Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Chinga,
Basi jipongeze kwa vile ulivyokula sahani moja na Mwanasiasa na kuweza kufumua fumua wote wazushi Jasusi na nani yule wa Hai. Naona wewe mahiri sana.

Since umeshatubatiza kuwa tumetumwa ( kwa kuwa hatuna akili ya kujituma) na wewe je nani kakutuma? It takes one to know one.
 
by the way wanasiasa as long as wako kwenye public domain private lives zao nazo zitakuwa zinamulikwa kwa sababu kuna wengine wanataka kuwa moral guardians wa wananchi hivyo all bets are open
 
Today, 05:35 PM
chinga
Senior Member Join Date: Nov 2006
Posts: 112
Rep Power: 1


Mnyika.
wewe ni mkurugenzi wa chama ina maana huna access za mtandao? ulisema utakuja kujibu humu tarehe 5 na leo 11.
chama utaendesha vipi? kama huwezi kufanya vitu within a deadline?
kuna kazi huko chadema.
 
nadhani CHADEMA inabidi wafungue department ya PR ili kudeal na watu kama akina chinga kwa sababu hii inonekana kuwa wanaudhaifu mkubwa sana ku back up statements na arguments zao


saa zingine ni vizuri kukiri wanapokosea at least watu wanaweza kuwaelewa lakini kama itakuwa kila kitu wanataka ligi sasa kuna hao ma UNGUIDED MISLES kama Chinga wanawafanya wachanganyikiwe na hiii ni hatari

I cant imagine wanadeal vipi na magazeti ya udaku bongo
 
Wanabodi.
huyu bwana nimemkurupua na hiyo post yangu hapo juu.
Mnyika acha uongo nitajie chuo kimoja tu kilichoanza holiday last two weeks? vyote vinaenda holiday this friday. tizama wewe unasema nini na Mwanasiasa anasema nini?

kweli hujui mwenyekiti wako yupo wapi hadi apige simu moshi? jee makao makuu ya chama yako Moshi? kesi hiyo hiyo Nchimbi atapiga simu bagamoyo kwa Kikwete au makao makuu ya chama?

unazidi kuudanganya umma kuwa gazeti lilikosea kwa kawaida gazeti likikosea story basi siku ya pili tu, linasema ktk toleo la jana kulikuwa na habari ambayo usahihi wake ni huu, basi tunasubiri usahihi wa gazeti wa habari hii, hizi justification zako za uongo tu.

na mimi nimepiga simu chuoni namba hizo nimeziweka kila mwanabodi apige, Mwenyekiti katoroka hayuko chuoni na kuomba na wewe piga chuoni hao ulioongea nao Moshi lazima watamficha kuwa jamaa yuko chuoni kwani ni jambo la aibu kwa chairman kuwa mtoro na inawezekana umeongea naye mwenyewe ila kabadilisha sauti, yeye anajua sisi tumewaka humu kwenye forum unategemea mtuhumiwa huyo huyo akwambie ndio nimetoroka shule?, si bora angenunua cheti kama Mrema?

Tafuta independent body kuliko kuuliza mhusika mwenyewe, hata kama angekuja kwa roketi ilibidi ujue ujue Chairman yuko wapi?nazidi kuamini si chama hicho ni NGO tu.

umesema hao kanisa la KKKT walileta maombi nami nimeomba kusaidiwa vijana 10 kwa elimu ya juu, hakuna aliyenijibu, hata kusema kwa sasa maombi yako, hayakufanikiwa ila jaribu next time.

unasema alitoa pesa Taifa stars hayo ndiyo yalinifanya niulize nani zaidi kati ya Mbowe na Chifupa? kwani alipoona Amina Chifupa kapeleka pesa naye akapeleka, wamekuwa wanashinda na kushabihiana kwenye mambo mengi.
 
Mnyika.
naomba university moja tu iliyoanza holiday japo last week ya UK,
ukiipata nitakuwa chadema damu.
cha ajabu wewe kusoma hutaki utajua mambo ya semister za chuo? hujui hata Mwenyekiti kaja lini.
 
admin umeanza kukoroga mambo, topic unataka kuidilute ilikuwa ina analysis za mtandao wa chadema familly ltd sasa umeichanganya na hoja nyingine itakosa ladha, tafadhali restore things back to normal....ni ombi tu!
 
Kwa kawaida huwa Admin anatoa kijipendekezo kuwa anakusudia kumerge topic flani na flani kabla ya kufanya hivyo, au huwa wanabodi wenyewe wanaomba topics zichanganywe... lakini katika hizi mmmh!

Kwa kumbukumbu zangu ... kabla ya thread za 'tajiri' kufutwa na mpya kupotea potea ... zilianza kuchanganywa na kuvurugwa kama zilivyofanywa thread hizi.

And my guess ni kuwa mtaambiwa kuwa kwa bahati mbaya mitambo hairuhusu ku-undo.
 
HATA ushauri hatukuombwa, jana chadema walishusha timu yao yote na wakafeli totally.
kumbukumbu niliyo nayo ADMIN alisema hata changanyanga mada bila kuomba ushauri,
sijui ameghafirika?
 
Invisible alisema hatakuwepo kwa muda pengine kuna tatizo. Tuweke subira.
 
hata murugenzi wa fedha naye ni MTEI jee ni hiyo hiyo family business? huyu ni mtoto wa Mtei AU MJUKUU?

mwanasiasa na Mnyika.

naomba majibu.
 
Samahani hapo juu, nilikusudia Mkurugenzi wa Fedha wa chadema bwana Mtei sio edwin, ndio nataka kujua kama ni mtoto,mjukuu au mkwe naye kamuua kutumia jina la baba mkwe?

nilikusudia mkurugenzi wa fedha, najua kuna makengeza wengi ndani ya chadema wasije ku take advantage kama akina Kichuguu,Lunyungu,mwanasiasa n.k
 
Kama nilivyoaidi kuwa nitarudi kupitia matokeo ya utafiti yaliyowasilishwa na ndugu yetu Tafiti. Kwanza nampongeza ndugu Tafiti kwa kujenga hoja kwa kutumia mantiki ya takwimu. Yeye anaibuka na issues, hajadili pua za watu kama kina fulani.

Tafiti, matokeo ya utafiti wako yamenifurahisha sana. Hii ni kwa sababu lengo kubwa la utafiti wako lilikuwa kuthibitisha kuwa CHADEMA ni family business. Yaani ni chama cha familia. Lakini matokeo yako umeibuka na conclusion kuwa ni chama cha ukanda bila hata ku-refute initial hypothesis yako ya kuwa chama hiki ni family business! Kabla ya kurukia hypothesis ya pili ya ukanda, mtafiti mzuri alipaswa kwanza aikatae hypothesis yake ya kwanza ili aendelee na ingine. Anyway, I hope in future you can do better than this!

Nikija katika utafiti wako mpya wenye kutaka ku-prove hypothesis kuwa CHADEMA ni chama cha ukanda, there are two critical biases which water down the credibility of your results. Kwanza, huwezi kufanya such a bold conclusion on 50%. Asilimia 50 katika utafiti inakuacha ukiwa puzzled na inakwambia utafute factors zingine katika ku-explain your findings. So, you cannot prove your hypothesis on the basis of such a small margin which is really insignificant by an statistical test of significance! Pili, ambayo ni muhimu zaidi, ni pale ulipoamua kutunga tafsiri yako ya neno uongozi katika chama cha CHADEMA. Mtafiti mzuri angehakikisha anajiridhisha na maana ya uongozi kutoka kwa wahusika kabla ya kwenda mbele zaidi. Wewe umeamua kuchagua watu sita tu katika kukamilisha utafiti wako. Kwa hakika uongozi wa chama cha siasa serious kama CHADEMA hauwezi kupimwa kwa kuangalia watu sita tu. Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA (nayo ipo katika mtandao) huwezi kukamilisha kuzungumzia uongozi wa CHADEMA bila kutaja Kamati Kuu. Hiki ndicho chombo kinachofanya maamuzi ya kisera ya chama chetu, na nafikiri hata vyama vingine. sasa twende kwenye kamati kuu halafu tupate jibu katika hypotheses zako mbili zifuatazo:

i) kwamba chadema ni chama cha familia. Familia kwa mujibu wa Tafiti na Chinga inamaanisha ukoo wa Mbowe, Mtei na Ndesamburo
ii) kwamba chadema ni chama cha watu wa kanda ya kaskazini. Kanda ya kaskazini kwa mujibu wa mtafiti Tafiti ina maanisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara

Wafuatao ni majina na mikoa watokako wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA:
F. Mbowe (Kilimanjaro)
W. Slaa (Manyara)
S. Mzee (Zanzibar)
E. Mtei (Kilimanjaro)
B. Makani (Shinyanga)
S. Akwilombe (Lindi)
H.M Yusufu (Zanzibar)
M. Abama (Zanzibar)
J. Kasisiko (Kigoma)
P. Ndesamburo (Kilimanjaro)
L. Massay (Manyara)
S. Srfi (Rukwa)
C. Wangwe (Mara)
S. Lyimo (Kilimanjaro)
H. James (Dar)
P. Shelembi (Shinyanga)
M. Baregy( Kagera)
C. Abwao (Iringa)
V. Kimesera (Arusha)
M. Majala (Dodoma)
A. Ame (Zanzibar)
Z. Kabwe (Kigoma)
M. Mzirai (Dar)
S. Kahatau (Kagera)
M. Meleky (Dar)
M. Said (Kigoma)
A. Bishaga (Mtwara)
I. Ndowa (Dar)
L. Swala (Pwani)
A. Komu (Zanzibar)

Kwa kufuata utaratibu wa utafiti wako wa kugawa viongozi wa CHADEMA katika kanda, ukiangalia hapo wajumbe wa kamati kuu wanatoka katika mikoa 13 na kanda saba zifuatazo: Kaskazini, Kusini, Nyanda za juu, Ziwa, Pwani, Kati na Zanzibar. Idadi ya wajumbe katika kila kanda na asilimia zao ni kama ifuatavyo:

Kaskazini: 7 (23.3%), Ziwa: 5(16.7%), Nyanda za juu: 4(13.3%), Kusini: 3 (10%), Zanzibar 5 (16.7%), Kati 1( 3.3 %) na Pwani 5 (16.7%).

Katika wajumbe hawa wote (30), wenye mahusiano ya kindugu ni wanne ambao ni Freeman na Mtei na Ndesamburo na Grace. Hawa ni sawa na asilimia 13.3 ya wajumbe wote. Katika hypothesis ya pili utaona kuwa wajumbe watokao kanda ya kaskazini ni saba tu ambao ni sawa na asilimia 23.3 ya wajumbe wote.

Ni ushabiki pekee na wala sio utafiti na uchambuzi unaoweza kukufikisha katika majumuisho kuwa CHADEMA ni chama cha kikanda au cha kifamilia.
 
Kichuguu.

Unachekesha sana mbona unaleta Udikteta wa chadema humu? unasema nisikuulize chochote wala nisikujibu huku ukijenga hoja, hapa hatupo Chadema kusiko na uhuru wa kuhoji.katika haki ndogo kabisa za binadamu ni kumpa nafasi ya kujibu au kuhoji ina maana Chadema wakiingia madarakani mtu akituhumiwa tu basi anawekwa ndani hana nafasi ya kujitetea?someni adminstrative law kuna kitu judicial review halafu tizama natural justice inasema nini?
Inaelekea una ushabiki wa kisiasa badala ya kuchambua issues. Sasa swala la Chadema na post yangu limekujaje hapa. Mimi si mwanachama wa chama chochote pale Tanzania; sishabikii wala kumchukia mwanasiasa yeyote ila ninasupport mambo mema au kukemea mambo mabaya wanyofanya wanasiasa wote bila kujali vyama, makabila, dini au elimu zao.

Nimekuambia usinijibu wala kuniuliza swali kusudi nisikutoe nje ya mada yako. Maoni yangu hayako kwenye mwelekeo wa mada yako, kwa hiyo kuendelea kujibizana nitakuwa ninayumbishwa mwelekea wa mada yako bure tu.

Ufinyu wa akili yako.
Kwa hiyo wewe unajidhani kuwa una akili pana ndiyo maana unakaa kujadili watu binafsi tena kwa kwa jazba hivyo? Watu wenye akili pana wanachambua mambo kwa jumla na kupokea mwazo ya upande mwingine. Wewe siyo mmja wao kwa vile unapigania kuwa usikilizwe na ajenda yako hata kama kuan uwongo

Watu wanaposema Bush kachukua kazi ya baba yake haina maana kuwa alipotoka baba yake aliingia yeye,kwa akili zako za kichadema utasema NO alichukua baada ya Clinton.
No, wacha upumbavu hapa. Hujui kuwa baba yake Bush alikuwa President na Bush mweyewe naye ni President; kwa hiyo kuna kosa gani kusema kuwa Bush alichukua kazi ya baba yake. Bush aliinga madarakani baada ya Clinton je unaona hiyo siyo kweli? Kama ungekuwa na akili pana usingeweka upupu kama huu.
kuna mifano mingi ya hilo nenda kwenye Taasisi mbalimbali hasa hizo za fedha hapa nyumbani utaona labda hazina kuna watu wengi wa kaskazini, jibu kuwa huko nyuma kulikuwa na mtu au watu toka maeneo hayo wameacha athari kwangu mimi ni athari mbaya, ukienda Bima, Nbc,jeshini na hata polisi ndio utakuta kuna misemo ya maeneo fulani ya kazi imeathiriwa na huo mfumo mbaya wa kupendeleana au kujaza watu wake mfano mtu anasema" harrow liafande" na huo msemo unakuta umetawala ktk kitengo fulani ni kuonyesha jinsi watu hao walivyomiliki eneo hilo. samahani Jasusi kama nimegusa,

Kichuguu.


Nimesema Mtei alimpa kazi Mbowe na yeye mwenyewe hajakanusha kwanini wewe uje kujibu wakati mwenyewe yupo hai na ametoa ahadi hiyo?, bahati ya mwenzio usi ilalie mlango wazi, unashangaa kupewa kazi na mke?, yote yanawezekana. hakuna principle yeyote inayosema mtu akikupa kazi hawezi kukupa mwanawe.
Kurundikana kwa makabila fulani katika taasisi fulani fulani kulitokana na ama makabila hayo kupenda kazi hizo sana (kwa mfano wakurya na jeshi) kiasi kuwa mamobi yao yalikuwa ni mengi kupita maombi ya makabila mengine, au kuwa na afisa utumishi mweye ukabila.

Mtei hakuwa ofisa utumishi wa benki kuu wakati huo, kwa hiyo asingefanya hivyo labda kwa kumwomba afisa utumishi ambayo sioni mantiki yake kama nitakavyoeleza huko mbele.


Mtei na Mbowe kutokanusha unayoandika haina maana kuwa wameyakubali. Nimeonyesha kuwa Mtei asingempa kazi kulingana na timeline ya Mtei alipokuwa madarakani na umri wa Mbowe. Mimi ninakupinga siyo kuwa ninawatetea ila ninapinga kwa vile taarifa unazotuletea siyo za kweli. Mengine uliyoandika ni upuuzi tu.
kukusaidia uelewa wako mdogo tizama suala la Mkapa kuwa rais wa Tanzania watu wengi wanasema na kuamini kuwa Marehemu mwalimu Nyerere alimsaidia kumpata hayo madaraka, na kuna wengi wanasema na kuamini kuwa Malecela na Lowassa walikosa nafasi za kuwa marais 1995 kwa mkono wa mwl. jee mwaka 1995 mwl Nyerere alikuwa rais wa Tanzania? au alikuwa Mwenyekiti wa chama? au alikuwa makamu mwenyekiti? au alikuwa katibu mkuu wa CCM?

na hakuna mahala kusikia watu wakisema aliyekuwa rais na mwenyekiti wa chama Alhaji Mwinyi alimsaidia Mkapa kupata nafasi ile, au kusikia Malecela ana kinyongo naye kwa kuikosa nafasi ile.

kwani hiyo ni siri? Wewe ndiye kipunga kweli kweli, hata hujui kuwa Nyerere alikuwa powerhouse wa Tanzania. Kwenye kamati kuu ya CCM hakuna aliyekuwa akimpinga. Umesahau kuwa ndoto ya Lowasa na Kikwete kwenye kinyang'anyiro hicho kilizimwa na Nyerere? Alilokuwa akisema lilikuwa linafuatwa? Halafu bado unajifanya kuwa na ulewa mpana wa mambo? Unataka kusema kuwa Mtei alikuwa powerhouse wa Benki kuu hata baada ya kuondoka kama Nyerere kiasi kuwa kila alichosema kilifanyika?

kumbuka hayo ni madaraka makubwa kabisa ktk nchi.
jee Mtei atashindwa kumpa kazi ya ukalani BOT bwana Mbowe?

Unachosema ni kuwa Mtei alimpa kazi Mbowe, na hilo ndilo sijakubaliana nalo. Ungekuwa unapanga mawazo yako kwa makini labda nigewezea kukuelewa lakini kwa vile unabwatuka bila mpangilio ndiyo maana labda sikuelewi. Kupata kazi ya ukarani kulikuwa hakuhitaji high level authority ya Mtei ambaye wakati huo alikuwa aidha World Bank au IMF. Kwanza kumbuka kuwa miaka hiyo ya 70na mwanzoni mwa miaka ya 80 vijana wote wa form six walikuwa wakipangiwa kazi na utumishi; ni watu wa utumishi ndio waliokuwa wakigawa post zile kiupendeleao. Kwa vile Mtei hakuwa serikalini tena, kama ilikuwa ni lazima amsaidie Mbowe kupata ukarani wa direct employment pale benki kuu, ni kwamba alitakiwa ama "amwombe" afisa utumishi wa Benki Kuu au "afanye mipango huko utumishi" ili post ya Mbowe iwe ni benki kuu, tena hilo lifanyike wakati angali JKT. Umuhimu wa Mbowe kwa Mtei wakati huo hadi Mtei afikie hatua ya kufanya mojawapo la hayo mawili siuoni na ndiyo maana jambo hilo haliingii kichwani mwangu. Kwa bahati mbaya umeshindwa kunionyesha hilo, badala yake unabwatuka tu.
Kichuguu sitakwenda mbali naona uoni wako mdogo sana.
Nimeshakuonyesha kuwa wewe ndiyo kipunga kabisa; kelele tupu, mantiki hamna. Mifano yako yote uliyoweka hapo kuhalalisha kuwa Mtei alimpa kazi Mbowe pale BOT haina mantiki yoyote. Kuna upupu mwingi sana ulioandika ambao hauna mantiki yoyote. katika yote uliyoandika nimefurahishwa na jambo moja tu la matumzi ya helikopta ingawa baadaye umeshindwa kulisupport vizuri, mengine yote unayoandika ni ya ki-KCC tu.
 
mwanasiasa.

ulikuwa unajibizana na Ttj,lakini umekuja kwangu.
anyway nitakupa hoja.

unadai H.James ni mjumbe toka Dar, je hujui kama ni mtu wa kaskazini? na mambo yao yote yako kaskazini.

kuna M.Mziray amabye naye ni wa Kilimanjaro ila mnadanganya katoka Dar,

mwingine ni Melecky naye ni kilimanjaro ambaye naye mnadai katoka Dar,

tizama wajumbe kutoka Dar ingekuwa ni wale wenye kuielewa Dar, nilitegemea majina ya kina JONGO, Jumbe, akida, Manitu au ngozoma matunda ndio kuwa wajumbe wa Dar.

Akwilombe ilitakiwa awe toka Dar, kwani siku zote maisha yake yapo hapo ila kuna kiini macho. mlichofanya kama mashindano ya Miss TZ, unakuta binti anaishi Dar ila kuchukua advantage ya mashindano anasema yeye ni Miss -Lindi ambako hana mizizi nako nahajui chochote hata mashindano ya disco ni hivyo hivyo utasikia John Bosco cool J toka Songea kumbe kazaliwa na kukulia Kurasini-shimo la udongo, inawezeka mmekopi pale Mbowe club vijana wanavyotumia mikoa kuingia kwenye mashindano na Mwenyekiti akaleta hiyo idea hapo.

Hapa umeweka Anna Komu kuwa anatoka ZNZ.

tizama wewe mwenyewe Komu akiwa ana lake jambo linalohusu ZNZ huwa hatumii ANNA ana jina lingine hulitumia unalijua sana, na akiwa na Jambo linalohusu kilimanjaro anatumia ANNA KOMU maadamu limetumika Anna Komu huwezi kunishawishi kuwa ni mtu wa ZNZ.

Tume ya uchaguzi mwaka jana ilimpa mashaka makubwa juu ya Uzanzibar wake, kilichotea kuona Chadema imeondekewa na Marehemu Jumbe na huku imekosa mtu yeyote ikija huruma tu,

Anna Komu ni mtu ambaye mambo yake yote yako Kilimanjaro na alipofika huko akaamua hata kubadili jina lake ili wenzake wasimjue, kama mjumbe toka ZNZ angeitwa bi Zuhra bint Shaaban, bi ZULEKHA, bi mwanakombo umesikia bwana eehh.

lakini ANNA KOMU kusema ni mjumbe toka ZNZ ni utapeli tu kama unaotumika kwenye mamiss Tanzania.

Ukitizama utaona data zako ni za uongo kama Kichuguu, jasusi au Mnyika ambaye anadai gazeti liliandika kwa makosa kuwa mwenyekiti yuko Moshi , huku hiyo habari haijakanushwa na hilo gazeti, kakanusha yeye tu tena kwenye Jambo forum na si vyombo vyovyote vya habari-Tanzania.

wewe ukatudanganya kuwa holiday imeanza kwa baadhi ya University U.K na kuna special arrangement yake huku ukijua unaongopa vyuo vyote vinaanza holiday this friday.

tumewasiliana na registrar wa university ya Hull on 441 482 465136 wamesema Mbowe hayupo shule na chuo hakijafungwa. jee Mnyika kwanini hakupiga cm chuoni kujua wapi jamaa yupo?

Akili ndogo tu, ilikuwa hivi mtu kaaga anaenda chuoni-Hull na kila mtu anajua yuko chuoni na kama kumetokea dharura yeyote ya kumtafuta basi kama mimi kwa ujinga wangu ningemtafuta kwanza chuoni ambako ndiko kwenye last contact zake?
lakini Mnyika kapiga Moshi kumuuliza Mwenyekiti huo ni usanii tu.

Kichuguu.

Naona umepita mlemle kwenye njia zangu- huna jipya Pumba zilezile za chama chako.
wewe umedai Mtei alikuwa hayuko na mimi nitakupa mifano zaidi ya mia 100, kukuonyesha kuwa watu wangapi wameingia kwenye kazi kwa nguvu za watu waliopo au waliokuwepo kwenye hivyo vitengo, ndio nikakupa akina Bush, Mkapa, Lowassa na Malecela ili uelewe, lakini kwa akili zako za kushikiwa unanielekeza tena mimi maelekezo niliyokupa wewe upate kuelewa. hiyo akili au matope?

nikakwambia hawa niliwataja wamepata kazi kubwa kabisa za urais itakuwa kazi ya ukarani? kwani Mbowe alikuwa ni karani tu pale kazi ya tatu toka chini kulikuwa na wafagiaji na walinzi halafu ni ukarani. narudia tena aliyempa kazi yupo hai(Mtei) na aliyepewa kazi yupo hai(mbowe) na wanapita humu kama ni uongo wangesema wao sio wewe kichuguu? na dalili ya uongo na uoga wako ni hii unaleta hoja halafu unajiwahi " usiniliulize swali wala usinijibu Chinga" umewahi kuona wapi mijadara ya namna hiyo? kwanini uogope maswali kama huongopi?

Mbowe alisema atajibu maswali akipata nafasi hakuna sehemu alisema atakuja kichuguu kumjibia.
 
Kichuguu.

Naona umepita mlemle kwenye njia zangu- huna jipya Pumba zilezile za chama chako.

wewe umedai Mtei alikuwa hayuko na mimi nitakupa mifano zaidi ya mia 100, kukuonyesha kuwa watu wangapi wameingia kwenye kazi kwa nguvu za watu waliopo au waliokuwepo kwenye hivyo vitengo, ndio nikakupa akina Bush, Mkapa, Lowassa na Malecela ili uelewe, lakini kwa akili zako za kushikiwa unanielekeza tena mimi maelekezo niliyokupa wewe upate kuelewa. hiyo akili au matope?

nikakwambia hawa niliwataja wamepata kazi kubwa kabisa za urais itakuwa kazi ya ukarani? kwani Mbowe alikuwa ni karani tu pale kazi ya tatu toka chini kulikuwa na wafagiaji na walinzi halafu ni ukarani. narudia tena aliyempa kazi yupo hai(Mtei) na aliyepewa kazi yupo hai(mbowe) na wanapita humu kama ni uongo wangesema wao sio wewe kichuguu? na dalili ya uongo na uoga wako ni hii unaleta hoja halafu unajiwahi " usiniliulize swali wala usinijibu Chinga" umewahi kuona wapi mijadara ya namna hiyo? kwanini uogope maswali kama huongopi?

Mifano yako haifanani na unachodai. Mfano wako wa Bush na baba yake haufanani kabisa na Mtei na Mbowe benki kuu, mfano wa Nyerere na Mkapa pia haufanani kabisa na kesi ya mtei na Mbowe unayodai; hiyo ndiyo imenifanya nihoji busara zako. Vile vile kudai mimi ni chadema ni upuuzi kabisa, siko hapa kupiga kampeini za vyama hapa kama wewe; nilikwambia kuwa ninatafuta habari tu, hainifurahishi kama habari hizo ni za uzushi.

Timeline ya Mtei serikalini hafanani na madai yako ya kumweka Mbiowe benki kuu. Hii ndiyo inanifanya nihoji ukweli wa mambo yote unayoandika. Jambo la maana ambalo ungefanya niku-elaborate madai yako hayo badala ya kuanza kutukana wanaokuhoji.

Mtu kutokukujibu haina maana anakubaliana na madai yako, inawezekana anamkudharau; ukiona mtu anaacha kukujibu bila ku-acknowledge basi usichukulia kuwa amekubaliana nawe. Afterall, hata hata kama Mbowe asipokujibu itakuwa ni sawa tu kwa vile wewe umekuwa kwenye upande wa kumshambulia binafsi kuliko kutafuta ukweli; sidhani kama kweli atakuja kukujibu.
 
Chinga,

Kusema Freeman alipewa kazi benki kuu na Mtei hapo mshikaji umeteleza. Sii kweli na sisi tuliokuwa karibu naye enzi hizo tunajua Freeman alikuwa na nani. Walipita wengi kabla ya huyo bii mkubwa. Kisha Freeman alikuwa akikamata kitu hukamata hasa mji mzima huipata.
 
Nilishagive up on this topic kwa vile I am angered by Admin kwa kukoroga mambo mambo, we were fine all along lakini akaona afanyizie....nimetumiwa PM kumbe Admin na wewe ni wa kaskazini?!! pole najua unaumia tukiiisema hii familly business....



Mwanasiasa, I acknowlefdge to have read your arguments and will be back.

Ingawa the swali langu sasa nakuuliza mara ya nne:

Ulikuwa unajua kwamba Ndesamburo, Grace na Lucy wana mahusiano ya kifamilia kabisa? Hukuhisi kama kuna ka-upendeleo kwa Mzee Ndesamburo?

Au kama umejua sasa what is your reaction.

Swali hili umelikimbia sana na linazidi kufuel speculations kwamba unahide kitu.....
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom