Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

]Tatizo lako unafikiri hili ni kwa ajili ya MKJJ, sina interest yoyote.[/B] Kama mnakubali na mmeridhika na misukule yenu, well and fine. Lakini wenye kuuliza maswali wana haki ya kuuliza na kama ndugu wanataka kuchunguza au vyombo vya usalama vinataka kufanya hivyo watu wasipige kelele kuwa watu wanapinga miujiza!

Kilichokufanya uanzishe thread ni nini kama huna interest?
 
Nadhani ushauri wa FL ni mzuri sana MKJJ.

Kila aliye na wasiwasi na aende Mikocheni B Assemblies Of God muda wowote akajionee na kumaliza ubishi.

Hivi vitu havihitaji Test Tubes, Bunsen Burner wala catalyst.You just go and see for yourself

Unajua mzee wa G kabla hatujaenda mikocheni hapa ni vizuri tukamchunguza Mama Lwakatare juu ya uchungaji wake kwanza.
Tukishapata majibu kuwa uchungaji wake hauna shaka yeyote
Nadhani itakuwa mwanzo mzuri wa kupata majibu sahihi na kuwahimiza watu waende wakajionee maajabu ya mchungaji Mwanasiasa wa Ukweli.
Lakini Pia kama uchungaji wake tu ni wa mashaka, haueleweki (ni wa kisiasa, kibiashara au kimungu?) Bila shaka hata yanayotokea Mikocheni(Kanisani kwake) itakua 'simpo' kutambua kinachoendelea.
 
Ningekuwa na Uwezo wa Kumchukua Watu Msukule; RA angekuwa # 1 kwenye list yangu.

Ujuzi huu unafundushwa wapi?
 
Hapana; dhambi ya kumfukuru Roho Mtakatifu haijatajwa adhabu yake; tunachofahamu ni kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti, na karama ya Mungu ni uzima wa milele". Hivyo dhambi zote mshahara wake ni mauti.

Hilo la kutumia Roho Mtakatifu kuponya lazimwe lipimwe. Siyo kila mtu anayesema anatumia Roho Mtakatifu basi anafanya hivyo. Tunda la Roho ni nini basi? Utaona basi kazi ya Roho Mtakatifu haipimwi kwa miujiza; never. Miujiza kamwe haithibitishi huduma ya mtu au ujumbe wake. Miujiza peke yake au kusema "Kwa jina Yesu inuka" haisemi lolote juu ya yule afanyaye hiyo. Biblia husema hata "Shetani anaamini na kutetemeka"!

So anayefuata miujiza tu kwa vile inamshangaza na kumfanya amuamini mjumbe anafanya makosa ya Kibiblia. Mkristu hafuati kamwe muhubiri wa miujiza au Mchungaji wa Kanisa lililoko Mikocheni B. Mkristu anayemfuata mtu anapingana na Biblia inayosema "amelaaniwa anayemtumaini mwanadamu, anayemfanya mtu kuwa kinga yake".

Kama haya yanayofanywa hayana ulaghai na ya kuwa hawa watu walikuwa wamechukuliwa kimazingara na kurudishwa itakuwa ni utukufu wa Mungu kama itathibitishwa pasipo shaka kuwa ndivyo ilivyo na siyo kuogopa kuchunguza kwa sababu labda mtu atakuwa anamkufuru Roho wa Mungu. Biblia ilisema "zipimeni kila roho"! Na ndiyo maana kwenye karama za Roho Mtakatifu kuna moja inaitwa "Kupambanua roho".

Nashangaa watu ambao wanamtetea Lwakatare na huduma yake kwenye suala hili hawataki hata kutumia karama ya kupambanua roho (aidha ya hao ex-misukule au ya Lwakatare"!

Ndio maana nikasema haya ni masuala ya IMANI. Ni sawa na watu wanaosema mbona Yesu harudi?, ni IMANI tu.

Ila tusi question mambo ya KIROHO. Maana hatutapata majibu, mwishoni mtaanza kuuliza KWANI HUYO MUNGU yeye ALIUMBWA NA NANI?

Bwana ahidimiwe!
 
Unajua mzee wa G kabla hatujaenda mikocheni hapa ni vizuri tukamchunguza Mama Lwakatare juu ya uchungaji wake kwanza.
Tukishapata majibu kuwa uchungaji wake hauna shaka yeyote
Nadhani itakuwa mwanzo mzuri wa kupata majibu sahihi na kuwahimiza watu waende wakajionee maajabu ya mchungaji Mwanasiasa wa Ukweli.
Lakini Pia kama uchungaji wake tu ni wa mashaka, haueleweki (ni wa kisiasa, kibiashara au kimungu?) Bila shaka hata yanayotokea Mikocheni(Kanisani kwake) itakua 'simpo' kutambua kinachoendelea.

Ndibalema,
Suala la uchungaji haliwezi kuchunguzwa kwenye forum au mahakamani na ushahidi kutolewa.Kazi ya Mungu hujipambanua kwa matokeo yake na kama yupo mtu anayelitumia jina la YESU kuhadaa watu haihitajiki mahakama wala PCCB kutoa ushahidi,Mungu humuumbua mtu huyo "kwa maana yeye huwajua walio wake na walio wake huyafanya yaliyo mapenzi ya MUNGU"

Nafikiri hoja hapa jukwaani ingekuwa siyo kuhukumu na kutoa misimamo ya kiimani kuwa ni uongo au siyo uongo.Hili ni suala la kiimani na ushahidi unapatikana kwa kuanzia na kuamini kwenyewe.
 
Biblia imeweka wazi kuwa dhambi ya kumkashifu ROHO MTAKATIFU haisameheki ,hakuna ubishi hapo MKJJ.

Hatumtetei Mama Lwakatare kama unavyodai bali tunatetea na kushuhudia kuwa ipo nguvu ya MUNGU itendayo kazi ndani ya wanadamu na mama Lwakatare ni mmoja wa hao wanadamu.

Karama ya kupambanua Roho kama ulivyosema haipo kwenye Jamii Forum wala haipo mahakamani.Masuala ya imani huenda kwa imani.Kama ukitaka sheria ichukue mkondo huko siyo kupambanua roho bali kuthibitisha mashaka ya kibinadamu ambayo humpofusha mtu asione nguvu za MUNGU.
well said 100%
 
Hivi aliyojisalimisha kama mchawi pale kanisani na kutaja hao misukule kwa nini hao wengine asiwarudisha alikowatoa??
 
Kila mtu amchunguze kwa wakati wake.Lakini mwenye akili haambiwi tazama.
 
Mtu yeyote anayejua historia ya huyu mama (angalau robo tu), bila ya shaka anajua dira ya ishu yote hii.

Bila ya shaka ilibidi aingie kwenye political system. Kwa sababu, ishu kama hii inahitaji 'baraka' za nguvu kutoka kwa watawala. Kwenye nchi ambayo inafuata mkondo wa sheria vilivyo na kuthamini watu wake, hii ishu ingechukulia very serious na serikali haraka iwezekanavyo.

Oh well, only in Tanzania and alike.
 
Ukweli wa hili utajulikana tu na Mungu atatukuzwa; mwanadamu atashushwa! Kwani Mungu husimama mwenyewe na ahadi zake ni za milele. Lakini wakati huo huo Mungu hutuma wajumbe wake kuwaambia wenye nguvu ukweli.
 
Mkuu Tanzania hatufuati mkondo wa sheria, Ndo maana wale walioiba pesa za EPA raisi wako anawaomba na kuwaongezea muda warudishe, sijui kazi za mahakama na vyombo vingine vya dola ni nini! Gray Mgonja ansema aachwe na ufisadi wake.....Mzee Luhanjo anasema wale wa EPA wanafamilia kwa hiyo tusiwe na haraka any legal action itaathiri wengi...sasa hili la mama Rwakatare mwenye akili hata kidogo atajua kuna usanii wa hali ya juu hapo hasa kama waijua vizuri historia ya huyu mchungaji wa kuchonga.

Ushi
 
Tupeni basi historia yake!
 
Nguvu anazotumia mama Lwakatare si za Mungu, kwa vile matendo yake mengi yanapingana na Mungu!Kama anataka tumwamini atoe ufafanuzi juu ya mambo yafuatayo:
*Aweke bayana watu anao shirikiana nao kibiashara,hasa wale wa Marekani.
*Mume wake yuko wapi,na kwa nini aliachana naye.
*Haoni kwamba kushirikiana na mafisadi wa CCM ni kulitukanisha jina la
Yesu, na kwamba kwa kufanya hivyo anazidi kuwafukarisha watanzania,
kwa vile sasa hawezi kukosoa utendaji wa CCM, tendo ambalo ni kinyume na
mapenzi ya Mungu?Mungu ametukataza kukubaliana na waovu.
*Haoni kwamba kukubali ubunge uchwara aliopewa, ni sawa na kutumikia
mabwana wawili tendo ambalo Yesu mwenyewe alilipiga vita kwa
nguvu zote?
*Haoni kwamba anakubaliana na dhambi ya CCM ya ufisadi?Neno la Mungu limetukataza
kushiriki dhambi za watu wengine!
*Haoni kwamba kama kweli ni mtumishi wa Mungu anajipamba mno?Ingekuwa vema
kama angevaa kawaida,halafu ziada akagawana na maskini.

MTAWAFAHAMU KWA MATENDO YAO!
 
Ukweli wa hili utajulikana tu na Mungu atatukuzwa; mwanadamu atashushwa! Kwani Mungu husimama mwenyewe na ahadi zake ni za milele. Lakini wakati huo huo Mungu hutuma wajumbe wake kuwaambia wenye nguvu ukweli.

Unless Mungu afanye miujiza ya kuweka uwazi kweli, nina wasiwasi huo ukweli hautaweza kujulikana...sio leo wala kesho. Ili tuweze kujua ukweli, tunahitaji serikali iingilie na kuamuru mkondo wa sheria ufuatwe.

Sasa je ni serikali hipi hiyo yenye matakwa na ubavu wa kutekeleza hilo?
 
Ndibalema,
Suala la uchungaji haliwezi kuchunguzwa kwenye forum au mahakamani na ushahidi kutolewa.Kazi ya Mungu hujipambanua kwa matokeo yake na kama yupo mtu anayelitumia jina la YESU kuhadaa watu haihitajiki mahakama wala PCCB kutoa ushahidi,Mungu humuumbua mtu huyo "kwa maana yeye huwajua walio wake na walio wake huyafanya yaliyo mapenzi ya MUNGU"

Nafikiri hoja hapa jukwaani ingekuwa siyo kuhukumu na kutoa misimamo ya kiimani kuwa ni uongo au siyo uongo.Hili ni suala la kiimani na ushahidi unapatikana kwa kuanzia na kuamini kwenyewe.

Nimekuelewa vizuri Mzee wa G.
Lakini hebu tujiulize Mchungaji kwa upande wa pili anapofanya mambo kinyume(tofauti) na uchungaji wake, mathalani Uzinzi, Uongo, Wizi na Utapeli. Still tuendelee tu kuamini mambo anayoyafanya eti kwa kuwa Uchungaji hauchunguzwi mahakamani au PCCB?
Hapa nina shaka kwanza na uchungaji wa Lwakatare kabla ya kuangalia na kukubali yanayofanyika katika Kanisa lake.
 
Hapana; dhambi ya kumfukuru Roho Mtakatifu haijatajwa adhabu yake; tunachofahamu ni kuwa "mshahara wa dhambi ni mauti, na karama ya Mungu ni uzima wa milele". Hivyo dhambi zote mshahara wake ni mauti.
Kukusahihisha kidogo Mwanakijiji Mathayo12 ;32 "Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao"

FP kumbe Bible unainyaka nyaka mkubwa?
 
.....................a. Kama kuna kikundi cha watu (bila Rev. Lwakatare kujua) wameamua kuigiza, kujificha vichakani na wengine kwenda kudai kuwa wameona misukule wakiwa na lengo la kujipatia maisha ya bure nani atajua?....................

.............kwi kwi kwi kwi kwi..............Mzee MKJJ hiyo hapo juu imenivunja mbavu kweli leo..........
 
Back
Top Bottom