Mbunge Norah Mzeru Achangia Mifuko 50 ya Saruji, Matofali 500 na Laki Nne Ujenzi wa Nyumba ya Katibu UWT Morogoro Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MBUNGE NORAH MZERU AKABIDHI MIFUKO 50 YA SARUJI, MATOFALI 500 NA TSH. 400,000 KWAAJILI YA UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU UWT WILAYA YA MOROGORO VIJIJINI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Waziri Mzeru amekabidhi Mifuko 50 ya Saruji, Tofali 500 za Block na fedha kiasi cha Shilingi Laki Nne (400,000) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya katibu wa UWT Wilaya ya Morogoro Vijijini inayotarajiwa kujengwa Wilayani humo ambapo Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya UWT Wilaya ya Morogoro Vijijini Tarehe 19/08/2023

"Nimetimiza ahadi yangu niliyoiahidi kuhakikisha UWT wanapata nyumba ya Katibu, wiki iliyopita nimefanya Morogoro Mjini na leo nimekuja hapa Morogoro Vijijini na Bado nitaendelea kufanya kwenye Wilaya zingine. Ni hatua kwa hatua kwani nimedhamilia kwa dhati kuona tunaondokana na changamoto ya kupanga niombe" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Tuzidi kushirikiana ili kutatua changamoto hizi kwa Pamoja kwani Wanawake ni Jeshi kubwa na tunaongozwa na Jeshi Namba Moja Mama Yetu na Rais Wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni vyema kwa kumuunga mkono tuepukane na kupanga Nyumba za Watumishi ili fedha ambazo tumekuwa tukitumia kulipa nyumba za watumishi wetu zielekezwe katika Upanuzi wa Miradi Ya UWT" - Mhe .Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Changamoto kubwa tuliyokuwanayo UWT ni nyumba za watumishi tumeona viongozi wetu wa Chama na Jumuiya wanahamasisha ujenzi wa nyumba hizo. Mimi Mbunge wenu nimekuja Wilaya hii ya Morogoro Vijijini kutoa Vifaa vya Ujenzi, nawakabidhi Matofali Mia Tano (500) na Mifuko 50 ya Saruji na fedha ya fundi Shilingi Laki Nne ili muanze ujenzi kwa wakati" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Tunashukuru sana Mbunge wetu, umekuja wakati sahihi, tulikuwa hatujaanza ujenzi lakini kwa Vifaa hivi ulivyotuletea tutaanza ujenzi haraka na tunakuahidi tutasimamia vizuri" - Ndugu Sigilinda Ngwenda, Katibu wa UWT Wilaya ya Morogoro Vijijini

Vilevile, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru ameendelea kuwahimiza Wanawake wa Mkoa wa Morogoro kuanzisha na kuisimamia vizuri miradi mbalimbali ili kuweza kukuza pato la Jumuiya ya UWT kuanzia Mashina, Kata, Wilaya Wikaya na Hata Mkoa.

Ofisi ya Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mjini
Mhe. Norah Waziri Mzeru
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.43.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.43.jpeg
    68.6 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.44(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.44(2).jpeg
    123.2 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.44.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.44.jpeg
    56.9 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.43(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.43(3).jpeg
    122.1 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.42(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.42(3).jpeg
    50.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.41.jpeg
    42.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.38.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-20 at 23.44.38.jpeg
    83.2 KB · Views: 6
Back
Top Bottom