Mbunge Martha Mariki Atoa Zaidi ya Milioni 4 Kusaidia Ujenzi wa Ofisi za CCM Wilaya - Katavi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944
Mbunge Martha Mariki Atoa Zaidi ya Milioni 4 Kusaidia Ujenzi wa Ofisi za CCM Wilaya - Katavi

MBUNGE wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Mariki ametoa Mifuko 50 ya Simenti kwaajili ya Kusaaidia Ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi [CCM] Wilaya ya Mlele.

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha Mariki ametoa Mifuko 50 ya Simenti kwaajili ya Kusaaidia Ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mlele.

Akikabidhi Simenti hiyo Kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mlele Worfgang Pinda Mbunge Martha amesema kuwa ameguswa kuchangia mchango huo Ili kusaidia chama kuwa na ofisi za kisasa Ili kazi za Chama ziendelee kufanyika katika mazingira salama.

"ndungu Wanachama wenzangu nikiwa nipo kwenye ziara hii katika Wilaya ya Mlele nimeona ni vema kuchangia Mifuko hii 50 ya Simenti yenye thamani ya shilingi Milioni 1 na lakimoja na Elfu Hamsini isadie katika ujenzi wa ofisi yetu ya Chama Wilaya ya Mlele" Amesema Martha

Amesema kuwa Chama Cha mapinduzi katika mkoa wa Katavi kipo katika mikakati ya kuhakikisha ofisi za CCM Wilaya kwenye mkoa wa Katavi zinajengwa Ili zisaidie kazi za Chama ili kuwatumikia wanachama Kwa uhakika.

Chama chetu kina mkakati wa kujenga Ofisi za wilaya za Kisasa na ukienda Tanganyika ujenzi unaendelea hapa Mlele pia na Ofisi yetu ya wilaya ya inaendelea kufanyiwa Ukarabati amesema Mbunge Martha

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi [CCM] Wilaya ya Mlele Worfgang Pinda amemshuru Mbunge Martha Kwa kuchangia Mifuko hiyo 50 ya Simenti.

‘’Kuna wakati ujenzi wa Ofisi ya Chama chetu ulisimama Kwa muda ila kwa sasa tunaenda kuanza maramoja nimushukukuru Mbunge wetu Kwa mchango wake tunataka ofisi yetu iishe haraka hata nyie mnaona hapa tuna banana sana"Amesema Worfgang

Worfugang amewashukuru wanachana wote ambao wamekuwa wakiguswa na ujenzi wa ofisi hiyo Kwa kutoa michango yao Ili kufanikisha ujenzi huo.

Hivi karibuni Mbunge huyo wa Viti maalumu Mkoa wa Katavi Martha mariki alitoa Mifuko 50 ya Simenti Kwaajili ya kusaaidia Ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Tanganyika yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 na Lakimoja na Elfu Hamsini pamoja na kuchangia shilingi Milioni 2 katika chama Cha mapinduzi [CCM ]Wilaya ya Mpanda ili kusaidia Ukarabati wa ofisi hiyo unaondelea na kufanya jumla ya Shilingi Milioni 4 na Laki tatu.

Ziara ya Mbunge huyo wa Viti maaalum Mkoa wa Katavi imetamatika katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele katika Jimbo la Katavi Kwa Kuzitembelea Kata zote Sita za Jimbo Hilo na ziara hiyo inaendelea katika Jimbo la Kavuu Halmashauri ya Mpimbwe kwa Kuzitembelea Kata zote za halmashauri ya Mpimbwe.

11.JPG
mbiliq.JPG
tatu.JPG
nee.JPG
sitaa.JPG
tano.JPG
 
Back
Top Bottom