Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Hii nayo kali jamani kila siku ina kituko chake.
 
Hapana; dhambi ya kumfukuru Roho Mtakatifu haijatajwa adhabu yake; tunachofahamu ni kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti, na karama ya Mungu ni uzima wa milele". Hivyo dhambi zote mshahara wake ni mauti.



Mwanakijiji,

Tunaelemishana tu hapa. Hakuna mjuaji zaidi. Naanza kuthibitisha maneno yangu:

Marko 3:28:29 Amini nawaambia dhambi zote watasamehewa wanadamu na kufuru zao watakazokufuru zote, bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele.

Luka12:10 Na kila mtu atakayenena neno juu ya mwana wa adamu atasamehewa. bali atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa

Mathayo 12:31-32 Kwasababu hiyo nawaambia Kila dhambi na kila neno la kukufuru wanadamu watasamehewa, ila kumkufuru Roho hawatasamehewa.

Nadhani mwanakijiji na wenzake watakuwa wamejifunza kitu kipya hapo.

Asanteni

FP
 
Originally Posted by GAME THEORY

Nakumbuka mwaka 1992 gazeti la BUSINESS TIMES (enzi hizo lilikuwa refu kama mzalendo) lilitoa mlolongo wa tuhuma dhidi ya huyo mama na ile kesi yake na Mumewe.

Unajua pamoja na fitna zote hizo huyu mama mimi kwangu ni true definition of a HUSTLER...na kama nilivyosema hapo awali ile vita ya RWANDA ilimsaidia kwa kiasi kikubwa kwani aliwatumia vilivyo wale wakimbizi aliowajaza kwa MOSHI MAJUNGU... na wazungu wa CHICAGO lile liliwagusa mno na ukizingatia wengi wa wale wakimbizi walikuwa ni wakatoliki lakini huyu mama yeye hakujali na along the way wale ma evangelists toka CHICAGO waliona why not give her more money...na of course na yeye hapo akajipanga vizuri na zile TAX EXEMPTIONS alizokuwa akipata achilia mbali ukaribu wake na LUHIGO pale bandari ya Dar ambako of course alipewa misamaha ya kila namna

Sikumbuki kuandikwa na kwenye Business Times, lakini nakumbuka alishawahi kuandikwa kwenye Family Mirror na mhariri mmoja wa kizungu (Mama Tarimo)ambaye alikuwa anaishi jirani yake kule Mikocheni. Na issue iliyoandikwa kwenye hilo gazeti ilikuwa ni ile ya kontena la mitumba aliloliingiza nchini kwa ajili ya walio athirika na mafuriko ya Tanga.

Kuhusu wakimbizi wa Rwanda, ni kweli wale ndio waliompa breakthru. Alifanikiwa kuwashawishi baadhi ya Wanyarwanda wale kusali katika kanisa lake wakati huo lilikuwa linaendeshwa katika madarasa ya shule ya Ushindi, Mikocheni. Hapo ndipo wazungu wake waakanza kumwaga misaada. Wale wazungu walikuwa wanatuma kuanzia pesa, nguo, mpaka madawa. Speaking of madawa, guess yule mama alifanya nini na kontena za madawa?....Hint: Alifungua pharmacy yake pale kinondoni. You can guess the rest....

Wakati huo wa makontena ya madawa, kulikuwa na tetesi kwamba alikuwa anashirikiana na drug dealers wa kibongo kupenyesha madawa ya kulevya. Kuna dealer mmoja, ambaye alikuwa ni raia wa nchi mmoja West Africa (siikumbuki) alikuwa anaishi pale pale mikocheni. Na ilikuwa inasememkana kwamba yule dealer alikuwa anapenyeza mizigo yake ndani ya zile kontena. Na kwa sababu zile kontena zilikuwa zinaingizwa kupitia umbrela ya udini na kwa misaada ya wakimbizi, basi yalikuwa hayakaguliwi. Na kumbuka kipindi hicho tulikuwa na Bw. Rukhusa as our Head of State, plus MD wa bandarini alikuwa utahadhi Mzee Athumani Janguo. Hebu niambie mzigo gani ambao umgekumbwa na bughudha za kukaguliwa kama mwenye mzigo hataki uguswe?

Ile St. Mary alifungua na Filbert Bayi. Lakini down in the road, waligongana, basi yule mama akaamua kununua share zote za F. Bayi. Hapo ndipo F. Bayi akaenda kufungua shule yake. .

I'm not gonna get into details about watoto wake na uchungaji wake. kifupi ni kwamba, kama kuna kitu ame fail basi ni ulezi. Kati ya watoto 4, 1 tu ndio afadhali. Na hiyo afadhali yake ni kasheshe.

Anwyay, kama ulivyosema GT, huyu mama ni true hustler. Siku zote huwa ninasema, kati ya mama wajanja Tz, huyu mama ni #1...yuko chini sana #2 au 3. Ni mmoja wa wabongo walichuma juani na kula kuvulini kisawasawa. Kwa bahati mbaya michezo michafu mingi imekuwa involved in the process. But that's what Tanzania ilivyokuwa na ilivyo hivi sasa, who can blame her?? Hopefully, tunakokwenda ni kuzuri.
Kama shutuma zake za kuhusika na biashara ya bwibwi hawezi kukosa kuwarubuni kondoo wa bwana wajifanye misukule ili apate kodi ya jumapili nyingi
 
YOYO,

Biashara zake mi sijui. Ila mi nipo kwenye kuponya au kusaidia matatizo katika jamii.

FP
 
Mwanakijiji,

Tunaelemishana tu hapa. Hakuna mjuaji zaidi. Naanza kuthibitisha maneno yangu:

Marko 3:28:29 Amini nawaambia dhambi zote watasamehewa wanadamu na kufuru zao watakazokufuru zote, bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele.

Luka12:10 Na kila mtu atakayenena neno juu ya mwana wa adamu atasamehewa. bali atakayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa

Mathayo 12:31-32 Kwasababu hiyo nawaambia Kila dhambi na kila neno la kukufuru wanadamu watasamehewa, ila kumkufuru Roho hawatasamehewa.

Nadhani mwanakijiji na wenzake watakuwa wamejifunza kitu kipya hapo.

Asanteni

FP

FP; sikuwa sahihi kuwa adhabu ya kumkufuru Roho haikutajwa, imetajwa nayo ni kutokusamehewa. NIlikuwa nataka kusema uliposema kuwa adhabu ya kumkufuru Roho Mtakatifu siyo "kifo" haikuwa sahihi at least technically. Nilimaanisha kuwa kifo ni "mshahara wa dhambi" zote.

Nashukuru kwa kunielemisha!
 
Naona tunachanganya mada,hapa tunajadili uhusiano wa wafu,misukule,ndugu zao na process nzima ya kuwarejesha kwa ndugu zao. Na suala hapa si uwezo wa Kristo kuponya au uwezo wa mama mchungaji kuombea. Mungu ni Mungu na daima atabaki kuwa mwenye uwezo wote mamlaka yote ikiwa uponyaji,na miujiza. Suala hapa ni mtu kutumia vibaya uwezo na mamlaka hayo kusema Mungu kafanya hivi na kwa kuwa Mungu ni ultimate basi no one should dare question.

Leo mtoto wako akirudi nyumbani akasema baba nina hii alfu kumi,ukahoji umepata wapi, akakujibu ahh kweli Yesu ni mwema nilliishiwa pesa nikaomba,nikaomba na basi nilipomaliza kusali nikakuta hii alfu kumi kwenye kompasi langu. Na wewe kama mzazi utafanyaje?utasema Haleluya Bwana muweza yote kwa kumpa alfu kumi mtoto wangu au utapenda kujua kutoka kwa mwanao mazingira yaliyopelekea Muujiza utendeke?
Na je unapomuhoji mtoto juu ya hayo inamaana unamquestion Mungu juu ya nguvu zake au unapenda kujua zaidi ili umtukuze zaidi na uweze kumshuhudia kwa wengine?

Wakati mwingine huwa naishangaa hata idara zetu za upelelezi. Tunaambiwa watu walikufa ila hawakufa kweli (walichukuliwa misukule) baadae mchungaji kasaidia kuirudisha misukule hiyo. Theory is so simple, ili mama aongezewe credibility aseme jamani watu hawa walikufa na makaburi yao ni haya, na ndugu zake waliomzika ni hawa. Next aseme misukule yao ni hii tumeipata sehemu fulani na kwa neema za Mungu muweza yote (which I so firmly believe can do anything) amewarejesha uzimani.

Kuna tatizo gani kuainisha hata uhusiano wao na ndugu?
Je tutajuaje kama hao binadamu ni misukule au vichaa wa porini?
Tunajuaje hao waliowafuata ni ndugu zao?

wengine wanaweza kufikiri tunapohoji taarifa hizi hatuna imani na Nguvu za mungu, La hasha. Mbona akija mtu na magongo akaponywa hatuhoji? si tunamuona alikuwa mitaani anachechemea na sasa ameombewa amepona?


Binafsi napenda kujua uhusiano kati ya waliokufa,waliozikwa,misukule,ndugu za misukule na ikibainika ni kweli misukule ndiye waliezikwa na ndugu wanauhusiao na misukule hapo kiu itaisha na Mama apewe shukrani kwa maombi dhabiti irudishayo misukule,as simple as that.

Tusigubikwe sana na uhitaji wa uponyaji kiasi cha kutufanya tukubali njia zozote (hata za kilaghai) kutufariji kwa matatizo yetu.
Tatizo dunia ya leo binadamu anaweza kufanya chochote hata kile kionekanacho ni kitakatifu sana ili ajipatie pesa,nguvu na madaraka. Na iwapo hisia au mazingira ya jamii yanatafuta ukweli basi vyombo vyetu (polisi) vitusaidie kuondoa hisia tata miongoni mwetu ili Binadamu abaki kuitwa binadamu na Mungu aitwe Mungu na si Vinginevyo.
 
Kuna wakati fulani Yesu alimponya mtu mmoja mwenye ukoma; akamwambia "nenda kwa makuhani ukajioneshe". Lengo lilikuwa ni kuthibitisha kuwa ameponga kweli na haikuwa hoax.

Wakati mwingine alimponya mtu mmoja aliyezaliwa kipofu. Wakuu wa Makuhani waliposikia habari hiyo hawakuamini na wakawaita wazazi wa huyo jamaa na kuuliza habari zake. Wale wazazi wakasema "yeye ni mtu mzima muulizeni mwenyewe". Yule bwana alipoitwa akawaambia kuwa "mimi sijui kama huyo aliyeniponya ni mtakatifu au la, ninachojua ni kuwa nilikuwa kipofu na sasa naona".

Katika mifano hiyo miwili utaona kuwa kwenye mambo ya miujiza kufanya uchunguzi siyo kukana miujiza bali kuondoa uwezekano wa uongo. Ninaamini miujiza lakini miujiza yote inafanywa kwa kutumia vitu vya asili. So, kuhoji suala la misukule si kukana uwezo wa Mungu kutenda miujiza bali kuthibitisha nguvu hizo na kuzikiri lakini wakati huo huo kuondoa uwezekano wa roho ya mwanadamu kujikweza na kujiinua na kujisamamisha mahali pa Mungu!

Mkjj post yako hii ni reference yangu kuu katika maswali mengi. Thanks a lot!
 
The bottom line ni kwamba kwa jamii inayoelekwa katika umasikini uliokithiri mambo haya ni aghalabu kutokea!
 
Kama kuna watu wenye imani kiasi cha kukubali kuchomwa moto kanisani..kama imani ya wale waliokufa kutokana na kumwamini Mchungaji Kibwetere sitoona ajabu kwa Mchungaji Mama Lwakatare na misukule yake.Soko lipo kwa nini asilitumie kwa matangazo na maigizo nk..?

Kwa maana nyingine kama kulikuwa na soko la waumini wa aina ya wale wa mchungaji Kibwetere bila shaka hata hawa nao ni waumini wa mama Lwakatare nao ni imani yao inawafanya wamuone kama nabii na binadamu mwenye uwezo kuliko hata wa St.Peter,ambaye pamoja na kuwa na Bwana Yesu physically lakini maskini alishindwa kutembea kwenye mto Galilaya kwa kuwa hakuwa na imani ya kutosha.

Bravo Mama Lwakatare.Kula nchi kuna watu wanakuamnia au siyo?
 
Bottom line, huyu Mchungaji Rwakatare is a big fraud!!!
Mikono imejaa dhambi na uongo uliovuka mipaka.Using the Lord's name
or any other religion for personal gain is beyond condemnation.The Lord
has alredy judged her, is judging her and will judge her in the future.(if you are
a believer)

Mungu si Athumani,halali wala hali ugali!!!
 
So, Miujiza tunaizungumzia lazima itoke from the natural to the supernatural;

e. Muujiza usiofuata (d) hapo juu hauko katika realm ya miujiza kwani unahusu uumbaji na kazi ya Mungu moja kwa moja anapofanya something out of nothing.

Na Mana waliokula wana Israeli jangwani ilitoka wapi?
 
Haya mambo mbona hayasikiki katika makanisa mengine kama anglikana, RC, lutherani n.k.

YESU aliacha maagizo ambayo makanisa lege lege hushindwa kuyatekeleza......!
KWA JINA LANGU WATAFUFUA WAFU.....!
 
YESU aliacha maagizo ambayo makanisa lege lege hushindwa kuyatekeleza......!
KWA JINA LANGU WATAFUFUA WAFU.....!

Ina maana hayo makanisa yaliyotajwa ni legelege? Ulegelege wao upo wapi? Ina maana Kibwetere na kanisa lake hawakuwa legelege? Ina maana Wasabato masalia sio legelege?
 
YESU aliacha maagizo ambayo makanisa lege lege hushindwa kuyatekeleza......!
KWA JINA LANGU WATAFUFUA WAFU.....!

Mkuu hapa kinachoulizwa ni rahisi sana....madai ya kufufua watu (au kurudisha misukule) ni ya kweli? Haikatazwi kutaka uthibitisho wa hilo.
Mtu akitaka kupata ukweli wa madai yako, mthibitishie....huenda nae akawa mfuasi wako.
 
Mtu akitaka kupata ukweli wa madai yako, mthibitishie....huenda nae akawa mfuasi wako.[/QUOTE]

100% answer that is what we need to know, ili na sisi imani hio itujae na tuendelee kulitukuza jina la bwana.
 
Jamani, naomba wenye Biblia msome Ufunuo 18: 11 -13
Haya mambo ya kiroho ni magumu sana kuyaelewa.
Has anybody ever thought inakuwaje kuna watu wanauza viungo madukani mwao, but they are damn rich!! Kwanini? Jibu liko ktk huo mstari wa 13
 
Kuna kipindi miaka ya 2000 kanisani kwakwe kulikuwa na mkutano, kuna kijana akadai ameponyeshwa uhanithi, Watu wacha washangilie, basi muda ukazidi kwenda Kijana akaoa pale pale kanisani, ikidaiwa ya kwamba huyo kijana katengwa na ndugu zake, kanisa likabidi libebe mzigo wa kwanzia kumlipia mahali mpaka sherehe......... Mh baada ya mwaka kupita ikaja bainika yule kijana hakuwa hivyo, bali alilipwa ajidai kaponyeshwa huo ugonjwa.. na kisa cha kija kusema hivyo ilikuwa ni kwa sababu huyu mama aligoma kumlipa kiasi walichokubaliana, mwanamke kumbe nae alilazimishwa kwa makubaliano ya kwamba atalipwa pesa(naye akupewa) akakimbia ndoa. Kijana alipoona hayo ikabidi awafwate wazee wakanisa baadhi na kuwaambia, akaachishwa kazi St. Mary's, ikabidi kijana ahame kanisa............Jamani mambo haya yanasikitisha, cjui nini kimeikumba kanisa la leo.
 
Back
Top Bottom