Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 23, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu katika kanisa hilo, unaonyesha kuwa kati ya watu hao Misukule nane waliopatikana katika misitu hiyo baada ya waliowachukua kimazingira kumrudia Mungu, watano wameshachukuliwa na ndugu zao ambapo watatu bado wanaendelea kutunzwa na kusali katika kanisa hilo, hali iliyowafanya baadhi ya waunimi kusema kuwa ndugu zao watakuwa wamewasusa.

  Baadhi ya waumini waliozungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini kwa kuwa si wasemaji wa kanisa, walidai kuwa wanaamini kwamba vijana hao watatu ambao ndugu zao hawajajitokeza licha ya habari zao kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, inawafanya waamini kuwa jamaa zao bado wana imani kuwa wamekwisha fariki dunia.
  [​IMG]
  Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa baadhi ya waumini walikuwa na mawazo tofauti kwa kusema kwamba uwenda ndugu zao hawajapata taarifa kuhusiana na vijana wao kwa kuwa wengi walipoteza kumbukumbu na endapo wangepatiwa taarifa wangeweza kujitokeza.

  Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu jana, Mchungaji Lwakatare alikiri kuendelea kuwa na misukule hao katika kanisa lake.

  “Hata kama ndugu zao watawasusa nitaendelea kuwalea na baadaye wakiwa na akili safi nitawapa ajira,” alisema mchungaji huyo.
  [​IMG]
  Akifafanua zaidi, Mchungaji Lwakatare alisema kuwa watu hao wengi wao awali walikuwa wamepoteza kumbukumbu kabisa lakini sasa wana afadhali kwa kuwa wanaanza kuelewa mambo.

  Hivi karibuni gazeti hili na vyombo vingine vya habari viliripoti kukamatwa kwa misukule katika Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na kusababisha wasomaji wetu wengi kutaka kujua kinachoendelea, hivyo kuanzisha uchunguzi kujua kama bado wapo au la.
  [​IMG]

  My Take:
  Kanisa la huyu mama naamini linaeneza one of the most elaborated scheme of deception a.k.a a hoax! Inanikumbusha kisa cha Mchungaji Gilbert Deya wa Uingereza (raia wa Kenya) ambaye alikuwa amedai yeye na mke wake kuwa wanauwezo wa kuombea wa kina mama na wakapata mimba na kuzaa watoto hata kama kina mama hao walishapita uwezo wao wa kuzaa n.k

  Ingawa mwanzoni mambo hayo yaliweza kuonekana ni miujiza, utaalamu wa kisayansi ulionesha kuwa mke wa mchungaji huyo na washirika wao kule Kenya walikuwa wananunua watoto wadogo na kuwapa kina mama wengine na kwa kufanya hivyo kufanya biashara ya watoto lakini wakati huo huo kulifanya kanisa la Mchungaji huyo kukua zaidi na kuwa na ujiko usio kifani kutokana na kazi ya "Mchungaji huyo".

  Mwishoni, sheria ikakutana naye, mke wake akaswekwa jela na yeye mwenyewe mchungaji kutakiwa kurudishwa Kenya kukabiliana na mashtaka ya usafirishaji haramu wa watoto.

  Naamini, kama kuna mtu ana ujasiri wa kuchunguza hii "misukule" na kanisa hilo kutaonekana pasipo shaka jinsi gani this hoax was propagated and carried out na hivyo kumpa mama Lwakatare ujiko na kumuongezea sadaka.

  Natoa hoja, kanisa lake na yeye mwenyewe achunguzwe pamoja na hao "misukule" kwani anachezea imani za watu na hasa hofu yao ya mambo ya kishirikina.

  Kwa vile tuna utaalamu wa DNA, basi misukule hao na "familia" zao na hata makaburi wanayodaiwa kuzikwa yachunguzwe ili wananchi wetu wasitekwe na ulaghai wa kidini unaoendeshwa kwa jina la dini.

  Endapo uchunguzi wa kisayansi utaonesha kuwa kweli hawa watu walikufa, wakazikwa na baadaye kukutwa porini wakiwa wamechukuliwa misukule nitamwomba radhi; Lakini nasimamia kusema this is a HOAX inayofanywa na Mbunge Mchungaji!
   
 2. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #2
  Sep 23, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Very complicated, almost beyond comprehension!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Sep 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  WTF!?!?!?!?!?!?!? Miafrika Ndivyo Tulivyo.....
   
 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,

  Mimi naamini kwa YESU YOTE yanawezekana!

  Isimuhukumu huyu mama. Ina maana waumini wote hapo kanisani hawayaoni hayo yote?

  FP
   
 5. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,724
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Complicated? Sidhani. Hapa ni ujuha wa waumini; na utapeli wa mchungaji. Hakuna la ziada.
   
 6. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #6
  Sep 23, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Makongoro Going’ na Issa Mnally
  Vijana waliochukuliwa kimazingira (Msukule) na kuhifadhiwa katika misitu ya Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na wachawi ambao baadaye waliokolewa na Kanisa la Mikocheni B Assembies of God linaloongozwa na Mchungaji Getrude Lwakatale, Baadhi yao bado hawajachukuliwa na ndugu zao kitendo kilichowafanya watu kupigwa na butwaa...

  ‘Misukule’ hao wanaaminika kuwa walichukuliwa na mtu mmoja mshirikina ambaye alijisalimisha kanisani hapo na kusababisha baadhi ya waumini wa Kanisa hilo kupigwa na butwaa na wengine kuangua vilio kuona baada ya kuwa kuwaona watu hao waliokuwa wanateseka.

  Kama ilivyokuwa kwa wengine watatu ambao gazeti hili liliwahi kuandika habari zao hivi karibuni . ‘misukule’ hao inadaiwa walichukuliwa kwa nguvu za giza na wakawa wanatumikishwa huku ndugu zao wakiamini kuwa wamekufa.

  Aidha, watu waliokuwa wakiwamiliki baada ya kujisalimisha kanisani hapo inadaiwa waliwaeleza wachungaji wa kanisa hilo waende wakawachukue misukule hao huko walikowekwa katika msitu wa Chalinze mkoa wa Pwani.

  Habari zaidi zinaeleza kuwa kwa kipindi kifupi wachungaji wa kanisa hilo walifanikiwa kwenda katika pori hilo huku wakifuatana na wachawi hao na tayari wameshawapata ‘misukule’ wanane ambapo walifikishwa pale kanisani kuombewa, kuogeshwa na kupewa chakula.

  Habari zinasema watatu kati yao wameshapata ndugu zao huku wengine watano wakiendelea kupata huduma hapo kanisani wakati wakisubiri kutambuliwa na ndugu zao ili wachukuliwe.

  Baadhi ya misukule ambao majina yao yalipatikana ni pamoja na John Charles, Richard Lugolay, Enerico Samson, na wengine waliofahamika kwa jina moja moja la Jenifa na Sauda.

  Hata hivyo, wengine majina yao hayajapatikana mara moja kwa kuwa bado hawajaweza kujieleza.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipohojiwa na mwandishi wetu hatua wanazoweza kuchukua ili kusaidiana na kanisa kutafuta ndugu wa ‘misukule’ hao ili waje kuwachukua, alisema kuwa hawajaombwa msaada huo na wahusika.

  Kamanda Kova aliongeza kuwa licha ya kutoombwa msaada lakini ni vigumu serikali kushughulikia mambo ya kishirikina kwa kuwa haiamini kama uchawi upo.

  “Hatuna ujuzi katika mambo ya kishirikina, hivyo si rahisi kuyashughulikia, bali tunaweza kufanyia kazi mambo yanayotendeka yanayoonekana kwa macho,” alisema Kova na kuuhakikishia uongozi wa kanisa hilo kuwa wakiombwa na uongozi watatoa ushirikiano.


  [​IMG]

  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]

  Global Publishers - Tanzania Newspapers
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli ukistaajabu ya wasabato masalia utayaona ya mama Lwakatare...
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Beyond explanations. Isijekuwa wamewaokota watu wenye maradhi ya akili kusikojulikana, wakawapeleka msituni. Hii bwana ni biashara na biashara lazima utangaze vinginevyo huta uza kitu. Strategic Church Management ya Mch, Mh,Dr. Lwakatare
   
 9. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  Ya kaisari mpe kaisari ya MUNGU mpe MUNGU!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Sep 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna wakati fulani Yesu alimponya mtu mmoja mwenye ukoma; akamwambia "nenda kwa makuhani ukajioneshe". Lengo lilikuwa ni kuthibitisha kuwa ameponga kweli na haikuwa hoax.

  Wakati mwingine alimponya mtu mmoja aliyezaliwa kipofu. Wakuu wa Makuhani waliposikia habari hiyo hawakuamini na wakawaita wazazi wa huyo jamaa na kuuliza habari zake. Wale wazazi wakasema "yeye ni mtu mzima muulizeni mwenyewe". Yule bwana alipoitwa akawaambia kuwa "mimi sijui kama huyo aliyeniponya ni mtakatifu au la, ninachojua ni kuwa nilikuwa kipofu na sasa naona".

  Katika mifano hiyo miwili utaona kuwa kwenye mambo ya miujiza kufanya uchunguzi siyo kukana miujiza bali kuondoa uwezekano wa uongo. Ninaamini miujiza lakini miujiza yote inafanywa kwa kutumia vitu vya asili. So, kuhoji suala la misukule si kukana uwezo wa Mungu kutenda miujiza bali kuthibitisha nguvu hizo na kuzikiri lakini wakati huo huo kuondoa uwezekano wa roho ya mwanadamu kujikweza na kujiinua na kujisamamisha mahali pa Mungu!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Sep 23, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  na ya matapeli yanapelekwa mahakamani!
   
 12. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Kumbuka ndugu yangu watu siku hizi wanatumia kila njia kufanikisha wanachotaka. siku zote sijawahi kumkubali huyu mama hasa baada ya kuanza kutoa vioja na jamii nzima kumtegea sikio zaidi na kuuliza "yule mama mwenye shule za st. mary's" "aaah yule mama mwenye radio eenh" wengine wakisema "aliyewatoa misukule ni yule mama mbunge" na title zake nyingine nyngi. wakati watu wanaongelea misukule anayoijua yeye (am not conviced) kumbe mnamtangaza na kutangaza biashara zake bila watu kujijua!

  umaarufu gharama ati, maana hata imani ya dini yake yenyewe inasema wazi kuwa sku za mwisho watakuwa manabii wengi wa uongo (sijasema yeye mmoja wapo) hivyo wananchi hasa wenye kutaka kuondolewa matatizo yetu kwa urahisi na haraka tuwe makini!
   
 13. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  ..... Dini Biashara, ndio maana inafanya matangazo na mamilioni ya pesa kulipia vipindi vya TV, na kutoa mabango mitaani, kwa namna hiyo unategemea asile mingo? tena katika hali ya sasa ya wachungaji kibao wanaoponya DHAMBI (ya ngono, ulevi na nyinginezo)

  mimi wala sishangai kwa huyu mama. hivi ile kashfa ya kuwa anajihusisha na madawa ya kulevya ilithibitishwa au? kwa anayejua nitafurah akinifahamisha
   
 14. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Waandishi wetu wa habari wa Tanzania wako wapi? Hakuna journalist investigation jamani? Sio lazima kila kitu polisi waachiwe, kwanza hawawezi hao. Waandishi makini (achana na hawa wa Shigongo) wanaweza kutusaidia kumuumbua huyu mama. Huu ni utapeli period!
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  With all due respect, mapema sana nilishasema kuwa huyu mama mimi ninamshitukia sana kwa sababu ninajua according to the dataz, kuwa anajirusha na Mkulu mmoja wa CCM,

  Kwa hiyo haya mengine yote ni tisa, kumi Mungu hawezi chezewa na bina-adam hata siku moja, ndio maana yanaanza kujitokeza, ni aibu sana kwa wale tunaomuamini Mungu.
   
 16. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  Sep 23, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  ..........kanisa katoliki kinaamini kuwa miujiza yote ni lazima ichunguzwe kabla ya kutangazwa kikanisa......!!!..kwa utaratibu huo kwenye kanisa katoliki mtumishi au muumini yeyote akifanya miujiza hatakiwi kuanza kujitangaza hadi ...uchunguzi na maombi ufanyike kubaini kama uponyaji au miujiza umetokaana na jina la bwana yesu au tofauti!!!..na ikiweza kudhibitika kuwa mtu ana nguvu hizo basi huwekwa kwenye kundi la watakatifu....

  makanisa mengi yanaibuka siku hizi ie mtume na nabii mwingira,askofu mkuu kakobe na wengine.......wanafanya kazi nzuri ..lakini kinachonitia hofu ni kuwa wengi kati ya hawa..hawapendi MASWALI KWENYE MIUJIZA WANAYOTENDA ...WALA HAWATAKI UCHUNGUZI....!!!

  LAKINI BADO NAAMINI umuhimui wa nadharia ya kanisa katoliki na makanisa mengine ya asili kama orthodox ,lutheran etc .....kwenye "kusikiliza kwa makini sauti"...kwani hata shetani anaweza kuiga sauti ya Mungu!!
   
 18. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Clear as glass. I dont have none to add this is wht I was thinking since yule kijana Ramadhani aliyekamatwa na kichwa cha mtoto alipodondoka pale Kanisani. Mwanzo alisema ametokea mikoa ya kusini walikuwa wakisafiri kwa ungo yeye na bibi yake baada ya muda si akakamatwa na kichwa cha mtoto na kudai kuwa anakaa maeneo ya segerea na yeye na mama yake huwa wanakunywa damu za watu na huwa wanafanya ajali zitokee.

  Missing point:

  Kama huwa wanafanya ajali zitokee ndipo wanywe damu kanini walimchinja yule binti wa miaka mitatu? na makazi ya huyu kijana mbona yana utata kuanzia story ya mwanzo na story ya pili? Ninazidi kuchanganyikiwa zaidi na hili la misukule.
   
 19. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tusubiri tuone na kusikia, maana macho na masikio tunayo.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Sep 23, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Misukule ndo nini?
   
Loading...