Mbunge Mhandisi Aisha Ulenge - Sipingi Matumizi ya Force Account Lakini Tusiifinyange Sheria ya Manunuzi ya Umma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946
"Ibara (75) ya Matumizi ya rasilimali za ndani. Lengo la kupitia sheria ya Manunuzi ya Umma ni ili ziende kuboreshwa. Moja ya kitu ambacho kitakwenda kukinza utekelezaji wa sheria ya Manunuzi ya Umma ni pamoja na kutokufanya tathmini ya kina kwenye miradi iliyojengwa kwa fedha nyingi za Umma" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Kama kungekuwa kumefanyika tathmini ya kina kuona kiasi gani fedha za Umma hazijatumika ipasavyo kwa kutumia Force Account tusingeruhusu Sheria hii kikomo cha thamani kuwekwa kwenye kanuni ilitakiwa sheria iende moja kwa moja izungumze kiwango cha fedha kitakachotumika kwenye Force Account" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Katika sheria ya Manunuzi ya Umma iliyopita miradi mikubwa mingi imetekelezwa kwa Force Account. Hospitali ya Uhuru Chamwino imejengwa kwa Force Account na mpaka leo mradi imeshindwa kufungwa kwa sababu ya Changamoto zilizojitokeza na ukienda Mapokezi tu unaweza kuona fedha za Umma jinsi zilivyofinyangwa katika mradi ule kwasababu tumeamua kuifinyanga sheria ya Manunuzi ya Umma" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Sipingi kabisa matumizi ya Force Account katika nchi yetu lakini lazima tukubaliane na sheria ilivyoelekeza. Ibara (75)(2) inasema "Matumizi ya rasilimali za ndani endapo kazi za ujenzi ni ndogo zimetawanyika na ziko katika maeneo yasiyofikika kwa urahisi kiasi kwamba wakandarasi wenye sifa hawawezi kushiriki na kufanya kazi kwa bei nafuu" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Je, Uhuru Hospitali ya Chamwino eneo lile halifikiki, Mradi ule ni mdogo? Ni wazi kwamba tunaamua kuifinyanga. Force Account itatumika endapo taasisi nunuzi ina wafanyakazi wenye sifa na vifaa vya kusimamia na kutekeleza kazi za ujenzi zinazohutajika" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Nani asiyefahamu kwamba kwenye Mamlaka za Serikali hakuna Idadi ya Wahandisi wa kutosha, hakuna mafundi mchundo wa kutosha? Lakini miradi mingi imetekelezwa kwenye Serikali za Mitaa kwa kutumia Force Account, ni tunaifinyanga Sheria" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Sheria inazungumzia wazi kuwa Matengenezo au ujenzi iwe ni shughuli za kawaida za kila siku za taasisi za ununuzi. Angalia ukubwa wa kazi za Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"TAMISEMI ina majukumu makubwa mazito kwa Taifa hili, lakini mnakwenda kuchanganya majukumu yale yanayokwenda kuchangia upotevu wa fedha za Serikali. Wataalam hawapo, majukumu ya TAMISEMI ni mengi bado mnatumia nguvu kufanya Vitu ambavyo vingeweza kufanywa na watu wengine" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga.

WhatsApp Image 2023-09-12 at 11.18.54.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 11.18.53(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 11.18.53(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-12 at 11.18.53.jpeg
 
Back
Top Bottom