Mbunge Eng. Ulenge: Ifike Wakati Tuangalie Vipaumbele vya Taifa Letu Ili Tuweze Kusonga Mbele

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE ENG. ULENGE: IFIKE WAKATI TUANGALIE VIPAUMBELE VYA TAIFA LETU ILI TUWEZE KUSONGA MLELE

"Kamati ya Miundombinu tulikutana na Kamati ya Wizara ya Fedha, kiliniumiza ni kuwepo na miradi mingi ya maendeleo ambayo Fedha haziendi kwa wakati. Ifikie wakati tuangalie vipaumbele vya Taifa letu ili tuweze kusonga mbele na tupange Mipango ya Taifa letu" - Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Ili Mipango ya Taifa itekelezeke ni lazima pawe na Ufuatiliaji na tathimini ya Mipango iliyopo. Lakini sikubaliani ni Wizara ya Mipango na Uwekezaji kuzifanyia Ufuatiliaji na tathimini, hii haiko sawa, jambo hili liangaliwe" - Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema wazi Fedha nyingi ambazo zinapotea katika Taifa letu, tulikuwa tunaamini sana mifumo kwamba itatusaidia kupunguza na kuziba mianya lakini mfumo nayo inachezewa. Ni lazima tuje na Ufuatiliaji na tathimini ya mara kwa mara ya miradi ya Maendeleo" - Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Kwenye bajeti ya mwaka 2023-2024 Serikali imeamua kuanzisha Directorate of Monitoring and Evaluation ambayo iko ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Tunaomba wabunge muendelee kutushauri, mwaka 2024 tutakuja na ripoti mpya ya Ufuatiliaji na tathimini itakayoangalia utendaji kazi wa Taifa kwa ujumla wake" - Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) na Mbunge wa Jimbo la Peramiho

"Sheria iliyopitishwa na Bunge ya kuanzisha Tume ya Mipango ya Taifa, Bunge liliipa nguvu Tume ya Mipango ya Taifa ifanye tathimini ya Sera za Wizara zote ili tuweze kujua kama tunakwenda kwa mujibu wa sheria" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

Mpango wa Taifa uliowasilishwa na Waziri wa Mipango na Uwekezaji umeweka mkazo katika kuimarisha uzalishaji katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Naipongeza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwakopesha maboti wavuvi na sisi Mkoa wa Tanga tumepata Maboti 14 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.2" - Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Malengo ni kuhakikisha thamani ya mazao yatakayouzwa nje ya nchi inaongezeka. Je, Maboti yakishazalisha kwa zaidi tunaongezaje thamani kama Ukanda wote wa Pwani ya Bahari ya Hindi takribani Kilomita 1,400 kutoka Tanga mpaka Lindi hakuna Viwanda vya kuchakata Samaki, kwanini Viwanda visijengwe Ukanda wa Bahari ya Hindi" - Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Nchi zilizoendelea kama Singapore 🇸🇬 na South Korea ni kutokana na rasilimali Bahari. Serikali iweke macho kwenye Bahari za pembezoni, Fedha nyingi zimepelekwa takribani Shilingi Bilioni 500 Bandari ya Tanga na kina kimeongezwa lakini bila kuchechemua uchumi wa maeneo Meli kubwa haziwezi kwenda" - Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga
 

Attachments

  • y2mate.com - Mbunge ENG ULENGE Angaka Bungeni Ataka Tathimini na Ufuatiliaji Serikali Kushika ...mp4
    55.5 MB
Back
Top Bottom