Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

Hili na lenyewe la kushabikia na kufurahia?Mtanzania mwenzetu kupigwa?

Labda ninaishi karne ingine..hili ni jambo la kukemea kabisa..

Pole zake,nitawauliza watu wa nyumbani kujua zaidi..
 
hili na lenyewe la kushabikia na kufurahia?mtanzania mwenzetu kupigwa?

Labda ninaishi karne ingine..hili ni jambo la kukemea kabisa..

Pole zake,nitawauliza watu wa nyumbani kujua zaidi..
ukiona hivyo ujue mapinduzi yamepiga hodi, yameshatokea kenya, libya, ethiopia nigeria nk. Uionayo ni ishara tosha kwamba maskini wamechoka na umaskini wao!!
 
Ama kweli Amaghana ga sarikire Mura nshe nkugeche mura!!!!! hii inaashiria nini? Tanzania tumekalia utambi wa baruti... na bado kidogo kuna mtu atawasha uo utambi na kitakacho tokea ni madhara makubwa. Nafikiri ni wakati muafaka kwa watawala wetu wakasoma nyakati hizi. Tusichukulie kirahisi rahisi tu kwamba ahaa hao ni WAKURYA. Serikari inabidi ku review hii mikataba tata na kuacha kuwakumbatia hawa WAWEKWEZAJI uchwara. Kuna kitu tunakosa nacho ni MORAL IMAGINATION.... nikimaanisha kwamba its the wearer of the shoe who can tell u where it pinches most. Jamani hawa wananchi wana madai na sio kama inavyo elezwa kwamba ni majambazi. Hivi kweli majambazi wanaweza wakaenda mchana kweupe na fimbo na marungu kuiba?? Hapana kuna madai tena madai ya kina kabisa nachelea kusema. Tatizo ni kwamba tunawaona hawa watu hawajui na sie ndo tunajua hence tunaweza amua chochote. Lakini kwa vile wao ndo wanajua uchungu na historia ya eneo husika ndo maana waliamua kujitokeza na kuchukua hatua hiyo hatarishi. Wana JF tuwashauri watawala wetu wajirekebishe na tumuombe mola aepushie balaa ili mbali. Watu watano wasinge kufa kama mambo haya yangerekebishwa mapema. I can write and write lakini..........bye kwa sasa. Vita ni vita Mura!

Nilibahatika kufika Srilanka, wana madini mengi ya VITO lakini bado uchimbaji wake ni ule wa asili yaani raia wanatumie "Labour Intensive" kuibua hayo madini na vile vile Jewellers zote zinamilikiwa na wao wenyewe. Kutembea Jewellers na kununua vito vyao kwao ni sehemu ya utalii na hili huwekwa kabisa kwenye Safari Itenery.

Sipingani na uchimbaji mkubwa lakini kama hauna manufaa kwa maisha ya Mtanzania hatujachelewa tukirudi kwenye zama za ujima tukawa tunavuna kidogo kidogo tuu kwa kutumia nguvu kazi yetu na pato lote likabaki hapa hapa nchini.
 
Hawakumchagua ndiyo maana wanampiga...........hata kikwete hakuchaguliwa ndiyo maana baadhi ya sehemu km mbeya akitia maguu tu wanampopolea mawe.............tehe...tehe..te...te...ccm inachechemea

wamchague wenyewe kwa kishindo alafu wanampiga tena??!
 
Hili na lenyewe la kushabikia na kufurahia?Mtanzania mwenzetu kupigwa?

Labda ninaishi karne ingine..hili ni jambo la kukemea kabisa..

Pole zake,nitawauliza watu wa nyumbani kujua zaidi..
Yeye kwa kushabikia wawekezaji feki si anataka kuua wananchi wengi bora kipi kumpoteza yeye au tupoteze ukoo mzima.
 
Hili na lenyewe la kushabikia na kufurahia?Mtanzania mwenzetu kupigwa?

Labda ninaishi karne ingine..hili ni jambo la kukemea kabisa..

Pole zake,nitawauliza watu wa nyumbani kujua zaidi..

kama serikali ingekemea yale mauaji ya watu watano na kumuajibisha mkuu wa polisi kanda maalum sidhani kama haya matatizo yangetokea. lakini hili linatokea kwa ajili wahusika wakuu wako pale pale.
Mtu yeyote anayezulumiwa siku akichoka zuluma usipomsikiliza basi ujue ni balaaaaa
angetakiwa kuside na wananchi na kushinikiza mkuu wa polisi atolewe badala yake yeye anaenda kuwaadaa wananchi
 
Habari zilizonifikia dakika 20 zilizopita ni kuwa mbunge wa TARIME mh.Nyangwine kapigwa vibaya sana na wananchi wa Nyamongo na gari lake limechakazwa vibaya sana ...Alikuwa amekwenda Nyamongo kufuatilia suala la kuuwawa kwa wannnchi wa 5 katika mgodi wa North Mara....

Mdau anayenipa habari hizi yuko ndani ya mgodi wa North mara na anasema security status imewekwa RED.......

ANGALIZO: Staki mambo yenu ya kisharobalo kuanza kuniuliza source hapa...habari ndo hiyo mura

Hii pia na mimi nimeisikia kwa mbali ikiripotiwa na Joji Malato kwenye brekin nyuzi ya ai ti vii na redio wani....Mbona kazi mwaka huu wanayo?Tehe tehe tehe tehe tehe......
 
Ingekuwa Mbeya ninge sema wananchi wamefuata amri ya Sugu......... Wakina Mura hawataki siasa kwenye misiba, wamempiga mbunge wako kisa ameenda kwenye msiba na watu walio valia nguo za kijani(magamba ya CCM)
Yaani natamani mitama ile ndo angekuwa anapigwa babake rizi
na matege yake yake sijui anagekimbiaje...
 
Nyangwine wa Mkwawa complex ?, nakumbuka Majembe ilikuwa ndiyo ya Wasichana, kama ni uzao wa Mkwawa kwanini hana utetezi kwa wapiga kura wake, ila poa tuu, apate kichapo naamini kinatoka pande zote mbili za waliomchagua kwa maana wameshamchoka,na ambao hawakumchagua
Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli.
 
Yaani natamani mitama ile ndo angekuwa anapigwa babake rizi
na matege yake yake sijui anagekimbiaje...
mkuu kwani wewe hukumbuki kilichotokea kule mbeya? uwe unasomaga na kusikiliza /kuangalia vyombo vya habari!!
 
kwa mujibu wa Nywangwine mwenyewe yeye hajapigwa mawe bali walinzi wake na gari lilopopolewa mawe ni la halmashauri na anadai kuwa kuna diwani wa Chadema ktk sehemu alipokuwa akienda kufanya mkutano ndie kapanga njama za kumpopoa mawe na kumfanyia fujo..habari ndio hiyo MUaraaaaaa,,anachafua chadema bila ushahidi kazi ipo.
 
Mbunge nyangwine amesema ni diwani wa Chadema aliwapanga vijana ili akifika waweze kumshambulia, hvyo alichosema n baadhi ya vijana kujifanya na hasira zinazohusiana na mambo ya kisiasa.
 
kwa mujibu wa Nywangwine mwenyewe yeye hajapigwa mawe bali walinzi wake na gari lilopopolewa mawe ni la halmashauri na anadai kuwa kuna diwani wa Chadema ktk sehemu alipokuwa akienda kufanya mkutano ndie kapanga njama za kumpopoa mawe na kumfanyia fujo..habari ndio hiyo MUaraaaaaa,,anachafua chadema bila ushahidi kazi ipo.
hahahahahahah!! chadema itakuwa ni chanzo cha kila kitu mwaka huu, sasa wachaga wameenda kufannya nini tena huko mara? si Nape kaseam kuwa chadema ni ya wachaga? au walibebwa kwa malori hadi huko mara. ists so strange
 
Back
Top Bottom