria watumishi wote waliohusika kama walivyobainishwa kwenye matokeo ya ukaguzi na ufuatiliaji maalumu kwa kila eneo lenye kasoro.

Aidha mwisho Mchengerwa amepigilia msumari kuwa kuanzia sasa mtumishi yeyote wa mamlaka ya Serikali za mitaa atakayetenda kosa katika halmashauri X na kuhamishwa ama kustaafu atarejeshwa kwenye kituo chake cha kazi cha awali alichotenda kosa hilo na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: Mwananchi
 
Nayeye achukuliwe Sheria kutumia Mali ya umma gari la serikali la maliasili kwa matumizi binafsi wakat alishatoka kule, muosha uoshwa sio kwa wengine tu, matokeo mwandishi wa habari kaonekana mbaya aende polisi kutoa maelezo, wakati yule aliyechukua gari ndio haojiwe nchi gumu hii, kisa Kuna vichengera au watu wazito wanafanya watakavyo.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuwachukulia hatua watumishi wote waliobainika kusababisha changamoto kwenye miradi inayotekelezwa Sumbawanga akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa hiyo Jacob Mtalitinya.

Hatua hiyo inakuja baada ya Tamisemi kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na vituo vya afya vya Mollo na Matanga katika halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga na kubaini kasoro zikiwemo ukiukwaji wa taratibu za fedha na ununuzi.

Kasoro nyingine ni usimamizi hafifu wa miradi uliochangia kutokamilika kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya pamoja na kukosekana kwa ushirikishwaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa kitengo cha mawasiliano Tamisemi, miradi hiyo ilipokea jumla ya Sh3.99 bilioni na Sh3.93 bilioni zimeshatumika sawa na asilimia 98.5 lakini kumekuwepo kasoro zilizosababisha kutokamilika kwa miradi hiyo.

“Kutokana na taarifa ya ukaguzi huo Waziri Mohamed Mchengerwa ameielekeza Takukuru kuwachukulia hatua watumishi wote waliobanika kusababisha changamoto kwenye miradi hiyo ikiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jacob Mtalitinya ambaye kwa sasa amehamia taasisi nyingine.

“Halkadhalika, amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi kuwasimamisha kazi watumishi wafuatao: aliyekuwa mganga mkuu wa manispaa Dk Archie Hellar, aliyekuwa kaimu mkuu wa Idara ya Ujenzi Mhandisi Denis Eliakim pamoja na Obedi Mwakalinga ambaye alikuwa mkuu wa kitengo cha manunuzi” imeeleza taarifa hiyo.

Pia amemuelekeza Katibu Mkuu kuwachukualia hatua za kinidhamu na kisheria watumishi wote waliohusika kama walivyobainishwa kwenye matokeo ya ukaguzi na ufuatiliaji maalumu kwa kila eneo lenye kasoro.

Aidha mwisho Mchengerwa amepigilia msumari kuwa kuanzia sasa mtumishi yeyote wa mamlaka ya Serikali za mitaa atakayetenda kosa katika halmashauri X na kuhamishwa ama kustaafu atarejeshwa kwenye kituo chake cha kazi cha awali alichotenda kosa hilo na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: Mwananchi

Hii safi, kila mmoja abebe msalaba wake.
 
Mh wazuri piga marufuku walimu kusimamia ujenzi wa madarasa unaoendelea ,miradi mingi inashindwa kukamirika au inakamilika ukiwa chini ya kiwango
 
Back
Top Bottom