Mbunge Santiel Kirumba agawa taulo za Kike, Mashuka na sukari zahanati ya Bulige katika Maadhimisho ya Wanawake Duniani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Kirumba ameongoza wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huku akigawa taulo za kike na madaftari kwa watoto wanaotoka katika mazingira magumu, kugawa sabuni na sukari kwa wanawake wajane katika kata ya Bulige na shuka 20 katika zahanati ya Bulige ambayo zilizopokelewa na mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Khamis Katimba na wauguzi wa zahanati hiyo.​

Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 6, 2024 katika Kata ya Bulige ambapo Mhe. Santiel ametumia fursa hiyo kuwashauri wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi na kushiriki katika ngazi za maamuzi.

"Tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, naomba wanawake mjitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi lakini pia niwasihi wanaume watuunge mkono ili kuhakikisha tunafikia usawa wa kijinsia kwa asilimia 50 kwa 50" - Mhe. Santiel Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga

"Tukitumia falsafa ya 4R za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni rahisi kufikia kauli mbiu ya 'Wekeza kwa Wanawake: Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii" - Mhe. Santiel Kirumba, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga

Aidha, Santiel amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi kwa ajiki ya miradi ya maendeleo mkoani Shinyanga na kwa upande wa kata ya Bulige tayari serikali imepeleka huduma ya umeme na maji pamoja na ujenzi wa zahanati ya Bulige.

IMG-20240307-WA0100.jpg
IMG-20240307-WA0102.jpg
IMG-20240307-WA0069.jpg
IMG-20240307-WA0090.jpg
IMG-20240307-WA0107.jpg
IMG-20240307-WA0021.jpg
IMG-20240307-WA0097.jpg
IMG-20240307-WA0081.jpg
IMG-20240307-WA0111.jpg
IMG-20240307-WA0094.jpg
IMG-20240307-WA0073.jpg
 
Back
Top Bottom