Mbunge Zainab Katimba aiomba Serikali kuyajengea uwezo makampuni ya ndani Ili kupata Fursa ya Mikataba ya manunuzi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
"Asante sana Mheshimiwa Spika kwa kupata fursa ya kuchangia hoja ya Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Ni dhahiri asilimia 70 ya bajeti ya Serikali inaenda kwenye Manunuzi. Ni dhahiri katika kipindi hiki cha hivi karibuni sisi sote tumekuwa mashahidi ni kiwango gani cha fedha nyingi zinatafutwa na Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan lakini ni kwa kiasi gani kuna fedha nyingi sana za walipa kodi zinahitaji zionekane katika maendeleo ya nchi hii. Ni dhahiri ili fedha hizi ziweze kuonesha tija tunahitaji kuhakikisha kwamba kunakuwa na thamani halisi ya fedha inapatikana (Value for Money) - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum.

"Muswada umekuja kipindi muafaka kwasababu Sheria ya mwanzo ilikuwa na dosari mbalimbali ambazo tunatarajia Muswada huu au marekebisho ya Sheria hii yatakuja kutatua changamoto hizo na kuondoa upotevu wa fedha nyingi zilizotokana na mapungufu kwenye Manunuzi" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Ibara ya 72 ya Muswada inatoa sharti la Manunuzi yote yatakuwa yanafanyika kwa njia ya mtandao (Electronic). Kwa muda mrefu tumekuwa tunasema tunataka kuondoa ushiriki wa Mkono wa Binadamu kwenye masuala ya Manunuzi na fedha" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Kutumia mifumo ya TEHAMA (Electronic) ni namna nzuri zaidi ya kuondoa mianya ya upotevu wa fedha katika Manunuzi. Changamoto ya Ibara hii ni Ibara ndogo (2) inasema "Endapo mfumo haufanyi kazi Mamlaka itatoa Notice ya muongozo kwa watumiaji wa mfumo na kwa umma"" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Swali, kwanini mfumo haufanyi kazi? Tumeanza kutumia Bunge Mtandao, Benki tunatumia Mtandao, Tiketi za Ndege tunatumia Mtandao na hatujawahi kutengeneza mbadala wa hii Mitandao. Kifungu hiki kisiwe ni Mwanya wa kuacha Kutumia mifumo ya mtandao na ikawa ndiyo sehemu ya kutengenezea muongozo wa kufanya Manunuzi nje ya mfumo wa mtandao (Electronic)" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Nadhani, msingi hapa ni tukazanie mifumo ya mtandao (Electronic) iwe ni lazima ifanye kazi. Naiomba sana Serikali katika Ibara ndogo (2) isije ikatumika kama kichaka cha kutengeneza Manunuzi nje ya mfumo wa mtandao kwa sababu Ibara (72) inasema Manunuzi yote yatafanyika kwa njia ya mtandao" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Ibara (63) ya Muswada inazungumzia upendeleo kwa makundi Maalum ya kijamii. Ibara ni nzuri kwasababu inatoa sharti kwamba taasisi nunuzi zitatenga kiwango fulani cha Manunuzi yake kila mwaka wa fedha kwaajili ya upendeleo pekee kwa makundi Maalum na kilikuwepo kwenye Sheria ya zamani ya PPRA" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Kulikuwa na Kanuni 30 (c) ambayo ilitoa sharti Maafisa Masuuri wote wa taasisi za umma watenge asilimia 30 ya Manunuzi ya taasisi zao kwaajili ya kuziwezesha na kutoa kwa makundi Maalum. Kanuni ikasisitiza Taasisi yoyote inayoshindwa kutenga asilimia 30 ya fedha za Manunuzi na kuziweka kwaajili ya Makundi Maalum zitatoa maelezo kwamba kwanini zimeshindwa kusimamia sharti la kutenga fedha asilimia 30 za makundi Maalum" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Kanuni ikaenda mbele kutaka kwamba maafisa masuuri wote ambao wameshindwa kutekeleza takwa la kikanuni la kutenga asilimia 30 ya Manunuzi mahususi kwaajili ya makundi Maalum watachukuliwa hatua za kinidhamu. Mpaka leo hii Sheria tunayotumia ya Manunuzi, nataka kufahamu ni Maafisa Masuuri wangapi wametoa maelezo kwanini hawajatenga fedha na wangapi wamechukuliwa hatua?" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Msingi wa kuuliz maswali hayo ni kwasababu tunakion kifungu kwenye Muswada huu Ibara (63) inaweka upendeleo kwa makundi ya kijamii na kifungu kimeborehswa, Waziri atashauriana na Wizara zinazohusiana na makundi Maalum. Tunajuaje kama itakwenda kutekelezeka? Tumekuwa na Sheria, Kanuni na Miongozo ambayo haijazingatiwa, haijatekelezwa na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Tunarudi Bungeni kufanya marekebisho ya Sheria, nataka kufahamu hapa tunatokaje! Kwasababu hizi ni ajira za Watanzania. Tunataka tutengeneze ajira kwaajili ya Wananchi wetu. Tunapokuwa hatusimamii utekelezaji wa sheria, Kanuni na Miongozo tunatokaje? - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Nina Imani kubwa na Mheshimiwa Waziri, Serikali. Naomba sana twende tukatekeleze Ibara (63) kwenye Sheria ya Ununuzi wa Umma. Tunapitisha lakini tunataka utekelezaji. Changamoto tulizoziona nyuma hatupendi kuziona, tunaamini tunaanza upya, lengo ni kutengeneza mazingira mazuri katika Sheria zetu" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Ibara (21) ya Muswada inazungumzia adhabu au mapendekezo ya kinidhamu, inatoa hatua zinazoweza kuchukuliwa na Mamlaka (PPRA) pale kunapokuwa na ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo yake. "Endapo kuna ukiukwaji wa Mara kwa mara au ukiukwaji mkubwa wa Sheria, Kanuni na Miongozo iliyotolewa, Mamlaka itapendekeza kwa chombo chenye Mamlaka..."" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Unaposema Endapo kuna ukiukwaji wa Mara kwa mara au ukiukwaji mkubwa wa Sheria, Kanuni au Miongozo tafsiri yake inaenda vipi? Kama tunafanya marekebisho ya kuziba mianya ya upotevu wa fedha nyingi ambazo zinatokea kwenye Manunuzi kwanini tunakuwa na kifungu kinaruhusu ukiukwaji wa Mara kwa mara na Mara kwa mara Je, ni Mara moja, Mbili Tatu, Tano au Mara Kumi. Au ukiukwaji mkubwa wa Sheria, sasa ukiukwaji upi ni mkubwa na upi ni mdogo" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Napendekeza Kifungu hiki kiweze kuboreshwa ili kuondoa mianya au kichaka cha wale watakaotuingiza sisi Watanzania kwenye hasara, wamepewa dhamana na maamuzi yao yakasababishia Taifa Taifa hasara basi wasiwe na kichaka cha kupotea kwa misingi ya kwamba hawajafanya uvunjifu wa sheria wa mara kwa mara au hawajafanya uvunjifu wa sheria mkubwa" - Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Ibara (61) inazungumzia kuhakikisha kunakuwa na Mazingira ya kuwajengea uwezo makampuni ya ndani ili ziweze kushiriki vizuri katika Manunuzi na Mikataba mbalimbali ili na sisi Watanzania wapate Mikataba ya kufanya Manunuzi na tuondokane na umasikini kwa watanzania. Naomba tujielekeze zaidi kuwajengea uwezo wazawa wetu" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Huko nyuma sababu mojawapo ya kutokutenga fedha asilimia 30 za Manunuzi, Maafisa Masuuri sababu zao wanasema Makampuni hayana uwezo wa kuja kushiriki kwenye Tenda na kupata Mikataba ya kutoa huduma. Naomba Serikali ijengee uwezo makampuni ya ndani, sheria imeonyesha maeneo mengi ya upendeleo wa kipekee kwa wazawa, katika utekelezaji tunahitaji sana kuona ni namna gani wanapata manufaa ya Sheria hii nzuri" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum

"Nina Imani kubwa na Mheshimiwa Waziri na timu yake yote. Nina Imani mchango wangu na michango ya waheshimiwa wabunge ambao unalenga kuwasaidia watanzania na kuondoa mianya ya upotevu wa fedha kwenye Manunuzi, nina Imani Serikali itapokea ushauri na yale yote tuliyoyapokea na kuyafanyia kazi" - Mhe. Zainab Athuman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum.

sddefaultkoli.jpg
 
Back
Top Bottom