Mbunge Martha Mariki Achangia UWT Milioni 2 na Mifuko 60 ya Saruji Ujenzi Nyumba za Makatibu UWT Wilaya ya Mpanda na UWT Mkoa wa Katavi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
MBUNGE wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ametoa Shilingi Milioni 2 na Mifuko 30 ya Simenti kwaajili ya Kusaidia Ujenzi wa Nyumba za watumishi wa UWT Wilaya ya Mpanda na UWT mkoa wa Katavi.

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ametoa Shilingi Milioni 2 na Mifuko 30 ya Simenti kwaajili ya Kusaidia Ujenzi wa Nyumba za watumishi wa UWT Wilaya ya Mpanda na UWT mkoa wa Katavi.

Akikabidhi mifuko hiyo ya Simenti kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda Sadiki Kadulo katibu wa Mbunge Tedy Ndasi amesema kuwa Mbunge Martha Mariki ameguswa na ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi wa UWT Wilaya ya Mpanda na kuchangia mifuko 30 ya simenti pamoja na Shilingi Milioni moja kwaajili ya kusaidia ujenzi huo.

''Simenti hii amenituma Mbunge wa Viti maalumu Martha Mariki kukabidhi kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa UWT Wilaya ya Mpanda ametoa mifuko 30 ya simenti pamoja na Shilingi Milioni Moja kwaajili kusaidia ujenzi wa Nyumba ya mtumishi wa UWT wilaya ya Mpanda'' amesema Katibu huyo wa Mbunge Tedy Ndasi

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Katavi Fortunata Kabeja amemshukuru Mbunge wa viti maalumu Martha Mariki kwa kuwachangia UWT mkoa wa Katavi Mifuko 30 ya Simenti pamoja na Shilingi milioni moja.

''Upendo aliouonyesha Mbunge wetu Martha Mariki kwenye jumuiya yetu ni mkubwa sana tunakili kupokea msaada wake wa ujenzi Mifuko 30 ya Simenti na shilingi Milioni Moja amesema ''Mwenyekiti huyo wa UWT Mkoa wa Katavi Fortunata Kabeja

Katika hatua nyingine Katibu huyo wa Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki amekabidhi shilingi Milioni Moja kwa ofisi ya UWT mkoa wa Katavi kwaajili ya kusaidia Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi wa UWT Mkoa wa Katavi pamoja na kutoa Mifuko 30 ya simenti kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Nyumba ya mtumishi wa UWT Mkoa.

Mifuko hiyo 30 ya Simenti aliyoitoa kwa UWT na Mifuko 30 Kwa UWT Wilaya inafanya jumla ya Mifuko 60 iliyotolewa na Mbunge Martha mariki ikiwa na Thamani ya Shilingi Milioni 1 na Laki Tatu na Hamsini Elfu.

''Kwa kutambua umuhimu wa ujenzi wa Nyumba ya mtumishi wa UWT mkoa wa Katavi Mbunge viti maalumu Martha mariki amenituma kukabidhi shilingi Milioni Moja kwa ofisi ya UWT mkoa wa Katavi ili kusaidia ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa UWT mkoa wa Katavi ''amesema katibu huyo wa Mbunge Tedy Ndasi

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mpanda Sadiki Kadulo amemshukuru mbunge wa viti maalumu Martha mariki namna ambavyo anajitolea kukisaidia chama cha mapinduzi na UWT Wilaya ya Mpanda.

''Namshukuru sana Mbunge wa Viti maalumu Martha Mariki kwa kuonyesha upendo na uzalendo wa chama kwa vitendo siyo tu hii mifuko 30 ya Simenti lakini mwanzoni mwa mwezi huu alitupatia Milioni 2 kwaajili ya kusaidia ukarabati wa ofisi ya chama chetu tunamshuru sana Mbunge Martha ''amesema Sadiki Kibwana Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mpanda Tausi Ramadhani amemshuru Mbunge Martha mariki kwa kuendelea kuishika mkono UWT kwa vitendo kupitia michango mbalimbali ambayo amekuwa akiisaidia jumuiya ya UWT Wilaya ya Mpanda.

''Tunamshuru sana Mbunge Martha mariki kwa kutupatia Mifuko hii 30 ya Simenti na Milioni moja kwaajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba yetu ya mtumishi wa UWT Mungu ambariki sana alipotoa amwongezee zaidi ''amesema Tausi Ramdahani Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mpanda.

Ikumbukwe hivi karibuni Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Katavi Martha mariki katika ziara yake ya kuzitembelea kata zote 58 za mkoa wa Katavi aliweza kutoa Milioni 29 kwa UWT Katika Ngazi ya Kata kwa kuwapatia shilingi laki Tano Kila kata ili kujikwamua kiuchumi kupitia miradi midogomidogo ya kiuchumi.

6NMJ.jpg
4QWE.jpg
2VBG.JPG
3QWE.jpg
1FR.JPG
2SD.jpg
1AZ.jpg
 
Back
Top Bottom