Mbunge wa TARIME apigwa na wananchi

agalizo kwa nape:ukija kilimaniaro mfano ndo huo,tutakugombania

aombe radhi kabla hajaja kujitambulisha milimani au laa aje na defender za ffu zaidi ya 100 na ahutumie akiwa kavaa helmeti muda wote.
 
hii issue sio ya leo
North Mara mgodi wa kashfa au dhahabu?

lC.gif
Godfrey Dilunga​
Julai 8, 2009
rC.jpg


JUNI 29, mwaka huu, ilikuwa zamu ya serikali kukasirishwa na mwekezaji wa sekta ya madini. Ni siku hiyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Sued Kagasheki, alidanganywa na menejimenti ya kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick.

Yapo mengi ya kujadili ambayo ni pamoja na kitendo cha menejimenti kuwa na ujasiri wa kumdanganya waziri.
Tuugawe mjadala huu katika vipande kadhaa, kama ifuatavyo.

Nafasi ya Barrick nchini, ulimwenguni
Shirika la Dhahabu la Barrick ni kampuni ya uchimbaji madini inayoongoza ulimwenguni.

Hisa za Barrick zimeorodheshwa katika soko la hisa la Toronto, Canada na New York, Marekani.

Barrick Tanzania inaendesha migodi minne ya Bulyanhulu, North Mara, Tulawaka na Buzwagi.

Barrick ilianza shughuli mgodi wa North Mara, miaka 14 iliyopita (1995) kwa uwekezaji wa dola za Marekani milioni 210 ( Sh zaidi ya bilioni 210).

Mgodi huu umekarabati na kujenga shule mpya katika baadhi ya vijiji vya Tarime, kujenga visima vya maji,
kujenga na kukarabati vituo vya afya, na kukarabati barabara za baadhi ya vijiji Tarime.

Swali la kujiuliza ni je, shughuli hizi za kijamii zinawiana au kukaribia thamani ya mavuno ya dhahabu mgodini humo?

Hiki kinachotolewa kama msaada kwa jamii inayozunguka mgodi au kama kodi kwa serikali kinalingana au kukaribia mavuno halisi ya dhahabu? Au ni sawa na tone la damu baharini?

Hapa busara ya kawaida inatutaka kuwa na vipimo sahihi vya ulinganisho, kati ya tunachostahili kupata kutoka katika mavuno ya dhahabu.

Hivyo basi, tutakuwa watu wa ajabu kama tutasifia misaada hiyo au kodi hizo bila kuwa na uhakika wa kiwango cha mavuno ya dhahabu, kwa siku, wiki, mwezi au mwaka.

Lakini, tutakuwaje na vipimo sahihi wakati serikali imezubaa kuchangamkia kuanzisha kiwanda cha kusafisha dhahabu nchini?

Badala yake, mchanga wa dhahabu unachimbwa na kusafirishwa nje ya nchi ili kusafishwa bila jicho la serikali.

Mvutano wa mgodi na wenyeji
Wakazi wa vijiji vitano vinavyozunguka mgodi huo wamewahi kumtaka Rais Kikwete kuunda tume ichunguze mauaji ya wenzao sita waliopigwa risasi na walinzi wa mgodi, mwaka 2005.

Tangu mwaka 2001, wanavijiji wamekuwa wakipinga vitendo vya unyanyasaji vinavyodaiwa kufanywa na mgodi huo.

Serikali ya Awamu ya Tatu iliwahi kushutumiwa moja kwa moja na wanavijiji kufumbia macho unyanyasaji huo.

Kauli ya mwisho ya Chacha Wangwe
Saa kadhaa kabla ya kifo chake, aliyekuwa mbunge wa Tarime, ulipo mgodi huo alizungumza bungeni.

Akasema: "Wasiwasi wangu ni kuwa kuna watu wanaotumia madaraka yao vibaya ndani ya Jeshi la Polisi.

"Hadi kufikia jana watu 84 wamekamatwa eneo la Nyamongo Tarime palipo na Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Barrick, kwa madai kuwa walikuwa wanajiandaa kuingia ndani ya mashimo ya mgodi kuiba mawe ya dhahabu.

"La kushangaza. kamata kamata hiyo, hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kueleza ni vipi wananchi hao waliingia ndani ya mgodi wenye uzio na ulinzi mkali wa polisi, walinzi wa mgodi na mbwa wakali.

Mbali na Wangwe, Diwani wa kata ya Kemambo, Augustino Sasi, aliwahi kukaririwa akiishutumu Serikali ya Awamu ya Tatu.

Mwaka 2002, akiwa mwenyekiti wa kijiji cha Kewanja wilayani Tarime, alidai kukamatwa na polisi.

Akabambikiwa kesi ya kutishia kuua kwa silaha, baada ya kuhitilafiana na mwekezaji (mgodi). Alihukumiwa kifungo miaka 30 jela, lakini alikata rufaa Mahakama Kuu na kuachiwa.

Alithubutu kuwataja majina waliouawa na walinzi wa mgodi. Maelezo ya viongozi hawa wa kisiasa yanadhihirisha mpasuko wa makundi mawili, wilayani Tarime.

Kundi la kwanza ni la taasisi za serikali likiwamo Jeshi la Polisi Tarime/Mara, na viongozi wengine wa serikali, mfano mkuu wa wilaya au mkoa.

Pili ni kundi la wanavijiji na viongozi wao wa kisiasa, madiwani na mbunge. Kila kundi linajivunia uwezo wake, na daima kuota ndoto ya ushindi dhidi ya kundi jingine.

Mgodi unajivunia rafiki wake na vyombo vya dola na viongozi wake, na wananchi wanajivunia umoja wao unaolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa vyovyote vile, ili kundi moja lishinde ni lazima damu imwagike na mgodi ugeuka wa kashfa badala ya dhahabu.

Wangwe alijua kiini cha tatizo?
Inawezekana uhasama uliopo chanzo chake si tuhuma za wizi wa dhahabu au petroli kutoka mgodini kama inavyodaiwa. Umeanzia mbali na kuishia kutiririsha sumu mto Tigithe.

Wangwe tena aliwahi kusema bungeni; "Wananchi wa Tarime wanasubiri maamuzi ya serikali katika kutatua mgogoro wa ardhi baina ya kampuni ya Barrick na wananchi wanaozunguka mgodi huo wa North Mara, ambao umedumu tangu mwaka 1994.

Serikali itoe tamko kwamba mgogoro huo utatatuliwa kwa njia ya mazungumzo na siyo nguvu za dola zinazosababisha mateso makubwa kwa wananchi wa Tarime.

Kwa kuwa Waziri Mkuu alituhakikishia hapa bungeni kwamba serikali haitatangaza hali ya hatari wilayani Tarime na Rorya ila zitatumika juhudi za mashauriano yatakayohusisha viongozi wa wananchi, wananchi wa Tarime wanaiomba serikali itazame upya utendaji wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Mkoa na Wilaya.

Anataja jeshi la polisi, mkuu wa wilaya na mkoa, ambao hivi karibuni yametimia kwa wakuu hao kushiriki mchakato wa kumdanganya naibu waziri.

Mbali na mgogoro wa ardhi, Wangwe alionya kuwa viongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya ni tatizo.

Na kweli ni tatizo, kama wasingekuwa tatizo wangegundua maji ya sumu yanatiririshwa kutoka mgodini kuelekea mto Tigithe mapema.

Walikuwa na uwezo wa kugundua hilo kabla ya naibu waziri kutumwa na Waziri Mkuu, na hatimaye kudanganywa. Ikumbukwe viongozi hao ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama, je, wametimiza wajibu?

Kwa nini kamati ya ulinzi ya wilaya na mkoa ifumbie macho malalamiko ya wanavijiji? Je, wametiwa mfukoni mwa Barrick? Je, inalinda kamati ya ulinzi inalinda maslahi ya mgodi dhidi ya wananchi?

Uwezo na sababu za kamati ya ulinzi kubaini na kuzuia utiririshaji sumu mto Tigithe walikuwa nao. Kwa nini hawakutimiza wajibu wao? Je, kikwazo ni jeuri ya menejimenti ya mgodi au uzembe wa kamati ya ulinzi na usalama?

Kuna uhusiano wa Barrick na Ikulu?
Rais Kikwete amewahi kuzungumzia mahsusi kampuni ya Barrick, kwa mantiki inayosifia mgodi huo.

Inawezekana alikuwa sahihi kufanya hivyo, lakini binafsi naamini pia ni sahihi kurejea kauli yake.

Rais alihutubia wakazi wa wilayani Geita, mkoani Mwanza, mwaka 2007.

Akazungumzia uamuzi wake wa kutaka serikali na mgodi kunufaika sawa kwa sawa (win-win situation).

Akajivunia Barrick kwamba; imekubali kulipa kodi ya asilimia 30 badala ya asilimia tatu. Akawadokeza wananchi kuwa; baada ya Barrick sasa majadiliano yanendelea na kampuni nyingine.

Mei 8, 2007, Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga, akatoa taarifa kufafanua (kusisitiza) alichosema Rais.

Akasema; serikali imekubaliana na kampuni za Barrick Tanzania Ltd na Resolute Tanzania Ltd, kwamba zimekubali kuondolewa kwenye mikataba baadhi ya vivutio vya ziada ikiwa ni pamoja na nyongeza ya asilimia 15 kwenye mtaji wa uwekezaji ambao haujarejeshwa au kukombolewa.

Tafakari kwa kujiuliza, kwa nini Rais asiwe na subira hadi mazungumzo na kampuni nyingine yakamilike, ili taarifa ya jumla itolewe? Kwa nini serikali isijadiliane kwa pamoja na wachimbaji wote?

Je, ni dhambi kuamini kuwa Rais alikuwa na lengo la kusafisha Barrick na Resolute mbele ya Watanzania waliokasirishwa na migodi kuvuna zaidi huku serikali ikiambulie kiduchu?

Kama si hivyo, ni kwa nini Rais achukue jukumu la wizara kwa jambo jepesi kama hilo la kutangaza mchakato wa majadiliano na wawekezaji, tena kabla ya kufikia tamati?

Hapa utaona mwanga wa mbali unaothibitisha uhusiano rasmi au usio rasmi tena wenye shaka, kati ya Ikulu na Barrick.

Lakini pia uhusiano huo wa Ikulu na Barrick umepokewa kwa mikono miwili na Wizara ya Fedha na Uchumi.

Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2009/2010, Waziri wa Fedha na Uchumi alitaja msamaha wa ushuru wa mafuta kwa kampuni mpya zitakazotaka kuchimba dhahabu nchini umefutwa, lakini kampuni za zamani serikali itafanya mazungumzo nao.

Bado unaweza kuona urafiki maalumu wa serikali (viongozi wachache) na migodi ya dhahabu hapa nchini.

Kuna aina ya upendeleo unaothibitisha urafiki wa serikali na wawekezaji hao.

Kwa nini serikali ijadiliane nao kuwaondolea ushuru wa mafuta, na hasa kwa kuzingatia maelezo ya Rais Kikwete kuwa, bei ya dhahabu ni nzuri mno wakati huu wa mtikisiko wa uchumi.

Kwa nini kuwe na mazingira ya kuhofia kwamba kama wataondolewa ushuru ghafla watapata hasara kubwa, wakati ikifahamika wazi kuwa, msamaha wa ushuru huo haukutamkwa kwenye mkataba wa uchimbaji dhahabu kati yao na serikali?

Kashfa ya sumu mgodini
Hivi karibuni mgodi huo umeingia katika kashfa kubwa ya kutiririsha maji yenye sumu kuelekea mto Tigithe, na wananchi wengi kudhurika na wengine kufa.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alimtuma Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Suedi Kagasheki, kufika mgodini huko.

Lakini kabla ya ziara hiyo ya naibu waziri, vyombo vya habari viliripoti tukio la mgodi kutiririsha maji yenye sumu.

Juni 26, 2009, mgodi ulikanusha taarifa za vyombo vya habari na kutishia kuchukua sheria.

Ukanushaji huu unazidi kutia shaka ustaarabu na malengo ya mgodi huu kwa umma.

Ukanushaji huo unathibitisha kuwa mgodi una nia mbaya na wananchi. Kwanza umekanusha ukweli ulioandikwa na vyombo vya habari, pili umetaka kuficha ukweli mbele ya naibu waziri.

Tutafakari, juhudi hizi za kuficha ukweli dhidi ya serikali na wananchi lengo lake ni nini? Ni kwa manufaa ya nani?

Jeuri hii ya kuficha ukweli inatoka wapi? Je, ni kutokana na urafiki wa mgodi na viongozi waandamizi nchini? Au ni jeuri inayotokana na utajiri wa mabilioni yanayotokana na mauzo ya dhahabu yetu?

Ni vigumu kuwa na jibu la moja kwa moja kuhusu kiburi chao hicho cha kumdanganya naibu waziri.

Wakati akidanganywa, Kagasheki alikuwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Enos Mfuru, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Frank Uhahulla na Meneja Mkuu wa mgodi huo, Kevin Moxam. Kwa lugha rahisi, viongozi hawa wamefanywa wajinga!

Sasa Rais anapaswa kuchagua mambo mawili. Mosi, kuendelea kuwa na viongozi waliogeuzwa wajinga kwa kudanganywa; pili aendelee kubaki na mgodi uliogeuza viongozi aliowateua kuwa wajinga.

Hii maana yake ni kwamba, kama viongozi walioteuliwa na Rais wamegeuzwa wajinga, basi tafsiri sahihi ni kuwa menejimenti ya mgodi pia imemtukana Rais.

Na kama baadhi ya viongozi wamewahi kuhongwa na mgodi ili washiriki kuficha ukweli maana yake ni kwamba wamemtukana Rais. Hawafai, wavuliwe uongozi. Ndugu Rais utavumilia matusi haya? Kama utaweza tutakushangaa!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
hs3.gif
 
wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo wanauwawa kwa kupigwa risasi na polisi jambo ambalo ni aibu na kashifa kubwa kwa kuwa inaonekana serikali inawathamini zaidi wawekezaji kuliko raia wake.




serikali ilidai dai haina fedha ya kutafiti kemikali za mgodi wa North Mara ambao maji yake yanatiririka katika mto tigiti na kuongeza vifo vya watu na mifugo kila siku.



Athari nyingine za kemikali hizo ni kuharibika kwa mimba kwa akina mama wajawazito.

hii nimeinyofoa sehemu inahusu mgodi wa north mara , about 3 years sgo
 
WHat might be the reason behind kwa wananchi kumpiga muwakilishi wao?!

Chanzo cha habari kutoka Nyamongo: Ukweli ni kwamba huyu mwakilshi amepigwa na gari lake limeharibiwa vibaya, si unafahamu tene akina Mura kwa mawe, rungu na panga lililonolewa pande zote ni vitu ambavyo muda wote viko karibu nao. Sababu kubwa ni kwamba amejitokeza wakati tukio tayari limeishatokea, watu watano tayari wamekufa, sasa kama mwakilishi anaenda kufuatilia mauaji, alitakiwa kuzuia yasitokee kwa sababu hayo sio mauji ya kwanza maana kama unafuatilia mahusiano baina ya mgodi wa North Mara na wanakijiji sio mazuri kwa muda mrefu. Yeye kama mwakilishi alishachukua hatua gani kurejesha mahusiano hayo? SAWA TATA?
 
yaani nafanya mipango nipate picha...nasikia kapigwa mitama mpaka shati wamemchania kitambi nje....daa nakukumbuka NYANGWINE wakati tuko mkwawa na lile kombe lako la uji ukitoka DH unashuka zako makongoro east.....eti leo mbunge!!!! mambo haya bwana


Haaaa kigogo kumbe tulikuwa wote mkwawa? mie nilikuwa magembe east.....wewe ulikuwa kongoro wa shaban robert au lumumba! laaah nimefurahi kukumbushwa mkwawa....nguyi ,mwangoka na kuleeeee mlikokuwa mnakimbizana nao nimepasahau jina....kuna pombe za kienyeji na minuso baaada ya main gate

mix with yours
 
ANGALIZO: Staki mambo yenu ya kisharobalo kuanza kuniuliza source hapa...habari ndo hiyo mura[/QUOTE]


Source si ndo wewe au vipi hapo?
 
wamchague wenyewe kwa kishindo alafu wanampiga tena??!

haaa haaa alichakachua yule, yeye anafikiri kazi yake yakuandika na kuhariri vitabu ni sawa na kuongoza wananchi.....
Pumbafu zake kwanza hawa ndio waliosababisha elimu yetu hapa bongo kushuka, maana wanafunzi walikuwa wavivu hawataki kujisomea na michepuo ya sayansi na biashara ikakosa kabisa wanafunzi maaana wengi walikimbilia Arts...
 
Jamani wabunge wa ccm acheni kwenda na vibaraka wenu kwenye mikutano ya umma wakiwa na mavazi ya kijani mtapokea vichapo tu
 
Back
Top Bottom