Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 2,958
- 8,130
Hivi Kombo anatuchukulia sisi watani zake eeeeh? 
Halafu hapo hapo anakwambia tumewaalika Maseneta waje wahakikishe kama hatuuani kidini! Sasa kama walielewa somo kwanini mmewaalika?
Halafu hivi Maseneta walisema nchini kuna vita ya kidini? Serikali kuambiwa mnakandimiza uhuru wa kuabudu ambao tulishuhudia kwa Gwajima na waumini wake kila siku kunyanyaswa, yule kaka mwimba injili Mwanza mpaka leo hajulikani alipo, ndio mseme maseneti walisema tunachinja wenyewe kwa wenyewe sababu ya imani zetu? Masheikh nao wakaingia mzima mzima, japo siwashangai sana maana wao ni kasuku... lakini mnafikiri wananchi ni wajinga kiasi hiki? Eti guys Dr. Mwigulu Nchemba
Alipowasilisha hotuba ya Wizara ya Mambo ya Nje na kupata michango kutoka kwa wabunge, Kombo alisema.....
Baada ya kuapishwa mheshimiwa Rais na baada ya kututeua akanikabidhi barua 25 ambazo mimi nimekwenda nazo duniani kueleza nini kilichotokea Tanzania.
Kote nilikokwenda mimi duniani nimeulizwa, "Kwa nini hamkuja mapema?" Nikajibu tulikuwa kwenye uchaguzi. "Kwa nini hamkuja mapema?" Rais wetu alikuwa hajaapishwa. "Kwa nini mlikuwa hamkuja mapema?" Serikali ilikuwa haijaundwa na mawaziri bado hawajachaguliwa.
Lakini kote nilivyokwenda wakasema, "Tumedanganywa sisi. Taarifa tulizoletewa siyo hizi alizoandika Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kalamu yake na amesign kwa wino wake." Kuanzia siku hiyo Tanzania ilibadilika na wakatukubalia, mpaka Papa, mkuu wa madhehebu ya Katoliki duniani. Mimi ndiyo niliyotumwa kwenda. Mheshimiwa Palamagamba Aidan Kabudi tulikwenda naye pamoja, yuko wapi?
Nilimweka yeye kiongozi kwa sababu yeye mavitabu yale ya historia na vitu yale anayajua zaidi yale. Na yeye huwa anabeba mafaili huku na huku. Akianza kumsimulia Mwalimu Nyerere na 1961 alionekana yeye anajua zaidi, maana mimi 1961 hata kuzaliwa sijaizaliwa, wala mama yangu hawajaoana bado.
Yeye alionekana, na kufika kule akampa Papa vitu vyake na Papa akatupa vitu vyake. Tukarudi hapa kwa mafanikio yameisha mpaka leo. Sasa leo nchi yetu iko calm, iko cool, kila mmoja anakwenda kazini, kila mmoja anakwenda kutekeleza majukumu yake, ya nini chochoko jamani? Ya nini tunataka kurudi kwenye chokochoko?...

Halafu hapo hapo anakwambia tumewaalika Maseneta waje wahakikishe kama hatuuani kidini! Sasa kama walielewa somo kwanini mmewaalika?Halafu hivi Maseneta walisema nchini kuna vita ya kidini? Serikali kuambiwa mnakandimiza uhuru wa kuabudu ambao tulishuhudia kwa Gwajima na waumini wake kila siku kunyanyaswa, yule kaka mwimba injili Mwanza mpaka leo hajulikani alipo, ndio mseme maseneti walisema tunachinja wenyewe kwa wenyewe sababu ya imani zetu? Masheikh nao wakaingia mzima mzima, japo siwashangai sana maana wao ni kasuku... lakini mnafikiri wananchi ni wajinga kiasi hiki? Eti guys Dr. Mwigulu Nchemba