Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Mch. Mhe. Dr. Getrude Lwakatare achunguzwe!

Nchi ya wajinga wanapenda na kuamini "miujuza agh!

Hakuna miujiza "isipokuwa" huyo mtu awe mjumbe na nabii kutoka kwa Muumba

Unabii haupo tena kwahiyo "hakuna" miujuza tena

Ujinga utawamaliza wana kondoo poleni...
 
Nakumbuka Tujisenti alisema kitu fulani kuhusu huyu mama kwenye thread hii.. is this something personal?
MZ MWanakijiji there is nothing personal na huyo mama, ila nimekua nafuatilia kwa karibu issue ya watoto yatima.Wewe fikiria mtu ana mashule 27 lakini unarudisha yatima kwao hata wale wa darasa la saba!!!! Kwa nini alichukua watoto na kuwapa matumaini????
 
Mch Lwakatare ni fake nawashangaa na hao wanayompa sadaka kila kukicha. Anatumia uchawi aliojifunza Nigeria. Yeye ni mfanya biashara hakuna cha Mungu wala nini. Wewe mtu wa Mungu gani ananyanyasa yatima??
 
These are very dangerous days my friend,the devil can do anything.Wingi wa watu hapo kanisani sio hoja.Kumbuka kwamba njia iendayo mbinguni ni nyembamba,kwa hiyo wengi hawaioni.Binafsi nashuhudiwa kwamba huyu mama has something to hide,ukiachilia mbali hili la misukule!

Mwanakijiji,

Mimi naamini kwa YESU YOTE yanawezekana!

Isimuhukumu huyu mama. Ina maana waumini wote hapo kanisani hawayaoni hayo yote?

FP
 
Kuna wakati fulani Yesu alimponya mtu mmoja mwenye ukoma; akamwambia "nenda kwa makuhani ukajioneshe". Lengo lilikuwa ni kuthibitisha kuwa ameponga kweli na haikuwa hoax.

Wakati mwingine alimponya mtu mmoja aliyezaliwa kipofu. Wakuu wa Makuhani waliposikia habari hiyo hawakuamini na wakawaita wazazi wa huyo jamaa na kuuliza habari zake. Wale wazazi wakasema "yeye ni mtu mzima muulizeni mwenyewe". Yule bwana alipoitwa akawaambia kuwa "mimi sijui kama huyo aliyeniponya ni mtakatifu au la, ninachojua ni kuwa nilikuwa kipofu na sasa naona".

Katika mifano hiyo miwili utaona kuwa kwenye mambo ya miujiza kufanya uchunguzi siyo kukana miujiza bali kuondoa uwezekano wa uongo. Ninaamini miujiza lakini miujiza yote inafanywa kwa kutumia vitu vya asili. So, kuhoji suala la misukule si kukana uwezo wa Mungu kutenda miujiza bali kuthibitisha nguvu hizo na kuzikiri lakini wakati huo huo kuondoa uwezekano wa roho ya mwanadamu kujikweza na kujiinua na kujisamamisha mahali pa Mungu!

Nimeipenda hii verse. Agreed bro
 
SIMPLE LOGIC: Inasemwa kuwa hao "misukule" walichukuliwa na watu ambao wamejisalimisha kanisani (ndipo "siri" ya kuwepo kwa hao misukule msituni ikfahamika, nadhani walishuhudia au kuungama kwa mchungaji)

Sasa kwanini hao hao "waliookoka" wasiwajibike kuwarudisha misukule hao kwa ndugu zao? Yaani kweli hata waandishi wa habari wanashindwa kuunganisha hizi doti na kuishia kukuza vitu na kujengea watu hofu? Kanisa lilikuwa na haja gani ya kutangazia ndugu "kuja kuwatambua" kama waliofanya tukio hilo wapo?

I didnt think of that, ni kweli kama hao watu wapo kwa nini wasiwajibishwe sasa na kusema walikowatoa wapi hao misukule? Serikali inasema nini kwa watu wanaochukuwa watu misukule, ina maana imewaachia kwa kuwa wameokoka?
 
Kwa mujibu wako inaonyesha wakatoliki tu wa zamani ndio walikuwa wanafanya miujiza , humjui mkatoliki yeyote kwa sasa anayefanya miujiza, inspite tha fact that we hanve milions of them now adays.

Ok, nadhani maada ni Lwakatare tuache ya wakatoliki, maana hali ya hewa inaweza kuchafuka humu ndani.

We have been blindly following these denominations, hatujui wala hatufuatiliil history zake, vitu vingine ni sometime hata common sense zetu hazifanyi kazi sawa sawa.

1.Mtu anasema tutumie sanamu ya fulani tunafuata hata hatuulizi mara mbili.

2.Mtu anasema ukifa utaombwa uende peponi , tutakuombea utoke pagatori , tunakubali , we dont ask.

3.Bible tells clearly that we should ask and pray by the name of Jesus, LEO mtu anasema tutumie jina la Maria , with no bibilical evidence, tunakubali

4.Mtu anasema tufungishe au tufunge ndoa ya jinsia moja, tunasema sawa.

5.Watu wanasema twende tukaubiri injili ulaya, bila passport, viza wala nauli, still people say Yes

6.Kuwa tukamsubiri Yesu porini anarusi tarehe 30/4 /2008 WATU wanasema ndiyo..

7.Kuwa kuna watu wanachukiliwa msukule, na kurudishwa still people say Yes...

8.Kuwa Yesu alibatizwa maji mengi, let us by our reasoning with no biblical proof tubatizane kwa maji machache, we say YES.

9.Kuwa fanyeni kazi wee, sisi wachungaji tunataka fungu la KUMI inspite the fact that, hakuna uthibitisho wa kutoa fungu la kumi kwa wakristo wa agano jipya still people say YES.

10.Wengine wanaambiwa dini yao ndiyo ya kweli, na ukijiua unaenda peponi , huko unakutana na wanawake bikra 7, bila kuwaza kuwa vitabu vinigine vyote vya dini tofauti na ya kikristo vilikuja 600 years latar! bado watu wanasema YES!

COMMENT

WACHUNGAJI WAONGO, WALIKUWAPO EVEN BEFORE JESUS WAS BORN refer Balaam! WATAKUWAPO TU.SWALA NI KWA KIASI GANI TUNASOMA BIBLIA NA KUWEZA KUCHAMBUA MAANDIKO SISI WENYEWE NA KUJUA ZIPI PUMBA NA ZIPI MAHINDI THATS IS OUR TASK. Mfano wengi wanamsema mama Lwakatare vibaya still we can not stand for our faiths! Be honest most of us hatuja question kuhusu dini zetu, tunakuwa wakali zinapoguswa hata kama kuna ukweli, kwa sababu ndiko tuliko zaliwa, kulia ,olea n.k

watu wasome biblia, waamue wenyewe based on the fact of bible....no compromise, no meander.

THIS WAS JUST ANA ALERT:

1Corinthians 4:14 :I do not write these things to shame you, but to admonish you as my beloved children.

Waberoya

Half knowlegde is very dangerous. Kanisa na biblia ilianza nini?. Unatafuta muujiza mbali wakati Mungu yupo moyoni mwako? Miujiza ikitendeka hata sasa ndani ya kanisa
 
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu katika kanisa hilo, unaonyesha kuwa kati ya watu hao Misukule nane waliopatikana katika misitu hiyo baada ya waliowachukua kimazingira kumrudia Mungu, watano wameshachukuliwa na ndugu zao ambapo watatu bado wanaendelea kutunzwa na kusali katika kanisa hilo, hali iliyowafanya baadhi ya waunimi kusema kuwa ndugu zao watakuwa wamewasusa.

My Take:
Kanisa la huyu mama naamini linaeneza one of the most elaborated scheme of deception a.k.a a hoax! Inanikumbusha kisa cha Mchungaji Gilbert Deya wa Uingereza (raia wa Kenya) ambaye alikuwa amedai yeye na mke wake kuwa wanauwezo wa kuombea wa kina mama na wakapata mimba na kuzaa watoto hata kama kina mama hao walishapita uwezo wao wa kuzaa n.k

Ingawa mwanzoni mambo hayo yaliweza kuonekana ni miujiza, utaalamu wa kisayansi ulionesha kuwa mke wa mchungaji huyo na washirika wao kule Kenya walikuwa wananunua watoto wadogo na kuwapa kina mama wengine na kwa kufanya hivyo kufanya biashara ya watoto lakini wakati huo huo kulifanya kanisa la Mchungaji huyo kukua zaidi na kuwa na ujiko usio kifani kutokana na kazi ya "Mchungaji huyo".

Mwishoni, sheria ikakutana naye, mke wake akaswekwa jela na yeye mwenyewe mchungaji kutakiwa kurudishwa Kenya kukabiliana na mashtaka ya usafirishaji haramu wa watoto.

Naamini, kama kuna mtu ana ujasiri wa kuchunguza hii "misukule" na kanisa hilo kutaonekana pasipo shaka jinsi gani this hoax was propagated and carried out na hivyo kumpa mama Lwakatare ujiko na kumuongezea sadaka.

Natoa hoja, kanisa lake na yeye mwenyewe achunguzwe pamoja na hao "misukule" kwani anachezea imani za watu na hasa hofu yao ya mambo ya kishirikina.

Kwa vile tuna utaalamu wa DNA, basi misukule hao na "familia" zao na hata makaburi wanayodaiwa kuzikwa yachunguzwe ili wananchi wetu wasitekwe na ulaghai wa kidini unaoendeshwa kwa jina la dini.

Endapo uchunguzi wa kisayansi utaonesha kuwa kweli hawa watu walikufa, wakazikwa na baadaye kukutwa porini wakiwa wamechukuliwa misukule nitamwomba radhi; Lakini nasimamia kusema this is a HOAX inayofanywa na Mbunge Mchungaji!

Mwanakijiji, hivi uchunguzi huo una tija gani? Rwakatare hajaonekana akijaza watu kanisani sababu ya miujiza. After all, mara nyingi wanaoombea pale ni kikundi cha wanamaombi na yeye ni mara chache huhusika,tofauti na huyo wa Kenya na mkewe na wengine wengi. Nimewahi kufika pale na sikuona dalili za kiutapeli (hoax) na wala sio muumini wake. Badala yake niliona wanamaombi wake wa siku ile wakiwa hawajatulia hata sikushawishika kabisa kurudi pale na mgonjwa tuliyempeleka kwa ushauri wa watu. Hiyo ilikuwa kikwazo changu mimi kutofanikiwa labda, maana nilikuwa na mashaka na waliokuwa wanamwobea.

Ameshakuambia kwamba anao misukule ambayo imepata nafuu na wandugu zao hawajaonekana kutaka kuwachukua. Labda useme watangazwe misukule hao ndugu zao wanaofikiri labda jamaa zao ni marehemu waamke na kuwachukuwa. UCHUNGUZI mimi binafsi sioni ulazima.

Labda kama ungesema anadanganya kuponya watu wakati sivyo. Hata wanaodanganya Mungu hakai kimya milele, wanachapwa na miisho yao haipendezi hata kusimulia

Leka
 
mwe...mwe...mwe...Lekanjobe mwana gwa kumietu..ukuburunguka mo mumo...ujobie fiki, leka njobe une.......mzee yaani hapa hata sielewi unasemaje..mzee mwanakijiji kashika jembe saa hizi..na simu yake mkononi anasoma meseji yako sijui kama anakuelewa...tutakosa mazao safari hii..unazunguka humo humo tu eenh...umeweka labda kama nne hivi...ukuti fiki?

MUUJIZA UNAOTUFAA

Nasubiri muujiza wa Afrika nzima kuwa dunia ya kwanza na Tanzania kuongoza kiuchumi Duniani. Eee Mwenyeji Mungu tupe muujiza huu. Ndio unaotufaa sisi. Amin.....Amin...
 
Source p/se?, la sivyo itakuwa majungu. Kufungua Univ. haiwezi kuwa ndio sababu, akitaka anaweza kujenga vituka. Analo eneo kubwa kuliko lile la Tbt, ingawa kwa kujenga chuo kikuu bado ni dogo.
Nenda paleTabata watoto yatima walipokua utakuta imeandikwa ukutani
 
msukule gani hata upele mwilini hana!Acheni kuongopea watu,U can fool some people sometime but U cant fool all the people all the time!
 
msukule gani hata upele mwilini hana!Acheni kuongopea watu,U can fool some people sometime but U cant fool all the people all the time!

Upele wa nini? Misukule wanaishi maisha ya kawaida na hawana matatizo yoyote ya kiafya.
 
Huyu mama ana kila sababu ya kuchunguzwa...kila siku ni vioja..nasikia ametimua watoto wote yatima waliokuwa wakisoma kwenye shule zake.
 
Beyond explanations. Isijekuwa wamewaokota watu wenye maradhi ya akili kusikojulikana, wakawapeleka msituni. Hii bwana ni biashara na biashara lazima utangaze vinginevyo huta uza kitu. Strategic Church Management ya Mch, Mh,Dr. Lwakatare

Hivi nilikuwa wapi sikuiona hii thread before?.....shame on me...aiseee

Hosftede.....ukurasa mmoja hapo! Nimekuwa ni question hii miujiza ya aina hii kwa kweli.

Kwa nini hawa jamaa hawajaweza fanya miujiza ili watu waliorepotiwa kupotea ktk mazingira ya kishirikina wakaonekana? kwa nini, they clearly know, pale Ocean Road.....kuna kila aina ya taabu iletwayo na kansa...they don't go ''market'' their miujiza pale pale hospital? bali kny majukwaa, ma-TV etc etc?

Why, wanajua wakipita mitaa ya Amana, Muhimbili, Temeka,M/Nyamala etc wanapata ''wateja'' kibao, wanaosumbuka na migonjwa ambayo akili ya madaktari mpk imeshindwa hata kuyafikiria.....why can't they go there and do marketing kwa kuwaombea hata kwa imani zao (incase mgonjwa hana imani)?

Agreed with MM, we are witnessing very sophisticated ''HOAXES''
 
Huyu mama ana kila sababu ya kuchunguzwa...kila siku ni vioja..nasikia ametimua watoto wote yatima waliokuwa wakisoma kwenye shule zake.
Wakati anawakusanya watoto alisema atawasomesha mpaka chuo ki kuu!!!!!!!!!!!!!!!!!Leo hii anawaacha kwenye mataa, wengine walezi waowamisha kufa!!!!
 
Half knowlegde is very dangerous. Kanisa na biblia ilianza nini?. Unatafuta muujiza mbali wakati Mungu yupo moyoni mwako? Miujiza ikitendeka hata sasa ndani ya kanisa

Religion is an opium to the poor mkuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu katika kanisa hilo, unaonyesha kuwa kati ya watu hao Misukule nane waliopatikana katika misitu hiyo baada ya waliowachukua kimazingira kumrudia Mungu, watano wameshachukuliwa na ndugu zao ambapo watatu bado wanaendelea kutunzwa na kusali katika kanisa hilo, hali iliyowafanya baadhi ya waunimi kusema kuwa ndugu zao watakuwa wamewasusa.

Baadhi ya waumini waliozungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini kwa kuwa si wasemaji wa kanisa, walidai kuwa wanaamini kwamba vijana hao watatu ambao ndugu zao hawajajitokeza licha ya habari zao kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, inawafanya waamini kuwa jamaa zao bado wana imani kuwa wamekwisha fariki dunia.
1217917692_mfuhai2eweb.gif

Hata hivyo, uchunguzi unaonesha kuwa baadhi ya waumini walikuwa na mawazo tofauti kwa kusema kwamba uwenda ndugu zao hawajapata taarifa kuhusiana na vijana wao kwa kuwa wengi walipoteza kumbukumbu na endapo wangepatiwa taarifa wangeweza kujitokeza.

Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu jana, Mchungaji Lwakatare alikiri kuendelea kuwa na misukule hao katika kanisa lake.

“Hata kama ndugu zao watawasusa nitaendelea kuwalea na baadaye wakiwa na akili safi nitawapa ajira,” alisema mchungaji huyo.
1217917692_msukuleweb.gif

Akifafanua zaidi, Mchungaji Lwakatare alisema kuwa watu hao wengi wao awali walikuwa wamepoteza kumbukumbu kabisa lakini sasa wana afadhali kwa kuwa wanaanza kuelewa mambo.

Hivi karibuni gazeti hili na vyombo vingine vya habari viliripoti kukamatwa kwa misukule katika Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na kusababisha wasomaji wetu wengi kutaka kujua kinachoendelea, hivyo kuanzisha uchunguzi kujua kama bado wapo au la.
1219302231_jenifaweb00.jpg

My Take:
Kanisa la huyu mama naamini linaeneza one of the most elaborated scheme of deception a.k.a a hoax! Inanikumbusha kisa cha Mchungaji Gilbert Deya wa Uingereza (raia wa Kenya) ambaye alikuwa amedai yeye na mke wake kuwa wanauwezo wa kuombea wa kina mama na wakapata mimba na kuzaa watoto hata kama kina mama hao walishapita uwezo wao wa kuzaa n.k

Ingawa mwanzoni mambo hayo yaliweza kuonekana ni miujiza, utaalamu wa kisayansi ulionesha kuwa mke wa mchungaji huyo na washirika wao kule Kenya walikuwa wananunua watoto wadogo na kuwapa kina mama wengine na kwa kufanya hivyo kufanya biashara ya watoto lakini wakati huo huo kulifanya kanisa la Mchungaji huyo kukua zaidi na kuwa na ujiko usio kifani kutokana na kazi ya "Mchungaji huyo".

Mwishoni, sheria ikakutana naye, mke wake akaswekwa jela na yeye mwenyewe mchungaji kutakiwa kurudishwa Kenya kukabiliana na mashtaka ya usafirishaji haramu wa watoto.

Naamini, kama kuna mtu ana ujasiri wa kuchunguza hii "misukule" na kanisa hilo kutaonekana pasipo shaka jinsi gani this hoax was propagated and carried out na hivyo kumpa mama Lwakatare ujiko na kumuongezea sadaka.

Natoa hoja, kanisa lake na yeye mwenyewe achunguzwe pamoja na hao "misukule" kwani anachezea imani za watu na hasa hofu yao ya mambo ya kishirikina.

Kwa vile tuna utaalamu wa DNA, basi misukule hao na "familia" zao na hata makaburi wanayodaiwa kuzikwa yachunguzwe ili wananchi wetu wasitekwe na ulaghai wa kidini unaoendeshwa kwa jina la dini.

Endapo uchunguzi wa kisayansi utaonesha kuwa kweli hawa watu walikufa, wakazikwa na baadaye kukutwa porini wakiwa wamechukuliwa misukule nitamwomba radhi; Lakini nasimamia kusema this is a HOAX inayofanywa na Mbunge Mchungaji!

Haya ni mambo ya imani, kama umaamini kwamba ushirikina upo na wachawi wana uwezo wa kumchukua mtu kumfanya msukule na kama unaamini kwamba Mungu yupo na anauwezo kuliko viumbe vyote na Binadamu anayemwamini Mungu na kutenda kama anavyotaka Mungu anapewa uwezo wa kutumia nguvu za Mungu (kwa sala) wa kuwashinda wachawi, mapepo, majini, magonjwa na maadui wote hapa duniani.
Sasa iweje ishindikane hilo ambalo ni dogo sana kwa Mungu?
 
Back
Top Bottom