Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Ya kaisari mpeni kaisari na ya MUNGU muachieni MUNGU!miujiza haijaanza leo toka kabla ya YESU ilikuwepo na Enzi za YESU ikawepo na itaendelea kuwepo!MKJJ hulazimishwi kuamini!Kwanza YESU mwenyewe alisema watu watafanya miujiza kuliko hata aliyofanya yeye!hapa ni IMANI tu!hakuna jipya alilofanya mtumishi wa MUNGU kwanza yeye hajafufua!ila hao misukule hawakufa kifo cha kawaida!kama YESU aliweza kumfufua Lazaro tena aliyekufa kiukweli!leo watumishi wake washindwe kuibua misukule!Kwa MUNGU yote yewezekana!

Good First lady,
Kila mwenye kuelewa ataelewa asiyelewa itakuwa ngumu kumwelimisha
 
FL, my argument ni kuwa ili kujua ni "mambo ya kichawi" ndio maana twende tuangalie huko walikozikwa kwani tukiikosa miili, ina maana hakuna mtu alizikwa hapo, na ndipo tuangalie uhusiano wa damu wa former "Msukule" na familia yake. Lakini tukiangalia kaburi alilodaiwa kuzikwa na kukuta mabaki ya mwili mle tutaelezeaje mabaki hayo wakati kuna mtu kasimama pembeni anasema nini ndiye aliyezikwa humo?

Hayo ya kufukua kaburi ni kukubaliana na ndugu!mbona kuna siku ITV tuliona kaburi limefukuliwa na walikuta mabaki si ya yule binti waliyezania kafa!
 
Nadhani ushauri wa FL ni mzuri sana MKJJ.

Kila aliye na wasiwasi na aende Mikocheni B Assemblies Of God muda wowote akajionee na kumaliza ubishi.

Hivi vitu havihitaji Test Tubes, Bunsen Burner wala catalyst.You just go and see for yourself
 
wewe unataka uchunguzi wa DNA mbona ni kazi rahisi kama kweli umedhamiria wala haihitaji
polisi!ni pesa tu hapa kama una pesa ya kulipia vipimo katafute ndugu wa hao misukule na misukule yenyewe hivi vipimo vifanywe!usiisumbue serikali kwa mambo ambayo hata wewe usieamini TOMASO type unaweza kuyafanya!kutokuamini kwako ni sawa Tomaso nae hakuamini mpaka alipoona alama za misumari!
 
Inawezekana MKJ haamini kama kuna misukure (He calls them a vacum?). Nafikiri akiamini/akithibitisha kuwa ipo hatakuwa na shida tena na Rwakatare
 
Serikali haiwezi kukaa pembeni na huku ikiona hatari ya jamii yetu kuendelea kuwa na imani potofu.
Kwanini kusiwe na kampeni ya kuumaliza uchawi badala ya kutegemea makanisa?
Kwani hata makanisani si ndio mafisadi waliko na wachawi?
Hapo jmushi1 nakupinga.Ufisadi haupo kanisani bali upo kwa mtu mwenyewe.Kanisa kama taasisi nyingine inasimama kaka ilivyo.Uchafu au usafi wa watu ndio unaoipambanua taasisi fulani kuwa chafu au safi.

Siyo uungwana kumnyooshea mtu kidole na kumwita mwizi, mnafiki ,mwongo n.k kama hauwezi kuuthibitisha msimamo wako.Suala la imani laweza kudhaniwa rahisi sana lakini ukitafuta ukweli wa kiimani kimwili hautauona kamwe.Ndiyo maana watu kama Stefano wa kwenye Biblia walipigwa mawe na wale waliotegemea akili zao na shahada zao za kidini na kisheria kuutenganisha ukweli na uongo wa kiimani
 
mimi sijakubaliana na wewe mimi sina shaka na Nguvu za MUNGU!wewe mwenye mashaka ndo uende!

mimi pia sina shaka na nguvu za Mungu, nina shaka na nguvu za mwanadamu; wewe huna shaka na nguvu za mwanadamu zinapodaiwa kuwa ni nguvu za Mungu! well, the different then is as clear as day and night!
 
  • Thanks
Reactions: Wit
Mlalahoi kumbuka kuwa Biblia kwenye Yoh. 4:1 inasema msiziamini kila roho bali mzijalibu kama zinatokana na Mungu maana manabii wengi wametokea duniani sasa unaposema watu waamini bila kuzijaribu hizo roho unawapotosha, harafu kumbuka kuwa Yesu alisema, ponyeni watu fufueni wafu, maana umesema tuamini yanapotendeka aliyo fanya yesu, sasa Yesu alifufua wafu walio kuwa wamekufa hawajazikwa hakufufua wafu waliochukuliwa misukule, kumbuka hata mitume walifufua wafu si misukule, na wafu wanao fufuliwa ni wale ambao kifo kinatokea kwaajili ya utukufu wa Mungu, wakati Razaro alipokufa wakina mathar walipo muita Yesu alisema kifo hiki ni kwaajili ya utukufu wa Mungu. Halafu tambua kuwa mtu anapochukuliwa msukule anageuzwa kuwa pepo na shetani anakuwa amesha muweka kwenye himaya yake, sasa wewe unaye waambia watu kuwa umefufua misukule, lazima watu washituke yawezekana upo katika ulimwengu huo. Biblia inasema sisi hatulichanganyi neno la Mungu na uwongo, ndiyo maana watu ambao Mungu amewajalia ufahamu wake wanahoji, wanaijaribu hiyo roho inayofufua misukule ili wapate jibu kama inatokana na Mungu, Mtu wa Mungu mwenye uwezo wa mungu ataonekana tu bila hatakujitangaza, mtamtambua kwa matunda yake (matendo) hatafuti utukufu wa wanadamu wala hatafuti kusifiwa na wanadamu, sifa yake inatoka kwa mungu, sijawahi ona wala kusikia mtu wa mungu anafufua misukule, labda kwa mungu wa mikochenikama wanavyo muuta wao, si mungu huyu muumba mbingu na nchi. Rwakatale amejichanganya mno ndiyo maana watu wengi wanakuwa na mashaka naye.
Maswali ya kujiuliza: Wakati huo misukure walikuwepo? Je Yesu angeweza kuwarudisha kama wangekuwepo?
Yesu na mitume walijitangaza saaana kasome biblia "yako" vizuri mkuu.
 
Hayo ya kufukua kaburi ni kukubaliana na ndugu!mbona kuna siku ITV tuliona kaburi limefukuliwa na walikuta mabaki si ya yule binti waliyezania kafa!

huwezi kufukua kaburi la mtu yeyote tu bila kuihusisha serikali, mahakama au ndugu wa Marehemu. Na linapokuja suala la uchunguzi wa kihalifu, lazima uwe na probable cause na hilo huanzia na vyombo vilivyopo.
 
mimi pia sina shaka na nguvu za Mungu, nina shaka na nguvu za mwanadamu; wewe huna shaka na nguvu za mwanadamu zinapodaiwa kuwa ni nguvu za Mungu! well, the different then is as clear as day and night!
Lakini nguvu za Mungu haziji kupitia vaccum, Mungu anatumia wanadamu. Ukiamini nguvu za Mungu utaamini na mwanadamu ambaye Mungu kamtumia. You cant separate the two mkuu.
 
Kuna wakati fulani Yesu alimponya mtu mmoja mwenye ukoma; akamwambia "nenda kwa makuhani ukajioneshe". Lengo lilikuwa ni kuthibitisha kuwa ameponga kweli na haikuwa hoax.

Wakati mwingine alimponya mtu mmoja aliyezaliwa kipofu. Wakuu wa Makuhani waliposikia habari hiyo hawakuamini na wakawaita wazazi wa huyo jamaa na kuuliza habari zake. Wale wazazi wakasema "yeye ni mtu mzima muulizeni mwenyewe". Yule bwana alipoitwa akawaambia kuwa "mimi sijui kama huyo aliyeniponya ni mtakatifu au la, ninachojua ni kuwa nilikuwa kipofu na sasa naona".

Katika mifano hiyo miwili utaona kuwa kwenye mambo ya miujiza kufanya uchunguzi siyo kukana miujiza bali kuondoa uwezekano wa uongo. Ninaamini miujiza lakini miujiza yote inafanywa kwa kutumia vitu vya asili. So, kuhoji suala la misukule si kukana uwezo wa Mungu kutenda miujiza bali kuthibitisha nguvu hizo na kuzikiri lakini wakati huo huo kuondoa uwezekano wa roho ya mwanadamu kujikweza na kujiinua na kujisamamisha mahali pa Mungu!

Ninachofahamu na kuamini ni kwamba hakuna jambo gumu la kushinda Mwenyezi Mungu. Kwake kila kitu kinawezekana na hujibu maombi kwa saa na majira yake. Kinachotakiwa ni imani yako.

Kwa sayansi ilivyokuwa kwa sasa kumezuka vikundi vya dini au makanisa yenye itikadi mbalimbali za kidini. Katika yote hayo kuna wasanii wale Yesu mwenyewe alisema tujihadhari nao "Manabii wa Uongo". Pia kuna wale kweli walioitwa kwa kazi na makusudi ya Mungu. Inakuwa vigumu sana kuyatenganisha makundi hayo mawili "wakweli na waongo".

Kwa mantiki hiyo si mimi wala wewe unaweza kumsemea Mch. Lwakatare kuwa huenda yupo kundi lipi katika haya mawili. Kinachotakiwa hata wewe hapo ulipo kwa imani yako uliyo nayo unaweza kumwomba Mungu aweze kumdhihirisha huyu mama kama kweli ni tapeli au la. Na mwisho wa siku uovu huwa unajitokeza tu kwani kila kitu kiovu kina mwisho wake kama vilivyo vitu vingine.

Wito, tumweke kwenye maombi na Mungu atajibu. Naona pia media imemwandama sana siku hizi katika itikadi zake na mali zake ikiwa ni pamoja na shule zake.
Pia tuwe makini sana katika kuhukumu tusikute kuna kundi au mtu yuko behind all these. Maadui aweza kuwa nao ukianzia mtalaka wake (sijua kama wamesha divorce rasmi) na wanasiasa pia. Unajua tena ujiko wa Siasa.

Mengi ya huyu mama yameanza kushamiri sana kuandikwa magazetini baada ya kwenda Bungeni. Sisemi kuwa huko awali hajaandikwa but kwa sasa kasi ni kubwa ya kuandikwa.

Hata mimi huwa napata tabu sana kuamini hizi dini na makanisa ya siku hizi maana yamekuwa "profitable business". Tuwe tu makini, fahamu utashi wako na kuwa kiimani unahitaji nini katika masuala ya kumtumikia Mungu. Kuna baadhi ya waumini wamefilisika kwa imani hizihizi za dini na makanisa uchwara na wako kijiweni na wachungaji wanapeta. Ikumbukwe kuwa ukishatoa sadaka au kitu kwa kanisa ni ngumu kukirudisha na pia wachungaji hawa ukiishiwa wanakukimbia. Ukipata tu bahati ya kuonana nae baada ya kufilisika atakupa tuu mistari ya biblia na kukutia moyo kwa mdomo. Hawezi hata kukusaidia lolote physically.

Kwa ukweli wengine, ni vile tu hatuna taarifa za account zao bank, yaani wana pesa nyingi sana na ambazo hazina hata Bodi za kanisa zinazochunguza wala kufahamu idadi ya fedha hizo na matumizi yake.

Nyingi ya makanisa hayo yanaendeshwa kifamilia, Mara Baba Mtume au Nabii, Mama Mchungaji Mkuu au Kiongozi, watoto ushers, waweka hazina etc. So please, be carefully na nyumba yako ya ibada uliochagua. All the best.
 
Wakristo tunaamini kuwa dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu haisameheki na adhabu yake ni kifo.

Mama Lwakatare anatumia nguvu ya roho mtakatifu kuponya. Wale misekule haikuwa imekufa kwahiyo hajafufua wafu.

Sioni tunachobishiana hapa, ni suala la imani.

Bwana asifiwe!
 
Hayo ya kufukua kaburi ni kukubaliana na ndugu!mbona kuna siku ITV tuliona kaburi limefukuliwa na walikuta mabaki si ya yule binti waliyezania kafa!

Nakumbuka vizuri tukio hilo lilitokea huko Machame kwa Wachaga. Ila wahusika waliomba kibali cha kufukua na wakaiomba Halmashauri ya Wilaya ikachukue mabaki yale yakazikwe makaburi ya manispaai. Sijui tena kilichoendelea baada ya hapo kama wameshahamisha masalia au la. Mwenye taarifa kamili atupatie.
 
Wakristo tunaamini kuwa dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu haisameheki na adhabu yake ni kifo.

Mama Lwakatare anatumia nguvu ya roho mtakatifu kuponya. Wale misekule haikuwa imekufa kwahiyo hajafufua wafu.

Sioni tunachobishiana hapa, ni suala la imani.

Bwana asifiwe!
Amina mkuu, lakini una uhakika gani kama ni nguvu za Roho Mtakatifu?
 
Nakumbuka vizuri tukio hilo lilitokea huko Machame kwa Wachaga. Ila wahusika waliomba kibali cha kufukua na wakaiomba Halmashauri ya Wilaya ikachukue mabaki yale yakazikwe makaburi ya manispaai. Sijui tena kilichoendelea baada ya hapo kama wameshahamisha masalia au la. Mwenye taarifa kamili atupatie.

Ndo hapo MKJJ aende akakutane na ndugu waombe kibali ili hiyo kazi ifanyike
 
Wakristo tunaamini kuwa dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu haisameheki na adhabu yake ni kifo.

Hapana; dhambi ya kumfukuru Roho Mtakatifu haijatajwa adhabu yake; tunachofahamu ni kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti, na karama ya Mungu ni uzima wa milele". Hivyo dhambi zote mshahara wake ni mauti.

Mama Lwakatare anatumia nguvu ya roho mtakatifu kuponya. Wale misekule haikuwa imekufa kwahiyo hajafufua wafu.

Hilo la kutumia Roho Mtakatifu kuponya lazimwe lipimwe. Siyo kila mtu anayesema anatumia Roho Mtakatifu basi anafanya hivyo. Tunda la Roho ni nini basi? Utaona basi kazi ya Roho Mtakatifu haipimwi kwa miujiza; never. Miujiza kamwe haithibitishi huduma ya mtu au ujumbe wake. Miujiza peke yake au kusema "Kwa jina Yesu inuka" haisemi lolote juu ya yule afanyaye hiyo. Biblia husema hata "Shetani anaamini na kutetemeka"!

So anayefuata miujiza tu kwa vile inamshangaza na kumfanya amuamini mjumbe anafanya makosa ya Kibiblia. Mkristu hafuati kamwe muhubiri wa miujiza au Mchungaji wa Kanisa lililoko Mikocheni B. Mkristu anayemfuata mtu anapingana na Biblia inayosema "amelaaniwa anayemtumaini mwanadamu, anayemfanya mtu kuwa kinga yake".

Kama haya yanayofanywa hayana ulaghai na ya kuwa hawa watu walikuwa wamechukuliwa kimazingara na kurudishwa itakuwa ni utukufu wa Mungu kama itathibitishwa pasipo shaka kuwa ndivyo ilivyo na siyo kuogopa kuchunguza kwa sababu labda mtu atakuwa anamkufuru Roho wa Mungu. Biblia ilisema "zipimeni kila roho"! Na ndiyo maana kwenye karama za Roho Mtakatifu kuna moja inaitwa "Kupambanua roho".

Nashangaa watu ambao wanamtetea Lwakatare na huduma yake kwenye suala hili hawataki hata kutumia karama ya kupambanua roho (aidha ya hao ex-misukule au ya Lwakatare"!
 
wakristo tunaamini kuwa dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu haisameheki na adhabu yake ni kifo.

Mama lwakatare anatumia nguvu ya roho mtakatifu kuponya. Wale misekule haikuwa imekufa kwahiyo hajafufua wafu.

Sioni tunachobishiana hapa, ni suala la imani.

Bwana asifiwe!

amen fp!!!!
 
Ndo hapo MKJJ aende akakutane na ndugu waombe kibali ili hiyo kazi ifanyike

Tatizo lako unafikiri hili ni kwa ajili ya MKJJ, sina interest yoyote. Kama mnakubali na mmeridhika na misukule yenu, well and fine. Lakini wenye kuuliza maswali wana haki ya kuuliza na kama ndugu wanataka kuchunguza au vyombo vya usalama vinataka kufanya hivyo watu wasipige kelele kuwa watu wanapinga miujiza!
 
Hapana; dhambi ya kumfukuru Roho Mtakatifu haijatajwa adhabu yake; tunachofahamu ni kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti, na karama ya Mungu ni uzima wa milele". Hivyo dhambi zote mshahara wake ni mauti.

Hilo la kutumia Roho Mtakatifu kuponya lazimwe lipimwe. Siyo kila mtu anayesema anatumia Roho Mtakatifu basi anafanya hivyo. Tunda la Roho ni nini basi? Utaona basi kazi ya Roho Mtakatifu haipimwi kwa miujiza; never. Miujiza kamwe haithibitishi huduma ya mtu au ujumbe wake. Miujiza peke yake au kusema "Kwa jina Yesu inuka" haisemi lolote juu ya yule afanyaye hiyo. Biblia husema hata "Shetani anaamini na kutetemeka"!

So anayefuata miujiza tu kwa vile inamshangaza na kumfanya amuamini mjumbe anafanya makosa ya Kibiblia. Mkristu hafuati kamwe muhubiri wa miujiza au Mchungaji wa Kanisa lililoko Mikocheni B. Mkristu anayemfuata mtu anapingana na Biblia inayosema "amelaaniwa anayemtumaini mwanadamu, anayemfanya mtu kuwa kinga yake".

Kama haya yanayofanywa hayana ulaghai na ya kuwa hawa watu walikuwa wamechukuliwa kimazingara na kurudishwa itakuwa ni utukufu wa Mungu kama itathibitishwa pasipo shaka kuwa ndivyo ilivyo na siyo kuogopa kuchunguza kwa sababu labda mtu atakuwa anamkufuru Roho wa Mungu. Biblia ilisema "zipimeni kila roho"! Na ndiyo maana kwenye karama za Roho Mtakatifu kuna moja inaitwa "Kupambanua roho".

Nashangaa watu ambao wanamtetea Lwakatare na huduma yake kwenye suala hili hawataki hata kutumia karama ya kupambanua roho (aidha ya hao ex-misukule au ya Lwakatare"!

Biblia imeweka wazi kuwa dhambi ya kumkashifu ROHO MTAKATIFU haisameheki ,hakuna ubishi hapo MKJJ.

Hatumtetei Mama Lwakatare kama unavyodai bali tunatetea na kushuhudia kuwa ipo nguvu ya MUNGU itendayo kazi ndani ya wanadamu na mama Lwakatare ni mmoja wa hao wanadamu.

Karama ya kupambanua Roho kama ulivyosema haipo kwenye Jamii Forum wala haipo mahakamani.Masuala ya imani huenda kwa imani.Kama ukitaka sheria ichukue mkondo huko siyo kupambanua roho bali kuthibitisha mashaka ya kibinadamu ambayo humpofusha mtu asione nguvu za MUNGU.
 
Back
Top Bottom