Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Oleshangai: Wananchi wapatao 31 wamejeruhiwa vibaya sana. Wanatibiwa nchini Kenya

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Oleshangai Naomba kuthibitisha kuwa wananchi wapatao 31 wamejeruhiwa vibaya sana kwenye zoezi la uwekaji wa beacons kwenye ardhi ya vijiji, Ngorongoro.

Wananchi hao wanapatiwa huduma nchi ya jirani ya Kenya baada ya kunyimwa huduma zahanati ya Osero kata ya Ololosokwan bila PF 3, na waliowapiga ndiyo wanatakiwa kutoa PF 3.

Ikabidi wakaamua kwenda Kenya kutibiwa, Waliopigwa ni wapiga kura wangu halali na siyo wakenya.
Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Oleshangai

====

Katika Ukurasa wake wa Facebook, Mbunge wa Ngorongoro ameandika hivi:

Naomba kuthibitisha kuwa wananchi wapatao 31 wamejeruhiwa vibaya sana kwenye zoezi la uwekaji wa beacons kwenye ardhi ya vijiji, Ngorongoro.

Wananchi hao wanapatiwa huduma nchi ya jirani ya Kenya baada ya kunyimwa huduma zahanati ya Osero kata ya Ololosokwan bila PF 3, na waliowapiga ndiyo wanatakiwa kutoa PF .3.

Ikabidi wakaamua kwenda Kenya kutibiwa,
Waliopogwa ni wapiga kura wangu Halali na siyo wakenya.

Viongozi wenzangu Hawa waliitwa ofisi ya DC Ngorongoro; kwa kigezo kwamba wangeenda kushauriana vizuri namna ya kuendea zoezi, walihojiwa mpaka saa SITA nikiwa nafuatilia mpaka baada ya hapo wa mwisho kuingia ndiyo mwisho wa kujua walipo.

Dc Mwangala aeleze walipo viongozi Hawa na kwanini watu wakamatwe wakiwa kwenye vikao vya kisheria vya Halmashauri na kuwapeleka kusikojulikana ?

Kama zoezi ni shiriki mbona mbunge aliyepo ndani ya jengo la nchi hana hata taarifa ? Waziri Pindi chana nilimuomba appointment akawa ananichenga kila siku.

Zoezi hilo halikuwa shirikishi hata kidogo, mimi nipo bungeni na waziri wa maliasili hajawahi kunikejeli hata kidogo kuhusiana na hili.
Viongozi Hawa waachiwe mara moja,

Madiwani waliokamatwa na mpaka leo hawajulikani walipo.
1. Luka Kursas -oloipiri
2. Moloimet Saing'eu (Ololosokwan)
3. Mathew Siloma(Arash)
4. Rago mbeka (Maaloni)
5.Joel Reson(Malambo)
6. Simon Nairiamu (Piyaya)
7. Shengena Killel(Oloirien -magaiduru)
8. Kijoolu kakiya(Viti Maalum)
9. Rebecca Leshoko(Viti Maalum)
10.Ndirango Senge (Mkiti Ccm wilaya ya Ngorongoro).

Kutokana na vurugu zile Loliondo, kuna wazee na vijana wamepotea na hawajulikani walipo mpaka sasa.

Pikipiki nne zimechomwa eneo la oltulelei kata ya Maaloni na vijana wawili kupelekwa na hawajulikani walipo mpaka sasa.

Baadhi ya wazazi na watoto wametoroka manyumbani na sasa wanaishi pasipojulikana na baadhi yao kukimbilia nchi ya jirani ya Kenya kwa kuhofia usalama wao.
 
huyu mbunge anaelewa wajibu wake wa kuwatumikia wapiga kura wake, ubunge wa CCM ni kitu kisicho na thamani kwake kama walivyo wapiga kura wake anao wawakilisha bungeni, kongole kwakwe kwa kuyapiga chini ma CCM!
Hao ndiyo wamasaai hawanaga uoga wa kijinga
 
nadhani tuingie kwenye 'civil war' kama ilivyokuwa sudan, ethiopia, Palestine, ndiyo adabu na heshima vitakuepo
Kwa akili za wachumia tumbo za watanzania wengi ambao wanaangalia darubini ya maisha kwa mita moja mbele hakutawahi kuwa na civli war.

Kiminyo kitaendelea na Ologarchs wanapasua anga tu, nasubiria yule aliyeitaka Coco Beach nae akaichukue sasa kwa raha mustarehe iwe mali yake. Marufuku kwa mshenzi yeyote kutoka Mbagala au uswahili kokote iwe K nyamala au Tandale kusogelea ufukwe bila kukabidhi "Luteni" au TZS10,000 kwenye lango la Beach!
 
Wameogopa kukamatwa baada ya kufanya mauaji ya askari hivyo wanatibiwa kienyeji na wengine wapo Narok Kenya kwa wamasai wenzao na mbunge ndiye anayehamasisha wananchi wafanye vurugu badala ya kuwaelimisha wamasai wenzake nini kinafanyika na nini lengo la kuweka alama kwenye hifadhi.
 
Kwa akili za wachumia tumbo za watanzania wengi ambao wanaangalia darubini ya maisha kwa mita moja mbele hakutawahi kuwa na civli war....
Kama Koko imetengwa kama mali ya umma itakuwa.hivyo ila kama ni mali ya Serikali wanaweza ikodisha kukajengwa biashara ndefu itakayoleta pesa..
 
Back
Top Bottom