Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Serikali haiwezi kukaa pembeni na huku ikiona hatari ya jamii yetu kuendelea kuwa na imani potofu.
Kwanini kusiwe na kampeni ya kuumaliza uchawi badala ya kutegemea makanisa?
Kwani hata makanisani si ndio mafisadi waliko na wachawi?
 
Haya mambo mbona hayasikiki katika makanisa mengine kama anglikana, RC, lutherani n.k.
 
Nikisema ni "usanii" najua nitashambuliwa sana lakini nasema hivi: Yesu alifanya miujiza mingi km kufufua (Lazaro), kutembea juu ya maji, kuponya wagonjwa (ukoma, upofu), kulisha watu wengi (mikate 5 wakashiba watu 5,000), kutoa pepo na mingine mingi. Leo hii tunaona maigizo kama:
1. Uponyaji feki: Watu wanadai kuponesha viwete, vipofu nk, lakini sijawahi kushuhudia wala kusikia mtu anayefahamika kuwa kiwete wa polio ambaye sasa anatembea, au kiwete ambae sasa anaona kwa miujiza hii, ingawa wanatangaza kila kukicha. Hebu anayejua atutajie japo jina la mtu mmoja tu aliyekutana na miujiza hii. Wale walioandikwa kwenye biblia walijulikana kabisa kwa majina na wanakotoka. Nawachagiza wanaoshabikia haya mambo ya miujiza ya kina Lwakatare na wengine kama hawa, waje hapa na majina halisi na anwani (au angalao taja anakaa wapi au ilitokea wapi) ya watu waliopata miujiza hii.
2.Kunena kwa lugha "feki" kama "ooooh rrroboshankaraktsika rraboshhhh". Lugha zilizonenwa katika biblia zilieleweka kwa waliosikia, kwani walizisikia katika lugha zao wenyewe tofautitofauti. Mbona hii "ooooh rrrobosshhhh" haieleweki ni kitu gani?
3. Kufufua "misukule" feki. Hii ni tofauti sana na Yesu ambaye alimfufua Lazaro "live" kutoka kaburini, mtu aliyejulikana kabisa.

Na mengine mengi ya ajabu. Sasa hii "miujiza" kweli ni ya Mungu au ndiyo ibilisi mwenyewe?

Naunga mkono kuwa huyo Mch Lwakatare na wenzie wa namna hiyo wachunguzwe, tutajua zaidi.

Hapana sio usanii kuhusu Lzaro naungana na wewe Kithuku , kuhusu kunena kwa lugha usichanganye lugha za wanadamu, malaika , na lugha ya roho mtakatifu! Kunena Kupo kaka wala sio utani, ila kuwepo kwake haimaanishi wasanii hawapo nao wako kibao pia. Na wala usiponena haimanishi wewe sio mcha Mungu, nanena ndugu I can well explain on this

Waberoya
 
Kuna wakati fulani Yesu alimponya mtu mmoja mwenye ukoma; akamwambia "nenda kwa makuhani ukajioneshe". Lengo lilikuwa ni kuthibitisha kuwa ameponga kweli na haikuwa hoax.

Wakati mwingine alimponya mtu mmoja aliyezaliwa kipofu. Wakuu wa Makuhani waliposikia habari hiyo hawakuamini na wakawaita wazazi wa huyo jamaa na kuuliza habari zake. Wale wazazi wakasema "yeye ni mtu mzima muulizeni mwenyewe". Yule bwana alipoitwa akawaambia kuwa "mimi sijui kama huyo aliyeniponya ni mtakatifu au la, ninachojua ni kuwa nilikuwa kipofu na sasa naona".

Katika mifano hiyo miwili utaona kuwa kwenye mambo ya miujiza kufanya uchunguzi siyo kukana miujiza bali kuondoa uwezekano wa uongo. Ninaamini miujiza lakini miujiza yote inafanywa kwa kutumia vitu vya asili. So, kuhoji suala la misukule si kukana uwezo wa Mungu kutenda miujiza bali kuthibitisha nguvu hizo na kuzikiri lakini wakati huo huo kuondoa uwezekano wa roho ya mwanadamu kujikweza na kujiinua na kujisamamisha mahali pa Mungu!

Umesema vema Mwanakijiji kwa mifano uliyoitoa kutoaka kwenye Biblia Takatifu.Hata leo wanaponywa na watu wanashuhudia ila tatizo wasioamini ndio wa kwanza kusema hakuna miujiza.

Kama nia yako haikuwa kukataa kuwa miujiza ipo usingesema anachokifanya Mch.Lwakatare ni uongo kama hauna uthibitisho.
 
Hili suala watu wameligeuza kuwa ni la Biblia, imani na kuhoji uwezo wa Mungu.

a. Mungu is the absolute sovereign; Anaweza kutenda jambo lolote, wakati wowote ule na kwa namna yoyote ile. Lakini Mungu anafungwa na ahadi zake. Mungu hatofanya jambo ambalo litavunja ahadi zake au neno lake. Na kwa vile Mungu hasemi uongo basi kila asemacho hubakia kweli, na kama hakikuwepo basi kitakuwepo.

b. Matendo ya Miujiza ni urithi wa Ukristu (na hata dini nyingine); lakini ni Katika Ukristu ambapo JIna la Yesu linatumika kutenda miujiza. Wakristu wanaamini kuwa wamepewa mamlaka ya "kukanyaga, nyoka na nge" na ya kuwa hata wakinywa "kitu cha kuwafisha hakitawadhuru".

c. Muujiza wa Mungu si kitu cha kificho; Muujiza hauwezi kuwa muujiza hadi kuwe na vitu fulani; kwanza lazima watu wajue kulikuwa na tatizo mahali fulani na pili hakukuwa na maelezo mengine yoyote ya asilia (natural explanation) na tatu, muujiza ulikuwa mara, na kamili. Muujiza kutoka Mbinguni huingilia kati utendaji kazi wa asili na kuubadilisha, kuongeza mwendo, au kuleta matokeo (effect) kwa haraka.

d. Muujiza wa Mungu unahusisha vitu vya asili; mikate, mafuta, mwili uliokufa, n.k n.k Miujiza ya Kikristu haihusishi ombwe (vacuum). Yesu aliposimama kukemea upepo mkali na kuamuru "Tulia" alikuwa anazungumza kwenye kitu halisi; aliposimama na kugeuza maji kuwa mvinyo alihusisha kitu asilia (maji); alipoongeza samaki na mikate kwa watu 5000 hakutumia vikapo vitupu. Wakati Elisha ameenda kwa yule mama Mshunami alikuwa hana kitu kabisa cha kuwalisha yeye mwenyewe, Eliya na mtoto wake; alikuwa na mafuta kidogo na kibaba cha unga. Elisha akamuagiza huyo mama kutumia vitu hivyo (vya asili) kutenda muujiza.

So, Miujiza tunaizungumzia lazima itoke from the natural to the supernatural;

e. Muujiza usiofuata (d) hapo juu hauko katika realm ya miujiza kwani unahusu uumbaji na kazi ya Mungu moja kwa moja anapofanya something out of nothing. Mingine yote inahusisha vitu vya asilia kwenda kwenye supernatural.

f. Hivyo, suala hapa siyo kuamini utendaji miujiza au kutoamini utendaji miujiza; suala la Lwakatare halihusiani moja kwa moja na kama tunaamini Mungu anatenda miujiza au Biblia inasema nini. Suala hapa linahusu madai ya watu kuwa walikufa (kitu cha asili) na ya kuwa sasa wako hai baada ya kuchukuliwa na kutumikishwa kwa nguvu sehemu fulani.

Now,

- Aidha hawa watu hawakufa bali walizimia au walipigwa ganzi au walikufa.

- Kama walizimia na kupigwa ganzi, nini kilifuatia baada ya kifo hicho na kwenye makaburi kule alizikwa nani? Mtu akija na kusema "huyu ni x, alikufa tarehe hii na kuzikwa hapa" halafu tukamwambie twende tuoneshe hilo kaburi na akaenda na kutuonesha kaburi, tukalifukua na ndani yake tutakosa mabaki ya mwili, basi hapo tuna kesi kwa sababu tukikuta mifupa mle lazima tujiulize huyo aliyesema yu hai ni nani, na mifupa hii kwenye kaburi ni ya nani. Hapa inaweza kuwa mnazungumzia murder case!

- Kama tunakuta mwili, hatuna budi kumuuliza huyu "msukule" wetu na kupima undugu wake na ile familia. Sayansi inaweza kabisa leo hii kukuonesha kuwa fulani ni mtoto wa fulani, au fulani anaundugu wa damu na mtu fulani, siyo kwa kuangalia pua au paji la uso bali kwa ushahidi wa kisayansi. Sasa hawa jamaa wanaposema wanatoka familia fulani na walikufa, basi wale ndugu zao wanaojitokeza tupime kama wanahusiana nao kwa damu kwa sababu itakuwaje kama yote ni maigizo?

g. Nimeshiriki katika kila aina mikutano ya Injili kuanzia ya kina Kulola, Maboya, Mwakasege, Egan Falk n.k n.k I know more about this area kuliko watu wengine wanavyofikiria; ndio maana kwangu hoja yangu hapa has nothing to do with the idea and authenticity of Christian miracles. Kwangu inahusu combinationa ya biashara, siasa, dini na mahitaji ya watu. Kwamba sisi kama jamii tusije kukubali kuona mtu ambaye ana nguvu za kisiasa, nguvu za kidini na nguvu za kibiashara akianza kuabuse nguvu hiyo.

h. Kwa wale waliouliza kama nimeshasema ni hoax uchunguzi wa nini? Ukweli ni kuwa miye nimejenga proposal ambayo imetokana na kulifuatilia jambo hilo na ninasimamia kuwa ni hoax. Sasa hiyo ni kama theoretical position na uchunguzi utaithibitisha au kuikanusha. Haja ya uchunguzi ni kuni prove kuwa ninachosema si kweli na kama nilivyosema uchunguzi ukionesha ni kweli walikuwa ni misukule (watu waliodaiwa kufa, kuchukuliwa na kutumikishwa na baadaye kurejeshwa) basi nitafuta kauli yangu.

Wanaogopa nini kuacha uchunguzi ufanyike? nini watu wanaficha. Kama unaamini miujiza hauna hofu ya kuweka muujiza wako mbele ya uchunguzi ili Mungu atukuzwe na Jina la Bwana liinuliwe!
 
FMES,

Heshima yako natanguliza.

Swali: If the woman in question is a member of the National Assemmbly,
then why shouldn't this be a 'national' debate?

....To Whom Much Is Given, Much Is Required.

Only, kama kuna sheria ya jamhuri imevunjwa na hayo mambo yake otherwise tulipaswa kuwa tumejifunza sana na yale mauaji ya Shinyanga, yaliyompelkea Mwinyi kujiuzulu, kwa sababu yalianza na this kind of hype kwenye media, the next thing wananchi wakauwawa bila sababu za kisheria,

Naona tunataka kurudia yale yale, kwa sababu hii nothing to do hype, ambayo haielezei iwapo kuna sheria zetu za jamhuri kama zimevunjwa, the next thing wataumia wananchi bila sababu za kisheria, ni lazima tujifunze kutenganisha dini na sheria za serikali,

Mama Rwakatare, ni mbunge ni kweli na haya mambo yake yanatuhusu taifa iwapo, amevunja sheria za jamhuri na haya mambo yake otherwise serikali na taifa tujiepushe sana na kujiingiza na masuala ya dini za jamii.

It is about time hii topic ikahamishiwa inakostahili zaidi kuliko hapa kwenye serious siasa za taifa letu.
 
Huo ndio ukweli kaka, la muhimu tukisha jua ukweli, tunakaa humo humo kwenye makanisa yetu, hali ukijua kuna swala fulani personally hukubaliani nayo! Bible tells us tukiujua ukweli utatuweka huru.Kuna vitu vingi haviko sawa ukivijua hata siku kama kuna mtu anachokonoa imani yako, you just keep quiet, hakuna haja ya hasira,DINI HIZI ZINA WENYEWE. Our task ni kumwabudu Mungu, other politics ni kuwaachia wenyewe.

Nisaidie ndugu, nimesoma bible cover t0 cover, sijakutana na hiyo cases.Cases zilizopo za wafu ni nyingi , ila sio misukule-Nipe kipande

Kuna swala la Yesu kuwa transfigureed mlimani, wale wanafunzi wakawaona Musa na Eliya.Kuna swala

Lipo la Lazaro, mtoto wa Binti yairo , na mtoto wa mwanamke mjane kufufuliwa but was not misukule

Kuna wafu walionekana na wakapotea at the time Yesu anafufuka!

Nasubiri ipande cha misukule, kindly weka pia kwenye PM yangu

Waberoya

Mkuu, heshima mbele. Nili-quote uliposema hakuna wafu walioongea, nikakuambia wapo (hukusema misukure, labda kama nilipitiwa-samahani). Kumbuka stori ya Saul na Samwel. Saul alipokwenda kwa "mwonaji", akampandishia Samwel, Marehemu Samwel akatabiri mwisho wa Saul na ukatokea.
Suala la msukure labda tujiulize; Je wakati wa Agano la kale mpaka Yesu misukure walikuwepo? Je leo misukure wapo? Kama hawakuwepo wakati huo na sasa wapo, je tunawezapata biblical principles kukabili ishu hii? Kumbuka "yote yanawezekana kwake yeye aaminiye" - Bible. Kumbuka hakuna sehemu kwenye biblia inayoongelea "heroin", ila kutokana na principles za Biblia kutumia heroin ni dhambi.
Kama wafu walifufuliwa, kwa nini misukure wasirudishwe? Unless uniambie hawa-exist, kitu ambacho siwezi "ku-prove"
 
Hiyo mingine yawezekana kuwa ipo; lakini sidhani kama kuna muujiza mkubwa kama wa kudai kuleta watu uzimani na kuwaonesha kwenye picha kuwa waliwahi kuwa wamekufa. Miujiza mingine ya kupona mafua, viwete kutembea n.k ni miujiza ambayo binafsi hainisumbui kwani implication yake siyo kama hiyo ya Misukule.

Wengi tumeshazoea mikutano ambayo "miujiza kufanyika" "viwete kutembea, viziwi kusikia na maskini kuhubiriwa habari njema". All that is fine; lakini unapokuja na kudai kuwa kuna watu wamekufa na wewe unao wakiwa wazima unaenda kinyume kabisa na kanuni za asili za ulimwengu na maneno ya Biblia kuwa "baada ya kufa hukumu" na siyo kwenda kulima mashamba ya watu!

Burudani kwenye bulogu....mbavu sina....
 
Only, kama kuna sheria ya jamhuri imevunjwa na hayo mambo yake otherwise tulipaswa kuwa tumejifunza sana na yale mauaji ya Shinyanga, yaliyompelkea Mwinyi kujiuzulu, kwa sababu yalianza na this kind of hype kwenye media, the next thing wananchi wakauwawa bila sababu za kisheria,

Naona tunataka kurudia yale yale, kwa sababu hii nothing to do hype, ambayo haielezei iwapo kuna sheria zetu za jamhuri kama zimevunjwa, the next thing wataumia wananchi bila sababu za kisheria, ni lazima tujifunze kutenganisha dini na sheria za serikali,

Mama Rwakatare, ni mbunge ni kweli na haya mambo yake yanatuhusu taifa iwapo, amevunja sheria za jamhuri na haya mambo yake otherwise serikali na taifa tujiepushe sana na kujiingiza na masuala ya dini za jamii.

It is about time hii topic ikahamishiwa inakostahili zaidi kuliko hapa kwenye serious siasa za taifa letu.

Kuna ushahidi wa kimazingira na kisayansi kuwa inawezekana Rev/Mbunge anadanganya wananchi, surely hata imani ya CCM inasema "NITASEMA KWELI DAIMA".
 
Nakubaliana na wew ekaka, SWALA NI KUWA WAKATI HAWA WATU 'WANAKUFA' MUNGU ALIKUWEPO NA ALIWAONA! HAKUWASAIDIA.LEO HII ANAKUJA BINADAMU MWINGINE ANAMWOMBA MUNGU 'WASIFE -WAFUFUKE' MUNGU HAJICHANGANYI KIIVYO, HAWAKUFA(Hapo sawa) na kama ni kweli she still have opportunity akawaombee wafu wote pale kinondoni wafufuke. wengine waliuawa, walibakwa n.k..

Waberoya
Mkuu, thats being either biased or not knowing your bible. Yesu hakufufua wafu wooote. Alisema "... waache wafu wawazike wafu wenzao ..." Na alisubiri Lazaro akafa kwanza ndo akaenda kumfufua. Otherwise asingemfufua maana angekuwa hajafa.
 
Hili suala watu wameligeuza kuwa ni la Biblia, imani na kuhoji uwezo wa Mungu.

a. Mungu is the absolute sovereign; Anaweza kutenda jambo lolote, wakati wowote ule na kwa namna yoyote ile. Lakini Mungu anafungwa na ahadi zake. Mungu hatofanya jambo ambalo litavunja ahadi zake au neno lake. Na kwa vile Mungu hasemi uongo basi kila asemacho hubakia kweli, na kama hakikuwepo basi kitakuwepo.

b. Matendo ya Miujiza ni urithi wa Ukristu (na hata dini nyingine); lakini ni Katika Ukristu ambapo JIna la Yesu linatumika kutenda miujiza. Wakristu wanaamini kuwa wamepewa mamlaka ya "kukanyaga, nyoka na nge" na ya kuwa hata wakinywa "kitu cha kuwafisha hakitawadhuru".

c. Muujiza wa Mungu si kitu cha kificho; Muujiza hauwezi kuwa muujiza hadi kuwe na vitu fulani; kwanza lazima watu wajue kulikuwa na tatizo mahali fulani na pili hakukuwa na maelezo mengine yoyote ya asilia (natural explanation) na tatu, muujiza ulikuwa mara, na kamili. Muujiza kutoka Mbinguni huingilia kati utendaji kazi wa asili na kuubadilisha, kuongeza mwendo, au kuleta matokeo (effect) kwa haraka.

d. Muujiza wa Mungu unahusisha vitu vya asili; mikate, mafuta, mwili uliokufa, n.k n.k Miujiza ya Kikristu haihusishi ombwe (vacuum). Yesu aliposimama kukemea upepo mkali na kuamuru "Tulia" alikuwa anazungumza kwenye kitu halisi; aliposimama na kugeuza maji kuwa mvinyo alihusisha kitu asilia (maji); alipoongeza samaki na mikate kwa watu 5000 hakutumia vikapo vitupu. Wakati Elisha ameenda kwa yule mama Mshunami alikuwa hana kitu kabisa cha kuwalisha yeye mwenyewe, Eliya na mtoto wake; alikuwa na mafuta kidogo na kibaba cha unga. Elisha akamuagiza huyo mama kutumia vitu hivyo (vya asili) kutenda muujiza.

So, Miujiza tunaizungumzia lazima itoke from the natural to the supernatural;

e. Muujiza usiofuata (d) hapo juu hauko katika realm ya miujiza kwani unahusu uumbaji na kazi ya Mungu moja kwa moja anapofanya something out of nothing. Mingine yote inahusisha vitu vya asilia kwenda kwenye supernatural.

f. Hivyo, suala hapa siyo kuamini utendaji miujiza au kutoamini utendaji miujiza; suala la Lwakatare halihusiani moja kwa moja na kama tunaamini Mungu anatenda miujiza au Biblia inasema nini. Suala hapa linahusu madai ya watu kuwa walikufa (kitu cha asili) na ya kuwa sasa wako hai baada ya kuchukuliwa na kutumikishwa kwa nguvu sehemu fulani.

Now,

- Aidha hawa watu hawakufa bali walizimia au walipigwa ganzi au walikufa.

- Kama walizimia na kupigwa ganzi, nini kilifuatia baada ya kifo hicho na kwenye makaburi kule alizikwa nani? Mtu akija na kusema "huyu ni x, alikufa tarehe hii na kuzikwa hapa" halafu tukamwambie twende tuoneshe hilo kaburi na akaenda na kutuonesha kaburi, tukalifukua na ndani yake tutakosa mabaki ya mwili, basi hapo tuna kesi kwa sababu tukikuta mifupa mle lazima tujiulize huyo aliyesema yu hai ni nani, na mifupa hii kwenye kaburi ni ya nani. Hapa inaweza kuwa mnazungumzia murder case!

- Kama tunakuta mwili, hatuna budi kumuuliza huyu "msukule" wetu na kupima undugu wake na ile familia. Sayansi inaweza kabisa leo hii kukuonesha kuwa fulani ni mtoto wa fulani, au fulani anaundugu wa damu na mtu fulani, siyo kwa kuangalia pua au paji la uso bali kwa ushahidi wa kisayansi. Sasa hawa jamaa wanaposema wanatoka familia fulani na walikufa, basi wale ndugu zao wanaojitokeza tupime kama wanahusiana nao kwa damu kwa sababu itakuwaje kama yote ni maigizo?

g. Nimeshiriki katika kila aina mikutano ya Injili kuanzia ya kina Kulola, Maboya, Mwakasege, Egan Falk n.k n.k I know more about this area kuliko watu wengine wanavyofikiria; ndio maana kwangu hoja yangu hapa has nothing to do with the idea and authenticity of Christian miracles. Kwangu inahusu combinationa ya biashara, siasa, dini na mahitaji ya watu. Kwamba sisi kama jamii tusije kukubali kuona mtu ambaye ana nguvu za kisiasa, nguvu za kidini na nguvu za kibiashara akianza kuabuse nguvu hiyo.

h. Kwa wale waliouliza kama nimeshasema ni hoax uchunguzi wa nini? Ukweli ni kuwa miye nimejenga proposal ambayo imetokana na kulifuatilia jambo hilo na ninasimamia kuwa ni hoax. Sasa hiyo ni kama theoretical position na uchunguzi utaithibitisha au kuikanusha. Haja ya uchunguzi ni kuni prove kuwa ninachosema si kweli na kama nilivyosema uchunguzi ukionesha ni kweli walikuwa ni misukule (watu waliodaiwa kufa, kuchukuliwa na kutumikishwa na baadaye kurejeshwa) basi nitafuta kauli yangu.

Wanaogopa nini kuacha uchunguzi ufanyike? nini watu wanaficha. Kama unaamini miujiza hauna hofu ya kuweka muujiza wako mbele ya uchunguzi ili Mungu atukuzwe na Jina la Bwana liinuliwe!

Glory to God, well spoken

Nadhani ukisema uchunguzi ufanyike bila wewe kuonyesha wasiwasi wako ni unafiki wa nafsi yako, watu hatutakiwi kuishi hivyo, mtu akinipinga kwa wasiwasi au hukumu niliyoitoa atakuwa amenisaidia.Lakini kitu ninacho moyoni, eti nisikiseme, kwa sababu nikisema nitaonekana nimeshahukumu! HAIKO HII WA MWANADAMU MWENYE NORMAL REASONING.

waberoya
 
Halafu Lazaro, alikuwa na dada zaka Martha na Maria na watu walimjua mtaani, na hapo ndipo effect ya muujiza wa kufufuliwa kwake unapokuwa na nguvu. Na kumbuka kuwa Lazaro aliachwa akae kaburini kwa siku kadhaa ili effect of death zianze kuonekana "Bwana ni zaidi ya siku tatu sasa na ameanza kunuka".

Yesu hakuwa na wasiwasi na completeness of this miracle. Hakufanya gizani wala kusingizia "jamani ni kazi ya Mungu" Alifanya mchana kweupe mwenye kupinga alipinga mwenye kukubali alikubali, lakini kila mtu alijua Lazaro alikufa na sasa yuko mzima.

Kama Yesu alikubali kuchunguzwa, kwanini watu wanaogopa kumchunguza Lwakatare?
 
very good question!dawa ni kwenda kufukua na kuona walizika nini?lkn katika haya mambo ya kichawi huwa hawakuti mabaki ya yule waliemzania kafa!

FL, my argument ni kuwa ili kujua ni "mambo ya kichawi" ndio maana twende tuangalie huko walikozikwa kwani tukiikosa miili, ina maana hakuna mtu alizikwa hapo, na ndipo tuangalie uhusiano wa damu wa former "Msukule" na familia yake. Lakini tukiangalia kaburi alilodaiwa kuzikwa na kukuta mabaki ya mwili mle tutaelezeaje mabaki hayo wakati kuna mtu kasimama pembeni anasema nini ndiye aliyezikwa humo?
 
Mkuu, thats being either biased or not knowing your bible. Yesu hakufufua wafu wooote. Alisema "... waache wafu wawazike wafu wenzao ..." Na alisubiri Lazaro akafa kwanza ndo akaenda kumfufua. Otherwise asingemfufua maana angekuwa hajafa.

Najua hatukuelewana lugha tuko pamoja, Yesu alimfufua LAZARO, hakuwa msukule, hoja yangu ni kuwa kwa nini msukule is so special wakati watu wengi wanakufa kwa ujambazi, kubakwa, vifo vya kupanga n.k kwa nini wasifufuliwe hawa watu, ambao pengine siku zao za kufa hazikufika ila wamekuwa forced na external forces? kwa nini Rwakatare asiwageukie hawa? yeye na Gwajima wanadanganya watu

waberoya
 
Halafu Lazaro, alikuwa na dada zaka Martha na Maria na watu walimjua mtaani, na hapo ndipo effect ya muujiza wa kufufuliwa kwake unapokuwa na nguvu. Na kumbuka kuwa Lazaro aliachwa akae kaburini kwa siku kadhaa ili effect of death zianze kuonekana "Bwana ni zaidi ya siku tatu sasa na ameanza kunuka".

Yesu hakuwa na wasiwasi na completeness of this miracle. Hakufanya gizani wala kusingizia "jamani ni kazi ya Mungu" Alifanya mchana kweupe mwenye kupinga alipinga mwenye kukubali alikubali, lakini kila mtu alijua Lazaro alikufa na sasa yuko mzima.

Kama Yesu alikubali kuchunguzwa, kwanini watu wanaogopa kumchunguza Lwakatare?

Hao misukule wapo kanisani Mikocheni si uende ukafanye uchunguzi?hili nao mpaka ufanyiwe?acha uvivu!maneno matupu hayavunji mfupa chukua hatua nenda mikocheni kanisani kahakikishe ambacho unakitilia mashaka
 
[/B]

sina utaalamu, sina nyenzo, na maslahi makubwa si ya kwangu bali ya Taifa. Hivyo ungana nami kutaka Polisi wafanye uchunguzi wa kisheria. Mimi nikienda si nitawakodolea macho tu na kuwaangalia; sina mamlaka ya kumhoji mtu yeyote kisheria au kutaka makaburi yafukuliwe.

Kwa vile umekubaliana nami ipo haja ya uchunguzi, je uko tayari kuungana nami kutaka vyombo vya serikali kuanzisha uchunguzi wa misukule na huduma hiyo ya Mama Lwakatare?
 
mimi sijakubaliana na wewe mimi sina shaka na Nguvu za MUNGU!wewe mwenye mashaka ndo uende!
 
Back
Top Bottom