Mbunge MARTHA MLATA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge MARTHA MLATA

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Game Theory, May 8, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Huyu mama yuko UK sasa mwaka wa Pili anasoma pale Westminster. Lakini cha ajabu hatumuoni kwenye misiba wala magonjwa lakini anaonekana sana kwenye mikutano ya kufungua matawi ya CCM uingereza nzima.

  Swali ninalojiuliza ni je anasoma saa ngapi na saa ngapi anakuwa yuko kwenye shughuli alizochaguliwa kufanya?

  Maana Sumaye alipokuwa ansoma kule HARVARD huyu mama alikuwa haishiwi vijitripu vya kwenda kule Cambridge. Nimepata nafasi kadhaa kuongea naye kwa karibu lakini naweza kusema kuwa sijui alikuwa na sifa zipi mpaka JK akampa huo ubunge wa kuteuliwa

  Uwanja wenu wana JF
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  May 8, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa Naamini Na Nitaendelea Kuamini Kwamba Jk Sio Chizi Mpaka Kuamua Kumchagua Mtu Wowote Kuwa Mbunge Naamini Pia Wale Wote Walio Teuliwa Wameteuliwa Kutokana Na Uchapaji Kazi Wao Sehemu Kadhaa Walizowahi Kufanya Kazi Mpaka Hapo Walipo

  Hata Huyu Naamini Ni Mchapa Kazi Na Ni Mwaminifu Kwake Na Kwa Taifa Kwa Ujumla Ndio Maana Mheshimiwa Raisi Kampa Wadhifa Huo

  Sasa Tusianzishe Propaganda Ambazo Hazina Mpango Dhidi Yake , Au Kuanza Kumchokonoa Kama Amefanya Jambo Baya Ataambiwa Lakini Mtu Amekaa Ametulia Anajisomea Ya Nini Kuanzia Kumsumbua Na Kumsakama Kama Vile Na Yeye Ni Kafisadi ??
   
 3. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  sio kama anasakamwa bali anaelezwa ukweli,ukiwa kama binadamu bila ya kujali kama ni kiongozi au laa ni vizuri kuonekana katika misiba au maradhi pindi wale walio karibu nawe wanapopatwa.sasa yeye issue zake kwenda kwenye vikao vya ccm tu,kwenye misiba hatumuoni,je huu ni ubinadamu?
   
 4. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ukizungumzia uchapaji kazi, unamaanisha nini??
  Uchapakaji kazi unaozungumziwa ni hule wa kuwa na uwezo wa kuweza kulitumikia Taifa lako na kuleta maendeleo kwa wanchi wako kwa namna moja au nyingine.

  Sasa isije kuwa nawe unajiweka katika wale wanaochapa kazi ukiwa na matumaini ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa kuteuliwa

  Haya nipe sifa Tano bora ambazo Mkuu aliwateua wafuatao
  Makamba ni mbunge wa kuteuliwa na hapo hapo bado ni katibu wa chama cha Mafisadi, lakini ni wazi kuwa mzee huyu haya uwezo kabisa wa kufanya kazi walau moja kiufasaha kabisa, zaidi ya porojo tu, na hilo CCM mnalitambua (nukuu Kikwete akiongea na wazee Diamond pale juzi) sasa ukimpa kazi mbili zinajoitaji kushirikisha ubongo atafanya kweli?? Naomba vigezo na sifa za ufanisi za Makamba

  Haya Mchungaji G. Rwakatale, huyu naye unaweza kutoa sifa zake zilizomchukulia Mh. kumteua kuwa mbunge, kama sio kucheza na madaraka waliompa wananchi, toa siafa za huyu mama!!

  Haya Meghi, ndio bure kabisa, na aliteuliwa na Kikwete na akapewa na uwaziri, lakini kama utakumbuka alidhubutu kusema kuwa alidanganywa na Balali kusaini Vijisenti vya BOT, wakati yeye alipewa katiba na mwongozo wa serikali na kuhudhulia ngurudoto, sasa utasemaje kuwa Kikwete anajua sifa za hawa jamaa ndio maana anawateua??

  wako wengine wengi tu ambao nao no vilaza, ila nalazimika kusema kuwa, inawezekana hata President nae ndio wale wale ndio maana hata watu anaowachagua ni wa aina hiyo, kwahiyio msishangae, kwani hajafanya lolote likafanikiwa toka achukue upresident, zaidi ya kuonyesha usanii, na big failure kila siku ni kuchagua mijitu bure kabisa na pumba kichwani
   
 5. A

  ACHEBE JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2008
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 348
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nduguyangu nadhani jipange kwanza vizuri kisha uje na hoja yako nadhani sio mbaya isipokuwa inapungukiwa baadhi ya kweli/facts kadhaa, sasa kwa watu makini inakuwa kama vile uzushi flani...mfano Martha Mlata sio mbunge wa kuteuliwa ni mbunge wa viti maalum akiwakilisha kina mama wa mkoa wa Singida.Mkoa ule unawabunge wawili wa viti maalum yeye na Diana Chilolo.Alishindana na wanawake wenzie kumi na nne akawa mtu wa pili kwa kura nyuma ya Chilolo ,na mengine mengi umepotosha,but nianze na hili...wasalaaaam
   
 6. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SHy,
  Mbunge Tom Mwangonda hajawai kuchangia hoja yoyote tangu achaguliwe, na bungeni haonekani...ni uchapaji kazi gani huo unaosema
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Jadilini hoja ambayo imeletwa na GT acheni kuongea na kupoteza muda na chizi shy .Yeye yuko kazini .Nani hajui kwamba analawamba hao makalio ili apate kuishi? Hana kazi .Wewe Yona Maro unafanya kaiz gani ? Uandishi nauchambuzi ndiyo huu .Jamani the boy ni senior snitch .Endeleeni na hoja acheni kupoteza muda wenu kujadili utumbo wake .Akili zake zimfungwa kama avator yake sasa rudini kwenye hoja .Mbunge kwa shughuli za jamii haonekani lakini wale wale anawatumia kwa matawi ya CCM . Lakini nayi wa TZ wa UK mna laana .Si mwambieni LIVE mkiwa naye ?
   
 8. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kuna mwenye idea jinsi JK anavyoteua hawa wabunge - Special seats? Martha Mlata alikuwa akihojiwa kwenye TV wiki kadhaa zilizopita, nilipatwa na butwaa nikijiuliza amechaguliwa kwa vigezo gani. Her point of view was so shallow. Fani yake ni uimbaji kwaya, au sio huyu?

  Mwenye profile yake atupe hapa tafadhali, I'm so curiuos!
   
 9. Single D

  Single D JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 459
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wabunge wa viti maalum(special seats) hawateuliwi na JK.
  JK huteua wabunge wake ambao huitwa wabunge wa kuteuliwa (kama Mgosi makamba,Zakia Meghji n.k

  Hawa special seats hupeleka majina kwa ngazi ya mikoa ktk vyama vyao(CCM,CUF,CHADEMA n.k)na kupigiwa kura kwa kanuni za vyama vyao,
  Pia ndiye yule mwimba kwaya ambaye ktk uzinduzi wa album yake pale WET 'n WILD hotel mgeni rasmi alikuwa Waziri mkuu mstaafu Fred.ambaye alisema ukitaka biashara yako inawiri wewe ingia sisiem
   
 10. n

  nat867 Member

  #10
  May 8, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyo mbunge hamna kitu, kuna rafiki yangu alikuwa naye anasoma huko. kila kukicha anapigiwa simu na huyo mama akitaka asaidiwe kujibu essays/homeworks. hamna kitu!!!
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Tuna kazi kubwa sana .Sasa huko asomea kuimbisha kwaya ama inakuwaje ?Mnaoposema ni mtu jaribuni kutueleza .Kawekwa kiti moto ama swali la ghafla akaanza kumwagia sifa serikali ya Mh.JK maana kila wakiguswa utasikia sifa kwa Serikal ya Mh.JK .
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Katika utamaduni wa maisha ya kawaida ya Mtanzania, kushirikiana na wenzako katika masuala ya kijamii kama ugonjwa na vifo ni kitu muhimu sana. Iwapo utamuona mtu hashiriki katika masuala hayo, bila ya kuwa na sababu ya msingi, hasa akiwa ughaibuni ambako watanzania wote huwa ni ndugu moja, basi kuna tatizo fulani.
  Tena, iwapo atakuwa anapata nafasi ya kufika kwenye shughuli fulani tu na kushindwa kufika kwenye shughuli nyingine muhimu kijamii, kuna mushkemli mkubwa hapo.
  Nadhani itakuwa jambo la busara kwa walio karibu naye kumdodosa wapate fununu ya nini kiini cha tabia yake hiyo. Ikiwezekana ashauriwe kuwa anachokifanya, hakimjengi.
   
 13. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  mimi sijaona tofauti ya yeye na wabunge wengine wa bunge letu la jamuhuri ya muungano.bunge letu ni kokolo limesheheni kila aina ya watu na hiyo ndio picha kamili ya watanzania jinsi tulivyo kwa matendo na tabia.
   
 14. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  wakuu

  Hii Tabia Ya Kujadili Watu Bila Kuwa Na Facts Ikome Humu Forum.

  Watu Wazima Na Elimu Zenu Mnasema Hahudhurii Misiba; Hebu Toeni Data Ni Misiba Mingapi Imetokea Uingereza Na Nyie (hasa Gt) Mlikuwepo Kuhakikisha Kuwa Mb Hajahudhuria??!! Then, Kabla Hamjaleta Utumbo Hapa Forum Tuambieni Tena Kwa Nini Ahudhurie Kila Msiba.

  Hakuna Hoja Hapa, Sana Sana Mnashusha Heshima Ya Forum.

  Haya Ndio Maoni Yangu Kwenye Hii Fitina, Sina La Zaidi.
   
 15. green29

  green29 JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 35
  Whaaaaaaaaaaaaaaaaaat!!!?
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na yule Albino aliyekuwa uwanja wa ndege je, ana sifa gani za kuteuliwa na JK ubunge?
   
 17. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Mkuu GT,

  Kwa hili la Martha Mlata, naona unaning'nia kwenye "edge".

  Sidhani kama ni lazima aonekane katika hayo uliyosema labda anakuwa na shughuli zingine si unajua fika kwamba yeye ni mbunge?

  Ni ama umwage unachotaka kusema, au la, lete "facts" zaidi ili tuchambue, ama sivo GT unakwenda kusiko.
   
 18. w

  watu wewe Member

  #18
  May 8, 2008
  Joined: May 20, 2006
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na uteuzi wa JK kwa huyu mama albino. Kumekuwa na mauaji ya kutisha ya maalbino kwa imani za kishirikina siku za karibuni, na nadhani JK anataka kuona maalbino wanawakilishwa bungeni.
   
 19. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #19
  May 8, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Naona Admin ameshindwa kumshugulikia huyu na matusi yake okey ngoja tuone atafikia wapi
   
 20. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #20
  May 8, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mimi naona hoja hii ipelekwe kwenye udaku... tuleteeni basi sifa za huyo mama... tuzichambue, kama mnazo. Vinginevyo mada hii haijatulia. Haijatetewa wala haijakosolewa ipasavyo.

  My three cents.... :)

  ./Mwana wa Haki!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...