Mbunge wa Konde (ACT Wazalendo), Mohamed Said Issa ameitaka Serikali kurejesha upya utaratibu wa watu wote wanaoingia Zanzibar kuwa na hati ya kusafiria.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Makamu wa Rais kwa mwaka 2024/25 leo Jumanne Aprili 24,2024, Issa amesema lengo ni kuvilinda visiwa hivyo.

“Kwa nini waliweka pasipoti (hati za kusafiria) visiwa vile vinahitaji kulindwa, mimi sikubaliani na suala la kutovilinda visiwa saa hizi. Sasa hivi Zanzibar imejaa watu na tunavyoendelea hawatakuwa na sehemu ya kuishi,”amesema.

Issa amempongeza, hayati Abeid Karume kwa kujenga maghorofa yale (hakusema yako wapi) kwa kuwa alitaka Wazanzibar wote wakae humo, kwa sababu aliona ardhi ni ndogo sana.

“Sasa hivi ukienda pale Zanzibar utakuta viwanja vimechukuliwa, miti imekatwa, kulikuwa na zao la mikarafuu haliko tena, imebakia Pemba tu na kule Pemba linakwenda kuisha minazi hakuna sasa hivi tunaagiza kutoka Mafia ,”amesema.

Amesema jambo hilo sio zuri na hata ajira za watalii hawapati tena Wazanzibar wanaofanya kazi hizo ni wageni.

=====

My Take
Serikali puuzeni huu ushauri Ili mwisho wa siku tuwe na Tanzania Moja japo ana hoja na asikilizwe na kujibiwa Kwa hoja.
Kwanza mlichotuachia ni pasport tu mengine yoote watanganyika tunahesabika kuwa wageni hivo harakisheni kabisa. Act iliyokupa tonge ni ya Bara. Unakula mishahara miwili Baraza la wawakilishi na BJYMTZ umevimbiwa sasa unecheua bwege. Kwa sasa mmejaza watoto wenu kwenye mashirika nyeti kama TRA, TPA,Tanesco nk, wengine ni wakuu wa wilaya na mikoa, makatibu tawala.

Bado mkitangaza kazi upande wa pili ni za wazanzibari wenyewe. Shughulikieni matatizo ya msingi ya watu wenu. Kwa ujinga wenu zilitungwa sheria za kazi za kikoloni kwenye sekta binafsi mkifikiria kuwakomoa wabara kwa sasa ni watu wenu ndo wanakoma.

Fikiria mtu amefanya kazi hata miaka ishirini kwa kuwa alikuwa anasahinishwa mikataba ya muda mfupi mfupi, akifikia muda wa kustaafu mwajiri naye anamtega kwenye mkataba anahakikisha unaishia ule mwaka wa kustaafu, matokeo yake mbali na mshahara wa mwisho hapati hata shilingi bora hata bara kuna kuna kakipengele ka SEVERANCE (Severance pay means an amount at least equal to 7 days basic wage for each year of continues service up to a maximum of 10 years. However severance pay does not apply if termination is due to misconduct of employee. (e) Transport allowance to the place of recruitment).

Hebu fikiria miaka 20 au 30 kazini unasubiri huruma ya mwajiri na kikokotoo, Likizo kwa mwaka mzima siku 25. Mtu akifiwa na mke, mzazi au mtoto likizo ya kufiwa ni siku moja utafikiri anaenda kuzika mbwa. Mwisho wa siku inabaki huruma ya mwajiri ampe ruhusa baadae aikate kwenye likizo.
 
Tanganyika ilipewa kazi maalumu na US Zanzibar Isiwe huru hatadakika Moja.Ndio maana wakati wa mwalimu ukizungumzia muungano Yanakukuta🤣🤣🤣.
Hata Aboudu jumbe Raisi baada ya karume yalimkuta.
Acha uzushi!!!

Aliyekwenda kuomba msaada asipunduliwe na Hizbu ni Karume na siyo Wamarekani.

Ni Karume aliyekimbilia Kwa Nyerere kuomba asaidiwe John Okello aondolewe Unguja na siyo Wamarekani.

Vunjilieni mbali huo Muungano.
 
Nahisi Hili wazanzibar wanalitamani Sana sijui kwanini..
Sasa hapo Jiulize huyo ni Mbunge,Je wananchi watakuwaje?

..Waznz walioko Unguja na Pemba ndio watachukia muungano.

..Waznz walioko huku Tanganyika wanaopenda muungano kwasababu wanafaidika nao.

..Na Wazn walioko huku Tanganyika idadi yao ni kubwa sana. Ni kubwa kuliko Watanganyika walioko Znz.
 
Mbunge wa Konde (ACT Wazalendo), Mohamed Said Issa ameitaka Serikali kurejesha upya utaratibu wa watu wote wanaoingia Zanzibar kuwa na hati ya kusafiria.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Makamu wa Rais kwa mwaka 2024/25 leo Jumanne Aprili 24,2024, Issa amesema lengo ni kuvilinda visiwa hivyo.

“Kwa nini waliweka pasipoti (hati za kusafiria) visiwa vile vinahitaji kulindwa, mimi sikubaliani na suala la kutovilinda visiwa saa hizi. Sasa hivi Zanzibar imejaa watu na tunavyoendelea hawatakuwa na sehemu ya kuishi,”amesema.

Issa amempongeza, hayati Abeid Karume kwa kujenga maghorofa yale (hakusema yako wapi) kwa kuwa alitaka Wazanzibar wote wakae humo, kwa sababu aliona ardhi ni ndogo sana.

“Sasa hivi ukienda pale Zanzibar utakuta viwanja vimechukuliwa, miti imekatwa, kulikuwa na zao la mikarafuu haliko tena, imebakia Pemba tu na kule Pemba linakwenda kuisha minazi hakuna sasa hivi tunaagiza kutoka Mafia ,”amesema.

Amesema jambo hilo sio zuri na hata ajira za watalii hawapati tena Wazanzibar wanaofanya kazi hizo ni wageni.

=====

My Take
Serikali puuzeni huu ushauri Ili mwisho wa siku tuwe na Tanzania Moja japo ana hoja na asikilizwe na kujibiwa Kwa hoja.
Watu kama hawa hawahitajiki katika jamii kama kuna msitu au kisiwa apelekwe akaishi peke yake na manyani, huyo mtu ni hatari kwa usalama na ustawi wa taifa!
 
Ila wazenji tunavyowa treat kama mwanamke asiyekutaka waziwazi lakini wewe unamng'ang'ania.

Kwetu wanapaita Tanzania bara kwao ni zanzibar. Si uvunjwe tu huu muungano kila mtu abaki nchini mwake
 
Watu wenye akili za kibaguzi hata wakiwa wabunge hawasahau asili yao. Yeye alipoingia huku Tanganyika ameingia kwa passport? Ila sishangai sana maana watu au Mtu mbinafsi siku zote dalili yake ya kwanza huwa ni hii
“Chako ni chetu sote lakini chake ni chake peke yake”
Huyu mbunge ni wa hovyo sana, au ni wale Wamasai wamemkera kuwachapa barora walinzi wa hotel?

Hivi fundi anaenda kutafuta kibarua cha kujenga awe na passport?
 
Back
Top Bottom