Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

wananchi wakiwa na maisha duni, hawana uhakika na maisha yao(kukata tamaa) huku wakishuhudia mali zao zikichotwa kijanja janja, hivyo kilichotokea ni ishara ya hayo na kwa jinsi maisha yanavyo zidi kuwa magumu, tutegemee sehemu nyingine tena..
 
wanajf huyo mheshimiwa hajapigwa, bali kavuliwa gamba kwani wenzake walijivua wenyewe yeye na wengine
walikuwa bado.
 
Nakukumbusha jina la pale nje ya geti "Makanyagio" only to refresh your mind.
Usinikumbushe makanyagio na maandazi na ulanzi wake, by the way unakumbuka wanywa uji walivyokuwa wanadharauliwa mkwawa 🙂, kisa wanaonekana hawana pesa.
 
Dah,pendekezo lilitolewa na sugu mbeya,...
limeanza kufanyiwa kazi Tarime,...

Am proud to be a kurya

Kaka kuna watu wanatubeza wanatarime, but kama kuna kitu hawakijui ni furaha gani mwanatarime aliyonayo kuwa mmoja wapo wa jamii hii. Nafikiri unahisi hiyo hali kwa sasa
 
scape goat wao ni 'chama fulani cha kisiasa'!! hiyo chorus imechuja!! do you homework,CCM dudes!!
 
huyo mbunge aliingia kwenye mkutano wa kimila akiambatana na mabraza waliovalia uniform ya ccm walipomalizana naye walienda moja kwa moja kwenye mgodi kuuteketeza,teheeeetehee
source channel ten news
Hou r u what'z this?
 
mbona unajihami weka source tuwe na uhakika

hii thread imeandikwa pia na mwanajf KIBURUDISHO katika jukwaa la "habari na hoja mchanganyiko" na amedai source
ni ITV BREAKING NEWZ.
 
Habari zilizonifikia dakika 20 zilizopita ni kuwa mbunge wa TARIME mh.Nyangwine kapigwa vibaya sana na wananchi wa Nyamongo na gari lake limechakazwa vibaya sana ...Alikuwa amekwenda Nyamongo kufuatilia suala la kuuwawa kwa wannnchi wa 5 katika mgodi wa North Mara....

Mdau anayenipa habari hizi yuko ndani ya mgodi wa North mara na anasema security status imewekwa RED.......

ANGALIZO: Staki mambo yenu ya kisharobalo kuanza kuniuliza source hapa...habari ndo hiyo mura

source. ITV BREAKING NEWS
 
ingebidi wamnyoshe ki-sawasawa
hawajamvunja mguu au kumtoboa jicho?
bado kagasheki na uongo wake
 
Nani aliwadanganya mkivalia hayo mavazi yenu ya chukua chako mapema(ccm) ndo tutawaogopa? haya iabu hiyo,mmechezea kichapo pamoja na mavazi yenu!
 
Naona ipo kwenye headlines za ITV habari, tuisubiri tuipate kwa ufasaha!
 
Sasa naona CCM inapotea kweli .Watu wameend wenyewee huko kujitafutia maisha kwa kuokota wanacho kiamini kitawasaidia wameuawa leo wanasema Chama fulani ? Hizi siasa hadi kwenye maisha ya watu ? So hao wamekufa na kila kitu kimeisha kwa jina la chama fulani ?
Kuna haja ya watu kujipanga na kweenda mahakamani hakika
 
Nimeshangwazwa na kauli ya Naibu waziri wa mambo ya ndani, Mh. Kagasheki akiongea na waandishi wa habari kwamba mauaji ya Tarime Nyamomgo kwenye mgodi siyo ya kisiasa. Mauaji ya Tarime ni ya kisiasa kwa asilimia 100%. Ni siasa mbovu za CCM ndizo zimesababishwa wananchi wa Nyamongo na Watanzania kwa ujumla kuporwa raslimali zao na wezi ambao CCM wanawaita wawekezaji. Wezi hawa wanashirikiana na uongozi wa kifisadi wa CCM kupora urithi wa taifa letu huku wananchi wakibaki mafukara. Siasa za kifisadi ndizo zinasababishwa CCM kutunga sheria za kulinda wezi na waporaji wa maliasili zetu.

Sijui Kagasheki ametoa kauli ile kwa uelewa finyu au ni propaganda za uwongo ambazo CCM imezoea kutumia kuwapotosha wananchi. Inajulikana kuwa ndege za wezi zinatoka huko zinakotoka zinaingia moja kiwa moja kwenye mashimo ya machimbo, kupora na kuondoka bila kupitia uwanja wa ndege. Hakuna anayejua ni kiasi gani cha madini wezi hawa wanachukua. Kama wananchi wa Nyamomgo Tarime na sehemu nyingine Tanzania wangepatiwa maeneo yao ya kuchimba na kujipatia riziki yao hayo mauaji yasingetokea. Au kama wananchi wangemilikishwa ardhi yenye madini na kuingia ubia na wawekazaji nao wananchi wangefaidika na maliasili zao. Lakini CCM inalinda wezi wawekezaji na wezi viongozi wa CCM na serikali na kuwaua wananchi wa Nyamongo ambayo kimsingi walikuwa wanaonyesha kukerwa kwao na umasikini uliokithiri na kulinda maliasili za nchi. Kwa sasa wanachoambulia wanachi ni vumbi la machimbo , kubabuliwa na kemikali , kusababishiwa ulemavu, magonjwa na kuuawa kwa sumu za kemukali hizo.
Kagasheki asidanganye watu, hicho chama alichosema kinatumia mauaji ya Nyamongo kisiasa ni mawazo ya kisaliti na kiuaji ya waziri huyu. Chama chochote kinachojali wananchi lazima kithamini uhai wa wananchi. CCM imezama kwenye ufisadi haijali hata maisha ya watu. Chama hicho anachosema Kagasheki kinahaki ya kutetea uhai na maisha ya wananchi na wapiga kura wake. Siasa mbovu za CCM ndizo zinazopora wananchi raslimali zao. Wananchi na vyama vingine vya siasa vinavyojali maisha ya watanzania lazima vipinge mauaji hayo wa wezi na walinzi wao na kuendelea kupigania kurudisha mali hizo zinazoibiwa kwa wenyewe wananchi.
 
Mods nilidhani hii post inafaa kusimama kivyake ili waziri aione kirahisi.
 
Naangalia taarifa ya habari ya ITV ya saa 2 usiku na mtangazaji Mabere Maratho anairusha habari ya m'bunge wa Tarime alivyotolewa mkuku na wanatarime!! Duuh, kama movie vile alivyotoka mbio!! Wameapa hawataki mjinga mjinga yoyote wa CCM tarime!! Najiuliza huyu m'bunge alishindaje? atafanyaje kazi kama waajiri wake wanamfukuza kama mwizi?
 
Kumbe na viongozi wa halmashauri wamechezea kichapo!
Matokeo ya wananchi kujiongoza wenyewe ni mabaya mno!
 
Back
Top Bottom