Mbunge Norah Waziri Mzeru (Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro) Atembelea Katika Shule ya Sekondary Lupanga Mkoani Morogoro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Mbunge Norah Waziri Mzeru (Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro) Atembelea Katika Shule ya Sekondary Lupanga Mkoani Morogoro

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Mhe. Norah Waziri Mzeru amewaasa wahitimu wa Kidato cha Nne Katika Shule Ya Sekondary Lupanga Mkoani Morogoro wasome kwa bidii kwa Kipindi hiki kilichobakia kabla ya kuingia kwenye mitihani yao ya mwisho

Mhe. Norah Waziri Mzeru amesema hayo pindi alipokuwa akiwahutubia katika Mahafali yao ya kuhitimu kidato cha Nne kama mgeni rasmi katika Mahafali yaliyofanyika tarehe 07/11/2023 Lupanga Sekondari.

"Walimu wamefanya kazi kubwa sana ya kutulelea watoto zetu hapa Shuleni kwa Kushirikiana na ninyi Wazazi, sasa watoto hawa ni wa Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ndio Rais wetu Nikimaanisha ni wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania" - Mhe. Norah Mzeru

"Kwa muda watakuja kwenu wazazi, wapeni malezi bora watoto ili wasijiingize katika makundi mabaya pindi wanaposubilia matokeo yao baada ya kufanya mitihani yao ya kidato cha Nne" - Mhe. Norah Mzeru

Pia, Mhe. Norah Mzeru ameahidi kuchangia Tsh. 500,000/= kwaajili ya Ujenzi wa Uzio katika Shule ya Lapanga ikiwa kipindi cha nyuma Mbunge alishatoa mchango wa Mifuko 100 ya Saruji kwaajili ya Ujenzi Shuleni hapo

"Wazazi napenda niwaambie kuwa kuna wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia, niwaombe wazazi mtenge muda wa kutafuta fedha na kutenga muda wa kuzungumza na watoto ili kujua mienendo yao kwani watoto wetu wanapitia changamoto nyingi wakati wa kwenda shule na kurudi shule" - Mhe. Norah Waziri Mzeru

Imetolewa na Ofisi Ya Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Morogoro
Mhe. Norah Waziri Mzeru
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-11-09 at 13.16.56.mp4
    30.3 MB
  • WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.48.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.48.jpeg
    127.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.46.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.46.jpeg
    126.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.40.jpeg
    130 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.50.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.50.jpeg
    104.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.52.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.52.jpeg
    81.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.55.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-09 at 08.11.55.jpeg
    101.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom