Kongamano la Wanawake na Manunuzi ya Umma na Fursa za Kibiashara kwenye Bomba la Mafuta

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE AISHA ULENGE KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA MANUNUZI YA UMMA NA FURSA ZA KIBIASHARA KWENYE BOMBA LA MAFUTA

Mbunge wa Viti Maalum (Wanawake) Mkoa wa Tanga, Mhe. Aisha N. Ulenge ameshiriki Kongamano la Wanawake na Manunuzi ya Umma na Fursa za Kibiashara kwenye Bomba la Mafuta lililoambatana na uzinduzi wa Taasisi ya Ng'arisha Maisha Foundation na kuhudhuriwa na Wanawake 1400 wa Mkoa wa Tanga.

Kongamano hilo lililofanyika Mkoa wa Tanga, kwa niaba mgeni rasmi alikuwa ni Waziri, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ambaye alimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

"Tupo hapa kwaajili ya uzinduzi wa Taasisi ya Ng'arisha Maisha Foundation na kuambatana na Mafunzo yatakayopelekea kuongeza ushiriki wa Wanawake katika Manunuzi ya Umma na kuongeza ushiriki wa wazawa katika mradi wa bomba la mafuta. Taasisi itapeleka Mafunzo katika mikoa mingine ya Tanzania ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kutekeleza Mipango yake" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Tupenda kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu kwa uwezo mkubwa aliouonesha katika kutekeleza malengo endelevu ya Dunia ikiwemo Usawa wa Kijinsia. Taasisi yetu imedhamiria kuunga mkono jitihada za Serikali za kutatua changamoto za makundi Maalum wakiwemo Wanawake ili kuyafanya maendeleo ya Kiuchumi na kijamii na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika maendeleo endelevu" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Lengo la kuanzisha Taasisi ya Ng'arisha Maisha Foundation ni ili kuhakikisha fursa mbalimbali zinazotokana na utekekezaji wa Mipango ya Serikali zinawafikia walengwa wakiwemo wanawake" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Mimi binafsi nimekuwa nikifanya mambo mbalimbali kwa Jamii, nimeona ili dhamira yangu ya kuwahudumia itimie kwa ufanisi ninaoutamani nimeona ni bora nianzishe Taasisi (Ng'arisha Maisha Foundation) ili nipate fursa ya kuisaidia Jamii kwa upana zaidi" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Nimekuwa nikifanya mambo kadhaa kuhakikisha utekekezaji wa Mipango ya Serikali inawafikia walengwa na wanawake walionipa dhamana. Waziri Mkuu amekuwa mstari wa mbele kuhimiza Watanzania kulima Alizeti ili kuepukana na uhaba wa Mafuta ya kula nchini " - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Taasisi yetu ya Ng'arisha Maisha Foundation iliyabeba maono ya Serikali ya kuwafikishia mbegu bora za Alizeti na Mahindi kwa Wanawake katika Wilaya Sita za Mkoa wa Tanga kwasababu asilimia 70 ya wakulima Vijijini ni wanawake" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Tuna Kata zaidi ya 150 za Mkoa wa Tanga ambazo tumelima Alizeti, angalau ekari mbili kwa mbegu bora na Kata takribani 100 zimelima Mahindi kwa mbegu bora ikiwa ni kuunga mkono usambazaji wa mbegu bora za Kilimo na kupelekea wananchi kuachana cha asili na kupata tija zaidi kwenye kilimo" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga

"Matarajio yetu ni kuendelea kugawa mbegu bora kwa awamu ya pili ili kuhakikisha mbegu hizo zinaenea Mkoa mzima wa Tanga na wanawake wanapata tija katika Kilimo" - Mhe. Aisha N. Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-09-10 at 15.34.07.mp4
    34 MB
  • WhatsApp Video 2023-09-10 at 15.34.07(1).mp4
    34 MB
  • WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.23.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.23.jpeg
    49.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.22.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.22.jpeg
    77.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.21.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.21.jpeg
    64.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.20(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.20(1).jpeg
    57.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.20.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-10 at 16.58.20.jpeg
    36.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Video 2023-09-10 at 16.43.28.mp4
    19.4 MB
Back
Top Bottom