Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

Habari zilizonifikia dakika 20 zilizopita ni kuwa mbunge wa TARIME mh.Nyangwine kapigwa vibaya sana na wananchi wa Nyamongo na gari lake limechakazwa vibaya sana ...Alikuwa amekwenda Nyamongo kufuatilia suala la kuuwawa kwa wannnchi wa 5 katika mgodi wa North Mara....

Mdau anayenipa habari hizi yuko ndani ya mgodi wa North mara na anasema security status imewekwa RED.......

ANGALIZO: Staki mambo yenu ya kisharobalo kuanza kuniuliza source hapa...habari ndo hiyo mura
Chama cha magamba kusheyi,nawapongeza wananchi wa tarime watanzania tuamke!
 
jamani mmeona live newz toka itv hali ilivyotokea tarime nyamongo? Ama kweli nimeamini watu awaitaki ccm
 
Tarime kunani? Nadhani hii inatuonyesha kwamba kuwa mbunge wa tarime unahitajika kuwa timamu zaidi kwenye ubongo na siyo ku-reproduce materials ambazo unadurufu tu hali wananchi wako wana kero!
 
Kichapo kilikuwa kikali mno,wamepigwa ka wakimbizi,wananchi wanasema hawako tayari kuwasikilizaji viongozi wa magamba,ccm inabidi wakubali kusalimisha mamlaka kwa CDM waweze kuiongoza nchi,endapo wakiendelea kukahidi wasijejutia yatakayowapata ...huu ni ushauri wa bure
 
Nilibahatika kufika Srilanka, wana madini mengi ya VITO lakini bado uchimbaji wake ni ule wa asili yaani raia wanatumie "Labour Intensive" kuibua hayo madini na vile vile Jewellers zote zinamilikiwa na wao wenyewe. Kutembea Jewellers na kununua vito vyao kwao ni sehemu ya utalii na hili huwekwa kabisa kwenye Safari Itenery.

Sipingani na uchimbaji mkubwa lakini kama hauna manufaa kwa maisha ya Mtanzania hatujachelewa tukirudi kwenye zama za ujima tukawa tunavuna kidogo kidogo tuu kwa kutumia nguvu kazi yetu na pato lote likabaki hapa hapa nchini.

Ni kweli kabisa,kama wazawa hawanufaiki na huu uwekezaji ni bora waachiwe wachimbe taratibu mpaka hapo watakapopandisha mtaji na kuchimba kitaalam zaidi.
 
Wa Tz wote tungekuwa kama watu wa tarime,tungekuwa mbali,ebu tuige mfano mikoa mingine!😛ound:
 
Habari zilizonifikia dakika 20 zilizopita ni kuwa mbunge wa TARIME mh.Nyangwine kapigwa vibaya sana na wananchi wa Nyamongo na gari lake limechakazwa vibaya sana ...Alikuwa amekwenda Nyamongo kufuatilia suala la kuuwawa kwa wannnchi wa 5 katika mgodi wa North Mara....

Mdau anayenipa habari hizi yuko ndani ya mgodi wa North mara na anasema security status imewekwa RED.......

ANGALIZO: Staki mambo yenu ya kisharobalo kuanza kuniuliza source hapa...habari ndo hiyo mura

Haaaaaa! Sawa bwana hakuna swali! Atajuuta kuwa mbunge ndani ya chama cha magamba ! Halafu eneo lenyewe Tarime! Mimi simo
 
Wanachofanya wananchi wa Tarime ndicho kinatakiwa kufanywa na Watanzania wote. Wanatakiwa waungwe mkono hadi kieleweke
 
Hongera sana wananchi wa Nyamongo hakika mmekuwa mahakimu wazuri sana,maana huyo Mbunge asingechelea kusema kuwa wataunda tume na tume hizo huwa hazikamiliki mpaka watu wanakufa.
 
Leo kamanda Lema,yupo Tarime,katika harakati za kujenga chama,katika hali ya kuchanganyikiwa mkuu wa wilaya amemkimbia Mh Lema ofisini,baada ya kubanwa na maswali kuhusu hali ya usalama.Mh Lema alitaka kujua hali ya usalama kama waziri kivuli wa mambo ya ndani.Baada ya mkuu wa wilaya kushindwa au kwa makusudi au kwa uoga kueleza hali ya usalama ndipo akakimbia na kumwacha Lema ofisini kwake.
 
Mwaka huu watakimbia sana. hakuna kitakachosalia juu ya kingine hadi kuwe tambarare😛ound:
 
What a game! What a game?
Huku tarime ndo wamempiga mbunge wao leo hii?wakati kibano cha mbunge kikiendelea lema alikuwa wapi?
 
Hii ni matokeo ya siasa maji taka alizokuwa anasema spika mstaafu.
 
mchizi nilmuona jana dani ya corridor za ofisi ndogo ya bunge dar,yuko peace,yani anampa salam kila mtu,hakuna suti ni magwanda kwenda mbele kama field marshal castro
 
Back
Top Bottom