Mbunge MARTHA MLATA

Status
Not open for further replies.
Mimi sioni haya kila kundi kuwa na mwakilishi .Hii ni dhana mufilishi sana .Kazi moja Mbunge achaguliwe na achapa kazi awakilishe watu wote .Tabia za kusema mara Ma Albino mara akina Mama ni upuuzi Nchi ama Bunge haliwezi kuwa la namna hiyo na mwisho tunakuwa kama UK kuwapata wajanja kama akina Abuu na kuutumia Umoja wa TZ kwa maslahi yao .Ma albino ni watu walindwe kisheria watu wafikishwe polisi na baadaye Mahakamani .Soon tutakuwa na mashoga nao sijui wakisha tambulika kisheria mtawapa haki wapi .
 
Huyu mama yuko UK sasa mwaka wa Pili anasoma pale Westminster. Lakini cha ajabu hatumuoni kwenye misiba wala magonjwa lakini anaonekana sana kwenye mikutano ya kufungua matawi ya CCM uingereza nzima.

Swali ninalojiuliza ni je anasoma saa ngapi na saa ngapi anakuwa yuko kwenye shughuli alizochaguliwa kufanya?

Maana Sumaye alipokuwa ansoma kule HARVARD huyu mama alikuwa haishiwi vijitripu vya kwenda kule Cambridge. Nimepata nafasi kadhaa kuongea naye kwa karibu lakini naweza kusema kuwa sijui alikuwa na sifa zipi mpaka JK akampa huo ubunge wa kuteuliwa

Uwanja wenu wana JF

Hizi nafasi za wabunge wasio na majimbo zote zinafaa zifutwe kabisaa maana;
  1. Zinatumiwa vibaya kuendeleza nepotism na ukabila kwenye vyama.
  2. Zinaiongezea gharama nchi bila ridhaa ya wapiga kura
  3. Raisi ni vema akaruhusiwa kuteua mawaziri nje ya wabunge kuondokana na hiki kisingizio cha wabunge wa kuteuliwa
Kwa mtu ambaye ni muwakilishi wa wananchi, ni jambo la haki kabisa kudadisiwa jinsi anavyoshirikiana nao hasa wakati wa matatizo. Huu sio umbea ni haki ya kila mpiga kura.

---------------------------------------------
 
Mimi sioni haya kila kundi kuwa na mwakilishi .Hii ni dhana mufilishi sana .Kazi moja Mbunge achaguliwe na achapa kazi awakilishe watu wote .Tabia za kusema mara Ma Albino mara akina Mama ni upuuzi Nchi ama Bunge haliwezi kuwa la namna hiyo na mwisho tunakuwa kama UK kuwapata wajanja kama akina Abuu na kuutumia Umoja wa TZ kwa maslahi yao .Ma albino ni watu walindwe kisheria watu wafikishwe polisi na baadaye Mahakamani .Soon tutakuwa na mashoga nao sijui wakisha tambulika kisheria mtawapa haki wapi .

Kwa hili Mhe Lunyungu nakuunga mkono ingawa naona hapa (kwenye hii topic, sio mahali pake). Sera za siasa zetu (kama zilivyo, siasa nyingi Duniani) zinatokana sana na mtazamo wa wengi. Sisi tulichozidisha ni kutazama mno sera zenye kuleta umaarufu kuliko maendeleo. Hili la kuwa na mwakilishi katika kila kundi katika jamii yetu ni mojawapo.
 
Namfahamu sana huyu mama personal na ninakubaliana nayi kuwa ni optimistic wa kutupwa.
Ilibidi ajikombe kwenye ziara za viongozi mkoani kwake ili apate kuteuliwa ktk race ya viti maalum. Naambiwa na nikachunguza kuwa aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ktk taasisi fulani nyeti ambapo alipopata ubunge akaitupa nafasi yake bila hata ya taarifa hivyo naweza kusema hana nidhamu hata kidogo.
Kingine ukimwangalia umbo lake utapata jibu kwa nini amepata nafasi ya ubunge wa viti maalum kutoka kwa watu maalum.

Haya natoka tutaonana baada ya miezi miwili tena
 
Duh!Yebo Yebo kiboko

hata wewe?

mbona juzi hatukukuona kwenye msiba wa Lambi? wote mlikuwa pamoja kwenye T.A lakini hujaonekana hospitali,vikao vya mazishi mpaka kwenye mazishi

kwa taarifa yako huyu mama yuko hapo GANTS HILL (CENTRAL LINE) na si mbali na kituo cha HAINAULT, sasa alishindwa vipi kuhudhuria mazishi?

Huyu mama yuko hapa mjini takriban miaka 2 na si yeye wa la huyo mwenyekiti wa CCM LONDON ambao huwa tunawaona kwenye shughuliza jamiii

ABUU FARAJI tulikuwa naye na bila kusahau naibu balozi bwana kilumanga (ambaye nimetokea kumuamini kuwa atakuwa mchapa kazi bora kuliko balozi mwenyewe)

Vile vile nishahudhudhuria shghuli za misiba zaidi ya 15 mwaka huu peke yake na huyo Mbunge haonekani lakini shughuli za CCM zikianza tuu bas, yuko radhi kuahirisha madarasa ili apige mapicha

hilo nalo lisisimwe? ama kweli watu wa mtaa wa Cholmeley mna mambo!

any
 
Namfahamu sana huyu mama personal na ninakubaliana nayi kuwa ni optimistic wa kutupwa

Labda unamaanisha oppotunist kwamba huwa anataka awe katika kila picha za matukio!

Ilibidi ajikombe kwenye ziara za viongozi mkoani kwake ili apate kuteuliwa ktk race ya viti maalum. Naambiwa na nikachunguza kuwa aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ktk taasisi fulani nyeti ambapo alipopata ubunge akaitupa nafasi yake bila hata ya taarifa hivyo naweza kusema hana nidhamu hata kidogo.

Kingine ukimwangalia umbo lake utapata jibu kwa nini amepata nafasi ya ubunge wa viti maalum kutoka kwa watu maalum.

Alaaaah! tafadhali mkuu, mimi nilidhani ndio nafasi hizo wanawake wanahimizwa kuzichangamkia.

"All in all" tumwache mama wa watu asome na arudi nyumbani, hio ndio kumbukumbu ya pekee kwake, sasa atawaambia nini wananchi anaowawakilisha kule Singida.

Hivi kuna mwana JF yeyote huko Singida atuletee picha zenye mandhari ya Kondoa na vitongoji vyake?
 
Duh!Yebo Yebo kiboko

hata wewe?

mbona juzi hatukukuona kwenye msiba wa Lambi? wote mlikuwa pamoja kwenye T.A lakini hujaonekana hospitali,vikao vya mazishi mpaka kwenye mazishi

kwa taarifa yako huyu mama yuko hapo GANTS HILL (CENTRAL LINE) na si mbali na kituo cha HAINAULT, sasa alishindwa vipi kuhudhuria mazishi?

Huyu mama yuko hapa mjini takriban miaka 2 na si yeye wa la huyo mwenyekiti wa CCM LONDON ambao huwa tunawaona kwenye shughuliza jamiii

ABUU FARAJI tulikuwa naye na bila kusahau naibu balozi bwana kilumanga (ambaye nimetokea kumuamini kuwa atakuwa mchapa kazi bora kuliko balozi mwenyewe)

Vile vile nishahudhudhuria shghuli za misiba zaidi ya 15 mwaka huu peke yake na huyo Mbunge haonekani lakini shughuli za CCM zikianza tuu bas, yuko radhi kuahirisha madarasa ili apige mapicha

hilo nalo lisisimwe? ama kweli watu wa mtaa wa Cholmeley mna mambo!

any

Tatizo KUBWA hapa ni ile KASUMBA CHAFU ya Watanzania Wachache wa London kuwa iwapo mtu hajahudhuria Msiba London basi ndio ameshaonekana HADHURII KILA msiba UK nzima. UK is bigger than London...!!

GT, iwapo umehidhuria misiba ya Watanzania 15 UK hii ndani ya 2008 basi ni lazima kama kweli ulikuwa na nia ya kujua huwa nahudhuria misiba mingapi ungeambiwa kuwa nimehudhuria japo 6 (Slough 1, Reading 3, Coventry 1, London 1).

Misiba ya huku nje sio kama kule nyumbani; watu tukienda kwenye misiba huku hatulali hapo hapo (unless ni watu wa karibu sana); watu tunatoa pole na rambirambi, kusadia linalohitajika hapa na pale then tunawahi shughuli zetu. Sasa unless ulikuwa unaitisha majina kila siku nani kafika nani hajafika sijui kama unaweza kuthibitisha shutuma hizi.

Anyway, naomba mimi niishie hapa kwenye huu mjadala.
 
Kwa taarifa nilizosoma kwenye thread hii ni kubwa Mbunge huyu anasoma kwa muda wa miaka miwili. Mie nina maswali yafuatayo:
1. Taratibu za Bunge zinaruhusu Mbunge kuwa nje ya Bunge kwa kipindi kirefu kama hiki?
2. Je nini hatma ya watu anawaowakilisha hata kama ni viti maalumu?
3. Posho na mafao yake yanafata utaratibu gani?
Naomba kuwakilisha.
 
Kuna mwenye idea jinsi JK anavyoteua hawa wabunge - Special seats? Martha Mlata alikuwa akihojiwa kwenye TV wiki kadhaa zilizopita, nilipatwa na butwaa nikijiuliza amechaguliwa kwa vigezo gani. Her point of view was so shallow. Fani yake ni uimbaji kwaya, au sio huyu?

Mwenye profile yake atupe hapa tafadhali, I'm so curiuos!
JK hateui Wabunge wa viti maalum (special seats)kama Martha Mlata. Nimecheck CV yake: ni form IV aliyefeli flat ambaye sifa yake kuu ni kuimba Gospel Songs za Kiswahili. Kama alihojiwa na TV ya huko majuu, basi lazima ilikuwa balaa. Aliongea lugha gani, Kinyiramba? Ijabu
 
yaani mmefikia hadi kushindana nani anafika msibani nani hafiki? Mwisho mtaulizana nani anatoa zaidi msibani na nani bahili....

Na kuhusu huyo mbunge kuweka mbele CCM inashangaza mnaendelea kuuliza swali ambalo lilishajibiwa; Ibara ya 15:1

Lakini vinginevyo, naomba tuambiwe hasa kati ya Wabunge 322 hivi ni kwanini tumuanzishie mada huyu?

a. Kwa vile yuko London
b. Kwa vile yuko karibu na watu wa London ambao ni wanachama wa JF
c. Kwa vile akianza kuhudhuria misiba na sherehe anaonesha kitu fulani
d. Kwa vile yeye ametokea viti maalumu
e. Kwanini?

Lazima iwepo sababu kubwa sana ya kumuangalia Mbunge huyu mmoja na mahudhurio yake msibani, there had to be something more than funeral attendance.. what is it?
 
Hivi unawezaje kutumikia nafasi yako ya ubunge kama uko nje ya nchi kwa muda wote huo? Kwa nini kama umeamua kujiendeleza kimasomo (ambacho bila shaka unastahili pongezi) usimpishe mwenzio atakayeweza kuwakilisha jamii iliyokuchagua vyema zaidi? Hii ningependa kusisitiza holds kwa mbunge yeyote, wa chama tawala au cha upinzani.
 
JK hateui Wabunge wa viti maalum (special seats)kama Martha Mlata. Nimecheck CV yake: ni form IV aliyefeli flat ambaye sifa yake kuu ni kuimba Gospel Songs za Kiswahili. Kama alihojiwa na TV ya huko majuu, basi lazima ilikuwa balaa. Aliongea lugha gani, Kinyiramba? Ijabu

Mkuu, tuletee "copy" ya hio CV tuione.
 
yaani mmefikia hadi kushindana nani anafika msibani nani hafiki? Mwisho mtaulizana nani anatoa zaidi msibani na nani bahili....

Lazima iwepo sababu kubwa sana ya kumuangalia Mbunge huyu mmoja na mahudhurio yake msibani, there had to be something more than funeral attendance.. what is it?

{i} CHARACTER ASSASINATION
(ii} PERSONAL
{iii}ENVIOUS
 
.... Kama alihojiwa na TV ya huko majuu, basi lazima ilikuwa balaa. Aliongea lugha gani, Kinyiramba? Ijabu

We ulitaka aongee lugha gani?
Bado tumebaki na kasumba kuwa lazima tuongee kimombo....Ona kina Putin,Sarkozy n.k....sio kuwa hawajui english but they are proud kuongea lugha yao

Mimi ningesikia raha sana kama JK akiwa huko majuu aongee lugha yetu.....thanks JKN kuifanya swahili kuwa lugha ambayo inajulikana duniani
 
yaani mmefikia hadi kushindana nani anafika msibani nani hafiki? Mwisho mtaulizana nani anatoa zaidi msibani na nani bahili....

Na kuhusu huyo mbunge kuweka mbele CCM inashangaza mnaendelea kuuliza swali ambalo lilishajibiwa; Ibara ya 15:1

Lakini vinginevyo, naomba tuambiwe hasa kati ya Wabunge 322 hivi ni kwanini tumuanzishie mada huyu?

a. Kwa vile yuko London
b. Kwa vile yuko karibu na watu wa London ambao ni wanachama wa JF
c. Kwa vile akianza kuhudhuria misiba na sherehe anaonesha kitu fulani
d. Kwa vile yeye ametokea viti maalumu
e. Kwanini?

Lazima iwepo sababu kubwa sana ya kumuangalia Mbunge huyu mmoja na mahudhurio yake msibani, there had to be something more than funeral attendance.. what is it?

Mkuu MJJ,
Nafikiri hii ni haki ya mpigakura kujua jinsi mwakilishi wake anavyoshirikiana na anaowawakilisha hasa wakati wa shida.

------------------------------------
 
[Mama yangu weeeeeeeeeee, sitaki kuamini kuwa tuna wabunge Form IV leavers, this is too crazy to bear! kweli tumefikia hatua ya kuwa na wawakilishi vilaza namna hii kwenye nchi ambayo ina wasomi wa kutosha??? Sasa huko London anasoma nini?? This is just unbelievable crapp, labda kama si kweli huyu mama ameishia form four!!! Au uimbaji kwaya ndio umempeleka bungeni?? Je Tz tuna wizara/kitengo cha Gospel ili huyu mama akiendeleze?? otherwise it doesn't make sense at all how we end up with her as mbunge, haijalishi ni mbunge wa kuchaguliwa, kuteuliwa au kupewa chini ya uvungu kama shukrani!!! Kwleli mambo ninayoyasikia Tz yanatisha hata kuamini! This is the shock of the day...am out of here.

QUOTE=Ijabu Issa;192907]JK hateui Wabunge wa viti maalum (special seats)kama Martha Mlata. Nimecheck CV yake: ni form IV aliyefeli flat ambaye sifa yake kuu ni kuimba Gospel Songs za Kiswahili. Kama alihojiwa na TV ya huko majuu, basi lazima ilikuwa balaa. Aliongea lugha gani, Kinyiramba? Ijabu[/QUOTE]
 
Hizi nafasi za wabunge wasio na majimbo zote zinafaa zifutwe kabisaa maana;
  1. Zinatumiwa vibaya kuendeleza nepotism na ukabila kwenye vyama.
  2. Zinaiongezea gharama nchi bila ridhaa ya wapiga kura
  3. Raisi ni vema akaruhusiwa kuteua mawaziri nje ya wabunge kuondokana na hiki kisingizio cha wabunge wa kuteuliwa
Kwa mtu ambaye ni muwakilishi wa wananchi, ni jambo la haki kabisa kudadisiwa jinsi anavyoshirikiana nao hasa wakati wa matatizo. Huu sio umbea ni haki ya kila mpiga kura.

---------------------------------------------

Edwin I.M. Mtei said:
"...naamini kwa dhati kwamba kipengele kilichoingizwa katika Katiba ya Tanzania mwaka 2000 kumwezesha rais kuteua wabunge wasiozidi kumi, miaka 30 baada ya uhuru, ni kinyume kabisa cha uhuru na demokrasia na kinastahili kufutwa mapema iwezekanavyo. Hakina maana yoyote na kinafedhehesha na kudhoofisha maamuzi ya wapiga kura wakati wa Uchaguzi. Maamuzi hayo ni kwamba wawakilishi wao wawe na uwiano wanaoamua wanapopiga kura. Wabunge hawa kumi waondolewe katika Katiba."
SOURCE: Marekebisho ya Katiba nchini hayaepukiki

JK hateui Wabunge wa viti maalum (special seats)kama Martha Mlata. Nimecheck CV yake: ni form IV aliyefeli flat ambaye sifa yake kuu ni kuimba Gospel Songs za Kiswahili. Kama alihojiwa na TV ya huko majuu, basi lazima ilikuwa balaa. Aliongea lugha gani, Kinyiramba? Ijabu

Ilikuwa ni TV ya hapa Bongo
 
Good point Lunyungu!!!,

Kama hataki kujihusisha na masuala ya kijamii yanayowahusu wa-tz wenzake why don't you tell her direct??? Msiwe wepesi wa kusemea pembeni kuwa bibi amekaa uchi haisaidii huenda yeye kwa akili yake haoni kama ni kitu kibaya na kwa kuongea ongea pembeni haijengi tell her bibi umekaa vibaya rekebisha mkao hayo ndio mambo vijana... Punguzeni talalila sizizo na maana..Kama ni kilaza ni matatizo yake na aliyempeleka huwezi kulazimisha awe genius hata kama betri yake iko low kudaka full net work.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom